Mgomo wa madaktari - Updates

Serikali Lazima itishe isichezewechezewe; Naafiki maneno yako, hapa chini naweka nukuu kutoka kwenye Biblia
kitabu cha1 cha Wafalme sura ya 2;
the days of David drew nigh that he should die; and he charged Solomon his son, saying,
... I go the way of all the earth: be thou strong therefore, and shew thyself a man;


Wito kwa JK, ni wakati wa kutenda sasa, usitake kuwapendeza madaktari kwa kuwa wanaua watu na
kuuonesha uma kuwa wewe ni dhaifu, fuata maneno ya Mfalme Daudi aliyomwambia Mfalme Suleiman
wakati alipomtawaza... "be thou strong therefore, and shew thyself a man;"
Sheria zipo wazi wataalamu wetu wamevunja sheria, umewabembeleza vya kutosha, chukua hatua...muda wa kutafakari umepita.
Najua maneno haya yatawaudhi sana mashabiki wa mgomo lakini hata kama Dr. Slaa akiwa rais hawezi vumilia hali hii

Ameeeen! Biblia bila Quinine malaria itakuua mkuu.
 
Tatizo siyo Mponda wala Lucy Nkya, bali tatizo lipo Utumishi na Hazina.
Tulianza na Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa wizara tukadhani tumetatua
tatizo kumbe wapi? Sasa tutawafukuza Mponda na Lucy Nkya, kisha tutadhani
tatizo ni Pinda, tutamuondoa na yeye lakini bado tatizo litakuwa palepale na
hatutakuwa tumetatua tatizo kwa kuwa serikali haina hata senti Hazina.
Mishahara ya kuwalipa wafanyakazi wake inakopa kwenye taasisi binafsi,
balozi zetu hazina pesa, wanaishi kwa kuganga njaa kwa kuwa tulichopitisha
kwenye bajeti yetu kilikuwa ni kuchumia tumbo, tuna madini lukuki lakini
yote tunayagawa kwa mikataba isiyo na tija, mibovu kuliko ya enzi za kina
Karl peters, tunasamehe kodi wakati tunategemea misaada ya wahisani!

Waziri Mponda au Lucy Nkya watafanya nini endapo hazina imekataa
kutoa fedha? Watafanya nini wakati Hawa Ghasia (Utumishi) ni tatizo
katika utumishi wa umma? Tafakari, chukua hatua...
ndiye anayesababisha yote haya?

siyo hiyo tu, tatizo hapa ni katiba yetu mbovu ambayo ingeweza kumwajibisha huyu kiongozi dhaifu kabisa hajawahi kutokea duniani.
Hawa viongozi wasio na uwezo aliowaweka thru uswahiba, udini, ushikaji, upenzi hawezi kuwafanya chochote zaidi ya kuwakenulia meno
 
Serikali inampango kabambe wa kuonyesha makucha yake kwa madoctor na kuwa haitishiki na vifo vya raia wake na nilazima ishinde kwenye timbwili hili no matter what!

Hii ndio tafsiri niliyoipata baada ya tamko la waziri mkuu baada ya madaktari kutoa tamko takribani mwezi mmoja tangu wasitishe mgomo wakwanza ambao ulisababisha maafa makubwa baada ya kuvutana na PM wakutanie wapi mwisho PM akakubali kwenda kwenye venue ya madaktari.
we unaona ni akili kama hutushiki na vifo vya waliokuweka madarakani?yetu macho
 
Habari nilizozipokea sasa hivi kwa njia ya SMS kutoka kwa doctor mmoja pale Mhimbili zinasema hivi,nanukuu,"Hii ya sasa ni bab kubwa responce ni 100% MPAKA EMERGENCY,intern ndio wamemaliza kikao chao cha kupeana moyo na specialist ndio wanaanza Russian culture nw..together we can make it" mwisho wa kunukuu sms niliyoipokea.

My take; hivi serikali ina shindana na madaktari kwa ajili ya maslahi ya kisiasa? au inatakiwa kulinda afya za wananchi wake?
Maana kama mawaziri wamelalamikiwa na ni kweli wameshindwa kuwajibika kwa nini waendelee kuwepo hapo?na je inawezekanaje kupokea malalamiko ambayo kimsingi wao ndio wanalalamikiwa na kisha wakayafanyia kazi?
Nawasilisha wadau

du aisee bonge la update he he he he he he
 
sidhani kama madaktari wanaweza kugoma mara hii napata mashaka wacha tuone ila ni ngumu sana
 
Hivi huyu bwana anesema eti madakari ni magaidi,anajua kufikiri kweli? Au anaropoka kwa kutumia tumbo?kichwani mwake ni kama kuna makamasi tu,hakuna akili hata kidogo,Taaluma hii ni nyeti sana sio ya kufanyia siasa na ubabaishaji, ni ya kiutendaji sana kuliko chochote,la sivyo rais ajihudhuru tu! Wala sio dhambi akijihudhuru.
 
wengi mnaojadili humu mnajadili kwa upana mdogo sana, lamsingi madfaktari waangalie mipaka ya majukumu yao, wao ni wataalamu, hawawezi kumpangia Raisi nani wa kumpa wizara na nani wa kumtoa, na Raisi akiwakubalia matwakwa yao ya kuwaondoa mawaziri atakuwa hajatumia busara, nawasihi madaktari wasilegee kwenye kudai maslahi yao na waboreshewe mazingira yao ya kazi, lakini wasijiingize kwenye mambo ya kisiasa wawaachie wanasiasa mambo yao.

Wewe Kichwa box kabisa, hao ma md dr. kwa upande wa pili ni wenye nchi, mwenyenchi gani ambaye hana mamlaka ya kumpangia mwajiriwa wake ya kufanya?
 
Nailaumu serikali na viongozi wanaoenda kutibiwa nje ya nchi kuliko ninavyowalaumu madaktari, msimamo wangu uko pale pale, nawashauri wananchi wawe upande wa madktari endapo ni kweli madaktari wanasimamia uboreshaji wa huduma za afya.
 
wanaobisha kuwa kuwa mgomo upo, mie niko home nimepata update kwa breaking news za ITV kuwa madoc wameridhia mgomo kuanzia saa hz, na madoc wameonekana wakiwa ktk vikundi vikundi huku wengine wakipanda kwa magar yao na wengine daladala wakiondoka so habar ndio hyo jaman.
 
Mob psychology ime wa-affect madaktari wetu. Natoa ushauri kila mmoja atafakari ni nini anachogomea hasa kama yeye binafsi bila kutegemea vikao vyao wanavyokaa kupeana molali! Kama ni maslahi yake hayajatekelezwa au ni kuto kujiuzuru kwa mawaziri au vyote viwili. Na ukiangalia dai la kuto kujiuzuri/kutowajibishwa mawaziri imemeza madai yao yote ikiwemo ya masilahi yao. Sasa wawe makini katika madai yao wasije wakawa wanatumiwa na kundi fulani bila kujijua? na hii ndio madhara ya mob psychology. Nawashauri waonane na wataalam wapate ushauri?
 
Naomba ufahamu wenu tafadhali, unaendesha gari ya abiria, umepakia abiria 65, uko na speed 80kph, ghafla wananaingia watoto wawili wanakimbizana barabarani umbali wa 25m katika eneo ambalo kushoto ni ngema na kulia kwako ambako ndio unakunjia kona ni bonde, wewe kama dereva utafanyaje? kisha linganisha jibu lako na sakata la madaktari.
 
Huu mgomo ni batili kisheria. Serikali ina haki ya kuwashtaki au iwafukuze kazi wale watakaoendelea kukaidi rai ya kuwataka warudi kazini.

For Dr's info: ma-dr wa kutosha kutoa huduma za dharura wako stand-by toka nchi rafiki. Liwalo na liwe, watakuja kuokoa roho mnazotaka zipotee. In the meantime serikali inajipanga kushughulikia kiburi chenu na kuwarudisha kwenye saizi yenu halisi.

Kipindi hiki lazima jambo litafanyika, hata kama ni kwa gharama. Lazima kukomesha hii jeuri ya madaktari kuvunja katiba na kutaka kuingilia madaraka ya Rais ya kuteua wasaidizi wake.

Serikali kipofu na mbumbumbu itafanya hivyo. Kama wana uwezo huo kwanini hawakutatua mapema matatizo haya. Sipendi huu mgomo lakini musitoe vitisho vya kijinga kama hivyo kama wewe upo kwenye nafasi ya ushauri ungetumia hizo hela kumshauri atatue hata kabla ili. Serikali yenyewe imefulia hazina kuna mabox tu ya kuwekea hela, hela hakuna
 
Katika hatua kama hii ndipo ninamkumbuka Lowassa kijna wa maamuzi magumu angeamua liwalo na liwe. Fukuza bila gari waziri na naibu wake kuokoa roho za wengi kuliko kuwakumbatia huku tukila hasara lkuuubwa
 
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa..

Ni muhimu viongozi wetu kukaa chini na kuanza kijitafakari sasa, mambo wanayofanya siyo mazuri
 
Haiwezekani kuweka REHANI ya watanzania milioni 40 ili kulinda ajira za maswahiba wawili mponda na nkya.
Aluta kontinua.
 
Wajameni kwa walio katika maeneo husika tunaomba updates;

Naona blablabla zimezidi sasa hakuna updates.




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Back
Top Bottom