Torra Siabba
Senior Member
- Jul 24, 2016
- 105
- 102
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inaelezwa kuwa Wanawake takribani 287,000 hadi 300,000 hufariki wakati wa ujauzito na kujifungua na zaidi ya Watoto milioni mbili hufariki katika siku 28 za mwanzo baada ya kuzaliwa. Takwimu hizo ni za Mwaka 2020.
Takwimu hizo zimenisukuma kutoa ya moyoni kuhusu hospitali yetu pendwa ya rufaa ya Bugando iliyoko Jijini Mwanza ambapo naona tatizo linazidi kukuwa.
Kuna taarifa kwamba baadhi ya wakina Mama wanaojifungua kwa oparesheni katika Hospitali ya Bugando waliowengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na mgomo wa madaktari bingwa wa upasuaji kutolipwa stahiki zao kwa wakati jambo ambalo lina athari kubwa kwa jamii yetu maana kama wasipolipwa tutapoteza wagonjwa wangapi?
Taarifa nilizonazo ni kuwa hata viongozi wa Hospitali ya Bugando wanalijua hili suala la Wanawake wenye kujifungua kwa oparesheni kwamba hawapati huduma ipasavyo, hivyo viongozi waamke kabla hospitali ile haijaingia kwenye rekodi ya Hospitali inayoongoza kwa vifo vya Mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Jambo hili halizungumzwi lakini ndio ukweli wenyewe huo, mamlaka zifike hospitalini hapo na kufanya uchunguzi.
Kingine, hao Madaktari Bingwa wamekuwa wakiwaacha wagonjwa mikononi mwa madaktati ambao wako field (wanaojifunza kwa vitendo) wanaosoma Chuo cha Bugando bila kuwa na usimamizi wa mtaalam au wataalam zaidi yao, jambo ambalo ni hatari kwani Mwanafunzi anakuwa hana ujuzi wa kutosha.
Bugando iachane na tabia za kushindwa kuwahudumia akina mama wajawazito na wale wanaojifungua kwa uparesheni kwani wanategemewa na sehemu kubwa ya nchi yetu kwa kutoa huduma za kitabibu.
Serikali ya Rais Samia ifanye jambo kuhusu Hospitali ya Bugando, kwa hiki kinachoendelea kama kikisambaa, itamaanisha kuwa litakuwa pigo kubwa kwa sio tu kwa Mwanza au Kanda ya Ziwa bali Taifa kwa jumla.
Pia soma: DOKEZO - Hospitali ya Bugando hamuwaoni Manesi wanaoacha kuhudumia Wagonjwa na kuwa bize na Biashara kwa Wajawazito?
=================
Updates...
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachunzibwa alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema hana hizo taarifa lakini atafuatilia, baadaye alipotafutwa akasema atafutwe Mkurugenzi wa Bugando ndiye anaweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt Fabian Massaga alipoulizwa kuhusu hoja za Mdau akasema “Onana na PRO atakupa ufafanuzi wa kutosha.”
Upande wa Afisa Uhusiano wa Umma wa Hospitali ya Bugando, Evelyne Mahalu amesema “Tunalifanyia kazi kujua ukweli wake, pia BMC ni Taasisi inayosimamia taratibu na miongozo ya Nchi katika suala zima la kuzuia vifo vya mama na mtoto.”