Uhuru wa Habari Tanzania: Kati ya Waparaji na Wakunaji Wazuri, Nani Watamsaidia Zaidi Rais Samia?. Tunakuomba Mama, Usiwaparure Waparaji!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,576
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili hii
Screen Shot 2022-05-08 at 5.13.47 AM.png
Screen Shot 2022-05-08 at 5.22.59 AM.png

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"

Siku ya Mei 3 kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Nchini Tanzania, siku hii imeadhimishwa Kitaifa jijini Arusha, mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa JMT, Rais Mama Samia Suluhu Hassan, japo alisema mengi, Mimi kubwa lililonigusa ni hili...(nanukuu)

"Ukinikuna vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa na kukupuliza ufuu...ufuu... Lakini "Ukinipara..., Nakuparura!", (mwisho wa kunukuu).

Naomba kuianza makala ya leo kwa kumkuna vizuri Rais Samia, Kwa pongezi kwa yeye Rais Samia, ndiye Rais wa kwanza wa Tanzania kuwa mgeni rasmi Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa hapa nchini kwetu Tanzania.

Nimekuwa newsroom kwa zaidi ya miaka 30, hii ndio mara ya kwanza kwa event yetu wanahabari kuhutubiwa na Rais wa nchi. Kiukweli kabisa, Rais Samia, ametuheshimisha sana wanahabari!, asante sana Mama, kutuheshimisha sisi wanahabari, na sisi kwa upande wetu, tunakuahidi kufuata kanuni ya reciprocity, "ukipendwa, pendeka", "ukiaminiwa, jiaminishe" na "ukiheshimiwa, jiheshimishe".

Hivyo kwa jinsi Rais Samia alivyotuheshimisha sisi wanahabari, automatically na sisi wanahabari, tutamuheshimu, tutamkuna vizuri, sio ili atupapase na kutupuliza ufuu..., ufuu, no!, tutamkuna vizuri vile viwasho vinavyotokea sehemu za ngozi laini, vinavyohitaji ukunaji mzuri, ila kukitokea miwasho sehemu za ngozi ngumu, kama kwenye magaga, hakuna budi, ni lazima tutampara.

Kwa vile Rais Samia amethibitisha kuwa na yeye ana ngozi ngumu, ukitokea muwasho kwenye sehemu za ngozi ngumu kama kwenye magaga, hata ukune vipi, muwasho huo hauwezi kukunika ni lazima kumpara, hivyo ikitokea katika kumkuna, badala ya kumkuna vizuri, tukajikuta tumempara, tunamuomba sana Mama yetu, Mama Samia, asituparure!.

Pongezi zangu ziziishie kwa Rais Samia kutuhutubia, bali pongezi kwa vyama vyote vya Habari vikiongozwa na Jukwaa la Wahariri, TEF, MCT, MISA-Tan, TAMWA, TMF, UTPC na waandishi wenyewe wa habari.

Pongezi mahsus kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mwenyekiti mstaafu Absolom Kibanda, for their personal initiatives hadi...
Tena nilifurahi sana Rais Samia alipozungumzia SMS za Kibanda!.

Pongezi za tatu ni kwa Mama Samia, kuikuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kutuongezea misamiati mipya from time to time.
Alianza na neno "Kudemka", likaja neno "mkinizingua, tutazinguana", sasa ni neno "kupara".

Kukuna na Kupara.
Kukuna: ni kujikuna mahali panapokuwasha,
Kupara: Kuchuna magamba ya samaki, Kupara samaki.

Kwenye kujikuna, mtu hawezi kujikuna mwenyewe mgongoni, hivyo mtu ukiwashwa mgongoni ni lazima umuombe mtu mwingine akukune, ili na siku yeye akiwashwa mgongoni na wewe pia utamkuna Kwa kanuni ya "Scratch my back, and I'll scratch yours".

Kwenye kukuna kuna kumkuna na Kukuna, kuna kumkuna mtu vizuri, anayekunwa vizuri, anajisikia Raha, na ukimkuna mtu vibaya, kwa makucha makali kama unapara samaki, anayekunwa anajisikia karaha, na huko ndiko alikokusema Mama, ukimpara, anakuparura!.

Mama Samia katuasa sisi waandishi, tukimkuna vizuri, na yeye atatukuna vizuri, ila tukimpara atatuparua!.

Kila kazi ina kanuni zake, yaani rules of engagement, miongoni mwa kazi za dakitari ni kutibu, katika kutibu, sometimes dakitari anatoa dozi ya kidonge kichungu au kukudunga sindano yanye maumivu ili upone.

Kazi ya media ni kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha, kukosoa na kuwajibika kwa jamii. Media haiwajibiki kukuna vizuri tuu bali kwenye yale ya kustahili kumkuna vizuri, tutamkuna vizuri, Rais Samia hadi kusikia Raha, ila yale yanayostahili kumpara, media hatuna jinsi, ni lazima tuu tutampara, kwa jinsi ile ile ya dakitari kutoa kidonge kichungu au kumdunga sindano mgojwa ili apone, hivyo ni wajibu wa media, kumkuna rais panapostahili kukunwa, na kumpara pale panapostahili kuparwa, Ila kwenye kupara, hatutampara kwa kisu kikali kama kumpara samaki, tutatumia lugha ya heshima,na unyenyekevu mkubwa.

Kati ya media itakayo andika habari za kumkuna vizuri tuu Rais, na media itakayoandika habari za kumpara rais, ni habari gani zitamsaidia zaidi Rais Samia na kulisaidia Taifa?.

Kati ya mtu anayekusifu tuu wakati wote na yule anayekusifu ukifanya mazuri, lakini ukikosea anakukosoa na kukushauri, ni yupi atakusaidia zaidi?.

Huku kukuna na Kupara, kwa lugha nyingine, wakunaji wazuri ni zile media na wale waandishi ambao kazi yao siku zote itakuwa ni kusifu tuu na kumwandika vizuri bila kumkosoa, halafu wapara ni zile media au waandishi watakao mwandika vibaya au kumkosoa. Enzi za JPM, niliwahi kuileta hoja hii
Hivyo sasa kwa vile Rais Samia nae kaja na hoja kama hii hii, naomba tuutumie utaratibu ule ule

Rais Samia nae ni binadamu na sio malaika, hivyo, kama binadamu ni haki yake kukosea, kwasababu nobody's perfect, the only perfect being is God!, hivyo Rais Samia kama Binadamu, kuna mahali anaweza kukosea au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme sio kwa kubeza au kukejeli, bali kufanyike kwa heshima, kwa lugha ya staha na unyenyekevu kwa lengo la kutoa ushauri wa kusaidia, the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" in good faith kwaa nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa letu kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa.

Rais ana sehemu mbili, rais ni taasisi ya presidential institution hivyo rais kama taasisi hawezi kufanya kosa lolote ni perfect being kila kauli yake ni sheria, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na kuongozwa mtu ambaye ni binadamu tuu kama sisi anayeitwa Samia Suluhu Hassan, huyu ni binadamu wa kawaida kama sisi wengine wote, she is a human being, anaweza kukosea. Katika kumkosoa rais, tumkosoe kwa heshima in such a way tusije kujikuta tunakosa uzalendo, badala ya kumkosoa, tunamuaibisha na kujikuta tunajiabisha sisi kama taifa.

Enzi za JPM, kuna Mwandishi wa JF, Ben Saanane, alifanya IJ ya Ph.D ya mtu fulani. Ph.D za UDSM, zinasomewa kwa aina mbili, by thesis, or dissertation. Ph.D by thesis unaweza kuifanyia popote, lakini Ph.D by dissemination iliyochunguzwa imefanywa Full Time, ila hakuna wakati wowote mhitimu huyo alichukua likizo, hivyo Ben Saanane, akaichukua Ph.D yake hiyo, akaichambua jinsi ilivyo fanyiwa plagiarism. Ben Saanane just vanished into thin air!.

Azory Gwanda, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, aliandika makala jinsi watu wanavyoyeyuka kwenye familia mbalimbali huko Rufiki (Mkiru), mara na yeye siku moja, akafuatwa nyumbani kwake, akachukuliwa na gari jeupe Totara Landcruiser ya mkonga, akapotea jumla!.

Kuna siku kuna mwanasiasa fulani, aliitwa msaliti, mzungumzaji akasema wasaliti wa aina hii hawawezi wakaachwa kusurvive tuu!. Hazikupita siku mbili, yule mwanasiasa alimiminiwa pyu pyu za kutosha!, hivyo mtu mwenye kauli yenye mamlaka akisema ukinipara nitakuparura, itategemea utaparurwaje, kwa mtindo wa Ben Saanane, Azory Gwanda, kwenye viroba, au ki Lissulissu Kwa pyu pyu!, ndio maana tunamuomba Mama, haya ya kumparurana haya...

Naomba kauli hii ya Rais Samia, isitugawe sisi media na social media kugawanyika katika kambi mbili kuu, kambi ya kukuna ni kukuna tuu, na kambi ya Kupara, ni kupara tuu.

Kambi ya kukuna na kusifia, wao kazi yao ni kusifia tuu, hata kukifanyika mabaya au maovu kiasi gani, wao watasifu tuu!.

Kambi ya Kupara, ni kuponda na kukosoa tuu, nao kazi yao ni kuponda, kupinga na kukashifu kila kinachofanywa na Rais Samia na serikali yake, hata kiwe kizuri vipi, wao wataponda, watakosoa, watakashifu, wata tukana , watadhalilisha na kubagaza, mfano kazi nzuri ya Filamu ya Royal Tour, kuna watu wanasifu, na kuna watu wanaponda.

Na kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Samia na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watamkosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema, sio kwa lengo la kubeza, kukashifu, kudhalilisha au kubagaza, bali ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema kwa lengo la kusaidia, kutoa angalizo, kurekebisha na kutoa ushauri wa namna bora zaidi ya kufanya mambo. Ukosoaji wa aina hii, ni ukosoaji mzuri, na ndio unaomsaidia Rais Samia na serikali yake kuliko wale wanaomsifia tuu au wanao mpondea tuu.

Maadam Rais wetu Mama Samia, amekiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu na kuonyesha kwa dhamira, maneno na matendo, hivyo kwa niaba ya waandishi wenzangu wa habari, tunamuomba sana rais wetu Mama Samia, kama atafutahia kukunwa vizuri, tunamuomba pia atuvumilie tukimpara na tunamuomba asituparure waparaji, kupara pia ni jukumu muhimu la media, kama daktari kutoa dozi chungu na kudunga sindano.

Wasalaam

Paskali
 
Kiongozi yeyote yule anayejiamini kwenye mambo yake, angependa kusikia kelele nyingi kutoka kwa Waparaji ili aweze kufanya mambo mazuri zaidi kwa wale anao waongoza.

Ila Kiongozi Mwoga, asiyejiamini na Dikteta, atapenda kusikia kelele nyingi kutoka kwa Wakunaji. Na akitokea mtu kutaka kumpara, basi chamoto atakiona. Hivyo Mama ataangalia aende upande gani.
 
Kiongozi yeyote yule anayejiamini kwenyeambo yake, angependa kusikia kelele nyingi kutoka kwa Waparaji ili aweze kufanya mambo mazuri zaidi kwa wale anao waongoza.

Ila Kiongozi Mwoga, asiyejiamini na Dikteta, atapenda kusikia kelele nyingi kutoka kwa Wakunaji. Na akitokea mtu kutaka kumpara, basi chamoto atakiona. Hivyo Mama ataangalia aende upande gani.
Tofautisha kati ya kiongozi na mtawala
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"

Naomba kuianza makala ya leo kwa kumkuna vizuri Rais Mama Samia, pongezi Kwa yeye Rais Mama Samia, ndiye Rais wa Kwanza wa Tanzania kuwa mgeni rasmi Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Niko newsroom kwa zaidi ya miaka 30, hii ndio mara ya kwanza kwa event yetu wanahabari kuhutubiwa na Rais wa nchi. Kiukweli kabisa, Rais wetu Mama Samia, ametuheshimisha Sana. Asante sana Mama Samia, kutuheshimisha sisi wanahabari, na sisi tunakuahidi kufuata kanuni ya reciprocity, ukiaminiwa, jiaminishe, ukiheshimiwa, jiheshimishe, kwa jinsi Rais Samia alivyotuheshimisha wanahabari, automatically na sisi wanahabari, tutamuheshimu, tutamkuna vizuri, sio ili atupapase na kutupuliza ufuu..., ufuu, bali tutamkuna vizuri vile viwasho vinavyotokea sehemu za ngozi laini, vinavyohitaji ukunaji mzuri, ila kukitokea miwasho sehemu za ngozi ngumu, kama kwenye magaga, hakuna budi, ni lazima tutampara. Kwa vile Rais Mama Samia amethibitisha ana ngozi ngumu, ukitokea muwasho kwenye Magaga, hata ukune vipi, muwasho huo hauwezi kukunika ni lazima kumpara, hivyo Ikitokea tumempara, tunamuomba sana Mama Samia, asituparure!.

Pongezi zangu ziziishie kwa Rais Samia kutuhutubia, bali pongezi kwa vyama vyote vya Habari vikiongozwa na Jukwaa la Wahariri, TEF, MCT, MISA-Tan, TAMWA, UTPC na waandishi wenyewe wa habari.

Pongezi mahsus kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mwenyekiti mstaafu Absolom Kibanda, for their personal initiatives hadi...
Tena nilifurahi sana Rais Samia alipozungumzia SMS za Kibanda!.

Pongezi za tatu ni kwa Mama Samia, kikuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kutuongezea misamiati mipya.
Alianza na neno "Kudemka", likaja neno "mkinizingua, tutazinguana", sasa ni neno "kupara".

Msamiati: Kukuna na Kupara.
Kukuna: ni kujikuna mahali panapokuwasha,
Kupara: Kuchuna magamba ya samaki, Kupara samaki.

Kwenye kujikuna, mtu hawezi kujikuna mgongoni, hivyo mtu ukiwashwa mgongoni ni lazima umuombe mtu akukune, na siku yeye akiwashwa nawe utamkuna katika mtindo wa "Scratch my back, and I'll scratch yours".
Kwenye kukuna kuna kumkuna mtu vizuri, na kuna kumkuna mtu vibaya kama vile unampara samaki.

Mama Samia katuasa sisi waandishi, tukimkuna vizuri, na yeye atatukuna vizuri, ila tukimpara atatuparua!.

Kazi ya media ni kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha, kukosoa na kuwajibika kwa jamii. Media haiwajibiki kumkuna vizuri tuu rais, bali kwenye yale ya kustahili kumkuna vizuri, tutamkuna vizuri, ila yale yanayostahili kumpara, media ina wajibu wa kumpara kwa lugha ya heshima,na unyenyekevu mkubwa.

Kati ya media itakayo andika habari za kumkuna vizuri tuu Rais, na media itakayoandika habari za kumpara rais, ni habari gani zitamsaidia zaidi Rais Samia na kulisaidia Taifa?.

Kati ya mtu anayekusifu tuu wakati wote na yule anayekusifu ukifanya lakini ukikosea anakukosoa na kukushauri, ni yupi atakusaidia zaidi?.

Maadam Rais wetu Mama Samia, amekiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu na kuonyesha kwa dhamira, maneno na matendo, hivyo kwa niaba ya waandishi wenzangu wa habari, tunamuomba sana rais wetu Mama Samia, kama atafutahia kukunwa vizuri, tunamuomba pia atuvumilie tukimpara na tunamuomba asituparure waparaji, kupara pia ni jukumu muhimu la media.

Wasalaam

Paskali
Namshukuru sana Mungu nimefanikiwa kuziona awamu zote 6 zilizotawala Tanzania.

Msipoweza kumtumia huyu mama kupenyeza ajenda zenu mtasubili sana.

Baada ya utawala wa kikatili kuangushwa na Mungu, mama ameturudishia uhuru wetu uliyoporwa na muhuni mmoja tu.

Itoshe kusema tulipokuwa tumefikishwa na washamba na mama kuturudishia uhuru wetu mimi namuunga mkono mama mpaka pale atakapokosea dhahiri hata mimi nitampara.

Kwa sasa na mimi namkuna huku nampuliza ufuuu ufuuu naamini asali kama ipo hata mimi nitakamba tu.

Mkuu naomba kibarua temporary PPRA naona jambo letu la sabasaba limekaribia.
 
Kuwaogopa waparaji ni kielelezo cha mtu asiependa challenges, anataka kufanya kazi kwa mazoea, na haya mazoea ndio yanaturudisha mikononi mwa wapigaji.
 
Na wewe unamuuita mama

USSR
 
Mzee paschal Mayalla tunaomba hapo hapo kwenye kukuna na kupara kama utaweza utupatie uchambuzi, maoni, wawazo na mtazamo wako mahususi kuhusu haya masuala yanayoendelea÷

¶ Royal tour - umiliki yake,gharama, mapato, matumizi na faida kwa MAMA TANZANIA

¶ Kupanda gharama za maisha/ mfumuko wa bei na suala zima la bei za mafuta kwa kuzingatia migogoro ya kimataifa( Vita Urusi na Ukraine pamoja na Covid 19)

¶ Nyongeza ya mishahara kwa watumishi ukizingatia Sheria za kazi na mahusiano kazini kulingana na maendeleo ya nchi kisekta

¶ Suala zima la mwelekeo wa mringanyo wa madaraka(balance of power) kwa TAIFA ndani ya chama tawala na nje kwa vyama vya upinzani ukizingatia mwelekeo na dira ya maendeleo kama taifa 2020-2025
Naomba kuwasilisha uwe keen and no biased unapoweka hoja kwa faida ya wa Jamii forum
 
Namshukuru sana Mungu nimefanikiwa kuziona awamu zote 6 zilizotawala Tanzania.

Msipoweza kumtumia huyu mama kupenyeza ajenda zenu mtasubili sana.

Baada ya utawala wa kikatili kuangushwa na Mungu, mama ameturudishia uhuru wetu uliyoporwa na muhuni mmoja tu.

Itoshe kusema tulipokuwa tumefikishwa na washamba na mama kuturudishia uhuru wetu mimi namuunga mkono mama mpaka pale atakapokosea dhahiri hata mimi nitampara.

Kwa sasa na mimi namkuna huku nampuliza ufuuu ufuuu naamini asali kama ipo hata mimi nitakamba tu.

Mkuu naomba kibarua temporary PPRA naona jambo letu la sabasaba limekaribia.
Huu Uhuru unaosema umerudi bado sio kwa kiwango unachotaka kutuaminjsha kila post.
Nj kweli kwenye masuala ya Uhuru ana utofauti mkubwa na aliyepita
Lakini bado sio kihivyo Kama unavyosema na kutuaminisha. Juzi tu hapa mwanahabari mabere makubi anaomba msamaha serikali kwa kosa la kurusha habari ya wamachinga waliandamana mwanza. Serikali ikaenda kushinikiza ITV wamfukuze, na akafukuzwa. Alafu unasema waandishi wapo huru.
Kigamboni mkuu wa mkoa anafukuza waandishi na kuwatisha wasirushe habari ya mgogoro Kati yao na kiwanda Cha nyati. Na kweli habari haikuruka.
Mchora katuni opter hadi Leo ana kesi polisi kwa kuchora katuni ya mama samia akichezea maji.
Hayo ni machache tu.

Utofauti upo, lakini sio kihivyo.
Pia raisi sio malaika, watu watakosoa tu. Kwa kuwa bado makosa mengi yanafanyika
 
Na wewe unamuuita mama

USSR
Yes namuita Mama Samia, kama jina tuu la heshima, kiumri kwangu Mama Samia ni dada, kumuita Dada Samia sio heshima. Hata wife wangu home namuita mama, nina mabinti 5 na vidume 4. Vibinti, japo ni watoto lakini nawaita mama!.
P
 
Huyu bibi watu hawamjui vizuri ni katili hatari sn
Mkuu Bejamini Netanyahu , sii kweli!. Wewe ndio utakuwa humjui vizuri, hivyo najitolea kukusaidia wewe na wengine wa aina yako kukuendeshea somo la kumtambua mtu katili.

Ukatili wa mtu hukaa moyoni, hivyo kwa jicho la kawaida, sii rahisi kumjua mtu mkatili, lakini watu waliojaaliwa jicho la tatu, huona ndani ya moyo wa mtu kupitia macho yake.

Humu ndani nimeisha endesha masomo kibao ya utambuzi, moja ya masomo hayo ni somo kuhusu watu makatili na jinsi ya kuwatambua Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Watu makatili, huitwa ma sadist, namna rahisi ya kuwatambua watu hawa ni ukiona mtu anashangilia vitendo vya ukatili, na sisi Tanzania tuliwahi kuwa na viongozi wa type hii, sisi wengine tukasaidia kuwazungumzia, kama huyu This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?

Kwa vile ukatili hukaa moyoni, na sio usoni, ni vigumu kuubaini. Mimi ni miongoni mwa watu waliopitia changamoto kubwa za maisha. kwanza nilioa nikiwa na umri wa miaka 25, binti miaka 21, tukisoma darasa moja Chuo, TSJ. Hivyo by 30 years tuna watoto 2, wife akapata scholarship ya 4 years US na mimi kubaki na watoto wawili 4 years girl na 1.5 years boy. Hiyo scholarship ndio ikawa jumla!, hivyo kibarua cha kwanza ni kulea familia as a single parent father;. Kibarua cha pili ni search kumpata mama wa Kambi ambaye hata nitesea wanangu. Hapa ndipo nikaingia darasani kubaini Wanawake katili . Utambuzi wa Mama wa Kambi katili unafanyika kwa kumtazama machoni huyo mwanamke wakati akiwa na wewe pekeyenu na akiwa na wewe na watoto wako!.

Hivyo mtu mwenye macho kama haya Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? hawezi kuwa mtu katili!.

Hebu angalia hayo macho kwenye picha hii
1651980993145.png
1651981050482.png

1651981103884.png

Mtu kama huyu, kweli anaweza kuwa katili?. Angalia macho!.

Sasa Kwa faida ya wasiomjua vizuri huyu Mama, jielinishe hapa

Hitimisho
Ile kauli ya "wakinipara nitawaparura" sio kuparura kwa ukatili kutumia makucha kama paka akiparua, au kuparua kama yakupara samaki, hii ni kauli tuu ya tamathali ya semi, kwa media zitakazo mpara, zitaparuliwa kwa kutumia sheria zetu kandamizi zilizopo!

Paskali
 
Kiongozi yeyote yule anayejiamini kwenye mambo yake, angependa kusikia kelele nyingi kutoka kwa Waparaji ili aweze kufanya mambo mazuri zaidi kwa wale anao waongoza.

Ila Kiongozi Mwoga, asiyejiamini na Dikteta, atapenda kusikia kelele nyingi kutoka kwa Wakunaji. Na akitokea mtu kutaka kumpara, basi chamoto atakiona. Hivyo Mama ataangalia aende upande gani.
Mkuu Tate Mkuu , you are absolutely right and very correct, hiki ulichokisema hapa ndio essence ya bandiko hili, tumkune vizuri Mama yetu, only pale panapowashwa pa kustahili kukunwa vizuri, yale maeneo yenye ngozi laini, lakini kwenye maeneo yenye ngozi ngumu, kama kwenye magaga, hakuna jinsi ni lazima tuu tumpare kwenye sugua gaga. Nakumbuka mabafu ya kijijini kuna jiwe la sugua gaga. Siku hizi kwenye ma saloon ya kisasa kuna manicures na paddicures, miguu yenye magaga inarowekwa kwenye beseni la umeme, lina maji yenye dawa, magaga yote yanayeyuka yenyewe!. Kule Masaki kuna saloon wananyoa kwa kutumia lesser, ndevu hazioti tena!.

Nimeshauri wale wa kukuna, wakune vizuri ila na sisi wa kupara, lazima tumpare, ndiko kumsaidia!.

Mama ni Mama yetu, kumsaidia ni wajibu wetu. Tumsaidieni Mama.
P
 
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili hii
View attachment 2216032View attachment 2216034
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"

Siku ya Mei 3 kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Nchini Tanzania, siku hii imeadhimishwa Kitaifa jijini Arusha, mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa JMT, Rais Mama Samia Suluhu Hassan, japo alisema mengi, Mimi kubwa lililonigusa ni hili...(nanukuu)

"Ukinikuna vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa na kukupuliza ufuu...ufuu... Lakini "Ukinipara..., Nakuparura!", (mwisho wa kunukuu).

Naomba kuianza makala ya leo kwa kumkuna vizuri Rais Samia, Kwa pongezi kwa yeye Rais Samia, ndiye Rais wa kwanza wa Tanzania kuwa mgeni rasmi Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa hapa nchini kwetu Tanzania.

Nimekuwa newsroom kwa zaidi ya miaka 30, hii ndio mara ya kwanza kwa event yetu wanahabari kuhutubiwa na Rais wa nchi. Kiukweli kabisa, Rais Samia, ametuheshimisha sana wanahabari!, asante sana Mama, kutuheshimisha sisi wanahabari, na sisi kwa upande wetu, tunakuahidi kufuata kanuni ya reciprocity, "ukipendwa, pendeka", "ukiaminiwa, jiaminishe" na "ukiheshimiwa, jiheshimishe".

Hivyo kwa jinsi Rais Samia alivyotuheshimisha sisi wanahabari, automatically na sisi wanahabari, tutamuheshimu, tutamkuna vizuri, sio ili atupapase na kutupuliza ufuu..., ufuu, no!, tutamkuna vizuri vile viwasho vinavyotokea sehemu za ngozi laini, vinavyohitaji ukunaji mzuri, ila kukitokea miwasho sehemu za ngozi ngumu, kama kwenye magaga, hakuna budi, ni lazima tutampara.

Kwa vile Rais Samia amethibitisha kuwa na yeye ana ngozi ngumu, ukitokea muwasho kwenye sehemu za ngozi ngumu kama kwenye magaga, hata ukune vipi, muwasho huo hauwezi kukunika ni lazima kumpara, hivyo ikitokea katika kumkuna, badala ya kumkuna vizuri, tukajikuta tumempara, tunamuomba sana Mama yetu, Mama Samia, asituparure!.

Pongezi zangu ziziishie kwa Rais Samia kutuhutubia, bali pongezi kwa vyama vyote vya Habari vikiongozwa na Jukwaa la Wahariri, TEF, MCT, MISA-Tan, TAMWA, TMF, UTPC na waandishi wenyewe wa habari.

Pongezi mahsus kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mwenyekiti mstaafu Absolom Kibanda, for their personal initiatives hadi...
Tena nilifurahi sana Rais Samia alipozungumzia SMS za Kibanda!.

Pongezi za tatu ni kwa Mama Samia, kuikuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kutuongezea misamiati mipya from time to time.
Alianza na neno "Kudemka", likaja neno "mkinizingua, tutazinguana", sasa ni neno "kupara".

Kukuna na Kupara.
Kukuna: ni kujikuna mahali panapokuwasha,
Kupara: Kuchuna magamba ya samaki, Kupara samaki.

Kwenye kujikuna, mtu hawezi kujikuna mwenyewe mgongoni, hivyo mtu ukiwashwa mgongoni ni lazima umuombe mtu mwingine akukune, ili na siku yeye akiwashwa mgongoni na wewe pia utamkuna Kwa kanuni ya "Scratch my back, and I'll scratch yours".

Kwenye kukuna kuna kumkuna na Kukuna, kuna kumkuna mtu vizuri, anayekunwa vizuri, anajisikia Raha, na ukimkuna mtu vibaya, kwa makucha makali kama unapara samaki, anayekunwa anajisikia karaha, na huko ndiko alikokusema Mama, ukimpara, anakuparura!.

Mama Samia katuasa sisi waandishi, tukimkuna vizuri, na yeye atatukuna vizuri, ila tukimpara atatuparua!.

Kila kazi ina kanuni zake, yaani rules of engagement, miongoni mwa kazi za dakitari ni kutibu, katika kutibu, sometimes dakitari anatoa dozi ya kidonge kichungu au kukudunga sindano yanye maumivu ili upone.

Kazi ya media ni kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha, kukosoa na kuwajibika kwa jamii. Media haiwajibiki kukuna vizuri tuu bali kwenye yale ya kustahili kumkuna vizuri, tutamkuna vizuri, Rais Samia hadi kusikia Raha, ila yale yanayostahili kumpara, media hatuna jinsi, ni lazima tuu tutampara, kwa jinsi ile ile ya dakitari kutoa kidonge kichungu au kumdunga sindano mgojwa ili apone, hivyo ni wajibu wa media, kumkuna rais panapostahili kukunwa, na kumpara pale panapostahili kuparwa, Ila kwenye kupara, hatutampara kwa kisu kikali kama kumpara samaki, tutatumia lugha ya heshima,na unyenyekevu mkubwa.

Kati ya media itakayo andika habari za kumkuna vizuri tuu Rais, na media itakayoandika habari za kumpara rais, ni habari gani zitamsaidia zaidi Rais Samia na kulisaidia Taifa?.

Kati ya mtu anayekusifu tuu wakati wote na yule anayekusifu ukifanya mazuri, lakini ukikosea anakukosoa na kukushauri, ni yupi atakusaidia zaidi?.

Huku kukuna na Kupara, kwa lugha nyingine, wakunaji wazuri ni zile media na wale waandishi ambao kazi yao siku zote itakuwa ni kusifu tuu na kumwandika vizuri bila kumkosoa, halafu wapara ni zile media au waandishi watakao mwandika vibaya au kumkosoa. Enzi za JPM, niliwahi kuileta hoja hii
Hivyo sasa kwa vile Rais Samia nae kaja na hoja kama hii hii, naomba tuutumie utaratibu ule ule

Rais Samia nae ni binadamu na sio malaika, hivyo, kama binadamu ni haki yake kukosea, kwasababu nobody's perfect, the only perfect being is God!, hivyo Rais Samia kama Binadamu, kuna mahali anaweza kukosea au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme sio kwa kubeza au kukejeli, bali kufanyike kwa heshima, kwa lugha ya staha na unyenyekevu kwa lengo la kutoa ushauri wa kusaidia, the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" in good faith kwaa nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa letu kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa.

Rais ana sehemu mbili, rais ni taasisi ya presidential institution hivyo rais kama taasisi hawezi kufanya kosa lolote ni perfect being kila kauli yake ni sheria, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na kuongozwa mtu ambaye ni binadamu tuu kama sisi anayeitwa Samia Suluhu Hassan, huyu ni binadamu wa kawaida kama sisi wengine wote, she is a human being, anaweza kukosea. Katika kumkosoa rais, tumkosoe kwa heshima in such a way tusije kujikuta tunakosa uzalendo, badala ya kumkosoa, tunamuaibisha na kujikuta tunajiabisha sisi kama taifa.

Enzi za JPM, kuna Mwandishi wa JF, Ben Saanane, alifanya IJ ya Ph.D ya mtu fulani. Ph.D za UDSM, zinasomewa kwa aina mbili, by thesis, or dissertation. Ph.D by thesis unaweza kuifanyia popote, lakini Ph.D by dissemination iliyochunguzwa imefanywa Full Time, ila hakuna wakati wowote mhitimu huyo alichukua likizo, hivyo Ben Saanane, akaichukua Ph.D yake hiyo, akaichambua jinsi ilivyo fanyiwa plagiarism. Ben Saanane just vanished into thin air!.

Azory Gwanda, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, aliandika makala jinsi watu wanavyoyeyuka kwenye familia mbalimbali huko Rufiki (Mkiru), mara na yeye siku moja, akafuatwa nyumbani kwake, akachukuliwa na gari jeupe Totara Landcruiser ya mkonga, akapotea jumla!.

Kuna siku kuna mwanasiasa fulani, aliitwa msaliti, mzungumzaji akasema wasaliti wa aina hii hawawezi wakaachwa kusurvive tuu!. Hazikupita siku mbili, yule mwanasiasa alimiminiwa pyu pyu za kutosha!, hivyo mtu mwenye kauli yenye mamlaka akisema ukinipara nitakuparura, itategemea utaparurwaje, kwa mtindo wa Ben Saanane, Azory Gwanda, kwenye viroba, au ki Lissulissu Kwa pyu pyu!, ndio maana tunamuomba Mama, haya ya kumparurana haya...

Naomba kauli hii ya Rais Samia, isitugawe sisi media na social media kugawanyika katika kambi mbili kuu, kambi ya kukuna ni kukuna tuu, na kambi ya Kupara, ni kupara tuu.

Kambi ya kukuna na kusifia, wao kazi yao ni kusifia tuu, hata kukifanyika mabaya au maovu kiasi gani, wao watasifu tuu!.

Kambi ya Kupara, ni kuponda na kukosoa tuu, nao kazi yao ni kuponda, kupinga na kukashifu kila kinachofanywa na Rais Samia na serikali yake, hata kiwe kizuri vipi, wao wataponda, watakosoa, watakashifu, wata tukana , watadhalilisha na kubagaza, mfano kazi nzuri ya Filamu ya Royal Tour, kuna watu wanasifu, na kuna watu wanaponda.

Na kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Samia na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watamkosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema, sio kwa lengo la kubeza, kukashifu, kudhalilisha au kubagaza, bali ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema kwa lengo la kusaidia, kutoa angalizo, kurekebisha na kutoa ushauri wa namna bora zaidi ya kufanya mambo. Ukosoaji wa aina hii, ni ukosoaji mzuri, na ndio unaomsaidia Rais Samia na serikali yake kuliko wale wanaomsifia tuu au wanao mpondea tuu.

Maadam Rais wetu Mama Samia, amekiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu na kuonyesha kwa dhamira, maneno na matendo, hivyo kwa niaba ya waandishi wenzangu wa habari, tunamuomba sana rais wetu Mama Samia, kama atafutahia kukunwa vizuri, tunamuomba pia atuvumilie tukimpara na tunamuomba asituparure waparaji, kupara pia ni jukumu muhimu la media, kama daktari kutoa dozi chungu na kudunga sindano.

Wasalaam

Paskali
Hii habari ni Mali ya gazeti la mwananchi
 
Namshukuru sana Mungu nimefanikiwa kuziona awamu zote 6 zilizotawala Tanzania.
So do I, nimeripoti newsroom Jan 1990, hivyo nimefanya kazi miaka 5 ya Mwinyi, 10 ya Ben, 10 ya JK, 6 ya JPM na sasa Mama.
Msipoweza kumtumia huyu mama kupenyeza ajenda zenu mtasubili sana.
Naunga mkono hoja, na maadam Mama amethibitisha anapenda kukunwa vizuri, na Wakunaji wazuri tupo, tutamkuna vizuri tuu, ila tatizo ni kwa baadhi ya Wakunaji Wazuri pia ndio hao hao Waparaji, hivyo sijui itakuwaje huo mparuro pale watakapo mpara!. Jee Atawaparua kwa makucha, kwa kumtumia pilato, viroba, pyu pyu au ile ya vanishing into thin air kama Ben Saanane na Azory Gwanda?.
Baada ya utawala wa kikatili kuangushwa na Mungu, mama ameturudishia uhuru wetu uliyoporwa na muhuni mmoja tu.
Hivi hutuwezi kumsifu bila kumbagaza mtu na Kumuita muhuni mmoja wakati kwa wengine wetu huyu ni shujaa wetu!. Naomba usitake kutuudhi!
Itoshe kusema tulipokuwa tumefikishwa na washamba na mama kuturudishia uhuru wetu mimi namuunga mkono mama mpaka pale atakapokosea dhahiri hata mimi nitampara.
Hapa ungeweza kumsifu Mama bila kuita watu washamba.
Kwa sasa na mimi namkuna huku nampuliza ufuuu ufuuu naamini asali kama ipo hata mimi nitakamba tu.
Kwenye asali...ni alamba...alamba!.
Mkuu naomba kibarua temporary PPR naona jambo letu la Sabasaba limekaribia.
Most welcome!.
P
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom