Askarimaji

JF-Expert Member
Jan 28, 2016
253
611
Salaam Wakuu,

Thread hii ya Mwendelezo, itatumika kuangazia hali ya Usalama na matokeo yake katika Mzozo wa Ukraine na Urusi.
Tuzujane hapa kianachojiri..

1645701470915.png

Mvutano kati ya Ukraine na Urusi umefika kiwango cha zaidi kwa miaka mingi, lakini juhudi za kidiplomasia pia zinafanya kazi kwa bidii kutafuta suluhisho la mzozo huo. Kuna masuala mengi nyuma ya mzozo huo ambao ulianza miongo kadhaa iliyopita na kuhusisha nchi katika eneo zima. Hapa tunaangalia kile tunachojua kuhusu mgogoro huo.

Ulianzaje?
Mizizi ya hatua ya hivi punde kati ya nchi hizo mbili inaanzia Oktoba 2021. Hapo ndipo uwekaji mkubwa wa majeshi ya Urusi kwenye mpaka wa Ukraine ulipoanza. Ripoti za picha za satellite na kijasusi zimefichua kuwa zaidi ya wanajeshi 100,000 sasa wako karibu na eneo hilo. Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imetoa picha za mazoezi ya kijeshi. Vifaa vinavyohusika ni pamoja na bunduki za kujiendesha, mizinga ya vita, magari ya mapigano.

Ukraine imeibua wasiwasi juu ya majeshi hayo ya Urusi karibu na mpaka wake ingawa serikali yake pia ilisisitiza kuwa haiamini kuwa Urusi bado iko katika nafasi ya kuchukua hatua za kijeshi.

Msimamo wa Urusi ni kwamba kutumwa kwao kijeshi sio tishio kwa Ukraine na inasema ina haki ya kufanya chochote inachotaka na jeshi lake ndani ya eneo lake. Wengine wanasema huenda likawa jeshi kubwa zaidi la Urusi lililopelekwa karibu na Ukraine tangu Vita Baridi.

"Ukraine inataka kuimarisha usalama wake kwa sababu inahisi shinikizo kubwa kutoka kwa jeshi la Urusi, kwenye mipaka na pia ndani ya eneo la Kiukreni katika sehemu zinazokaliwa za Ukraine," anasema Orysia Lutsevych, mkuu wa Jukwaa la Ukrainia Chatham House huko London. Na njia moja ambayo inatazamia kufanya hivyo ni "kupitia muungano wa pamoja na Nato," anasema Lutsevych.

Lakini Urusi inaamini kwamba uwezo wa kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake ni haki ya uhuru. "Wako katika eneo la Urusi, hakuna anayeiambia Marekani mahali pa kuweka vikosi vyake katika eneo la Marekani," anasema Elena Ananieva, kutoka Taasisi ya Ulaya (RAS) yenye makao yake makuu mjini Moscow. "Kwa mataifa mengine inapaswa kuwa sawa"

"Kama nchi za Magharibi zinavyosema, kila nchi ina haki ya kuchagua jinsi ya kulinda usalama wake." "Lakini, tatizo kuu kwa mtazamo wa Russia ni tishio la Ukraine kujiunga na NATO na miundombinu ya kijeshi ya Nato kukaribia Urusi," anasema Ananieva.

Hii inatupeleka kwenye swali letu linalofuata.

Je, NATO itajipanua zaidi na kuijumuisha Ukraine kama mwanachama mpya?
Kando kupelekwa kwa wanajeshi katika mpaka wa nchi hizo mbili kumekuwa na kutoelewana kwa kidiplomasia kati ya Urusi na muungano wa kijeshi wa magharibi Nato.

"Upanuzi zaidi wa Nato kuelekea mashariki na kupelekwa kwa silaha, ambayo inaweza kutishia Shirikisho la Urusi, haikubaliki," kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov.

Urusi inapinga vikali uwezekano wa upanuzi wa Nato na inataka hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na Nato. Ni msimamo unaoshirikiwa na mshirika wake wa karibu China. Lakini madai haya yamekataliwa na Nato na nchi wanachama wake. Kwa sasa kuna nchi wanachama 30 katika Nato, lakini nchi nyingine zinaweza kujiunga. Ukraine si sehemu ya muungano bali ni 'nchi mshirika'.

"Jamii ya Kiukreni na vyama vya kisiasa vinaamini kwamba hakuna njia bora ya kulinda Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi kuliko kuwa sehemu ya muungano wa pamoja wa usalama," Lutsevich anasema lakini pia anaongeza kuwa uanachama wa Ukraine kwa Nato unaweza usitokee katika siku za usoni.

Huko nyuma katika miaka ya 1990, baada ya kumalizika kwa Vita Baridi na kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, Nato ilitafuta njia za kujenga uhusiano wa karibu na mataifa mapya ya Ulaya ya Kati na Mashariki yaliyojitegemea.

Huu ndio wakati muungano huo ulipopanuka kuelekea mashariki zaidi, kumaanisha uwezo wake wa kijeshi na silaha umekaribia mpaka wa Urusi.

Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev.

Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.'

Ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi" kulingana na Rais Vladimir Putin.

Mnamo Novemba 2021, alisema kuwa uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.

Lakini Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg aliweka wazi kuwa "Urusi haina kura ya turufu au kusema" kuhusu uwezekano wa upanuzi wa muungano huo.

Akizungumza na BBC, mtaalam wa Urusi Ananieva, alielezea wasiwasi juu ya uwezekano wa upanuzi wa Nato. "Miundombinu ya NATO inasonga karibu na mpaka wa Urusi. Nato inapaswa kuzingatia kanuni ya kutogawanyika kwa usalama," alisema.

"Hakuna uwezekano kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano. Nato inapaswa kufikiria mara mbili kuhusu usalama wake ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano."

Wakati juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea, utafutaji wa njia mbadala wa zabuni ya Nato ya Ukraine umeibuka.

'Finlandisation' ni nini na ina uhusiano gani na Ukraine?
Miongoni mwa viongozi wengi wa kisiasa wanaojaribu kutafuta suluhu la mzozo huo ni Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari alitaja neno la enzi ya Vita Baridi "Finlandisation" kwa waandishi wa habari wakati wa safari ya Moscow.

Iliripotiwa kwamba alipendekeza "Finlandisation ya Ukraine", kama sera iwezekanavyo ili kupunguza mvutano katika kanda.

Lakini baadaye, tarehe 8 Februari, Macron alikanusha kutoa maoni hayo yenye utata.

Neno hilo hurejelea hadhi ya Ufini kama jimbo lisiloegemea upande wowote wakati wa Vita Baridi. Nchi hiyo ilikuwa na mpaka mrefu na Muungano wa Sovieti lakini haikuegemea upande wowote.

Msimamo huu ulimaanisha kuwa Helsinki hangekuwa mwanachama wa Nato na Umoja wa Kisovieti haungeona Ufini kama tishio linalowezekana na Ufini ilitia saini mkataba mnamo 1948 na Moscow ilikubali kukaa nje ya Nato.

Hata hivyo, mkataba huo ulimalizika mwishoni mwa Vita Baridi na serikali ya Finland sasa inasema maamuzi kuhusu kujiunga na mashirika ya kimataifa kama vile Nato yanapaswa kuwa mikononi mwake pekee na si kwa nchi nyingine.

Ukraine imesema kwamba pia haitakuwa tayari kuambatana na sera ya "Finlandisation" ambayo ingezuia sera zake za kidiplomasia.

"Nadhani ni jambo lisilokubalika kabisa kwa Ukraine" Lutsevych anasema.

"Ukraine ilishambuliwa ilipokuwa nchi isiyoegemea upande wowote, na pili Putin haheshimu mamlaka ya Ukraine, iwe haina upande wowote au la.

"Ukraini inakataa wazo hili kwa sababu ni sehemu ndogo ya uwezo wa Urusi kudhibiti Ukraine."

Je, kweli Urusi inaweza kuivamia Ukraine?
Kwanza kabisa, Urusi imesema mara kwa mara haina mpango wa kufanya hivyo, lakini kwa baadhi ya taarifa hizi hazijawatia moyo. "Tayari wamevamia," anasema Lutsevych akirejelea mwaka wa 2014 wakati Urusi ilipotwaa rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, na kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi walioteka sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kuna zaidi ya watu 14,000 waliofariki, zaidi ya 33,000 wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Jumuiya ya Ukraine tayari inalipa gharama kubwa kwa uvamizi wa Urusi."

Nato haikuingilia moja kwa moja katika mojawapo ya matukio hayo, lakini jibu la muungano huo lilikuwa kupeleka wanajeshi wa ziada katika nchi za Ulaya Mashariki kwa mara ya kwanza, zikiwemo Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Romania.

Nato pia iliimarisha ulinzi wake wa anga/uwezo wa polisi katika mataifa ya Baltic na Ulaya Mashariki.

Moscow inataka vikosi hivi vya ziada kuondolewa katika nchi hizo.

Lakini kwa sasa, Nato inasema haina nia ya kufanya hivyo.

Nini kitatokea sasa?
Juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea ili kufikia makubaliano ya amani na kupunguza mvutano huo. Mnamo tarehe 9 Februari, katika mahojiano na BBC, Balozi wa Urusi katika Umoja wa Ulaya, Vladimir Chizhoz aliweka wazi mapendekezo ya Urusi ya kupunguza mvutano kuhusu Ukraine.

Alionyesha kuwa Moscow inaweza kujibu vyema ikiwa Ukraine ingekuwa nchi isiyoegemea upande wowote. Hata hivyo, Ukraine na Nato hapo awali walisema hawako tayari kukubaliana na hili. Katika hatua nyingine ya hivi majuzi, gazeti la Uhispania El Pais lilichapisha waraka uliovuja wa Marekani ukieleza msimamo wake wa mazungumzo.

Katika waraka huo, ilisema: "Marekani ilikuwa tayari kujadili... ahadi za kujiepusha na kupeleka mifumo ya makombora ya kurushwa ardhini na vikosi vya kudumu na misheni ya kivita katika eneo la Ukraine."

Wanadiplomasia na viongozi wa Ulaya pia wamekuwa wakichunguza njia za kufufua mpango wa kusitisha mapigano wa 2015 kwa mikoa ya Ukraine inayodhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga. Mkataba unaoitwa Minsk kati ya Kyiv na Moscow haujawahi kutekelezwa kikamilifu.

Mtaalamu wa Ukraine Lutsevych anasema "Kyiv hatakuwa tayari kutekeleza mpango huo isipokuwa kutakuwa na upunguzaji wa kasi na usitishaji mapigano." "Urusi inataka kutumia makubaliano haya kuunda klabu yenye silaha ndani ya Ukraine ambayo ina raia wa Urusi," anaongeza.

"Suluhu la mgogoro huo ni umoja wa Magharibi na Ukraine. Kilicho hatarini ni uhuru wa Ukraine."

NATO inatishia majibu gani?
Mnamo Februari 7, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema katika mkutano na Rais wa Marekani Joe Biden kwamba Ujerumani 'imeungana' na Marekani katika kuweka vikwazo dhidi ya Urusi ikiwa itaivamia Ukraine.

Vikwazo vinavyowezekana vilivyopangwa vya Washington vitamaanisha kulenga benki kuu za Urusi na kupiga marufuku Urusi kutoka kwa mfumo wa malipo wa kimataifa wa SWIFT ambao ni muhimu kwa miamala ya kimataifa. Uingereza ilisema itawawekea vikwazo watu binafsi na biashara karibu na Kremlin.

"Urusi ilistahimili vikwazo vya Magharibi" anasema mtaalamu wa Urusi Ananieva alipoulizwa kuhusu athari zake kwa Urusi. "Imegeukia uingizwaji wa bidhaa kutoka nje. Katika baadhi ya sekta za vikwazo vya uchumi wa Urusi vimeongeza uzalishaji, na kilimo. Wakulima wangependa vikwazo vya Urusi virefushwe," anasema.

Nato haijapendekeza kuwa ingetumia nguvu za kijeshi kukabiliana na uvamizi wa Urusi. Ingawa mazungumzo ya kimataifa yanaendelea kwa sasa hakuna njia wazi ya jinsi pande hizo mbili zitakavyofikia makubaliano.

Nani mwenye uwezo iwapo vita vitatokea?
===

Chanzo cha mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Ukraine na uwezekano wa vita kamili

Tangu mwaka Mpya wa 2022 uanze,vyombo vingi vya kiusalama vya kimataifa vimekuwa vikiripoti juu ya tishio la nchi ya Urusi Kuvamia kijeshi nchi ndogo jirani ya Ukraine,ambayo zamani ilikuwa katika muungano wa umoja wa kisoviet (USSR),Kabla ya kusambaratika vibaya Sana kwa umoja huo mwishoni mwa miaka ya 1990.

NINI CHANZO CHA MGOGORO HASA?
Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha.

Katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.

Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.

MGOGORO KAMILI?
Tangu mwaka 2014,Ukraine ilianza kupokea msaada wa vifaa vya kijeshi kutoka kwa washirika wa NATO. Ikumbukwe kuwa,Ukraine sio mwanachama wa NATO wala Umoja wa Mataifa. Vifaa vingi vya kijeshi vilitoka nchi za Marekani,Uturuki na Uingereza. Jeshi la Ukraine liliimarika zaidi baada ya kununua DRONES za kisasa kutoka Uturuki.

DRONES hizi zinajulikana Sana hasa zilipofanya vizuri kwenye mgogoro wa kijeshi Kati ya Armenia na Azerbaijan. Mwishoni mwa mwaka 2021 mwezi Desemba, Majeshi ya Ukraine yalianza kuyateka upya maeneo ya DONBASS kwa kutumia mashambulizi ya Anga kutoka kwenye DRONES. Majeshi ya Ardhini ya Ukraine yakashinda Nguvu Majeshi ya waasi na kuliteka Jimbo lote la DONBASS. Baada ya ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine katika Jimbo la DONBASS,ndipo Ukraine ikaanza mashambulizi ya Anga kwenye Jimbo la LUHANSK.

Baada ya Ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine,ndipo Majeshi ya Ukraine yakaingia Frontline ili kuwasaidia waasi. Pia,kikundi Cha Majeshi ya kukodiwa kutoka Urusi maarufu Kama WAGNERS kiliamua kuanzisha mashambulizi dhidi ya Majeshi ya Ukraine. Hata hivyo,Majeshi ya Urusi,Waasi na WAGNERS kwa pamoja yalishindwa kudhibiti mashambulizi ya DRONES za Ukraine.

Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK.

JE, ENDAPO URUSI IKIAMUA KUVAMIA NANI ATAIBUKA KIDEDEA?
Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.

JE,URUSI INAWEZAJE KUZUIA KUPOTEZA VIFARU VYAKE VINGI?
Kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi.

Kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.

Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.

PIA SOMA
1. Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi
2. Historia Iliyojificha Kuhusu Ukraine na Urusi
===
UPDATES
1647518717646.png


YALIYOJIRI FEBRUARI 21
Marekani yadai ina orodha ya wanaopaswa kuuawa na Urusi itakapoivamia Ukraine
Taarifa za kuaminika za Marekani zimesema Urusi inaandaa orodha ya watu watakaowaua au kupelekwa Kambini baada ya kuvamia Ukraine kutokana na mzozo unaoendelea.

Barua iliyotumwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) imeonesha miongoni mwa wanaolengwa ni wapinzani wa Kisiasa, watu wa Dini na makabila ya wachache. Moscow imekanusha kuwa na mpango wa kushambulia Ukraine, lakini inatafuta hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na NATO.

YALIYOJIRI FEBRUARI 23
Urusi kukabiliwa na vikwazo kutokana na mzozo na Ukraine
Urusi iko hatarini kukabiliwa na vikwazo kutoka Nchi za Magharibi kufuatia mgogoro unaoendelea kufukuta kati yake na Ukraine

Wakuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen na Charles Michel wamesema Umoja huo unatafakari kuwekea vikwazo Benki za Urusi zilizo na Matawi katika Majimbo yanayodhibitiwa na waasi wa Ukraine ya Luhansk na Donetsk. Hata hivyo, vikwazo hivyo vitahitaji ridhaa ya Nchi Wanachama zote 27

Bunge la Urusi limepitisha agizo la Rais Vladimir Putin kutambua Uhuru wa maeneo ya waasi Mashariki mwa #Ukraine, siku moja baada ya Rais Putin kulisaini na kuamuru Wanajeshi kuingia maeneo hayo

YALIYOJIRI FEBRUARY 24
Ukraine yatangaza hali ya hatari
Bunge la Ukraine limepitisha azimio la nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari kwa siku 30 kutokana na mzozo uliopo kati ya Nchi hiyo na Urusi.

Mamlaka nchini humo zimeruhusiwa kuzuia raia kutoka, kuzurura na kuzuia Mikutano ya Vyama vya Siasa na Taasisi kwa maslahi ya Taifa. Pia, Serikali imewalazimisha kujiunga na jeshi wanaume wote waliofikia umri wa kwenda vitani.

UN yaitaka urusi kuondoa wanajeshi Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amemtaka Rais wa Urusi, Vladimir Putin kurudisha Wanajeshi aliowapeleka Ukraine, akisema watu wengi wameshapoteza maisha na ni wakati wa kuipa nafasi Amani

Aidha, Rais Joe Biden amesema Urusi itabeba lawama kwa madhara yatakayotokea katika mzozo unaoendelea, akisisitiza Marekani pamoja na Washirika wake watajua cha kufanya

Papa Francis atangaza machi 2 kuwa siku ya kufunga na kuiombea Ukraine
Kufuatia kile kinachoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema hatari ya vita ilmesababisha maumivu makali moyoni mwake

Ametoa wito kwa watu wote kutumia siku ya Machi 2, 2022 ambayo ni Jumatano ya Majivu, kufunga na kuiombea Ukraine

Ripoti zinaonesha tayari Russia imeanza kuishambulia Ukraine. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema watashinda vita hivyo.

Putin: Atakayeingilia mzozo wa ukraine atapata pigo la kihistoria
Baada ya kutangaza mashambulizi dhidi ya Ukraine, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa onyo kwa Mataifa ya Magharibi kuingilia kinachoendelea baina ya Nchi hizo

Mara baada ya milipuko kuripotiwa katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv Putin alinukuliwa akisema, "Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia"

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha Kikao cha Dharura mara baada ya Urusi kuanza mashambulizi

Watu 10 na wanajeshi 40 wafariki katika shambulio lililofanywa na Urusi
akriban Raia 10 na Wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Anga yaliyofanywa na Urusi leo Februari 24, 2022 katika Mji wa Odessa

Taarifa ya Vifo hivyo imetolewa na Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alipozungumza na Waandishi.

Ukraine: Rais kumpatia silaha kila raia anayetaka kuipiga Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewahamasisha Raia kuwa tayari kupigania Nchi yao, na kusema silaha zitatolewa mtu yeyote anayetaka kushiriki katika vita dhidi ya Urusi.

Kufuatia uamuzi wa Urusi kuvamia Ardhi yake, Ukraine imekatiza rasmi uhusiano wake wa Kidiplomasia na Taifa hilo. Picha kadhaa za Mitandaoni hivi karibuni zilionesha Raia wa Ukraine wakipewa Mafunzo ya Msingi ya Kijeshi taharuki ya mzozo huo ilipopanda.

Schalke o4 kuondoa nembo ya kampuni ya Urusi kwenye jezi
Klabu ya Schalke O4 imethibitisha kuwa itaondoa mara moja kwenye jezi zake nembo ya Kampuni ya Gazprom inayomilikiwa na Serikali ya Urusi

Kampuni hiyo inayofanya biashara ya mafuta na gesi ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo. Sehemu ilipokuwa inakaa nembo hiyo yatawekwa maneno yatakayosomeka ‘Schalke 04’. Hatua hii inakuja baada ya Urusi kuivamia na kuishambulia Ukraine kivita

UK: Mbunge ataka Abramovich azuiwe kumiliki Chelsea
Chris Bryant amehoji iwapo Roman Abramovich ataendelea kuwa mmiliki wa Klabu ya Chelsea huku akitaka kuzuiwa kwa mali zake kama sehemu ya vikwazo dhidi ya Urusi

Ameeleza kuwa Abramovich amewahi kukubali Mahakamani kuwa alihusika kulipa fedha kwa ajili ya ushawishi wa Kisiasa na kuwa ana uhusiano na Serikali ya Urusi

Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa Abramovich amezuiliwa kuishi Uingereza na maafisa wa uhamiaji wamepewa maelekezo ya kuhakikisha Abramovich hakai Uingereza

Hatua hii inakuja baada ya Urusi kuivamia na kuishambulia Ukraine kivita huku nchi kadhaa ikiwemo England zikiangalia namna ya kuiwekea vikwazo Urusi

YANAYOJIRI FEBRUARI 25

Mashirika ya ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua Urusi
Mashirika ya Ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua katika Viwanja vya Ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye Anga lake

Uamuzi huo unafuatia uamuzi wa Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, Aeroflot kutua Nchini Uingereza. Marufuku ya Uingereza ni sehemu ya vikwazo vilivyowekwa ili kukabiliana na Uvamizi wa Nchini Ukraine.

UEFA: Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya haitafanyika Urusi
Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) limehamisha fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka Urusi kwenda Paris, Ufaransa baada ya Urusi kuishambulia Ukraine.

Fainali hiyo itakayofanyika Mei 28, 2022 itafanyika katika Uwanja wa Stade de France wa Ufaransa badala ya ule ulioko Urusi wa Gazprom Arena jijini Saint Petersburg.

Mara ya mwisho Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuchezwa katika Dimba la Stade de France ilikuwa miaka 16 iliyopita wakati Barcelona ilipoifunga Arsenal.

Serikali: Watanzania walio Ukraine wawe watulivu
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imewataka Watanzania walioko Ukraine ikiwemo Wanafunzi, Wafanyakazi na Wafanyabiashara kuwa watulivu kipindi hiki cha mzozo wake na Urusi na kushauriwa kufuata maelekezo yanayotolewa

Wanafunzi wametakiwa kufuata maelekezo ya uongozi wa Vyuo, na kuendelea kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania Nchini Sweden kwa kuwa ndio unawakilisha Ukraine. Serikali inaendelea kufuatilia hali za Watanzania walio huko, ikielezwa hadi sasa hakuna aliyepata madhara yoyote.

Ukraine yaomba msaada wa majeshi yenye nguvu
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ameomba Washirika wa Nchi za Magharibi waisaidie Nchi hiyo kukomesha mashambulizi ya Urusi

Amelalamika Mataifa yenye nguvu kuiacha Ukraine ijipambanie huku wakitizama kwa mbali. Amesema hata vikwazo vilivyowekwa havijamshawishi Rais Vladimir Putin kuacha kufanya mashambulizi

YALIYOJIRI FEBRUARI 26
1. UKraine yataka mazungumzo na Urusi
Rais Volodymyr Zelensky ametoa wito wa mazungumzo kati yake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ili kunusuru Raia wasio na hatia.

Viongozi wa China wamesema Urusi ipo tayari kwa mazungumzo. Walitoa kauli hiyo baada ya Rais Putin kuzungumza kwa njia ya simu na Rais Xi Jinping. Rais Putin ameonesha utayari wa kutuma wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo.

2. Ukraine: Mbunge asema wanawake watapigana kama wanaume
Kira Rudik amechapisha picha akiwa ameshika bunduki na kuandika anajifunza kuitumia ili kutetea ardhi yake dhidi ya Urusi. Mbunge huyo amesema Wanawake watatetea ardhi ya Nchi yao kama Wanaume.

3. Rais wa Ukraine avaa gwanda na kuingia uwanja wa vita
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amevaa Gwanda za Jeshi na kuingia "Uwanja wa Vita" kutetea nchi yake. Majeshi ya Urusi yameripotiwa kuzidi kuingia katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv. Awali, kulikuwa na tetesi kuwa Rais huyo amekimbia nchi, ambapo alijitokeza na kuomba Wananchi wapuuzie taarifa hizo.

4. Poland waungana na Sweden kukataa kucheza na urusi mechi ya kufuzu kombe la dunia
Poland imesema itakataa kucheza mchezo wao wa Machi 25, 2022 dhidi ya Urusi baada ya Nchi hiyo kuivamia Ukraine

Chama cha Soka cha Poland pia kimetoa msaada wa kuwa mwenyeji wa michezo yote ambayo Ukraine ilitakiwa kuwa mwenyeji ila itashindwa kutokana na vita.

Ukraine itakutana na Scotland katika mchezo wake wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia, kabla ya kukutana na mshindi kati ya Wales au Austria.

5. Ukraine: Mashambulizi yapelekea maelfu kukimbilia nchi jirani
Zaidi ya Raia 150,000 wa Ukraine wamevuka Mipaka kuingia Mataifa jirani katika upande wa Magharibi kutafuta usalama, wakati Urusi ikishambulia Mji Mkuu wa Nchi hiyo pamoja na Miji mingine kwa mashambulizi ya angani.

Idadi kubwa ya waliowasili katika mataifa jirani ni Wanawake, Watoto na Wazee baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kuwapiga marufuku Wanaume wenye umri wa kujiunga na Jeshi kuondoka.

Yaliyojiri February, 27
1. Ukraine: Wafungwa wenye uzoefu wa kijeshi kuachwa huru
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Ukraine ametangaza kuwaachia wafungwa wote wenye uzoefu wa kijeshi ili wasaidie kuipigania Nchi yao.

Baadhi ya wafungwa wameshaanza kuachiwa ili kuweza kupambana na majeshi ya Urusi ambayo yameendeleza mashambulizi dhidi ya Taifa hilo. Wanawake wamesema hawataweza kwenda vitani lakini watapambana kwa kuchangia damu ili kuwanusuru majeruhi wa vita.

2. Ukraine yakubali kukutana na Urusi kwa mazungumzo
Ukraine imeonesha utayari wa kufanya mazungumzo na Urusi mpakani mwa nchi hizo mbili ili kupunguza athari kwa raia wasio na hatia

Hatua imekuja baada ya Urusi kuonesha kuwa angeweza kutumia Bomu la Nyuklia kuipiga Ukraine. Aidha, ripoti zimesema Japan inaweza kuweka vikwazo vya kifedha kwa Urusi kama itaendelea na mashambulizi yake.

3. Umoja wa Ulaya (EU) wapiga marufuku ndege za Urusi
Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza marufuku dhidi ya Ndege za Urusi, ikisema inafunga Anga lake kwa Ndege zinazomilikiwa na zilizosajiliwa na Urusi. Inamaanisha Ndege hazitoweza kutua, kuruka au kupita juu ya anga la Nchi yoyote ya EU

Umoja huo pia umesema utapiga marufuku Vyombo vya Habari vya Sputnik na Russia Today vinavyomilikiwa na Serikali ya Urusi. Pia, umeweka vikwazo dhidi ya Rais Vladimir Putin na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Lavrov.

Yaliyojiri February 28, 2022
1. (UNHCR) limesema idadi ya wanaokimbia Vita Nchini Ukraine imefikia Watu 368,000
UKRAINE: Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema idadi ya wanaokimbia Vita Nchini #Ukraine imefikia Watu 368,000

Kamishna Mkuu wa Shirika hilo amesema idadi imekuwa ikibadilika kila wakati ambapo makadirio ya Jumamosi pekee zaidi ya Watu 150,000 wamekimbilia Poland, na Mataifa mengine ikiwemo Hungary na Romania

Poland imesema zaidi ya Wakimbizi 156,000 wameingia katika mipaka ya Taifa hilo.

2. Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru Urusi kucheza Mechi bila Bendera na Wimbo wa Taifa
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru Urusi kucheza Mechi bila Bendera na Wimbo wa Taifa katika viwanja visivyoegemea upande wowote, ikionya huenda Nchi hiyo ikaondolewa kwenye mashindano ikiwa hali ya Ukraine haitaimarika.

FIFA imesema Timu ya Taifa haitashiriki kama Urusi, bali kama Shirikisho la Soka la Urusi (RFU) na Michezo yote ya nyumbani itafanyika bila mashabiki kwenye eneo lisiloegemea upande wowote.

Aidha, Shirikisho hilo limelaani mabavu yaliyotumika kuivamia Ukraine na kusema hakuna Mechi ya Kimataifa itachezwa Nchini Urusi.

3. Ukraine yasaini maombi ya kujiunga Umoja wa Ulaya
Rais Volodymyr Zelenskyy amesema amesaini maombi rasmi ya kujiunga na Umoja wa Ulaya (EU). Pia, ameomba Umoja huo uiruhusu Ukraine ipate Uanachama mapema iwezekanavyo, chini ya Utaratibu Maalum wakati ikijilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi

Wakati huo huo, Jeshi la Ukraine limesema watu kadhaa wameuawa na mamia kujeruhiwa katika Mji wa Kharkiv baada ya Vikosi vya Urusi kufanya mashambulizi kwenye maeneo ya makazi ya Raia.

YANAYOJIRI MACHI 1
1. Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine licha ya mazungumzo
Mashambulizi ya Urusi Nchini Ukraine yameendelea kwa siku ya tano licha ya mazungumzo yanayolenga kusitisha mapigano

Inaripotiwa kuwa, mashambulizi ya makombora yameua watu kadhaa katika Mji wa Kharkiv, huku ving'ora vya mashambulizi ya anga vikisikika tena katika Mji Mkuu, Kyiv

Rais Volodymyr Zelensky amesema shambulio la Urusi huko Kharkiv ni uhalifu wa kivita.

2. Rais wa Ukrain ameiomba Marekani kufanya mchakato wa kukomesha urukaji wa ndege ktk anga la Ukraine (No-fly zone)
Rais wa Ukrain ameiomba Marekani kufanya mchakato wa kukomesha urukaji wa ndege ktk anga la Ukraine (No-fly zone) ili kuyastopisha mashambulizi ya anga yanayoendelea kutekelezwa na majeshi ya Russia.

Ombi hilo limekataliwa na Ikulu ya Marekani ikisema kuwa haifikirii kufanya kitu kama hicho kwani kufanya hivyo kutaiingiza Marekani ktk vita na Russia, jambo ambalo Marekani wanajitahidi kwa namna zote kuepuka.

3. Mamlaka nchini Ukraine zinasema shambulio la Urusi limeua Wanajeshi wapatao 70
Mamlaka Nchini #Ukraine zinasema shambulio la Urusi limeua Wanajeshi wapatao 70 kwenye Kitengo cha Kijeshi huko Okhtyrka, Mji ulioko kati ya Kharkiv na Kyiv

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya watu waliokimbia Nchini Ukraine kutokana na machafuko yanayoendelea imeongezeka kufikia 520,000.

Aidha, Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ambaye ni Mtu wa karibu wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema Vikosi vya Nchi hiyo haitaungana na vile vya Urusi dhidi ya Ukraine.

4. Adidas yavunja ushirikiano wake na chama cha soka cha Urusi
Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, Adidas imesimamisha ushirikiano wake na Chama cha Soka cha Urusi baada ya nchi hiyo kuvamia Ukraine.

Hatua hiyo inafanya Adidas ambayo ni Kampuni ya pili kwa ukubwa kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo kusitisha udhamini wa jezi za Urusi ulioanza tangu mwaka 2008.Adidas inaungana na Disney, Maersk, Shell na Twitter katika kuacha kutoa huduma nchini Urusi au kutoa msaada kwa Watu wa Ukraine.

5. Visa na Mastercard zafungia taasisi za fedha za Urusi
Kampuni za malipo ya kifedha za Marekani, Visa na Mastercard zimezifungia Taasisi kadhaa za Kifedha za Urusi kutumia huduma zake ikiwa ni sehemu ya vikwazo kwa Urusi.

Aidha, Kampuni hizo zimeahidi kutoa Dola za Kimarekani Milioni 2 kila moja kwa ajili ya kusaidia katika masuala mbalimbali ya Kijamii huko Ukraine.

Jumamosi,Februari 26, Marekani, Canada na Ulaya zilitangaza vikwazo vipya kwa Urusi ikiwemo kuzuia baadhi ya Wakopeshaji kutumia Mfumo wa Kimataifa wa malipo wa SWIFT.

Inaelezwa kuwa Februari 27 na Februari 28, Warusi walijipanga katika misururu mirefu na kusubiri muda mrefu katika ATM kutoa fedha wakiogopa huenda kadi zitaacha kufanya kazi au Benki zitadhibiti kiasi cha kutoa fedha.

Yanayojiri Machi, 2
1. Mahakama ya ICC kuchunguza uhalifu wa kivita nchini Ukraine
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Karim Khan amesema Mahakama hiyo itaanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita unaofanywa na Urusi Nchini Ukraine

Khan amesema baada ya kupitia uchunguzi wa awali wa hali hiyo, ameridhika kuna sababu za kimsingi za kuamini madai yote ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya Binadamu umefanyika Nchini Ukraine.

2. Kampuni ya Apple kutouza bidhaa zake Urusi
Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine.

Wafanyabiashara wengine wakubwa wa teknolojia kama Google na Twitter pia wamepunguza biashara zao nchini Urusi ‘tunaungana na wote wanaotaka amani duniani’ imeeleza taarifa ya Apple.

Pamoja na kusitisha uuzaji wa bidhaa, Apple inasema duka lake la programu za simu linazuia upakuaji wa RT News na Sputnik News kutoka nje ya Urusi zikiituhumu mitandao hiyo kuwa inarusha habari za propaganda kutokea Ofisi za Serikali ya Urusi.

Apple pia imesitisha kutuma location za moja kwa moja kwenye ramani za Apple nchini Ukraine kama hatua ya usalama, sawa na hatua ambayo tayari Google imechukua.

YALIYOJIRI MACHI 3

1. UKRAINE - UPDATES: Jeshi la Urusi linadaiwa kushambulia Shule Tatu katika Mji wa Kharkiv.

Jeshi la Urusi linadaiwa kushambulia Shule Tatu katika Mji wa Kharkiv. Pia inaripotiwa kuwa Majengo kadhaa ya Makazi ya Watu huko Okhtyrka nayo yameharibiwa kutokana na mashambulizi yanayoendelea

Umoja wa Mataifa (UN) umesema tayari Watu zaidi ya Milioni Moja wamekimbia Ukraine, ikiwa ni siku saba tangu uvamizi wa Urusi kuanza.

Kumekuwa na takwimu kinzani kuhusu idadi ya Raia waliopoteza maisha, lakini Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) imesema Raia 227 wameuawa na 525 kujeruhiwa. Hata hivyo, Ofisi hiyo imesema inaamini idadi halisi ni kubwa zaidi.


2. Urusi: Waziri wa Ulinzi asema Wapiganaji 498 wa Urusi wameuawa
Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Meja Jenerali Igor Konashenkov amesema wanajeshi wa #Urusi 498 wameuawa na 1,597 wamejeruhiwa. Idadi inatofautiana na iliyotajwa na mshauri wa Rais Vladimir Putin aliyesema wanajeshi 7,000 wameuawa.

Waziri wa Urusi amesema familia za wanajeshi waliopoteza Maisha zimeendelea kupata usaidizi wa serikali

Waziri amesema wamewaua wanajeshi 2,870 wa #Ukraine na wengine 3,700 wamejeruhiwa. Ukraine iliripoti kuwa raia 2,000 waliuawa kutokana na mzozo huo.

3. Wanachama wa UN Wapigakura kuhusu mzozo wa Urusi na Ukraine
Hatua hii ni shinikizo baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kuomba msaada wa Kimataifa zaidi ya mara moja kwa lengo la kudhibiti vita hiyo ambayo Nchi yake imeonekana kuathirika zaidi

Nchi 141 za UN zilipiga kura ya kuilaani vikali Russia (Urusi) na kuridhia kuwekewa vikwazo mbalimbali vya Kimaendeleo na Uchumi wake Duniani kote. Nchi zilizokubaliana na Urusi ni Belarus, Korea ya Kaskazini, Eritrea na Syria

Nchi 35 hazijafungamana na upande wowote ikiwemo Tanzania, China na Uganda. Nchi 11 hazikushiriki kupiga kura kabisa.

YALIYOJIRI MACHI 4
1. UFARANSA: Serikali imewaambia Raia wake waondoke Nchini Urusi
Ufaransa: Serikali imewaambia Raia wake waondoke Nchini Urusi kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Taifa hilo yanayoendelea Nchini Ukraine.

Serikali za mataifa mengine zikiwemo Uingereza na Marekani zimeshatoa tangazo la kuwaondoa Raia wake nchini humo kutokana na vikwazo ambavyo vimekuwa vikiendelea kuwekwa kwa Urusi kutoka mataifa mbalimbali.

2. Urusi: Meja Jenerali amshauri Putin wapige mapigo mabaya ili Ukraine ijisalimishe
Meja Jenerali wa Chechnya, Ramzan Kadyrov amemuomba Rais Vladimir Putin aruhusu mapigo mabaya ya kustukiza ili Ukraine isalimu amri ndani ya muda mfupi (saa 48)

Ramzan ambaye vikosi vyake viko vitani ameshauri kuachana na mapatano ambayo hayatakuwa na maana zaidi ya kusaini karatasi

Amesema haweza kuvumilia kuona wanajeshi wake wanauawa. Na kadiri wanavyozidi kuchelewa ndivyo watakavyokumbana na vikwazo zaidi

YALIYOJIRI MACHI 5
1. Ukraine: Kituo cha mitambo ya nyuklia chashambuliwa na Urusi
Kituo cha Mtambo mkubwa wa Nishati ya Nyuklia Barani Ulaya kilichoko Ukraine kimelengwa katika mashambulizi ya Urusi usiku wa kuamkia leo Ijumaa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba ametaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo ili kuepusha Maafa.

Msemaji wa Mtambo huo wa Zaporizhia, Andrei Tuz amesema shambulio la makombora lililofanywa na Vikosi vya Urusi, limesababisha Moto kuwaka katika mojawapo ya sehemu ya kituo hicho.

2. UPDATES: Ukraine na Urusi zimekubaliana kutengeneza na kuweka maeneo salama ya kibinadamu ili kuruhusu Raia kuondolewa
Ukraine na Urusi zimekubaliana kutengeneza na kuweka maeneo salama ya kibinadamu ili kuruhusu Raia kuondolewa. Hayo yameelezwa baada ya mazungumzo ya pili baina ya Mataifa hayo kufanyika.

Upande wa Ukraine umesema bado haujapata matokeo unayohitaji lakini makubaliano kuhusu maeneo salama yamefikiwa. Mwakilishi wa Russia naye amethibitisha makubaliano hayo, pamoja na uwezekano wa kusitisha mapigano.

YALIYOJIRI MACHI 6
1. UKRAINE: Wanajeshi wa Urusi wameukamata Mji Muhimu wa Bandari wa Ukraine
UKRAINE: Wanajeshi wa Urusi wameukamata Mji Muhimu wa Bandari wa Ukraine na kuuzingira mwingine kama sehemu ya juhudi za kuitenganisha nchi hiyo na Pwani yake

Jeshi la Urusi limesema limechukua udhibiti wa Kherson na Maafisa wa Ukraine katika eneo hilo wamethibitisha kuwa Wanajeshi wamechukua udhibiti wa Makao Makuu ya Serikali ya Mitaa katika Mji huo wa Bandari ya Bahari Nyeusi wenye wakazi 280,000

Kherson sasa ndiyo Mji wa kwanza mkubwa kuanguka tangu kuanza uvamizi wa Urusi wiki moja iliyopita. Wakati huohuo, umeme na mawasiliano ya simu vimekatwa, na makazi na maduka yanakabiliwa na uhaba wa chakula na maji.


2. Urusi: Vyombo vya Habari vinavyosambaza taarifa za uongo kufungiwa
URUSI: Bunge limepitisha Sheria inayoruhusu Mamlaka kuwafunga hadi miaka 15 watu walioshtakiwa kwa kusambaza makusudi taarifa zisizo na ukweli kuhusu Jeshi la Nchi hiyo. Sheria hiyo pia inafanya wito wa vikwazo dhidi ya Urusi kuwa Kosa la Jinai

Aidha, Umoja wa Mataifa (UN) umesema uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unaweza kusababisha wimbi la Wakimbizi wapatao Milioni 10 wanaokimbia Nchi.

YALIYOJIRI MACHI 7
1. Ukraine: Rais Zelensky ahimiza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa Mataifa ya Magharibi kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi, akikosoa Viongozi kwa kutojibu tangazo la awali la Wizara ya Ulinzi ya Urusi kuhusu kushambulia majengo ya Kijeshi na Viwanda ya Ukraine

Pia, ametoa wito wa kuwafikisha mahakamani wanaoamuru na kutekeleza uhalifu huo akisema hawajali na wanatangaza wazi ukatili uliopangwa kufanyika

Ameeleza kuwa, ujasiri huo ni ishara tosha kwa Nchi za Magharibi kwamba vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Russia havitoshi.

2. Urusi yatoa masharti ya kusitisha vita Ukraine
Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha operesheni "wakati wowote" ikiwa Ukraine itatimiza masharti ya Urusi. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Ukraine lazima itambue Crimea kama Urusi, na Donetsk na Luhansk kama mataifa huru.

Mbali na hayo, Peskov anasema Ukraine lazima irekebishe katiba yake na kukataa madai ya kuingia katika kambi yoyote (kama vile Nato, kwa mfano).

Anaongeza kuwa Urusi itamaliza "kuondoa jeshi" kwa Ukraine, na ikiwa masharti haya yatatimizwa hatua za kijeshi za Urusi "zitakoma mara moja".

Msemaji wa Kremlin amesisitiza kuwa Urusi haitaki kutoa madai yoyote zaidi ya eneo nchini Ukraine.

3. Urusi: Waandamanaji wanaopinga vita kukamatwa
URUSI: Baadhi ya raia wameingia mitaani kupinga hatua ya Nchi yao kuishambulia Ukraine wakitoa maneno ya ‘No to War’. Polisi wameripotiwa kuwapiga na kuwakamata waandamanaji hao katika Miji mbalimbali.

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema takriban Watu 3,500 wamekamatwa katika Miji 56 kwa kufanya maandamano hayo yasiyo halali.

4. Rais WA Marekani Joe Biden amepiga marufuku ununuzi WA mafuta ya Urusi
Rais WA Marekani Joe Biden amepiga marufuku ununuzi WA mafuta ya Urusi kuanzia Leo. Today, I’m announcing that the United States is targeting a main artery of Russia’s economy.

We are banning all imports of Russian oil and gas.

YALIYOJIRI MACHI 8

1. Ukraine waomba Urusi izidishiwe vikwazo
Serikali ya Ukraine imependekeza vikwazo vya kibiashara vya kimataifa dhidi ya Urusi ikiwemo kuzuia mafuta ya Taifa hilo, na kusimamishwa mauzo ya Nje kwenda Urusi ikisema 'Vita viwalishe'.

Vikwazo vya Magharibi vilivyowekwa kutokana na shambulio la kijeshi la Urusi tayari vimeitenga Urusi kwa kiwango kikubwa, lakini Ukraine inataka bidhaa zisusiwe ikiwa wanashindwa kuheshimu Taratibu za Kibinadamu.

Aidha, Kaimu Waziri Mkuu wa Ukraine, Iryna Vereshchuk amesema takriban Raia 300,000 wanasubiri kuondolewa katika Mji wa Mariupol ambao unashambuliwa na Vikosi vya Moscow.

2. Ukraine yataka Zelensky na Putin kufanya mkutano
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema Taifa hilo linataka mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Rais Volodymyr Zelensky na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwasababu wanatambua maagizo yote yanatoka kwake

Kuleba amesema Rais Zelensky haogopi Mkutano na Rais Putin, akisisitiza yupo tayari kukaa kikao na Kiongozi huyo ili wazungumze

Aidha, Balozi wa Ukraine Umoja wa Mataifa (UN) Sergiy Kyslytsya amesema Urusi imezuia jitihada kadhaa za kuwaondoa Raia maeneo ya Kyiv, Kharkiv, Donetsk na Kherson licha ya kuwepo Makubaliano.

3. Urusi yasitisha mapigano kupisha raia waondoke
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa (UN), Vassily Nebenzia, amesema Nchi yake itasitisha mapigano ili kuruhusu raia waliopo Kiev, Cher-nigov, Sumy na Mariupol kuondoka bila masharti kwa raia wanaopitia Urusi.

Hata hivyo, Rais Volodymyr Zelensky amelikataa pendekezo la kuwapitishia raia wake kwenye "Ardhi ya Mvamizi." Asema baada ya kutangaza makubaliano ya kuwepo kwa njia salama, Urusi inaongeza vifaru, makombora na mabomu.

YALIYOJIRI MACHI 9
1. Urusi yadaiwa kushambulia hospitali za Ukraine
Waziri wa Afya wa Ukraine, Viktor Liashko amesema Vikosi vya Urusi vimeshambulia na kuleta uharibifu kwa Hospitali takriban 61. Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) inasema Raia wapatao 474 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi kuanza.

Mbali na Vifo, inaelezwa kuwa Raia wengine 861 wamejeruhiwa na inahofiwa idadi halisi ya waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni kubwa zaidi. Kwa mujibu wa UN, vifo vingi vilivyorekodiwa vimesababishwa na milipuko.

Aidha, Rais Volodymyr Zelenskyy amepongeza Uongozi wa Rais Joe Biden kufuatia uamuzi wa Marekani kupiga marufuku mafuta ya Russi.

2. Umoja wa Mataifa (UN) inasema Raia wapatao 474 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi
Waziri wa Afya wa Ukraine, Viktor Liashko amesema Vikosi vya Urusi vimeshambulia na kuleta uharibifu kwa Hospitali takriban 61. Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) inasema Raia wapatao 474 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi kuanza

Mbali na Vifo, inaelezwa kuwa Raia wengine 861 wamejeruhiwa na inahofiwa idadi halisi ya waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni kubwa zaidi. Kwa mujibu wa UN, vifo vingi vilivyorekodiwa vimesababishwa na milipuko

Aidha, Rais Volodymyr Zelenskyy amepongeza Uongozi wa Rais Joe Biden kufuatia uamuzi wa Marekani kupiga marufuku mafuta ya Russia.

3. Kampuni kubwa zaendelea kusitisha biashara Urusi
Coca-Cola, Starbucks, Pepsi na McDonald's zimeungana na Kampuni nyingine kusitisha Biashara Nchini Urusi kutokana na uvamizi uliofanywa Ukraine. Kumekuwepo na shinikizo kutaka Kampuni za Biashara kuchukua hatua kama ishara ya kupinga mateso wanayopata Wananchi

Kwa upande wao, Pepsi imesema itasitisha kuuza kinywaji na kufanya uwekezaji mwingine lakini Kampuni hiyo itaendelea kuuza bidhaa muhimu zikiwemo Maziwa na Chakula cha Watoto.


YALIYOJIRI MACHI 10

1. Ukraine wajawazito yalipuliwa
UKRAINE: Hospitali ya Wajawazito ya Mariupol imeshambuliwa na Wanajeshi wa #Urusi katika shambulio la anga na kusababisha majeruhi 17

Inaelezwa kuwa, waliojeruhuwa ni Wafanyakazi na Wajawazito huku Watoto wakiwa salama.

2. Abramovich awekewa vikwazo na Uingereza
Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amewekewa vikwazo na Serikali ya Uingereza ikiwemo kuzuia Mali zake na marufuku ya kusafiri.

Abramovich na Mabilionea wengine saba wamepata vikwazo hivyo baada ya kuonekana kuwa washirika wa Rais Vladimir Putin wa Russia.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesema Uingereza haiwezi kuwa kimbilio salama kwa wanaounga mkono uvamizi wa Urusi kwa Ukraine.

YALIYOJIRI MACHI 11
Wanajeshi 250 wa Ukraine waliokuwa DR-Congo watakiwa kuondoka
Wanajeshi 250 wa Ukraine waliokuwa wakilinda amani DR-Congo wanatarajia kurejea Ukraine na vifaa na Helkopta zao.

Tangazo la kuondoka kwao limetolewa na Umoja wa Mataifa(UN). Baadhi ya wachambuzi wamesema hatua hiyo ni kutokana na yanayoendelea Nchini kwao.

Wakiongea na BBC Swahili baadhi ya raia wa Congo wamefurahishwa na hatua hiyo wakilaumu uwepo wa vikosi hivyo kunachochea vita katika Nchi yao.


YALIYOJIRI MACHI 12

Jitihada za kusitisha mapambano Mariupol zakwama
Kaimu Waziri Mkuu wa Ukraine, Iryna Vereshchuk amesema Wananchi wa Mji wa Mariupol wameshindwa kuondoka baada ya Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda kushindwa kutekelezwa.

Kutokana na hali inayoendelea, imeelezwa kuwa jitihada za kupelekea Chakula, Maji na Dawa kwenye Mji huo zimeshindikana.

Aidha, Waziri wa Elimu wa Ukraine amesema tangu mashambulizi ya Urusi dhidi ya Taifa hilo kuanza, zaidi ya maeneo 280 ya kutoa Elimu ikiwemo Shule, Vyuo vya Ufundi na Vyuo Vikuu yameharibiwa.


Facebook yaruhusu maneno ya chuki dhidi ya Urusi
Kampuni ya Meta ambayo ni mmiliki wa Mtandao wa Kijamii wa Facebook na Instagram imelegeza sera yake dhidi ya machapisho ya chuki ili kuruhusu maneno ya chuki dhidi ya Urusi

Katika tamko lao wamesema wataruhusu sentensi za chuki kama ‘Death to Russian Invaders’ lakini hawataruhusu maneno yanayoashiria chuki dhidi ya raia. Hata hivyo, Urusi imezuia Mtandao wa Facebook na Twitter Nchini humo.

YALIYOJIRI MACHI 14
1. UKRAINE: Urusi imeishambulia Kambi ya kijeshi ya Ukraine
UKRAINE: Urusi imeishambulia Kambi ya kijeshi ya Ukraine, Yavoriv iliyopo karibu na Mpaka wa Poland na kusababisha vifo 35.

Kambi hiyo ilikuwa inatumika na Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuwapa mafunzo Wanajeshi wa Ukraine. Katika shambulio hilo, watu 134 wamejeruhiwa na makombora 30 kuharibiwa.

2. Ukraine: Mwandishi wa habari wa Marekani auawa kwa risasi
Brent Renaud (50), Mwandishi wa Habari wa Marekani aliyekuwa akifanyakazi nchini Ukraine ameuawa kwa kupigwa risasi na Wanajeshi wa Urusi Mjini Irpin.

Mkuu wa Polisi wa Kyiv, Andriy Nebytov amesema Waandishi wa Habari wengine wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Mmoja wa Waandishi waliojeruhiwa ni Juan Arredondo wa Italia

Hii ni mara ya kwanza Mwandishi wa Habari kushambuliwa na kufariki katika mzozo unaoendelea kati ya Ukraine na Urusi.

YALIYOJIRI MACHI 15

UN: Vita ya Urusi na Ukraine inaweza kusababisha uhaba wa chakula duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres amesema Afrika na Dunia kwa ujumla inaweza kukumbwa na njaa kutokana na vita kati ya Urusi na Ukraine.

Amesema nchi nyingi Barani Afrika zinategemea ngano kutoka Russia na Ukraine, lakini kutokana na vita kutakuwa na uhaba wa mazao hayo. Tayari Burkina Faso, Somalia na Yemen zinahangaika kulisha Raia wake.

YALIYOJIRI MACHI 16
1. Urusi yamuwekea vikwazo rais wa Marekani na maafisa wa serikali yake pamoja na Canada
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema Rais wa Marekani, Joe Biden na Maafisa wengine 12 wamepigwa marufuku kuingia Nchini humo ili kulipiza kisasi juu ya vikwazo vya Marekani. Vikwazo hivyo pia vitamuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi, Lloyd Austin

Katika kukabiliana na Uvamizi wa Urusi Nchini Ukraine, Marekani iliwapiga marufuku Rais Vladimir Putin na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov pamoja na kupitisha vikwazo ambavyo kwa kiasi kikubwa vimeifanya Urusi kutojihusisha na masuala ya Kifedha na Mataifa mengine Duniani.

YALIYOJIRI MACHI 17
Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwA
Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwa na kuwa hatoiruhusu nchi hiyo kutumika kama uwanja wa kuitishia Urusi.

Akizungumza katika mkutano wa serikali uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Putin amesema operesheni yake inaendelea vizuri kwa kufuata kikamilifu mipango waliyoiweka.

Rais huyo ameongeza kuwa Benki Kuu ya Urusi haina haja ya kuchapisha pesa kwa kuwa nchi hiyo ina rasilimali za kutosha za kifedha za kukabiliana na changamoto za sasa za vikwazo.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili za kivita yanaendelea kwa sasa huku kila mmoja akielezea matumaini ya kupatikana suluhu.


YALIYOJIRI MACHI 18
1. UN: Raia takriban 700 wameuawa Ukraine tangu Urusi avamie
Umoja wa Mataifa umedai kuwa zaidi ya raia 700 wakiwemo watoto 52 wameuawa nchini Ukraine tangu Urusi ilipoivamia jirani yake wiki tatu zilizopita, lakini idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi.

Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo amelieleza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa "vifo vingi kati ya hivyo vimesababishwa na mabomu katika maeneo yenye watu wengi".

Ameongeza kuwa mamia ya makaazi ya watu yameharibiwa ikiwa ni pamoja na hospitali na shule. DiCarlo amesema kuwa "kiwango cha vifo vya raia na uharibifu wa miundombinu ya raia nchini Ukraine hakiwezi kupuuzwa na kwamba kunahitajika uchunguzi kamili na uwajibikaji".

Naye mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameshutumu athari za vita kwa watu wa Ukraine ambao wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma na matibabu.

2. Uswizi yatangaza kuzuia zaidi ya Tsh. Trilioni 350 za warusi
Jumuiya ya Wanabenki wa Uswizi imetangaza kuwa raia wa Urusi wameweka kati ya Dola bilioni 160 - 213 nchini humo. Fedha hizo ni sawa na Tsh. Trilioni 372 – 495.

Mbali na Uswizi kusifiwa kwa utunzaji wa taarifa za wateja Rais wa Nchi hiyo, Ignazio Cassis amesema watazuia fedha hizo za Rais Vladimir Putin, wanasiasa na wafanyabiashara.

Urusi imewekewa vikwazo na Jumuiya ya Ulaya (EU) kutokana na mashambulio ambayo Urusi ameendelea kuyatekeleza dhidi ya Ukraine.


YALIYOJIRI MACHI 19
1. Ukraine yaruhusu matumizi ya cryptocurrency
Rais Volodymyr Zelensky ameruhusu matumizi ya Cryptocurrency baada ya Benki za Ukraine kushindwa kufanya kazi vizuri kutokana na mzozo unaoendelea.

Waziri wa Maendeleo ya Digitali amesema Cryptocurrency zitatumika kihalali, ambapo Benki zitaruhusu akaunti za kampuni za Cryptocurrency.

Mgogoro wa Urusi na Ukraine umezorotesha Benki nyingi Nchini humo, na matumizi ya Cryptocurrency yameonekana kuwa moja ya suluhu.

YALIYOJIRI MACHI 20

1. UKRAINE: Wanajeshi wa Urusi wameripotiwa kuingia katika Mji wa Mariupol
UKRAINE: Wanajeshi wa Urusi wameripotiwa kuingia katika Mji wa Mariupol ulioathirika zaidi na vita vinavyoendelea. Mapigano makali yamepelekea kufungwa kwa Kampuni kuu ya chuma cha Pua.

Afisa mmoja wa Polisi wa Mariupol amesema Watoto na Wazee wanafariki kutokana na mashambulizi ya Urusi katika Mji huo. Kutekwa kwa Mji huo ni hatua kubwa kwa Wanajeshi wa Urusi.

Gazeti la New York Times limemnukuu Mwanajeshi mmoja wa Ukraine akisema shambulizi la roketi limesababisha vifo vya hadi Wanamaji 40 katika Mji wa Kusini wa Mykolaiv.

YALIYOJIRI MACHI 21
1. Rais Zelensky: kushindwa kwa mazungumzo kutamaanisha vita ya tatu ya dunia
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema kushindwa kumaliza mzozo uliopo na Urusi kwa njia ya mazungumzo kutamaanisha ‘Vita ya Tatu ya Dunia’

Amesema yuko tayari kwa mazungumzo lakini hatokubali masharti ya kutambua maeneo yanayojitenga kuwa huru ambayo yanafadhiliwa na Urusi

Aidha, ameonesha umuhimu wa NATO kwa kusema Nchi yake ingekuwa mwanachama vita hivyo visingeanza.

2. UN: Watu wapatao milioni 10 wameikimbia Ukraine
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR, Filippo Grandi amesema watu milioni 10, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi jumla ya raia wa taifa hilo wamelikimbia kutokana kile alichokiita vita vya maangamizi vya Urusi.

Grandi amesema idadi hiyo inajumisha wakimbizi wa ndani au waliovuka mipaka ya taifa hilo tangu Urusi ianze uvamizi wake Februari 24.

Asilimia 90 ya waliokimbia ni wanawake na watoto. Wanaume wa umri wa kati ya miaka 18 hadi 60 wanapsawa kuitika wito kusaidia jeshi na hawaruhusiwi kuondoka Ukraine.

Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhima na watoto, UNICEF nalo limesema watoto milioni 1.5 ni miongoni mwa waliokimbilia uhamishoni, na kuonya hatari ya kukabiliwa na biashara haramu ya usafirishaji watu na utumikishwaji mbaya.

Kabla ya mgogoro huu wa sasa Ukraine ilikuwa na jumla ya watu milioni 37. Idadi hiyo inajumushia maeneo yaliokuwa katika udhibiti wa serikali ukiliondoa eneo lililonyakuliwa na Urusi la Crimea na maeneo ya wanaotaka kujitenga yenye kuunga mkono Urusi.

YALIYOJIRI MACHI 22
1. EU waitaka Afrika iungane na dunia kuipinga Urusi
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuendelea kulaani kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine na kushawishi Mataifa mbalimbali zikiwemo Nchi za Afrika kujitokeza hadharani kuipinga Urusi

Tamko hilo limetolewa na baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Ulaya waliopo Tanzania ambao Nchi zao ni Wanachama wa EU, wakieleza kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionesha Urusi jinsi Dunia ambavyo haikubaliani naye

Walioshiriki kutoa tamko hilo Machi 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ni mabalozi wa Ufaransa, Ujerumani, Poland, Uholanzi, Sweden, Finland, Hispania, Italia na Balozi wa EU.

YALIYOJIRI MACHI 23
Ukraine: Mwanahabari picha adaiwa kutoweka
Maksym Levin ambaye ni Mwanahabari Picha wa Ukraine aliyekuwa anapiga picha Mjini #Kyiv hajulikani alipo.

Rafiki wa mwanahabari huyo, Markiyan Lyseiko amesema inawezekana rafiki yake amejeruhiwa au kutekwa na Wanajeshi wa Urusi walioko nchini Ukraine

Hivi karibuni kumekuwa na madai ya Uhalifu wa Kivita kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

YALIYOJIRI MACHI 24
1. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameomba dunia kuandamana kupinga operasheni ya Urusi nchini Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameomba dunia kuandamana kupinga operasheni ya Urusi nchini Ukraine. Operesheni ya Urusi nchini Ukraine imesababisha mapigano na vifo vya watu wengi tangu kuanza kwake Februari 24.

Rais Zelensky amesema kuisapoti Ukraine ni kusapoti uhuru na Maisha. Ametaka watu waingie mitaani an viwanjani kufanya sauti zao zisikike kuhusu kupinga hatua za Urusi.

Mgogoro wa Urusi na Ukraine umesababisha matatizo mengi duniani ikiwemo kupanda kwa bei za mafuta na chakula kwa nchi zinazoendelea.

YALIYOJIRI MACHI 27
Waandishi wa habari 12 wamekufa nchini Ukraine tangu kuzuka kwa vita
Waandishi wa habari 12 wamekufa nchini Ukraine tangu kuzuka kwa vita nchini humo mwezi mmoja uliopita taarifa hii ikiwa ni kulingana na mwanasheria mkuu Iryna Venediktova.

Ameandika kupitia ukurasa wa Facebook kwamba pamoja nao waandishi wengine 10 wamejeruhiwa wakati wa mapigano hayo.

Kulingana na Venediktova waandishi hao waliuawa na wanajeshi wa Urusi na kuongeza kuwa taarifa hizo zinaweza kuthibitishwa na vyombo huru.

Kulingana na uchunguzi uliofanyika hadi sasa karibu wawakilishi wa vyombo vya habari 56 wameshambuliwa ikiwa ni pamoja na vyombo 15 vya kigeni.

Venediktova amesema waandishi wa kigeni ni wa mashirika ya Uingereza, Jamhuri ya watu wa Czech, Denmark, Uswisi, Umoja wa Falme za Kiarabu na Marekani.

YALIYOJIRI MACHI 28
1. Ukraine: Rais Zelensky ayaita mataifa ya Magharibi vigeugeu na waoga
Rais wa #Ukraine, Volodymyr Zelensky amezishutumu nchi za Magharibi kwa woga, wakati ambapo nchi yake inapambana na #Urusi.

Akilihutubia taifa, Machi 27, 2022 usiku amesema nchi za magharibi ni vigeuge, hotuba aliyoitoa baada ya Rais wa #Marekani, Joe Biden kusema Urusi haihitaji mabadiliko ya Utawala.

Ukraine imeomba kupewa ndege za kivita na vifaru ili aweze kujilinda dhidi ya Urusi. Na wamesisitiza kuwa nchi za Magharibi zinahitaji ujasiri zaidi katika kuisaidia Ukraine

2. Ukraine: Waziri wa Uchumi, Yulia Svyrydenko amesema vita inavyoendelea imegharimu Nchi yao Dola bilioni 564.9
UKRAINE: Waziri wa Uchumi, Yulia Svyrydenko amesema vita inavyoendelea imegharimu Nchi yao Dola bilioni 564.9 (sawa na Tsh. trilioni 1,310)

Waziri amesema, gharama hizo ni pamoja na uharibifu wa miundombinu na kupoteza shughuli za kiuchumi. Barabara zilizoharibika ni kilomita 8,000 na mita za mraba milioni 10 za makazi.

YALIYOJIRI MACHI 29
1. Raia kutoka nchi zisizo rafiki wa Urusi kuzuiwa kuingia nchini humo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema wanaandaa Amri ya Rais itakayowazuia Raia kutoka Marekani na washirika wake kuingia nchini humo.

Orodha itajumuisha Marekani na Canada, Mataifa ya Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ukraine, Uswizi, Norway, Japan, Korea Kusini, Australia, New Zealand na Singapore.

Inaelezwa kuwa, hatua hiyo ni kulipa kisasi dhidi ya vitendo visivyo vya kirafiki vya mataifa kadhaa ya kigeni kwa Nchi ya Urusi.

2. Marekani: Biden akataa kuomba radhi kwa kauli yake dhidi ya utawala wa Urusi
Rais wa Marekani, Joe Biden amesema hataomba radhi kwa kauli yake ya hivi karibuni kuwa Rais Vladimir Putin wa #Urusi hawezi kusalia madarakani

Biden amewaambia Waandishi wa Habari kuwa alionesha hasira ya kimaadili kwa kauli yake na sikuwa nikieleza mabadiliko ya Sera au wito wa kuondoa utawala wa Urusi.

YALIYOJIRI MACHI 30

1. Marekani yawaonya raia wake waliopo Urusi
MAREKANI: Serikali imewatahadharisha raia wake walioko Nchini Urusi kufuata Sheria za ndani za nchi hiyo au kuondoka mapema iwezekanavyo kutokana na vitisho vya kuweza kunyanyaswa wakiwa nchini humo

Wamarekani walioko Urusi wametajwa kuwa katika hatari ya kuwekwa kizuizini au kutengwa na Jeshi la Urusi kutokana na mzozo unaoendelea.

2. MAREKANI: WASHAURI WAOGA WANAMPOTOSHA PUTIN
Marekani na Uingereza zimesema kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin anapotoshwa na washauri wake ambao wanahofu ya kumwambia ukweli jinsi ambavyo uvamizi wake kwa Ukraine ulivyo na madhara makubwa

Uingereza imesema kuwa Vikosi vya Urusi vilivyopo Ukraine vinazidi kupata tabu, huku wakiamini kuwa Rais Putin hajaambiwa madhara makubwa ya kuwekewa vikwazo

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Kate Bedingfield amesema vita hiyo itaifanya Urusi iwe dhaifu kwa muda mrefu na kutengwa kwa muda mrefu.

YALIYOJIRI MACHI 31
URUSI kuacha kuuza mafuta barani Ulaya kama hawatonunua kwa fedha yao
Rais Vladmir Putin amesema atasitisha mikataba ya kusambaza Mafuta Barani #Ulaya, ikiwa Mataifa hayo yatakataa kununua bidhaa hiyo kwa fedha ya Urusi
-
Aidha, Putin ametaka malipo ya ununuzi wa mafuta yafanyike kupitia Benki za Urusi hatua zinazoonekana kuwa zinachukuliwa ili kunusuru thamani ya fedha ya Nchi yake
-
Hata hivyo Nchi za Ulaya zimepinga masharti hayo ambayo yanapaswa kutekelezwa kuanzia Aprili, 1, 2022.

YALIYOJIRI APRILI 1
1. URUSI: Ghala la mafuta lashambuliwa
Gavana wa Jimbo la Belgorod, Vyacheslav Gladkov ameishutumu Ukraine kushambulia ghala la mafuta la Belgorod nchini Urusi na kujeruhi Watu wawili

Belgorod ni eneo la mpakani mwa Urusi na Ukraine na hii ni mara ya pili kwa eneno hilo kupata shambulio ambapo awali ghala la silaha lililipuliwa.

YALIYOJIRI APRILI 2
1. Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito kwa Ukraine kuanzisha uchunguzi wa uhalifu wa kivita
Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito kwa Ukraine kuanzisha uchunguzi wa uhalifu wa kivita, baada ya kuibuka mkanda wa video unaowaonesha Wanajeshi wakiwapiga risasi miguuni wafungwa wa kivita wa Urusi

Mkanda huo ulioanza kusambaa Machi 27, unaonesha Wanaume watatu waliovalia sare, Mikono yao ikiwa imefungwa Mgongoni, wakitupwa chini na Watu wenye silaha na kisha kuwafyatulia risasi Miguuni

Shirika la Habari la AFP limeoanisha Kijiografia na Kijiji cha Mala Rogan, nje ya Mji wa Kaskazini Mashariki wa Kharkiv, ambao vikosi vya Ukraine vilikuwa vimekiteka.

2. URUSI: Rais Vladmir Putin amesema atasitisha mikataba ya kusambaza Mafuta Barani Ulaya
URUSI: Rais Vladmir Putin amesema atasitisha mikataba ya kusambaza Mafuta Barani Ulaya, ikiwa Mataifa hayo yatakataa kununua bidhaa hiyo kwa fedha ya Urusi.

Aidha, Putin ametaka malipo ya ununuzi wa mafuta yafanyike kupitia Benki za Urusi hatua zinazoonekana kuwa zinachukuliwa ili kunusuru thamani ya fedha ya Nchi yake.

Hata hivyo Nchi za Ulaya zimepinga masharti hayo ambayo yanapaswa kutekelezwa kuanzia Aprili, 1, 2022.

YALIYOJIRI APRIL 3
1. Ukraine imetangaza kuchukua udhibiti wa eneo zima la Kyiv
Ukraine imetangaza kuchukua udhibiti wa eneo zima la Kyiv baada ya Wanajeshi wa Urusi kurudi nyuma kutoka katika baadhi ya Miji muhimu karibu na Mji huo Mkuu.

Naibu Waziri wa Ulinzi, Ganna Maliar amesema Miji ya Irpin, Bucha, Gostomel na eneo zima la Kyiv imekombolewa. Miji hiyo imeharibiwa vibaya kutokana na mapigano na raia wengi waliuawa.

Watu 280 walizikwa katika kaburi la pamoja katika Mji wa Bucha huku miili mignine ikiwa imesambaa. Mamlaka zimesema karibu watu 200 waliuawa katika Mji wa Irpin tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.

YALIYOJIRI APRILI 4

1. UN: Raia 1,471 wameuawa kutokana na mgogoro wa Urusi na Ukraine
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Binadamu (UN-OHCHR) limeripoti raia 1,417 kuuawa tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine, Raia wengine 2,038 wamejeruhiwa.

121 kati ya waliouwa ni Watoto. UN-OHCHR imesema idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa kuliko iliyoripotiwa.

YALIYOJIRI APRILI 6

1. Kampuni ya kutengeneza Chip za Marekani ya Intel Corp ilisema Jumanne kwamba imesitisha shughuli za biashara nchini Urusi
Kampuni ya kutengeneza Chip za Marekani ya Intel Corp ilisema Jumanne kwamba imesitisha shughuli za biashara nchini Urusi, ikijiunga na makampuni kadhaa kuondoka nchini humo kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.

Kampuni hiyo, ambayo ilikuwa imesitisha usafirishaji wa bidhaa kwa wateja wa nchini Urusi na Belarus mwezi uliopita, ilisema imetekeleza hatua za mwendelezo wa biashara ili kupunguza usumbufu kwa shughuli zake za kimataifa.

"Intel inaendelea kuungana na jumuiya ya kimataifa kulaani vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani haraka," kampuni hiyo ilisema.

Shirika la Kimataifa la Mashine za Biashara hapo awali lilisimamisha usafirishaji huku Ukraine ikizitaka kampuni za kompyuta za wingu na programu za Marekani kukata uhusiano na Urusi.

2. Putin: Vikwazo vimepelekea janga la chakula duniani
Rais Vladimir Putin amesema Urusi inalazimika kuangalia kwa karibu mauzo yake ya Chakula kwa Nchi zisizo rafiki, kwani vikwazo vya Magharibi vimechochea janga la chakula duniani na kuongezeka kwa bei za Nishati.

Vikwazo vya Nchi za Magharibi kutokana na uvamizi wa Putin mnamo Februari 24, 2022 Nchini Ukraine vimesababisha Urusi kutumbukia kwenye mzozo mbaya zaidi wa Kiuchumi tangu kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mwaka 1991.

Hata hivyo, Moscow inasema athari za vikwazo hivyo ulimwenguni kote zinaweza kuwa kubwa zaidi.

3. EU Yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Moscow
Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imependekeza vikwazo vipya dhidi ya Urusi, ikiwemo marufuku ya ununuzi wa Makaa ya Mawe.

Vikwazo vinavyopendekezwa vitazuia uagizaji wa bidhaa za Urusi zenye thamani ya Euro bilioni 9 na uuzaji wa bidhaa za Euro bilioni 10, zikiwemo Kompyuta. Pia, Meli za Urusi zimezuiwa kuingia Bandari za Umoja wa Ulaya.

Rais wa EU, Ursula von der Leyen amesema wanapanga kupiga marufuku uagizaji wa Mafuta pia. Hayo ni kutokana na ushahidi wa kuuawa raia katika Mji wa Ukraine uliokuwa umekamatwa na Warusi.

YALIYOJIRI APRILI 7
1. UN Yaisimamisha urusi katika baraza lake la haki za binadamu
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga Kura kuisimamisha Urusi katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja huo (UNHRC) kama adhabu kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

Kati ya Wajumbe 193 wa Baraza hilo, 93 walipiga Kura ya kuunga mkono kusimamishwa Urusi, 24 walipinga na 58 hawakupiga Kura.

Hii ni mara ya pili kwa Nchi kusimamishwa kwenye Baraza hilo. #Libya ilikuwa ya kwanza Mwaka 2011.

2. Mabinti wa Putin kuwekewa vikwazo
Vita ya Urusi na Ukraine: marekani imesema inaamini mali nyingi za rais wa urusi, vladimir putin zimefichwa na wanafamilia. Kauli hiyo inakuja kufuatia vikwazo vipya vilivyotangazwa dhidi ya watu wa karibu wa putin wakiwemo mabinti zake wawili

Taarifa ya marekani imemtaja katerina vladimirovna tikhonova kama mkurugenzi kwenye masuala ya teknolojia ambaye kazi yake inasaidia serikali ya urusi na sekta ya ulinzi

Binti mwingine wa putin, maria vladimirovna vorontsova anatajwa kuongoza programu zinazofadhiliwa na serikali ambazo zimepokea mabilioni ya dola


YALIYOJIRI APRILI 11
1. Ukraine: Uchumi kuporomoka kwa 45.1% kutokana na vita
Kwa mujibu wa tathmini mpya ya athari za kiuchumi za vita ya urusi na #ukraine, uchumi wa ukraine unatarajiwa kuporomoka kwa 45.1% mwaka 2022

Tathmini hiyo ya benki ya dunia (wb) inasema uvamizi wa urusi umelazimisha biashara kufungwa, kupunguza mauzo ya nje na kuharibu mifumo ya uzalishaji.

Aidha, wb inatarajia pato la taifa la #russia mwaka 2022 kushuka kwa 11.2% kutokana na vikwazo vilivyowekwa na marekani na washirika wake wa magharibi.

YALIYOJIRI APRILI 12

1. Urusi yazionya Finland na Sweden kujiunga na NATO
Urusi imetoa onyo kwa Finland na Sweden kuhusu mpango wao wa kutaka kujiunga na NATO, ikiamini kuwa mkakati huo hauwezi kuleta utulivu Ulaya

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema muungano huo unabaki kuwa kama 'chombo kinacholenga makabiliano' huku Ikulu ya Marekani ikiunga mkono mpango huo na kuamini nchi hizo zinaweza kuomba Uanachama Juni, 2022

Finland na Sweden zikijiunga zitaifanya NATO kuwa na Wanachama 32. Wiki iliyopita mazungumzo yalifanyika kati ya Viongozi wa NATO na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Helsinki na Stockholm kuhusu hilo.

2. Rais Zelensky aomba mazungumzo na Umoja wa Afrika (AU)
Rais wa Senegal ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Macky Sall amesema Rais wa #Ukraine, Volodymyr Zelenksy ameomba kuzungumza na Umoja huo. Wito huo unakuja kukiwa na mgawanyiko kuhusu uvamizi wa Urusi.

Nchi nyingi za Afrika zimeonesha kutofungamana na upande wowote katika vita ya Urusi na Ukraine ambayo imepelekea Mataifa mbalimbali Barani humo na duniani kwa ujumla kushuhudia athari za kiuchumi za mapigano yanayoendelea.

Hivi karibuni Nchi 58 hazikupiga kura katika Mchakato wa kuiondoa Urusi katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, na inaripotiwa 24 zilikuwa za Afrika.

YALIYOJIRI APRILI 13
Putin asema wataendelea kupambana hadi "malengo yao mema" yatimie
Rais Vladimir Putin ameahidi kuwa Russia itatimiza kile alichokiita ni "malengo mema" Nchini Ukraine. Amesema mazungumzo ya amani hajapata mwafaka, na uvamizi huo unaendelea kama ilivyopangwa.

Aidha, Kiongozi amedai hakuwa na uamuzi mwingine zaidi ya kuanzisha uvamizi huo, ikiwa ni jitihada za kuwalinda wazungumzaji wa Kirusi Mashariki mwa Ukraine.

YALIYOJIRI APRILI 16
1. Zelensky: Tumepoteza wanajeshi 3,000 tangu vita ianze
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema kati ya Wanajeshi 2,500 na 3,000 wa Taifa lake wamepoteza maisha hadi sasa katika vita ya taifa hilo dhidi ya Urusi na kwamba wengine 10,000 wamejeruhiwa.

Akizungumzia vita hiyo inayoelekea siku 52 tangu kuanza, Zelensky amesema kuna Wanajeshi wengi ambao ni ngumu kujua idadi yao kama wanaweza kupona na kurejea katika afya zao za kawaida kutokana na aina ya majeraha waliyopata vitani.

Hivi karibuni Urusi nayo ilitangaza kuwa Wanajeshi wake 1,350 wameuawa katika vita hiyo.

YALIYOJIRI APRILI 18
Ukraine yaapa kutosalimu amri kuuachia mji wa Mariupol
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelens amesema Urusi inajaribu kuliharibu kabisa Jimbo la Mashariki la Donbas lakini ameahidi kwamba atalilinda na wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho katika mji uliozingirwa wa Mariupol

Zelensky amesema vikosi vya Urusi vinajitayarisha kwa oparesheni kubwa Mashariki mwa nchi hiyo ambayo itaharibu kila kitu kwenye Jimbo la Donbas

Naye, Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal amesema saa kadhaa tayari zimepita tangu kumalizika kwa muda wa mwisho uliowekwa na Urusi na hadi sasa vikosi vya Ukraine havijasimu amri na vitaendelea kupambana

YALIYOJIRI APRILI 18
Watu zaidi ya 200,000 hatarini kupoteza ajira Urusi sababu ya vikwazo
Meya wa Jiji la Moscow Nchini Urusi, Sergei Sobyanin amesema kuwa takriban wafanyakazi 200,000 wa makampuni ya kigeni wanakabiliwa na hatari ya kupoteza ajira zao kutokana na vikwazo ilivyowekewa Urusi kufuatia uvamizi wake kwa Ukraine.

Sobyanin amesema wiki iliyopita, mamlaka iliidhinisha mpango wa dola milioni 41 kusaidia ajira katika Mji Mkuu wa Urusi na kwamba mpango huo unalenga wafanyakazi wa makampuni ya kigeni ambayo yamesimamisha shughuli zao kwa muda au kuamua kuondoka nchini Urusi.

Mamia ya makampuni hasa ya Magharibi yametangaza kusimamisha shughuli zao au kuondoka Urusi baada ya Rais Vladimir Putin kutuma wanajeshi wake Ukraine mnamo Februari 24, 2022.

Wataalamu wa uchumi wanaamini kwamba, vikwazo zaidi dhidi ya Urusi vinatarajiwa kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

YALIYOJIRI APRILI 20
1. Urusi yawataka Wanadiplomasia 31 kutoka Uholanzi, Austria na Ubelgiji
Taifa hilo limewataka Wanadiplomasia 31 kutoka Nchi Tatu kuondoka siku kadhaa zijazo. Wizara ya Mambo ya Nje imeagiza Wanadiplomasia 15 wa Uholanzi kuondoka ndani ya siku 14.

Agizo hilo pia limetolewa kwa Watumishi wa Ubalozi wa Ubelgiji baada ya Nchi hiyo kuwafukuza Wanadiplomasia 21 wa Urusi Mwezi Machi. Aidha, Wanadiplomasia wanne wa Austria nao wamepewa hadi Jumapili ili kuondoka.

Uvamizi wa Urusi Nchini Ukraine umeathiri uhusiano wake na Mataifa mbalimbali.

YALIYOJIRI APRILI 22
1. Bilionea Oleg Tinkov wa Urusi amelaani Vita inayoendelea Nchini Ukraine
Bilionea Oleg Tinkov wa Urusi amelaani Vita inayoendelea Nchini Ukraine akidai ni 'wendawazimu' na 90% ya Warusi hawaiungi mkono kwani hakuna anayenufaika nayo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tinkov amependekeza Mataifa ya Magharibi kumpa Rais Vladimir Putin njia ya kutokea na kukomesha mauaji ya Raia, akisisitiza ubinadamu na busara kutumika.

2. Kamala Harris na Mark Zuckerberg wapigwa marufuku kuingia Urusi
Marufuku ya kuingia Nchini Urusi sasa itawajumuisha Makamu wa Rais wa Marekani; Kamala Harris, Mwanzilishi wa Facebook (Meta); Mark Zuckerberg pamoja na Maafisa, Wafanyabiashara na Wanahabari 27 kutoka Taifa hilo.

Serikali ya Urusi imesema Watu hao wamezuiwa kwa muda usiojulikana, ikiwa ni hatua ya kujibu vikwazo vinavyozidi kuongezeka dhidi ya Urusi.

Tangu vita kuanza Nchini Ukraine, Viongozi na Watu mashuhuri kutoka Mataifa kadhaa yakiwemo Marekani, Uingereza na Canada wamepigwa marufuku kuingia Urusi

3. Benki ya Dunia: Uvamizi nchini Ukraine umesababisha hasara ya dola bilioni 60
Ukraine imepata hasara ya Dola Bilioni 60 hadi sasa kutokana na uharibifu wa majengo na Miundombinu uliosababishwa na uvamizi uliofanywa na Urusi. Kuna uwezekano wa hasara hiyo kuongezeka kutokana na vita kuendelea.

Rais wa Benki ya Dunia (WB), David Malpass ametoa takwimu hizo katika Mkutano wa Benki hiyo Aprili 21, 2022.

Naye Rais Volodymyr Zelensky amesema kuna gharama kubwa ya kifedha inahitajika kujenga Uchumi wa Ukraine, na wanahitaji Dola Bilioni 7 kwa mwezi kufidia hasara ya kiuchumi iliyotokana na uvamizi huo.

YALIYOJIRI APRILI 23
1. Zelensky: Ukraine ni mwanzo, Urusi inalenga nchi nyingine
Rais Volodymyr Zelensky ameonya kuwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Nchi yake ulikuwa mwanzo tu, na kwamba malengo ya Moscow yanavuka Mipaka ya Ukraine.

Katika jitihada za kuleta Amani na kumaliza Vita inayoendelea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anatarajiwa kukutana na Marais wa Ukraine na Urusi wiki ijayo.

Hivi karibuni UN imekuwa ikishinikizwa kuchukua hatua kubwa zaidi katika upatanishi wa mzozo huo.

YALIYOJIRI APRILI 24
1. Zelensky aomba tena kukutana na Putin kwa mazungumzo ya amani
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa mara nyingine kuomba kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika juhudi za kumaliza vita baina ya nchi hizo mbili.

Zelensky amesema hana hofu ya kukutana na Putin iwapo hilo litasababisha makubaliano ya Amani kati ya Mataifa hayo mawili.

Alituma maombi hayo jana Aprili 23, 2022 na kusisitiza kuwa watavunja mazungumzo ikiwa Urusi itawaua Wanajeshi wa Ukraine waliosalia katika Bandari iliyozingirwa ya Bahari Nyeusi ya Mariupol.

2. Urusi yapeleleza jeshi la anga la Uingereza kuisaidia Ukraine
Urusi inafanya uchunguzi kujua ukweli wa taarifa za Jeshi la Anga la Uingereza (SAS) kuwepo Nchini Ukraine na kushiriki katika vita baina ya nchi hiyo na Urusi.

Inaelezwa, kuna Wanajeshi 20 wa SAS waliopelekwa Ukraine kwa kazi maalum. Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Uingereza alipoulizwa alisema: "Hatuwezi kuzungumzia kuhusu SAS."

Pia, inadaiwa mwanzoni mwa mwaka huu, Wanajeshi wa SAS walikwenda Ukraine kutoa mafunzo kwa Majeshi ya Taifa hilo kuhusu matumizi ya silaha za kisasa wakati mgogoro dhidi ya Urusi ukiwa umekolea.

YALIYOJIRI APRILI 25
1. Uturuki yajitolea kuwa msuluhishi wa Urusi, Ukraine
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema Nchi yake ipo tayari kusimamia sehemu ya mchakato wa mazungumzo ya kumaliza mgogoro baina ya Ukraine na Urusi.

Rais Erdogan amemwambia Rais wa Ukraine, Volodymir Zelensky kuwa watatoa usaidizi unaohitajika katika mchakato wa majadiliano ya kumaliza vita ambayo imefikisha miezi mitatu.

Ofisi ya Rais ya Uturuki imesema ahadi hiyo imetolewa wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu baina ya Viongozi hao.

YALIYOJIRI APRILI 26
WB: Vita ya urusi na ukraine inaumiza kaya masikini duniani
Ripoti mpya kutoka Benki ya Dunia (WB) imeonya kwamba usumbufu unaosababishwa na vita ya Urusi na #Ukraine utachangia ongezeko kubwa la bei za bidhaa muhimu kuanzia gesi asilia hadi ngano na pamba.

Inakadiriwa bei zitapanda kwa hadi 50% na wasiwasi mkubwa ni kwa kaya masikini zaidi duniani ambazo hutumia sehemu kubwa ya mapato ya kila siku kwa chakula na nishati.

Aidha, ongezeko hilo linatajwa kuwa kubwa zaidi kushuhudiwa ulimwenguni ndani ya miaka 50 tangu ongezeko la bei ya mafuta mwaka 1973 wakati wa mvutano wa Mashariki ya Kati.

2. Marekani yaahidi dola milioni 10 kwa atakayetoa taarifa za wadukuzi 6 wa Urusi
Marekani imesema itatoa hadi Dola Milioni 10 (Tsh. Bilioni 23) kwa watu au mtu atakayetoa taarifa za watu 6 ambao ni Maafisa wa Ujasusi wa Jeshi la Urusi wanaodaiwa kuwa waliendesha mashambulizi ya mtandaoni yaliyoathiri miundombinu muhimu ya Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Maafisa wa Idara Kuu ya Ujasusi ya Urusi wanaohusika na Masuala ya Mtandaoni (GRU) walifanya shambulizo hilo mwaka 2017 ngazi ya kimataifa, kwa kusambaza kirusi kilichoharibu kompyuta za kampuni kadhaa ya binafsi ya Marekani, ikiwemo Mfumo wa Hospitali.

Aidha, shambulio hilo maarufu kwa jina la “NotPetya” lilidumaza sehemu ya miundombinu ya Ukraine na kuharibu kompyuta katika nchi nyingi ikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Italia na Marekani, hivyo kusababisha hasara inayokadiriwa kuwa ya mabilioni ya dola licha ya kuwa Urusi ilikana kuhusika.

YALIYOJIRI APRIL 27
Urusi yasitisha usambazaji wa gesi kwa Bulgaria, Poland
Urusi imesitisha huduma za kusambaza gesi katika Nchi za Bulgaria na Poland, hali ambayo inaonesha mwelekeo wa uhusiano wa Urusi na Mataifa ya Ulaya unazidi kuzorota.

Nchi hizo ni za kwanza Barani Ulaya kusitishiwa usambazaji kutoka Urusi tangu taifa hilo liingie kwenye na Ukraine, Februari 24, 2022. Vita ya Urusi na Ukraine imesababisha vifo zaidi ya 1,000.

YALIYOJIRI APRIL 28
1. Urusi kusitisha usambazaji gesi kwa mataifa mengine ya Ulaya
Baada ya kusitisha usambazaji wa gesi kwa Poland na Bulgaria, Urusi imesema itafanya hivyo kwa Mataifa mengine ya Ulaya ambayo hayatalipia huduma hiyo kwa Fedha ya Urusi (Rubles).

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amesema uamuzi huo ni agizo la Rais Vladimir Putin kutokana na Nchi za Magharibi kutaka kutumia Fedha ya Euro, kinyume na maelekezo/mikataba waliyosaini ya kununua gesi

Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen amesema wamekutana kwa dharura kujadili suala hilo na baadhi ya Nchi zimeanza kutuma gesi kwa Poland na Bulgaria

YALIYOJIRI APRILI 29
1. Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuiba Nafaka
Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuiba Nafaka Nchini humo ikisema kitendo hicho kinaongeza tishio la hali ya Chakula Duniani. Wizara ya Mambo ya Nje imedai Urusi inaiba mazao kutoka kwa Wakulima katika eneo la Kherson.

Sehemu ya Taarifa ya Wizara inasema, "Kupitia vitendo vyake haramu, Urusi haiibii Ukraine pekee bali hata watumiaji wa Nje ya Nchi. UN inakadiria takriban watu Bilioni 1.7 wanaweza kukabiliwa na Umasikini na Njaa kutokana na vita iliyoanzishwa na Urusi".

Hata hivyo, Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov alipoulizwa kuhusu tuhuma za Ukraine alisema hawafahamu taarifa hizo zinatokea wapi

YALIJIRI MEI 2
1. VATICAN: Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameikosoa Urusi
VATICAN: Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameikosoa Urusi akisema vita dhidi ya Ukraine ni ishara ya kudidimia kwa hali ya ubinadamu na imesababisha mateso na majonzi.

Papa Francis (85) amesema mashambulizi katika Mji wa Mariupol yamekuwa ya kinyama na kusababisha watu kuhamishwa kutoka katika Mji huo.

Amesema “Ninasikitika na kulia kwa watu wan Ukraine hasa wale ambao ni dhaifu, wazee, watoto. Ni habari ya kusikitisha kuona watu wakihamishwa katika Mji wao”.

YALIYOJIRI MEI 3
1. Papa Francis aomba kukutana na Rais Putin
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema aliomba kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ili kumshawishi kumaliza vita dhidi ya Ukraine lakini hajapata majibu ya maombi yake hayo.

Wiki ya tatu baada ya kuanza kwa vita Februari 2022, Papa Francis alituma maombi hayo kwa lengo la kutafuta amani lakini hajajibiwa licha ya kuwa bado nia yake hiyo ipo.

“Nahisi Putin hatakubali kuwa na mkutano wenye lengo hilo, lakini anaweza kutuma watu wake tukazungumza,” - Papa

YALIYOJIRI MEI 4
Rais Putin aonya nchi za magharibi kuisaidia Ukraine
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema Mataifa ya Ulaya yanatakiwa kusaidia Urusi kumaliza vita dhidi ya Ukraine kwa kuweka shinikizo kwa Rais Volodymyr Zelensky na kusitisha kumpelekea silaha.

Nchi za Magharibi zimekuwa zikiisaidia Ukraine kwa vifaa na jana Mei 2, 2022 Uingereza ilitangaza kutoa msaada wa vifaa vya dola milioni 376 ikiwemo vya kielektroniki, mfumo wa rada, vifaa vya GPS na vifaa vya kuona usiku.

Putin amesema hayo alipopigiwa simu na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron aliyempigia simu ili kumshawishi kumaliza vita hiyo.

YALIYOJIRI MEI 6

1. Zelensky: Urusi imeshambulia hospitali, vituo vya matibabu 400
Rais Volodymyr Zelensky amesema uamuzi wa Urusi kuivamia #Ukraine umeharibu Hospitali na Vituo vya Matibabu, hali iliyofanya madaktari kuwa na wakati mgumu katika kutoa huduma.

Amedai Vituo 400 vimeharibiwa na kuna changamoto kubwa ya Matibabu na Dawa hususan maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Nchi ambayo yanadhibitiwa na Urusi.

Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amesema oparesheni ya tatu ya kuwahamisha Raia kutoka Mji wa Mariupol na kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichozingirwa inaendelea.

2. Putin aomba radhi Israel kwa matamshi ya Lavror kuhusu Wayahudi
Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett amesema amekubali msamaha kutoka kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa matamshi yenye utata kuhusu mauaji ya kimbari yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi hiyo.

"Waziri Mkuu aliongea na kwa simu na Rais Putin, Mei 5, 2022 alikubali msamaha wake kwa matamshi ya Lavrov na akamshukuru kwa kufafanua mtazamo wa Rais dhidi ya Wayahudi na kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust," ofisi ya Bennett ilisema katika taarifa.

Hata hivyo taarifa ya Kirusi baada ya simu, ilisema walisisitiza umuhimu wa kuashiria kushindwa kwa Wanazi katika Vita vya Pili vya Dunia, ambavyo Urusi iliadhimisha tarehe Mei 2,2022.

YAIYOJIRI MEI 8
1. Marekani yatoa silaha za dola milioni 150 kwa Ukraine
Rais Joe Biden ametangaza kutoa silaha zenye thamani ya Dola Milioni 150 (Takriban Tsh. Bilioni 347.5) kuisaidia #Ukraine katika vita dhidi ya Urusi. Msaada huo wa ulinzi ambao utahusisha silaha za ziada na rada.

Kwa mujibu wa Ofisa mmoja wa Marekani msaada huo unajumuisha risasi 25,000 za 155mm, rada za kutambua chanzo cha moto wa adui na vifaa vingine vya umeme.

Marekani imesema imetoa misaada yenye thamani ya dola bilioni 3.8 kwa Ukraine tangu kuanza kwa vita Februari 24, 2022.

2. UNICEF: Vita ya Ukraine ina athari mbaya za kisaikolojia kwa watoto
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema vita inayoendelea Nchini Ukraine imekuwa na madhara makubwa kwa watoto, na wengi wanahitaji msaada wa kisaikolojia.

Ripoti imesema kwa muda wa miezi miwili, Watoto zaidi ya Milioni moja wamekuwa katika mateso kutokana na makombora na mabomu ya mara kwa mara, kukosa chakula, kushindwa kwenda Shule na kukosa huduma muhimu.

Zaidi ya watu Milioni 7 wanaripotiwa kukimbia makazi yao ndani ya Ukraine, na zaidi ya Milioni 5 wamekuwa wakimbizi katika Nchi jirani.

YALIYOJIRI MEI 9
1. G7 Yapiga marufuku ununuzi wa mafuta ya Urusi
Mataifa yanayounda Kundi la G7 yametoa kauli ya kupiga marufuku ya kununua mafuta ya Urusi ikiwa ni mwendelezo wa vikwazo kwa taifa hilo lililoingia katika vita na Ukraine tangu Februari 24, 2022.

G7 ilifanya mkutano wa mtandaoni jana Mei 8, 2022 na imechukua uamuzi huo ili kulenga moja ya chanzo kikubwa cha mapato cha Urusi.

G7 inajumuisha Nchi za Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani.

YALIYOJIRI MEI 12
1. Mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin amezionya Nchi za Magharibi kuisaidia silaha Ukraine
Rais wa zamani wa Urusi, Dmitry Medvedev ambaye pia ni Mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin amezionya Nchi za Magharibi, akisema ongezeko la Misaada ya Kijeshi Ukraine linaweza kusababisha mzozo kati ya Urusi na Muungano wa NATO.

Medvedev ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi amesema mzozo kama huo una hatari ya kugeuka kuwa vita kamili ya nyuklia.

Amesema Nchi za NATO kupeleka silaha na kutoa Mafunzo kwa Wanajeshi karibu na Mipaka ya Urusi kunaongeza uwezekano wa kutokea mzozo wa moja kwa moja kati ya NATO na Urusi.

YALIYOJIRI MEI 15
1. Ukraine: Majeshi ya Urusi yauachia mji wa Kharkiv
Wanajeshi wa Urusi wanadaiwa kuondoka katika Mji wa Kharkiv baada ya kufanya mashambulizi katika Mji huo kwa wiki kadhaa mfululizo.

Jeshi la Ukraine ndilo lililotoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa Urusi imeelekeza nguvu zake kufanya mashambulizi katika eneo la Mashariki ambapo ni njia ya kusambaza bidhaa kwa Wanajeshi wa Ukraine waliosalia huko.

Baada ya kushindwa kuikamata Kyiv tangu walipoanza Februari 24, 2022, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameagiza Jeshi lake kuelekeza nguvu katika mashambulizi ya Donbas, eneo la viwanda ambalo limekuwa likitaka kujitenga kutoka katika Utawala wa Ukraine tangu mwaka 2014

YALIYOJIRI MEI 19
1. Zelensky: Urusi inatumia silaha dhaifu katika vita
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky anasema Urusi inatumia silaha zisizo na nguvu dhidi ya Nchi yake, na hiyo ni ishara ya kushindwa kwao.

Amesema hayo baada Makamu Naibu Waziri Mkuu wa Urusi, Yury Borisov kudaia kuwa wana teknolojia yenye uwezo wa kuangusha ndege zisizo na rubani kwa umbali wa Kilometa 5.

Zelenskiy amekejeli tamko hilo la Urusi na kusema “Inaonesha wazi kushindwa kabisa kwa uvamizi. Urusi inaogopa kukiri makosa ya uvamizi wao kwa kuwa yalifanywa na Ngazi ya Juu ya Serikali na katika Ngazi ya Kijeshi".

YALIYOJIRI MEI 27

Zelensky asisitiza vikwazo viendelee kuwekwa kwa Urusi
Rais Volodymyr Zelensky ameyataka Mataifa ya Magharibi kuacha michezo na kuiwekea Urusi vikwazo vikali ili kumaliza vita, akisisitiza Ukraine itabaki kuwa Nchi Huru.

Siku za hivi karibuni, Zelensky amekuwa akikosoa vikali Nchi za Magharibi huku Vikosi vya Urusi vikijaribu kudhibiti Miji miwili ya Severodonetsk na Lysychansk.

Hata hivyo Urusi imeendelea kusisitiza kuwa inatarajia Ukraine ikubali matakwa yake katika mazungumzo yoyote ya Amani,

YALIYOJIRI MEI 30
1. ZELENSKY: Ukraine inahitaji silaha zaidi kupambana na Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema nchi yake inahitaji silaha zaidi kuendelea kupambana na Urusi kauli ambayo amesema inalenga washirika wake wenye nia ya kuwasaidia.

Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea eneo la mapambano Mji wa Kharkiv, Mei 28, 2022 na kuzungumza na Wanajeshi, akiwaambia "Hawakutegemea tutapigana hadi hatua ya mwisho, tutaendelea kupambana na tutashinda bila shaka".

Imedaiwa Ukraine imeendelea kupata misaada ya silaha kutoka Nchi mbalimbali ikiwemo Denmark ambayo imewapa makombora. Aidha, Jeshi la Urusi limenukuliwa likisema linaushikilia Mji wa Lyman uliopo Mashariki mwa Ukraine.

YALIYOJIRI MEI 31
1. Mwandishi wa habari wa Ufaransa auawa kwa bomu Ukraine
Frederic Leclerc-Imhoff (32) raia wa Ufaransa ameuawa kwa bomu Nchini Ukraine wakati mapambano ya vita dhidi ya Urusi yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Catherine Colonna amesema Imhoff aliuawa kwa mabomu ya Urusi akiwa amevaa sare za kazi. Alikuwa Mwajiriwa wa BFM TV na ilikuwa safari yake ya pili Ukraine akiripoti matukio ya vita

Shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka limesema jumla ya Wanahabari 8 wameuawa wakiwa kazini katika vita hiyo iliyoanza Februari 24, 2022

2. Viongozi wa EU wakubaliana kupiga marufuku mafuta ya Urusi
Baada ya wiki kadhaa za majadiliano, Viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kukata 90% ya Uagizaji wa Mafuta kutoka Urusi kufikia mwisho mwa Mwaka huu. Imeelezwa kuwa, uamuzi huo utakata chanzo muhimu cha ufadhili wa Vita inayoendelea Nchini Ukraine.

Umoja huo wenye takriban Nchi 27 umefikia mwafaka huo baada ya upinzani mkali kutoka kwa Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban aliyesema vikwazo vitaathiri Uchumi wa Nchi yake.

Awali, Rais Volodymyr Zelenskyy aliwakosoa Viongozi wa Umoja huo akisema wamekuwa wapole sana kwa Moscow akisema Urusi bado inatengeneza Mabilioni kwa kuuza Nishati.

YALIYOJIRI JUNI 1

1. Marekani yakubali kupeleka roketi za masafa marefu Ukraine
Inaelezwa kuwa Marekani imekubali ombi la muda mrefu la #Ukraine la msaada wa silaha nzito zikiwemo roketi hizo ili kupambana na vikosi vya #Russia kutoka umbali mrefu, ambalo hapo awali lilikataliwa.

Silaha hizo zitajumuisha Mfumo wa Roketi wa Kivita wa M142 (HIMARS), ambao unauwezo wa kurusha makombora mengi na kwa umbali wa hadi kilomita 70 (maili 45) - mbali zaidi kuliko mizinga ambayo Ukraine inayo kwa hivi sasa.

Aidha, Rais Biden amesema msaada huo utaimarisha msimamo wa Ukraine dhidi ya Urusi na kuleta suluhu ya kidiplomasia zaidi.

YALIYOJIRI JUNI 3
1. Zelensky: Urusi inashikilia 20% ya ardhi ya Ukraine
Akihutubia bunge la luxembourg kwa njia ya mtandao, Rais Volodymyr Zelensky amesema majeshi ya urusi yanashikilia 20% ya ardhi ya ukraine wakati mapigano yakiendelea.

Hii ni mara ya kwanza kwa Zelensky kutoa kauli hiyo tangu kuanza kwa vita baina ya mataifa hayo mwezi februari. Urusi imeendelea na mapambano na inakaribia kuushikilia mji wa Sievierodonetsk uliopo Mashariki mwa Ukraine.

YALIYOJIRI JUNI 6
1. Urusi: ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje nchini Serbia yakwama
Wizara ya Mambo ya Nje nchini humo, imethibitisha kuahirishwa kwa ziara ya Waziri Sergei Lavrov nchini Serbia kwa sababu ya majirani watatu wa Serbia (Bulgaria, Macedonia na Montenegro) kuzuia ndege yake kutumia anga lao.

Serbia inadaiwa bado kuwa na mahusiano mazuri na Urusi licha ya nchi nyingi za Umoja wa Ulaya kuiwekea nchi hiyo vikwazo, kutokana na uvamizi wake wa Mwezi Februari nchini Ukraine.

YALOYOJIRI JUNI 7
1. BALOZI WA URUSI ASUSIA KIKAO CHA UN
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa (UN), Vassily Nebenzia ametoka nje ya Kikao cha Baraza la Usalama baada ya Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel kuishutumu Moscow kwa kusababisha janga la Chakula duniani.

Michel ameyashutumu Majeshi ya Urusi kwa uhalifu wa kivita na makosa mengine ya kibinadamu ikiwemo ukatili wa kingono. Akizungumza moja kwa moja na Nebenzia wakati akitoka nje, Kiongozi huyo alisema, "Unaweza kutoka nje, huenda ni rahisi zaidi kutosikiliza ukweli".

Nebenzia amenukuliwa akisema alishindwa kuendelea kukaa kwenye kikao hicho kwasababu ya uongo uliokuwa ukisambazwa dhidi ya Taifa lake

YALIYOJIRI JUNI 12
1. PUTIN: NCHI ZA MAGHARIBI HAZIWEZI KUKATAA NISHATI YETU SIKU ZOTE
Rais Vladimir Putin amesema Nchi za Magharibi haziwezi kuendelea kugomea Nishati ya Mafuta na Gesi kutoka Urusi wa miaka mingi ijayo, akidai Kampuni zinaendelea kuchimba visima kwani zinajua Biashara itakuwepo.

Ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Maofisa wa Marekani kusema faida ya kuuza Nishati kwa Urusi imepanda kuliko wakati mwingine wowote licha ya vikwazo ilivyowekewa kutokana na vita inayoendelea Ukraine

YALIYOJIRI JUNI 16
1. CHINA YAAHIDI KUIUNGA MKONO URUSI KATIKA USALAMA, ULINZI
Rais wa China, Xi Jinping ameahidi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika masuala ya msingi hasa Uhuru na Usalama

Kauli hiyo imetolewa baada ya Viongozi hao kuzungumza kwa njia ya simu, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo tangu kuanza kwa Vita ya Urusi na Ukraine, Februari 24, 2022

China haijawahi kulaani vita hiyo lakini imekuwa ikiiunga mkono Urusi Kidiplomasia na kukosoa kitendo cha Nchi za Magharibi kuliwekea vikwazo taifa hilo huku wakiipatia Ukraine silaha

YALIYOJIRI JUNI 20
1. Ukraine yapiga marufuku muziki wa Urusi
Bunge la Ukraine limepiga kura kuunga mkono mswada unaopiga marufuku baadhi ya muziki wa Urusi kwenye vyombo vya habari na maeneo ya umma nchini humo.

Mswada huo, uliopata kura za uungwaji mkono 303 kati ya 450 unapiga marufuku baadhi ya muziki wa Kirusi kuchezwa kwenye televisheni, redio, shule, usafiri wa umma, hoteli, migahawa, sinema na maeneo mengine ya umma.

Marufuku hiyo itahusisha wanamuziki na watunzi ambao ni au walikuwa raia wa Urusi baada ya 1991, hata hivyo wasanii ambao wamelaani #RussiaUkraineWar wanaweza kutuma maombi ya kutohusishwa katika marufuku hiyo.

YALIYOJIRI JUNI 21
1. Zelensky: Vita ya Urusi imefanya Afrika kuwa "Mateka"
Akihutubia Umoja wa Afrika (AU), Rais Volodymyr Zelensky amesema Afrika ni "mateka" katika Vita ya Urusi dhidi ya Taifa lake, kwani kuzuiwa kwa usafirishaji wa Nafaka #Ukraine kumepelekea uhaba ambao unaweka Mamilioni ya watu katika hatari ya njaa.

Amesema inawezekana Vita inaendelea mbali na Mataifa ya Afrika, lakini ongezeko katika bei za Vyakula tayari limeileta Vita hiyo kwa Mamilioni ya Familia.

Inaripotiwa kuwa Viongozi 55 wa Nchi walikaribishwa kushiriki Majadiliano hayo kwa Njia ya Mtandao, lakini kwa mujibu wa BBC walioshiriki ni Wanne, huku wengine wakituma Wawakilishi.

YALIYOJIRI JUNI 22
1. Mwandishi auza medali yake tsh. Bilioni 239 kusaidia watoto wa Ukraine
Mwandishi wa Habari wa Urusi, Dmitry Muratov ameuza medali yake ya Amani ya Nobel kwa Dola Milioni 103.5 (Tsh. Bilioni 239.2) kwa lengo la kusaidia Watoto wa Ukraine ambao wameathiriwa na vita.

Medali hiyo ya Dhahabu iliuzwa katika mnada kwa mnunuaji ambaye hakutajwa jina Jijini New York na fedha hizo zitapitia katika akaunti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Muratov amesema "Nimeichagua UNICEF kwa kuwa haipo chini ya Serikali moja, hivyo ni rahisi msaada kufika bila konakona. Sikutegemea kama medali itanunuliwa kwa bei ya juu kama ilivyotokea".

2. Ukraine: Maafisa wanaodaiwa kutoa taarifa za kiintelijensia kwa Urusi wakamatwa
Kwa mujibu wa Idara ya Usalama ya Ukraine, Afisa wa Juu wa Serikali pamoja na Kiongozi wa mwingine katika masuala ya Biashara wanaoshukiwa kuwa sehemu ya Mtandao wa Urusi wamewekwa kizuizini.

Inadaiwa wametoa taarifa mbalimbali zikiwemo zinazohusiana na uwezo wa Ulinzi/Usalama wa #Ukraine na Taarifa Binafsi za Maafisa wa Vyombo vya Sheria.

Ukraine imesema Urusi iliwalipa kati ya Dola za Marekani 2,000 - 15,000 kwa kila kazi (Takriban Tsh. 4,665,314 - 34,989,045) kulingana na umuhimu wa taarifa.

YALIYOJIRI JUNI 23
1. Uingereza yatangaza vikwazo vipya vya kibiashara kwa Urusi
Serikali imetangaza awamu mpya ya Vikwazo vya kibiashara dhidi ya #Russia ikiwa ni mwendelezo wa Vikwazo kutoka nchi nyingi Duniani kutokana na kuendelea kwa #RussiaUkraineWar.

Vikwazo hivyo vinajumuisha marufuku ya kusafirisha bidhaa na teknolojia mbalimbali nchini humo, usafirishaji wa mafuta ya ndege na usafirishaji wa noti bora au za Umoja wa Ulaya.

YANAYOJIRI JUNI 27
1. Rais Putin kufanya ziara nje ya Urusi
Rais wa Urusi, Vladimir Putin anatarajiwa kuwa na ziara katika nchi mbili wiki hii, hiyo inatarajiwa kuwa ziara ya kwanza ya kiongozi huyo tangu kuibuka kwa vita ya Urusi dhidi ya Ukraine, Februari 24, 2022.

Anatarajiwa kutembelea mataifa ya Tajikistan na Turkmenistan kisha atarejea Urusi kukutana na Rais wa Indonesia, Joko Widodo.

Mara ya mwisho kwa Putin kutoka nje ya mipaka ya Urusi ilikuwa mwanzoni mwa Februari, 2022 alipotembelea China na kushiriki katika ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki.

YALIYOJIRI JUNI 28

1. Kombora la Urusi limelipua sehemu yenye maduka makubwa katika Mji wa Kremenchuk Nchini Ukraine
Kombora la Urusi limelipua sehemu yenye maduka makubwa katika Mji wa Kremenchuk Nchini Ukraine na kusababisha vifo vya tu kadhaa na uharibifu wa majengo.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema kulikuwa na watu 1,000 kabla ya taarifa za kombora hilo, wengi walitoka lakini baadhi hawakufanikiwa na inadaiwa watu 15 wamepoteza maisha na 58 wakijeruhiwa

Zoezi la uokoaji linaendelea na haijajulikana idadi ya watu ambao wamefukiwa na vifusi vya majengo hayo

Zelensky amesema hilo ni moja ya tukio baya la kigaidi kuwahi kutokea Ulaya.

Viongozi wa Umoja wa G7 wamelaani tukio hilo wakisema lilienga wananchi wa kawaida.

YALIYOJIRI JUNI 29

1. Zaidi ya watu milioni 6.2 wamepoteza au kuyakimbia makazi yao ndani ya Ukraine
Imefahamika kuwa zaidi ya watu milioni 6.2 wamepoteza au kuyakimbia makazi yao ndani ya Ukraine kutokana na vita inayoendelea kati ya taifa hilo na Urusi.

Umoja wa Mataifa (UN) umetoa ripoti hiyo na kusema kuwa watu hao bado wamo ndani ya Ukraine wakati watu milioni 5.26 wakikimbilia nje ya nchi tangu kuanza kwa vita hiyo Februari 24, 2022.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM zlimeeleza kuwa limekuwa likifanya utafiti mara kadhaa, kwa sasa kuna walioamua kurejea katika makazi yao kwa kuwa ripoti ya Mei 3, 2022 ilionesha kuna wakimbizi wa ndani milioni 8, ambapo 65% walikuwa wanawake.

YALIYOJIRI JUNI 30

1. Putin: Urusi itajibu ikiwa NATO itapeleka Vikosi katika Mataifa ya Sweden na Finland
Rais Vladimir Putin amesema Urusi itajibu ikiwa NATO itapeleka Vikosi na Miundombinu katika Mataifa ya Sweden na Finland baada ya kujiunga na Muungano huo.

Ameeleza, Nchi yake haina shida kama Sweden na Finland zinataka kujiunga NATO, Mataifa hayo lazima yaelewe kwamba hakukuwa na tishio awali, lakini hivi sasa mivutano inaweza kutokea.

Kuhusu Ukraine, ameeleza kuwa "Operesheni ya Kijeshi" inaendelea kama ilivyopangwa na Malengo ya Urusi hayajabadilika.

YALIYOJIRI JULAI 1

1. Mahakama yaitaka Urusi kutowanyonga Waingereza waliojisalimisha
Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) imeitaka Urusi kuzuia hukumu ya kunyongwa kwa raia wawili wa Uingereza waliohukumiwa kifo katika eneo la Mashariki mwa Ukraine.

Waingereza hao, Shaun Pinner na Aiden Aslin waliohamishia makazi yao Ukraine kisha kujiunga na jeshi la Nchi hiyo mwaka 2018, walihukumiwa kifo katika Mji wa Donetsk, Juni 2022 baada ya kujisalimisha kwa Jeshi la Urusi wakati mapigano yakiendelea.

Mahakama ya ECHR ni sehemu ya Baraza la Ulaya iliyoiondoa Urusi kuwa mwanachama wake mwezi Machi 2022 kufuatia hatua ya kuivamia Ukraine.

YALIYOJIRI JULAI 4

1. Urusi yadhibiti eneo la Mji wa Mashariki wa Lysychansk
Jeshi limethibitisha kuondoka katika Mji wa Mashariki wa Lysychansk unaoripotiwa kuwa mikononi mwa Wanajeshi wa Urusi. Rais Volodymyr Zelensky amesema Vikosi vya Ukraine vitarejea, na silaha za masafa marefu zitawawezesha kudhibiti eneo hilo.

Awali, Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu alisema Vikosi vyake vinaishikilia Lysychansk na vimedhibiti eneo la Luhansk kikamilifu. Kabla ya vita kuanza, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitambua Luhansk na Donetsk kuwa huru kutoka kwa Ukraine

YALIYOJIRI JULAI 15

1. Makombora ya Urusi yameua takribani watu 20 Ukraine
Makombora ya Urusi yaliyorushwa katikati ya Nchi ya Ukraine yameua takribani watu 20 kati yao wakiwemo watoto watatu na wengine 90 kujeruhiwa.

Msaidizi Mkuu wa Polisi, Kyrylo Tymoshenko amesema makombora matatu yameharibu ofisi na makazi ya watu maeneo ya Vinnytsia ambayo yapo kilometa 268 kutoka Mji Mkuu wa Kyiv.

Imeelezwa kuwa makombora hayo yalirushwa kutoka katika nyambizi ya Urusi ya Urusi.

YALIYOJIRI JULAI 18
1. UKRAINE: Zelensky awafuta kazi Mwendesha Mashtaka na Mkuu wa Usalama
Rais Volodymyr Zelensky ametoa amri ya kuwafuta kazi, Mkuu wa Idara ya Usalama, Ivan Bakanov na Mwendesha Mashtaka Mkuu, Iryna Venediktova na kumteua Naibu wake Oleksiy Symonenko kama Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya.

Amesema hatua hiyo ni kufuatia tuhuma za Maafisa wao kushirikiana na Urusi, huku kesi 651 za uhaini na ushirikiano zikifunguliwa dhidi ya Maafisa wa Idara hizo nyeti. Amebainisha kuwa hadi sasa zaidi ya Maafisa 60 wa Idara hizo wanafanya kazi dhidi ya Ukraine katika maeneo yanayotawaliwa na Urusi.

Yaliyojiri September 16
1. Urusi yaionya Marekani kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema iwapo Marekani itaamua kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu, itakuwa imevuka mpaka na kuwa ‘mshiriki katika mzozo’ baina ya mataifa hayo mawili.

Marekani imepitisha uamuzi wa kuipatia Ukraine Mfumo wa kurushia roketi nyingi (GMLRS) ambao unaweza kulenga shabaha hadi umbali wa Kilomita 80
 
Take it from me, hakuna vita hapo!

Kwa watu wa dini wenye mioyo minyoofu, hiyo ni ishara kubwa sana kwamba sasa uovu wa wanadamu umefikia kikomo kama ilivyokuwa wakati wa Gharika na Sodoma na Gomora.

Mungu yule wa Gharika na Sodoma na Gomora ndiye yule yule ambaye tunaye sasa. Hajabadilika.

Amekuwa na subira kwa muda mrefu, sasa:"Enough is enough "
 
Wakuu, Baada ya Russia kupeleka jeshi kubwa mno kwenye mpaka wake na Ukraine, mataifa makubwa Duniani yalihamaki yakiongozwa na Marekani.

NATO ilisema wazi kwamba haitaiacha Ukraine ikiwa yatima,na tayari muungano huo wa kujihami wa Ulaya magharibi na Marekani umeimarisha vikosi vyake Poland na Estonia.

Russia imepeleka zaidi ya wanajeshi 130,000 kwenye mpaka wake na Ukraine na wakati wowote wanasubiria amri ya Rais Putin Kuivamia Ukraine.

Baada ya Russia kuimega Crimea na Dunia kukaa kimya,Putin alidhani itakuwa rahisi pia Kuivamia Ukraine na kufanya lolote sasa mambo yamekuwa Tofauti.

Uingereza imepeleka shehena kubwa mno ya silaha mbalimbali Ukraine na makomandoo wa kikosi maalumu cha SAS.

Canada nayo imesema haitaiacha pekee yake Ukraine itaipa misaada yote ya kijeshi dhidi ya uvamizi wa Russia. Kwa hiyo Russia inafikia hatua wanaogopa wakijua wazi kwamba kushinda vita kwao itakuwa ngumu mno.

Na hakika Russia ikijaribu kuivamia Ukraine haitashinda hii vita zaidi ya kuharibikiwa kiuchumi. Russia ni nani hasa hata ashinde vita dhidi ya Marekani, Uingereza, Canada na mataifa mengine mengi ambayo yanaisaidia Ukraine bila kuitangazia Dunia.

Mengine yabakie ushabiki tu, lakini Russia haitashinda hii vita na wao wameshaliona hilo.

Screenshot_20220215-100107.jpg
 
Tatizo watz tuna ujuaji wa kinonko sana.

Urusi ikiamua itaivamia Ukraine na Marekani hatofanya chochote zaidi kulialia na kuweka vikwazo.

Marekani na vibaraka wake wangekuwa na nia ya kweli kuisaidia Ukraine wangeisadia kukomboa majimbo mawili yanayo shikiliwa na waasi.

Inashangaza eti jeshi ambalo limeshindwa na kukundi cha waasi chenye wapiganaji wasiozidi 50,000 eti kije kukabiliana na moja wapo ya jeshi kubwa duniani.

Iwapo vita itatokea nakuhakikishia jeshi la Ukraine halitaweza kuhimili nguvu ya jeshi la Urusi hata ndani ya wiki mbili.
 
Aivamie Ukraine akose mradi wa gas wa Nord Stream 2?..NATO walishamwambia Putin very clear,hawezi pata vyote,achague kimoja,aivamie Ukraine akose Nord Stream 2 au aachane na Ukraine inversion abakize Nord stream 2.

Unafikiri Putin ni mjinga hivyo akose mradi utaofaidisha genereations sababu ya vita Ukraine.

Kila kitu ni leverage boss sio ubabe wa kijinga mnaoupigania huku usio na kichwa wala miguu.

Leo Sergei Lavrov amesema baadhi ya wanajeshi waliokuwa mpakani Ukraine wameanza safari ya kurudi kambini,Hata satellites za Marekani wame confirm movements za wanajeshi ku withdraw.

Vita sio lelemama aisee
 
Aivamie Ukraine akose mradi wa gas wa Nord Stream 2?..NATO walishamwambia Putin very clear,hawezi pata vyote,achague kimoja,aivamie Ukraine akose Nord Stream 2 au aachane na Ukraine inversion abakize Nord stream 2...
Ndio maana nimemwambia mtoa mada ya kwamba Urusi inaweza isiivamie Ukraine kwa sababu zingine hasa za kiuchumi .

Lakini hoja ya kwamba Urusi inaogopa kuivamia eti kwa sababu ya kugopa Marekani itatuma wanajeshi wake sio kweli.

Na ndio maana nimemwambia ya kwamba Urusi ikiamua kuivamia Ukraine Marekani hatofanya chochote zaidi ya kuweka vikwazo vya kiuchumi ikiwemo kusitisha hilo bomba la gesi.

Na kama umeufatilia huu mgogoro hakuna kiongozi yeyote yule wa Urusi aliye sema ya kwamba Urusi inataka kuivamia Ukraine zaidi ya kusema wanafanya mazoezi ya kijeshi ya kawaida, hizo tuuma za Urusi kutaka kuivamia Ukraine zimekuwa zikitolewa na nchi magharibi na viongozi wa Urusi Mara kwa mara wamekuwa wakikanusha.

Na sisitiza USA na washirika wake wange kuwa na nia ya kuisaidia Ukraine wangeisaidia kwanza kukomboa majimbo mawili yanayo shikiliwa na waasi.
 

Similar Discussions

107 Reactions
Reply
Back
Top Bottom