Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Kwa vile zimebaki siku tatu tu kufikia kikomo cha siku saba zilizotolewa na Waziri Masha, nadhani wakati huu tusisumbuke kutafuta historia za key-players wa hii saga; badala yake, tusubiri siku hiyo ifike ili ukweli uanze kutolewa. Tukitaka kujadili historia zao, ni afadhali tuanzishe thread nyingine kule kenye folder ya Celebrities.

Nina imani kuwa kambi ya Masha inajiandaa vya kutosha kuhakikisha kuwa Mengi anakiona cha moto asipotoa ushahidi ndani ya siku saba, na kambi ya Mengi nayo inajitahidi kukusanya ushahidi wa kuthibitisha madai yao. Nadhani kambi hizo mbili zitakapoanza kupambana kwa facts ndipo mjadala utakapokuwa na maana kwa watanzania wote kwani mvutano huo unahusu maslahi ya demokrasi, utawala bora na utii wa sheria kwa watanzania wote. Kumtetea au kumponda mtu kutokana na matendo ama tabia yake ya zamani hakusaidii lolote katika mjadala huu kwa sasa hivi.

Usishike pumzi lakini (Don't hold your breath).

Nilisema awali, wanaojua nini kinaendelea hawasemi kitu. Na wanaosema sema hapa, hawajui nini kinaendelea.
 
Usishike pumzi lakini (Don't hold your breath).

Nilisema awali, wanaojua nini kinaendelea hawasemi kitu. Na wanaosema sema hapa, hawajui nini kinaendelea.

?????????????????????? sikukuelewa mzee wangu.
 
All things considered, Lau Masha is no Dr. Nchimbi (Education wise)

Why is he acting like a Nchimbi beats me, au ndiyo mambo ya kwamba ukikaa na wajinga wajinga wa CCM ambao kutwa kucha wanafikiri kuwa photioshop watu na kuwa portray wrongfully kwenye magazeti ndiyo siasa?

If the claims are true, if this is what a young minister, Georgetown graduate no less, with the advantage of having grown up in the US and the personification of the hope of the "Mizee iondoke, vijana wabadilishe mambo" mantra, is all about, I am simply appalled.

Why, he is giving the likes of Kingunge Ngombale Mwiru and Yuisufu Makamba a run for their reps!

Unajua Bwana Masha anastaajabisha, maana hata ukimwangalia katika education level yake na hata presentation yake, he is well educated and looks intelligent. Sasa anapoanza kujiweka group moja na Dr Nchimbi wasio kama yeye hapa anatushangaza sisi akina yakhe.

Wake up Masha... You are better than that...
 
Jamani Mwanakijiji kapotelea wapi?...
Ningeomba sana mkuu arudi na mada nyingine yenye nguvu tuondokane na upuuzi huu!..
Samahani wakubwa zangu, nitaondoa heshima yangu kwenu hapa na kusema hivi...
Mada hii haina tofauti na Ze utamu.... na kuendelea kuchangia inanipa picha mbaya sana kwa mchangiaji...
Wakuu zangu hata JF inaweza kufungiwa kwa sababu tunakosa heshima sasa hivi... Iwe kwa masha au Mengi, tumeshindwa kuzungumzia mapungufu ya viongozi ama mwananchi tunaingilia maisha ya watu hawa kwa kejeri za kipuuzi kabisa!..Hakuna madai yoyote humu yanayohusiana na sakata lililotokea isipokuwa masiha ya watu hawa..What's going on guys!
Personal life ya mtu yeyote ni private na tunapo invade privacy ya mtu yeyote acha kiongozi kwa maneno machafu kama haya tunavunja sheria na bila shaka tunajiweka ktk fungu la watu wenye akili ya kushikiwa (simple minded)...
 
1.
Na rest assured mzee, ukija huku nitakutandikia zulia jekundu kabisa. I got you covered. Hutahitaji hata kutumia senti moja toka mfukoni mwako na nitakupeleka kokote unakotaka kwenda ili

- Mkuu ubarikiwe kwa hili na I am down maana this is wasup, I mean for real! Wewe unafikiri nikienda kwa kina flani wataniendesha kweli? Si wataniitia police! Bwa! ha! ha! ha!

2.
na mimi baadae nije kuwaambia watu niliwahi kumwendesha Field Marshall Emergency System

- Ahsante mkuu, lakini kwangu Lau will alyways be Lau, the man ingawa kwa wengine ni waziri na all that stuff,

- kumuendesha sio big deal kwa sababu na yeye amewahi kuniendesha sana inapobidi, kwa hiyo mkuu ukiniendesha sawa na mimi siku moja nitakuendesha tu, hakuna noma, ila respect kwa offer! maana sio wote hapa wanaweza kutoa hiyo, ubarikiwe!

Wazee wa sauti ya umeme, kutoka radio station ya FMES!
 
My concern is he may not necessarily correctly gauge the intricacies of the nuanced crusade waged, and how some delicate info splurged here may be smithereensed and reassembled.

- Mkuu ninajua for a fact kwamba kinachoendelea sasa ni siasa chafu at its best, na it is all about 2010 na hii ishu ndio the moment of the truth of so many "political war games" which has been played toka 2005 na so far have claimed so many innocent politicians as victims,

- ninajua tembo wote walioko nyuma ya hivi vita na exactly kinachoendelea, sasa watch vitakavyoishia, itakua the best joke of all our times, kama vile kununua busara za Spika kwa Shillingi millioni 100, remember that? Now watch this one, maana tembo wawili huko nyuma wamekamatana pabaya!
 
Naona kama hapa mnaanza kupoteza muelekeo wa Topic. Suala liko kwenye (C)vyombo vya dola, ngoja walishughulikie tuone mkweli ni nani. Hata hizo siku 7 alizotoa Mh. Masha hazijaisha tunaanza kuingiza personal Affairs. Kama ni suala la kuoa Mnyarwanda huwezi jua ni kwa nini alimpenda huyo. Huenda alikuwa na ufundi zaidi kuliko ambao Mengi amewahi ku-experience. Ni wangapi raia wa Tanzania wameoa wageni na waliwahi kushika uongozi Tanzania lakini hatujasema? Mfano Prof. Sarungi, Prof. Mbilinyi, Fisadi Karamagi. Kama mapadri wanalawiti au kuwa mashoga ije kuwa Mfanyabiashara, Muwekezaji mzalendo Mengi hasijikwae kwenye matamanio ya kibinadamu!!

Jamani turudi kwenye issue hapa, tusubiri hizo siku 7 ziishe tuone nini next step toka serikalini kupitia kwa Masha. Kama Masha angekuwa credible basi na yeye angekubali kujiuzuru kama ingebainika kuwa Mengi hakudanganya suala la kuripoti polisi. Matokeo yake Masha alikuja na staili nyingine akisema hawezi kujiuzuru kwa sababu kutoa maagizo hayo ni hatua ya kumlinda Mengi. Ushahidi hauwezi kupelekwa kwa Masha kama Waziri, au kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais.
Kama serikali inaona au inafikiria kuwa Mengi ameongea uongo au kuwadhalilisha wanatakiwa kwenda Mahakamani na si kumtisha kwa siku 7. Ukweli ndipo utajulikana huko Mahakamani baada ya kupitia ushahidi. Ukishawatangulizia ushahidi wanaenda kuuchezea kama ambavyo wamekuwa wakicheza na sakata ya KAGODA. Mambo yapelekwe mahakamani na wananchi watashuhudia jinsi hiyo kesi inavyoendeshwa, then tunaweza kutoa analysis.

Magic Johnson ni muathirika wa UKIMWI kwa muda mrefu sana lakini bado ni muamasishaji mzuri katika kupambana dhidi ya huu ugonjwa. Kwa hiyo Mengi sioni kama ana kosa lolote unaposema alimwachia mwanaye akafa kwa Ukimwi. Huenda aliupata huo ugonjwa hata kabla Mengi hajapata hiyo dhamana. Na hata kama angekuwa keshapata hiyo dhamana huwezi kumzuia mtu mzima kutofanya anachotaka yeye. Naamini aliweza kumshauri lakini hasingeweza kum-track kila nyendo alizokuwa akifanya.

Narudi kwenye mada hatuwezi kupuuzia threats dhidi ya mwananchi yeyote eti kwa sababu mwanae alikufa kwa ugonjwa fulani wakati mzazi akiwa na dhamana fulani. Tuache sheria ichukuwe mkondo, uongo kawaida hujitenga.
 
Hizo comments za Game Theory ni uchochezi humu ndani na kutokuwa na heshima hata kwa watu waliofariki dunia (RIP), pse remove the unnecessary hate mongering.

Game Theory pse do the needful and remove the comments.
 
1. Jamani turudi kwenye issue hapa, tusubiri hizo siku 7 ziishe tuone nini next step toka serikalini kupitia kwa Masha.

2. Kama Masha angekuwa credible basi na yeye angekubali kujiuzuru kama ingebainika kuwa Mengi hakudanganya suala la kuripoti polisi. Matokeo yake Masha alikuja na staili nyingine akisema hawezi kujiuzuru kwa sababu kutoa maagizo hayo ni hatua ya kumlinda Mengi. Ushahidi hauwezi kupelekwa kwa Masha kama Waziri, au kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais.
Kama serikali inaona au inafikiria kuwa Mengi ameongea uongo au kuwadhalilisha wanatakiwa kwenda Mahakamani na si kumtisha kwa siku 7. Ukweli ndipo utajulikana huko Mahakamani baada ya kupitia ushahidi. Ukishawatangulizia ushahidi wanaenda kuuchezea kama ambavyo wamekuwa wakicheza na sakata ya KAGODA.

3. Mambo yapelekwe mahakamani na wananchi watashuhudia jinsi hiyo kesi inavyoendeshwa, then tunaweza kutoa analysis.

- Mkulu Indume Yene, najua kuwa wewe ni kichwa sana na huwa ninakuheshimia sana ndio maana huwa sigusi fimbo zako,

However, eti umesema tusubiri tusitoe analysis yaani sasa hii yako ni nini hasa? I mean umeniacha nje hapa bro, au Bwa! ha! ha! ah!?

yaani Indume Yene ni bwana ni balaaaaaa!

Anyways, Alyways Respect!
 
loyal friend exhibiting some spartan characteristics of a truly passionate and dependable ally.

Friends have credibility of being friends. If one doesn't have the credibility; he will not be a friend and betrayal will be the payback unknowingly.
 
Kama serikali inaona au inafikiria kuwa Mengi ameongea uongo au kuwadhalilisha wanatakiwa kwenda Mahakamani na si kumtisha kwa siku 7. Ukweli ndipo utajulikana huko Mahakamani baada ya kupitia ushahidi. Ukishawatangulizia ushahidi wanaenda kuuchezea kama ambavyo wamekuwa wakicheza na sakata ya KAGODA. Mambo yapelekwe mahakamani na wananchi watashuhudia jinsi hiyo kesi inavyoendeshwa, then tunaweza kutoa analysis.

Magic Johnson ni muathirika wa UKIMWI kwa muda mrefu sana lakini bado ni muamasishaji mzuri katika kupambana dhidi ya huu ugonjwa. Kwa hiyo Mengi sioni kama ana kosa lolote unaposema alimwachia mwanaye akafa kwa Ukimwi. Huenda aliupata huo ugonjwa hata kabla Mengi hajapata hiyo dhamana. Na hata kama angekuwa keshapata hiyo dhamana huwezi kumzuia mtu mzima kutofanya anachotaka yeye. Naamini aliweza kumshauri lakini hasingeweza kum-track kila nyendo alizokuwa akifanya.

Narudi kwenye mada hatuwezi kupuuzia threats dhidi ya mwananchi yeyote eti kwa sababu mwanae alikufa kwa ugonjwa fulani wakati mzazi akiwa na dhamana fulani. Tuache sheria ichukuwe mkondo, uongo kawaida hujitenga.

Ugomvi hapa ni dhana iliyokuwepo serikalini kuwa Mramba na Yona wakipelekwa mahakamani basi wananchi na vyombo vya habari vitakaa kimya au kuanza kuimba korasi za kuisifia serikali.

Kwa mshangao, thisday wakaendeleza bango la KAGODA na kashfa zingine. BTW, bado Kikwete hajasema chochote kuhusu kashfa zingine zinazoikabili serikali yake ( kuanzia Buzwagi...... nk).

Masha anajaribu kunyamazisha media Tanzania na katika hili, watanzania kwa sauti moja wanasema noooooo waaaay.
 
- Mkulu Indume Yene, najua kuwa wewe ni kichwa sana na huwa ninakuheshimia sana ndio maana huwa sigusi fimbo zako,

However, eti umesema tusubiri tusitoe analysis yaani sasa hii yako ni nini hasa? I mean umeniacha nje hapa bro, au Bwa! ha! ha! ah!?

yaani Indume Yene ni bwana ni balaaaaaa!

Anyways, Alyways Respect!

Mkuu FMES pole sana kama kulikuwa na mgongano hapo.
Analysis ambayo nilikuwa namaanisha ilikuwa ni juu ya ushahidi ambao Mh. Masha aliomba kutoka kwa Bw. Mengi. Naamini watanzania kwa ujumla tutakuwa na nafasi nzuri ya kutoa analysis ya kesi kama itakuwa imefunguliwa na serikali dhidi ya Mengi. Maana naamini Bw. Mengi atakuwa ana opportunity na kumwaga huo ushahidi wake mbele ya Hakimu au Jaji. Na kama kesi itakuwa open kama kesi zingine wananchi wataweza kusikiliza pande zote 2.

Pole kwa mkanganyo.
 
Kwa vile zimebaki siku tatu tu kufikia kikomo cha siku saba zilizotolewa na Waziri Masha, nadhani wakati huu tusisumbuke kutafuta historia za key-players wa hii saga; badala yake, tusubiri siku hiyo ifike ili ukweli uanze kutolewa. Tukitaka kujadili historia zao, ni afadhali tuanzishe thread nyingine kule kenye folder ya Celebrities.

Nina imani kuwa kambi ya Masha inajiandaa vya kutosha kuhakikisha kuwa Mengi anakiona cha moto asipotoa ushahidi ndani ya siku saba, na kambi ya Mengi nayo inajitahidi kukusanya ushahidi wa kuthibitisha madai yao. Nadhani kambi hizo mbili zitakapoanza kupambana kwa facts ndipo mjadala utakapokuwa na maana kwa watanzania wote kwani mvutano huo unahusu maslahi ya demokrasi, utawala bora na utii wa sheria kwa watanzania wote. Kumtetea au kumponda mtu kutokana na matendo ama tabia yake ya zamani hakusaidii lolote katika mjadala huu kwa sasa hivi.

- Mwalimu Kichuguu, kama kawaida yako, balanced bila ushaibiki wala unazi, ubarikiwe tu!
 
Mkuu FMES pole sana kama kulikuwa na mgongano hapo.
Analysis ambayo nilikuwa namaanisha ilikuwa ni juu ya ushahidi ambao Mh. Masha aliomba kutoka kwa Bw. Mengi. Naamini watanzania kwa ujumla tutakuwa na nafasi nzuri ya kutoa analysis ya kesi kama itakuwa imefunguliwa na serikali dhidi ya Mengi. Maana naamini Bw. Mengi atakuwa ana opportunity na kumwaga huo ushahidi wake mbele ya Hakimu au Jaji. Na kama kesi itakuwa open kama kesi zingine wananchi wataweza kusikiliza pande zote 2.

Pole kwa mkanganyo.

- Mkuu wangu Indume Yene, wewe najua ni balaaaaaa kwa hiyo ni amina tu, as of your wish, Bwa! ha! ha! ha!!
 
CHADEMA yanunua kesi ya Mengi, Masha
• Mbowe ashtuka Masha kumtisha Mengi

na Edward Kinabo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeinunua kesi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, dhidi ya Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, kwa kusisitiza kuwa kina ushahidi kutoka kwenye vikao nyeti vya serikali kuwa waziri huyo kijana ndiye aliyepeleka hoja ya kutaka mfanyabiashara huyo afilisiwe.

Hali hiyo ilibainishwa jana na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Mbowe aliithibitishia Tanzania Daima kwamba chama chake kina ushahidi wa kuaminika kutoka kwenye vikao nyeti vya serikali kwamba Waziri Masha ndiye aliyeishauri serikali ipange mkakati wa kumfilisi Mengi kwa lengo la kuvidhoofisha vyombo vyake vya habari visiendelee kuibua na kuandika habari zinazohusu ufisadi.

Alisema mwelekeo wa suala hili unamnyima Waziri Masha haki ya kuzungumza na hapaswi kujitetea wala kusema chochote zaidi ya kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake kwa uhuru.

“Kitendo cha Waziri Masha kumpa Mzee Mengi amri ya kuwasilisha ushahidi ndani ya siku saba kinashangaza, kwani Waziri huyo hana mamlaka kisheria ya kudai ushahidi na badala yake chombo chenye mamlaka ya kudai ushahidi ni mahakama,” alisema Mbowe. Mwenyekiti huyo alisema kama serikali inaona imeonewa au imechafuliwa katika suala hilo, iende ikashitaki mahakamani na si vinginevyo.

“Waziri hana mamlaka ya kisheria ya kudai kupelekewa ushahidi. Chombo chenye mamlaka hayo ni mahakama. Kama wao (serikali) wanaona wameonewa au wamechafuliwa waende mahakamani, kama ni uongo waende wakashtaki kama walivyokimbilia mahakamani kwenye sakata la mgomo wa walimu,” alisisitiza Mbowe.

Kwa mujibu wa Mbowe, Waziri Masha ameendeleza rekodi ya mawaziri wengine wa Serikali ya Awamu ya Nne ya kupenda kukurupuka na kupayuka hovyo bila kutafakari kwa makini na matokeo yake ni kuvuka mipaka ya mamlaka waliyonayo.

“Na hii imekuwa ni tabia ya Mawaziri wa Kikwete ya kukurupuka na kupayuka hovyo bila kutafakari kwa umakini hadi wanavuka mipaka ya mamlaka yao. Waziri hana mamlaka ya kudai apelekewe ushahidi……hiyo ni kazi ya mahakama,” alisema Mbowe.

Alisema mtu au chombo chochote kinachopinga ufisadi kinahitaji kulindwa kwa gharama yoyote badala ya kutishwa na serikali.

Aliitaka serikali kutumia vyombo vyake kufanya mambo ya maana na yenye maslahi kwa taifa . “Serikali itumie vyombo vyake kufanya mambo ya maana na yenye maslahi kwa taifa. Jambo hili la kumfilisi Mengi halina tija. Serikali inataka kuwawajibisha wananchi badala ya wananchi kuiwajibisha serikali. Serikali iache mchezo wa kutisha raia wake, iache kuwahujumu raia wa nchi. Jukumu la serikali ni kupambana na uhalifu si kufanya uhalifu dhidi ya raia wake wema,” alisema Mbowe.

Alisema inasikitisha kuona serikali inataka kumshughulikia Mengi kwa kumfilisi bila kujali mchango mkubwa wa vyombo vyake vya habari na biashara katika kupambana na ufisadi na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Alionya kuwa iwapo serikali itamfilisi Mengi kama alivyopendekeza Waziri Masha, uchumi utaathirika kwa pato la taifa kushuka kwa sababu itapoteza mapato ya kodi zinazotozwa kwenye makampuni ya mfanyabiashara huyo.

“Kumfilisi Mengi ni kuathiri ajira….hata uchumi wa nchi unaweza kuathirika. Ni wananchi wangapi wameajiriwa kwenye makampuni yaliyo chini ya Mengi…….Watanzania wengi watapoteza ajira. Pato la taifa linaweza kushuka…..serikali itapoteza mapato ya kodi inayopata kutoka kwenye makampuni anayoyamiliki Mengi. Serikali iache mchezo wa kushugulikia raia wake na kudai kuwa inawalinda,” alitahadhalisha Mbowe.

Juzi Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alisema ana ushahidi kuwa Waziri Masha, ndiye aliyepeleka hoja ya kumhujumu Mengi katika vikao vya juu vya serikali.

Zitto alisema yeye hana sababu ya kumtetea Mengi ila hawezi kunyamaza kuona Mtanzania anayeipenda nchi yake na kulazimika kupinga ufisadi, anafanyiwa hujuma. Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, jana alinukuliwa na vyombo kadhaa vya habari akimtaka Waziri Masha kuviacha vyombo vya upelelezi vifanye uchunguzi wake.

Kuibuka kwa sakata hilo kunatokana na Mengi kumtuhumu Waziri mmoja kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

Mengi akizungumza na vyombo vya habari wiki iliyopita, alimtuhumu waziri huyo ambaye hakumtaja jina, kuwa amekuwa akitumiwa ujumbe wa vitisho kutokana na vyombo vyake vya habari kuwa mstari wa mbele katika kupinga ufisadi.

Kutokana na hatua hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, alimpa Mengi siku 7 awe amekwisha wasilisha vielelezo vya kuthibitisha madai yake kwake yeye (Masha), vinginevyo atamchukulia hatua za kisheria.

Akijibu amri ya Masha, Mengi alisema yupo tayari kutupwa jela ikithibitishwa kuwa amedanganya na kumwomba Masha pia aseme kama atakuwa tayari kujiuzulu iwapo ukweli utathibitika.

Hata hivyo juzi jumapili, Masha alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hayuko tayari kujiuzulu kwa sababu nia yake ya kuwaagiza polisi kufanya uchunguzi inalenga kumlinda Mengi.

Alisema kutokana na taarifa ambayo Mengi aliipeleka kituo cha polisi cha Oysterbay, polisi wameamua kuifanyia uchunguzi ili kuhakikisha maisha yake yanakuwa salama.

Alisema, hata kama hawamuamini, basi waupeleke huo ushahidi kwa Rais au Waziri Mkuu kuuonyesha na kama ikibainika kama ni kweli yeye ndiye anayemhujumu Mengi, basi atajiuzulu.

Alidai kuwa yeye hakusema kuwa atamshughulikia Mengi kama alivyonukuliwa kwenye baadhi ya magazeti ila alisema kuwa sheria itachukua mkondo wake kama ikibainika kuwa tuhuma zilizotolewa ni za kweli.

Sijui sasa Masha atawapa CHADEMA siku ngapi baada ya tamko la Zitto la kumtaja Masha na hili la Mbowe.
 
Kwa vile zimebaki siku tatu tu kufikia kikomo cha siku saba zilizotolewa na Waziri Masha, nadhani wakati huu tusisumbuke kutafuta historia za key-players wa hii saga; badala yake, tusubiri siku hiyo ifike ili ukweli uanze kutolewa. Tukitaka kujadili historia zao, ni afadhali tuanzishe thread nyingine kule kenye folder ya Celebrities.

Nina imani kuwa kambi ya Masha inajiandaa vya kutosha kuhakikisha kuwa Mengi anakiona cha moto asipotoa ushahidi ndani ya siku saba, na kambi ya Mengi nayo inajitahidi kukusanya ushahidi wa kuthibitisha madai yao. Nadhani kambi hizo mbili zitakapoanza kupambana kwa facts ndipo mjadala utakapokuwa na maana kwa watanzania wote kwani mvutano huo unahusu maslahi ya demokrasi, utawala bora na utii wa sheria kwa watanzania wote. Kumtetea au kumponda mtu kutokana na matendo ama tabia yake ya zamani hakusaidii lolote katika mjadala huu kwa sasa hivi.

Kichuguu,
Ngoma ikikolea na mida ya kufuturu ikifika, Wasukuma tutaanza kuangalia Vimwali vinaenda wapi. Tukigundua kuwa wameshaondoka, hapo ni sisi na wao (Ukenya tupu) na tukiwakamata ni CHAGULAGA hadi kesho yake. Masanja jiandae huko na kaptura nyeupe......na chini KATA MBUGA.

Misukosuko ya FISADI, ukweli unapoingia,
VItisho watavitoa, Kwenye Luninga kutishia,
Wewe Mengi nakuambia, mtema kuni utauona (Makongoro).
Zitto, kamtaja Masha, Ahhh, sawa hiyo? Ahha!!
Hiyo Si Sawa kwa Mengi, Kaowa Mnyarwanda.
Dereva kalewa gongo, ahhh sawa hiyoo? Ahha ......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom