Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 3, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 3, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi amekutana na waandishi wa habari na kusema mambo mengi na baadaye kutoa tamko lifuatalo.


  TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI


  Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

  Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

  Nilitegemea waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi. Angalao angefahamu kwamba anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na siyo mmiliki wa vyombo vya habari.

  Kama mkiristo na kama alivyoagiza Bwana Yesu namsamehe kwa vile hajui atendalo. Baada ya kumsamehe ningetaka ajue yafuatayo.

  Asiyekemea maovu katika jamii, yeye ni sehemu ya maovu hayo. Waziri huyu na wale wote ambao wamekwishanitumia vitisho wakumbuke kwamba hata kama watafanikiwa kuvinyamazisha kwa hujuma zozote zile, vyombo vyangu vya habari, na hata kama mimi sitakuwepo tena, moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za wanajamii hauwezi kuzimika kamwe.

  Ieleweke pia kwamba sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi. Vyombo vya habari husaidia kupaaza sauti na vilio vyao katika vita dhidi ya maovu. Ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

  Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na Serikali yake dhidi ya ufisadi. Sisi sote ni lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribio makubwa.




  ____________________
  Reginald A. Mengi
  Mwenyekiti Mtendaji
  IPP Limited
  3 Desemba,2008

  NB: (Restored)NB: Vyanzo mbalimbali vimeihakikishia KLHN kuwa Waziri huyo ni yule mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya nchi. Vyanzo hivyo toka kwenye Jumba letu Kuu vimeihakikishia KLHN kuwa siku za hivi karibuni Waziri huyo amekuwa akijikuta akitajwa na vyombo mbalimbali vya habari na vile vya udaku wa mtandaoni akihusishwa na tabia mbalimbali ambazo kwa mujibu wa Jumba hilo vinaiweka vibaya sura ya uongozi wa Taifa.

  Kuna uwezekano mkubwa katika mabadiliko madogo ya Mawaziri ambayo yanatarajiwa wakati wowote Waziri huyo akatemwa.
   
  Last edited by a moderator: Dec 7, 2008
 2. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #2
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Ni waziri yupi huyo?
   
 3. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu MMJJ kwa taarifa. Mjumbe hauawi
  Huyo waziri kijana wa wizara nyeti ni nani?
   
 4. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti "

  Mzee wa kijijini na wakuu wengine, kwa hekima zenu mnaweza kutusaidia sisi vilaza kufumbua hilo fumbo hapo juu?

  Natanguliza shukrani.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hivi Masha naye anaweza kuwa anaropoka mambo bila kutumia akili?
   
 6. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mkuu kama unaelekea elekea... panaponitatiza kodi na masha wanaingilianaje?
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nilivyoelewa ni kuwa yeye alitoa pendekezo kwa wenzake (walanchi) namna ya kukabili vyombo vya habari vinavyopiga kelele: kata kichwa cha nyoka kwa kutumia upanga wa kodi.
   
 8. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Katika yote,

  Nimependa hii aliyosema hapa Mzee Mengi.

  Kuna juhudi kubwa sana zinafanyika kuzima upinzani na kuzima wana harakati wa kupambana na ufisadi Tanzania. Ukweli utabaki pale pale, huu moto hakuna yeyote anayeweza kuuzima.

  Hata wakiifunga mwanahalisi, wafukuze memba machachari JF (au waifunge JF kabisa), wafunge magazeti ya thisday na kulikoni (ya Mengi) bado tu kuna sehemu tutatokea na kuhakikisha mafisadi wanaoongozwa na Manji akifuatiwa na mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata (rostam azizi) wamefikishwa keko.
   
 9. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MJJ
  Nimekuwa nikitatizwa sana na utendaji wa huyu Masha. Nimesema sitashangaa tena vitendo vyake vya ajabu kwani vinajitosheleza. Wanasema ukitaka kujua tabia ya binadamu mpe madaraka ama fweza. Nahifadhi homoni zangu za kushangaa for other pertinent issues, let me take a break ggggggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!1
   
 10. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Masha yani miaka miwili yatari kashainga in the system deep?? dah..nyota yake itazima sasa.................nishai kweli...
   
 11. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Yule ni mmoja wa vilaza wakubwa kabisa. Ni kilaza hafai. Lakini politics tatizo hazitabiriki. Mtu yoyote anaweza kuwa vyovyote kwenye siasa. Sasa kilaza kwenye mambo ya Ndani?!
   
 12. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yote haya yanadhihirisha utendaji kazi wa Kikwete. Anajali urafiki kuliko nchi. NO wonder marafiki wake wa karibu (wana mtandao) bado wanapeta mtaani huku akijisifia kuwa anashughulikia mafisadi.
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mengi acha udaku!

  Kama ni kweli ongea kwa kujiamini!
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Watu walitegemea Masha Msomi kijana ametoka NYC atakuja kuweka mambo yaende kisasa, ameshindwa. Kama hizi habari ni kweli (who know with Tanzanian real-politik) basi Masha zaidi ya kushindwa, amedidimia kabisa katika lindi la ufisadi.Tunasubiri tu washkaji zake wazee wa datazz waje kumtetea hapa, watatetea sana mwaka huu lakini hili ni sinking ship kama Titanic.

  Na huyo Mengi naye kujifanya mstari wa mbele ananunua popularity kwa bei rahisi tu hana lolote.
   
 15. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  tafsiri yako ya kujiamini ni ipi?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Dec 3, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Raisi kilaza anateua watu vilaza....kuna Emannuel Nchimbi, huyu Masha, Raisi mwenyewe, na wengineo......
   
 17. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapo ndipo Mengi anapotofautiana sana na watanzania wengi! Yuko tayari kugombana na yeyote anayemgusa! With all his 'weaknesses' nadhani huyu kwenye vita ya ufisadi ni one of the leaders - we cannot ask for more from this one person.

  Kwa upande wa waziri - this is the problem ya kuwatunukia watu uwaziri bila kuwafahamu (vet) vizuri! Kila siku JK ataishia kukuna kichwa! - Still learning how to pick the right people for ministers! Kazi tunayo!
   
 18. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuhani ur clearly unfamiliar with the law of libel it seems.

  K, Attorney At Law.
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...huyo Masha kishalewa na kawa mjinga tuu hana lolote,juzi kaenda magereza kufanya ufisadi tuu,wizara yake ndio inaongoza kwa rushwa na huduma mbovu,nilitegemea angefanya improvement kubwa sana kwenye wizara yake especially kwenye IT lakini ni upuuzi mtupu..nasikia kazi yake wanawake tuu na ujiko wa kijinga jinga!
   
 20. m

  mkama Member

  #20
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama si masha ni adam malima.adam anahusishwa na mikakati mingi ya kummaliza mengi kwa kutumia propaganda za siasa na dini
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...