Hebu Tujadili Hatua (kama zipo) ambazo Waziri Masha anaweza kumchukulia Mengi kama alivyoahidi bila kuvunja sheria.
Mimi naona moja au mbili tu...kumtegea Gazeti lake lichemke kisha walifungie...
Yebo Yebo
Masha hahitaji kumtega Mengi na magazeti yake. Ameshasema ameharibu tayari kwa kutumia vyombo vyake vya habari kuleta hatari.
Hilo jambo nadhani tumelikosa katika huu mtafaruku mzima, kwa sababu, kwanza, wamali wa Waziri walikuwa wanatupurukusa, wanatu distract, kwa kusema tumshukuru kwa kurudi nchini kututumikia. Hilo nadhani tumelijibu, tumelimaliza. Lakini sababu nyingine ya kupurukuswa na kushindwa kuangalia vina vingine vya sakata hili ni kwamba sidhani kama tulikuchunguza sana kilichotamkwa na Masha hasa hasa:
``Hizi ni tuhuma nzito...Unapoituhumu serikali na unapomtuhumu waziri, ni lazima uwe na uthibitisho….Siyo tu aendelee kueleza hivi hivi tu, aje na amseme waziri huyo ni nani; na aje na ushahidi. Asipothibitisha tutamchukulia hatua.´´
``...Uhuru wa vyombo vya habari si kuvitumia kutangaza vitu ambavyo vinaleta athari katika jamii, hivyo tutaliangalia suala hilo na mimi kama waziri ninayesimamia usalama ndani ya nchi, ninawajibika moja kwa moja katika jambo hili´´
``…Asipoleta ushahidi wake ndani ya siku saba, serikali ina wanasheria wake, watapitia sheria zinasemaje ili ichukue mkondo wake hawezi kutoa madai mazito eti kwa vile ana vyombo vya habari, ni hatari...´´
``...Asitumie vyombo vya habari kutoa tuhuma kwa serikali. Ni kweli serikali inatambua kuwa kuna uhuru wa vyombo vya habari, ingawa uhuru hauna budi kutumiwa ipasavyo na si kutoa taarifa zisizo sahihi. Hii ni serikali si serikali ya kuifanyia mchezo.´´
``…Kama ni kweli Mengi ametumiwa ujumbe wa maneno ya kumtishia kuuawa, anatakiwa kuwa mkweli na muwazi huku akiwa na vithibitisho. ...madai yake ni mazito lakini kwa sababu ana ushahidi wa kuhujumiwa na waziri mmoja kijana, tutamuomba atupe ushahidi wa kuhujumiwa na waziri mmoja kijana, na leo namuandikia barua ili atulete.´´
Sasa, ukiweka pembeni utetezi ulioletwa na rafiki wa utotoni wa Waziri, wakitubeza tushukuru amerudi nyumbani kututumikia, na pia tukiahirisha maswali juu ya unyuma wa Waziri kuhusu alivyoweza kukwepa kujiunga JKT kabla ya chuo kikuu, tena akiwa na madarasa ya shule 10 badala ya 13 kama wengine, nadhani baadhi ya maswali na makamio dhidi ya hatua yake hii yana majibu ndani ya alichosema.
Kuna hili la Masha amemlenga Mengi kama nani, raia ? Utaona Masha kasema tatizo hapa ni kwamba mlengwa anatumia penyenye aliyonayo na vyombo vya habari kusema vitu vya kichochezi. Kwa hiyo Mengi hapa hajalengwa kama raia, na pia hapo hapo kuna jibu la swali la kosa ni nini hasa: uchochezi.
Hilo la kwanza na pili. La tatu ambalo limejibiwa hapo ni hili la usahihi wa nguvu yake kuhusika hapa: kasema usalama uko chini yake. Kwa hiyo maswali ya wakuu wengi hapa kwamba itakuwaje hawakuachiwa ma DPP na ma IGP na AG na wakuu wa tarafa na shina waongee hilo Masha kashasema usalama uko chini yake. Watume mkuu wa kituo au mkuu wa magereza, au mkuu wa kaya ya Wakwere, wote hawa ni eneo chini ya himaya ya usalama. Mkuu wa masuala ya usalama, kama alivyosema, ni yeye.
Kama ambavyo Mkuchika alichukua mikononi swala la uchochezi wa magazetini kama mkuu wa masuala ya uchapishaji habari, hapa Masha anachua mikononi swala la shutuma za kichochezi zinazohusiana na kutishia usalama wa raia yeye akiwa kama mkuu wa mambo ya usalama wa raia.
Kwa hiyo kosa ni uchochezi wa mwanahabari, mmiliki wa vyombo vya habari, Mengi. Kumbuka Mengi amechapisha matamko yake - hakunukuliwa na mwingine, na third party - yeye mwenyewe amechapisha, ametoa tamko ndani ya gazeti lake.
Hivyo ndivyo Masha atakavyomshitaki
mchapishaji Mengi, nadhani. Hatahitaji kumtega tena.