Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Field Marshall Es,
Sidhani kama Mengi alimtishia kiongozi isipokuwa alisema yeye ndiye anayetishiwa...(nitarudi kusoma) lakini mkuu, Masha kwa kila jinsi amekiuka sheria mwenyewe na wala sio swala la Mengi ambaye hakumtaja Masha kwa jina..
Kilichotokea ni wasiwasi ya Msha kufahamu kwamba aliyoyasema yamefika tena kwa mtu mwenye vyombo vya habari.. kusema kweli inatisha kwa kiongozi yeyote..Sasa tofauti inakuja tu pale kionmgozi huyo atakavyopokea lawama kama hizi na Masha kachemsha, kakurupuka na joho lake la uwaziri na kama angefanya alivyosema mwishoni kutaka kumsaidia Mengi angepeleka askari kumhoji kwa madhumuni ya kumlinda na sio kutoa majibu ktk vyombo vya habari ukitaka ushahidi within 7days wakati hufahamu hatari aliyokuwepo Mengi.
Sisi wote watoto wa mjini tunafahamu kilichotokea na Masha hawezi kutumia fimbo ya Uwaziri kujisafisha isipokuwa haya ni maswala ya mjini kutishana na kama kawaida ya wazee wetu wanafahamu kuwa ukitishiwa maisha kuwa wa kwanza kupiga mayowe!.. Hata simba hukimbia!

- Mkuu Bob, hapa, kwangu kuna a big picture ya Mengi kuruhusiwa kutishia wananchi na viongozi wa serikali kwa sababu ya vyombo vyake vya media, we can't do that, ndio maana ninasema kua hii ishu sasa imefika inapotakiwa sasa iachwe iende kwenye sheria, waziri amesema kama usahidi uko wazi kuwa ni yeye mwenye tatizo yuko radhi kujiuzulu, sasa hizi hukumu mnazitoa wapi kuwa kachemsha tu na Mengi ndiiye malaika hapa I do not get it?

- I mean Mengi amepataje nyaraka za siri za serikali, amepataje huu ushahidi sasa sheria itakposhika meno mtaanza kusema Mengi anaonewa, kujuana na muungwana sio sababu ya kufanya unayotaka tunataka sheria, that is a lesson kutoka Lowassa, yakifikia shingoni anakutosa, sasa acheni sheria ije ichukue mkondo wake au?

Lakini kwamba Masha kachemsha na the rest of the story I do not buy it! Anyways, sasa ni saa ya kulala naomba ku-retire.

Thanxs!
 
Masha amechemsha. Waziri hapaswi kutoa vitisho hadharani kwa raia( au mkazi yeyote halali) wa nchi yake. Vitisho vinajumuisha kumpa ultimatum ya kutoa ushahidi wa shutuma zake. Wanaomtetea are not doing him any favours. A-apologise na aache polisi waendelee na uchunguzi wao.

Personal life ya waziri Masha inaingizwa kwa sababu watetezi wake hawachelei kutuambia kuwa ametufanyia favour sana kuacha a bright future marekani na kurudi kuwa Company Secretary wa kampuni ya serikali, partner katika a prominent lawa firm na hatimaye waziri katika serikali. Hii ukilinganisha na umeneja wa amusement park ( ambao hata yeye hauweki katika official c.v. yake), offer ya kazi ( bila kuambiwa ni kazi ipi) ya Benki ya Dunia na kupasi mtihani wa ku-practise kama criminal lawyer ( maneno yangu) New York. Kwa wengine wetu yeye ndiye anayebidi kushukuru kupata opportunities alizozipata na kutumikia raia wenzake kwa uadilifu na heshima kubwa. Kwa bahati mbaya hii hajaionyesha hadi sasa. Wanaomshauri, wamwambie wakati uliobaki ni mfupi. Wizara aliyonayo ni nyeti na ajikite katika kuleta tofauti katika maisha ya mtu wa kawaida (mazeluzelu, wananchi wanaohofia vibaka, hali ya magereza n.k.) aishie Tanzania. Akifanya hivyo badala ya kuendeleza malumbano yasiyo na maana, jamii itamshukuru na kumuenzi. A little humility is in order.
 
Kuwa naye ndio nini, tehe tehe...eti nilimpeleka airport, so what? Unachekesha kweli wewe.
Sasa kwa taarifa yako, haya maneno yametoka kwake Masha mwenyewe. Obviously uhusiano wenu(if any) ulikuwa ndio huo wa wewe kumuendesha kumpeleka kwenye mitihani, playground, na airport...lakini vitu kama hivi alikuwa hakuelezi. Sasa ndio nakupa, Masha alirudi Tanzania kwasababu hakupata kazi wala prospects katika field yake! Habari ndo hiyo!

Kisura unatisha! Kwa hiyo tulikuwa tunadanganywa siku zote? Hakuna cha 'offer' wala nini! Iko kazi.
 
Field Marshall Es,
Mkuu bado unapoteza sheria hapa. Mengi amesema kuwa kuna kiongozi Kijana ana mpango wa kummliza kiuchumi.. Hakusema jina la mtu na Masha kakurupuka tena basi sio kisheria kwa kumfuata mhusika ila naye kenda ktk vyombo vya habari kuweka madai yake dhidi ya mengi akijitaja yeye mwenyewe kama mhusika.
Haya yaliyoajiri leo (jana) ya kupatikana kwa ushaidi yamekuja baada ya Zitto pia kusema tena kamtaja jina lake lakini ajabu ni kwamba Zitto aliyetaja jina hakuambiwa siku saba.
Mengi kaam raia ana kila haki ya kuzungumza malalamiko yake kuhusiana na kiongozi, utawala ama mtu binafsi anayekusudia kumfanyia mabaya na wizara ya mambo ya ndani ni kazi yao kufanya uchunguzi wa madai hayo.. Huhitaji ushahidi mkuu kwa sababu wewe ni victim mtarajiwa..
Kwa hiyo unakuwa protected kwanza kisha unaulizwa kama unataka kufungua mashtaka na hapo ndipo statement na ushahidi wako unapoweza kuombwa lakini kama hutaki kushtaki ama hakuna tishio hilo Polisi hawana haja ya kujhoji zaidi..
Mkuu nimekupa hoja za Obama na Lou Dobbs ambaye alifikia hata kusema ndani ya kipindi chake akisema Obama hajui yeye ni nani?.. who's got the Mike akiwa na maana yeye Lou Dobbs anaweza kummaliza Obama.. Obama alifuta vumbi mabegani akaendelea na kampeni zake. Kuna habari ya shangazi yake Obama ilivuma pia na ushahidi ulikuwepo ESPN lakini sikuona serikali ya Marekani wakidai ESPN waulete ushahidi laa sivyo watafungiwa ama kuona cha mtema moto.. Huyu ni mtu anayegombea Urais wa Marekani mkuu iwe leo Lau Masha waziri wa kuteuliwa! Hiyo nguvu kaipata wapi..
Kisheria Mengi halazimiki kutoa ushahidi unless kaenda mbele ya sheria kutaka kumshitaki huyo waziri..nje ya hapo masha kachemsha!..
 
Kisura,
Samahani bibie sasa hizi ni habari za jikoni, siye wanaume tupo barazani.. Masha kurudi TZ tayari janvi lilikwisha wekwa.. JK alijua nani anakuja baada ya kupewa info za kijana huyu na wala sio bahati mbaya kwamba kakosa kazi US..
Marekani huwezi kukosa kazi ukiwa na elimu kama yake..Hii sio Bongo kazi za kukamatana mashati, kwa mkosi gani alokuwa nao kukosa kazi Marekani - jaribu kufikiria...
 
Hapana...Lazima tujuwe kwanza hizo ajira zao zilizopita maana ni muhimu.
Ni lazima tuwe tunajifunza kukinga badala ya kusubiria kutibu tu...Sasa kama kila mtu anashangazwa na uwezo wa kufikiri wa Mh huyo...Then huwezi kushangazwa pale watu wanapojaribu kujiuliza...Kwanza tumefikaje hapa tulipo?

Meku,

well, kujua ajira zao zilizopita ni muhimu lakini kwa sasa ni a bit late. Hii ni kazi ya vijana wa JK walitakiwa wamvet kila kiongozi. Jibu zuri kwa swali la "tumefikaje hapa tulipo" ni kuwa hatuna uongozi mzuri; hatuna utaratibu mzuri wa kuchagua na kuteua viongozi
 
Katika thread hii nilikuwa na interest sana ya kujadili na kujifunza namna ya kudhibiti viongozi wanaoutumia madaraka yao kuwatishia raia, na vile vile namna ya kuwadhibiti raia wanaotumia utajiri wao kuzungumza lolote. Hata hivyo thread hii imeonekana kujaa upuuzi zaidi ya mada yenyewe na sasa hivi imekuwa inaboa sana.
 
Imeshakuwa taabu haya turudi kwa Mengi pia,
Nasikia kuwa mali yote sio yake kawekwa tu kama kina Manji kushika mali ya wakubwa (vigogo)waliowekesha IPP..


Manji tena, Mungu wangu...jua litachomozea magharibi.
 
Katika thread hii nilikuwa na interest sana ya kujadili na kujifunza namna ya kudhibiti viongozi wanaoutumia madaraka yao kuwatishia raia, na vile vile namna ya kuwadhibiti raia wanaotumia utajiri wao kuzungumza lolote. Hata hivyo thread hii imeonekana kujaa upuuzi zaidi ya mada yenyewe na sasa hivi imekuwa inaboa sana.

Niliyatabiri haya Ijumaa hii iliyopita.....
 
Kuna habari kama hii iliyowekwa kwenye website ya Ipp, ambayo kwa ushauri wangu ilibidi Mhe Masha ndio ilibidi azitoe ili aonekane anafanya kazi na mambo ambayo wanamlaumu aonekane anayafuatilia, Maana sasa hivi anaandamwa na negative vibes, inabidi afanye kitu +ve au mambo mengine, hiyo ya kutoa siku saba alichemka kwa kweli, utadhani alikuwa anasoma hapa JF na kuona kama watu wanaandika sanaa na kuja na jazba. Ilibidi atulie asikilizie na kuendelea kufanya kazi na kutoa habari kama hizi badala ya kuja na kuanza kutoa siku saba kama alikuwa anasoma "kitabu kilichoandikwa na Mrema".
Kuhusu suala la Mengi kasema nini angewaambia waandishi wa habari Mengi angepeleka madai yake polisi na sio kuongea tuu, kwa sababu yeye sio mtu wa kwanza kutishiwa na watu wote waliotishiwa wamepeleka malalamiko yao kunakohusika. anyways ni mawazo yangu tuu.
"Waua albino kibao wadakwa
2008-12-06 16:34:11
Na Badru Kimwaga, Jijini


Zaidi ya watu 57 wakiwemo waganga wa jadi na wafanyabiashara wa madini na uvuvi wamenaswa na kufunguliwa mashtaka kuhusiana na tuhuma za kuhusika na mauaji ya albino katika maeneo tofauti nchini.

Watuhumiwa hao wamedakwa katika jumla ya mikoa sita baada ya polisi kufanya msako mkali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo.

Mdhibiti Mkuu wa kitengo cha makosa dhidi ya wanadamu, Bi. Sidney Mkumbi, ametoa taarifa hiyo jana kupitia kipindi cha `Kipima Joto` kilichorushwa `live` na kituo cha ITV jana.

Akadai wengi wa watuhumiwa hao wanatoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Bi. Mkumbi amesema watuhumiwa hao wakiwemo wafanyabiashara ya uvuvi, madini na wengine wanaosaka utajiri kwa nguvu za giza, wamedakwa katika mikoa inayosifika kwa mauaji ya aina hiyo ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kigoma, Kagera na Mbeya.

``Watu wengi wanadhani sisi hatufanyi kazi dhidi ya matukio haya ya kikatili, juhudi zipo na mafanikio yake ni kukamatwa kwa watu zaidi ya 57 wakiwemo wafanyabiashara 13 miongoni mwao watano walikutwa na viungo vya binadamu amabvyo bado havijathibitishwa kama ni vya maalbino au la,`` amesema.

Akiungwa mkono na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Peter Kivuyo na msemaji wa jeshi la polisi nchini, Bw. Abdallah Msika, Bi. Mkumbi amesema jeshi lao liko bize katika kuhakikisha mauaji ya maalbino yanakoma nchini na kwamba sasa, wameongeza nguvu kwa kufanya upelelezi wao kimyakimya ili kutowastua wengine.

Makamanda hao wa Polisi wakasema jambo la muhimu ni kwa kila mmoja kuwa tayari kushirikiana na jeshi lao kwa kuwapa taarifa zitakazowasaidia katika kuwanasa wauaji hao.

SOURCE: Alasiri
 
Mbunge machachari wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe amemtolea uvivu Waziri Masha katika sakata kati ya Masha na Mengi. Kwa habari zaidi soma Nipashe hapa chini.

Zitto apasua jina la waziri kijana

2008-12-07 13:37:18
Na Mwandishi Wetu


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ana ushahidi kuwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ndiye aliyepeleka hoja ya kumhujumu Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi katika vikao vya juu na kwamba taarifa hizo alithibitisha kuzipata jana.

Akiongea na Nipashe Jumapili jana, Zitto alisema waziri huyo, kwa taarifa alizonazo za kuaminika, alitoa hoja kuwa vyombo vya habari vya IPP vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na hii inailetea matatizo serikali.

Hivyo, aliomba serikali ipange mikakati ya kumfilisi Mengi, kitendo ambacho kitasababisha kudhoofishwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vitashindwa kuendelea kuupinga ufisadi.

Zitto alisema yeye hana sababu ya kumtetea Mengi ila hawezi kunyamaza kuona Mtanzania anayeipenda nchi yake na kulazimika kupinga ufisadi anafanyiwa hujuma.

Aidha, Zitto aliliambia Nipashe Jumapili kwamba, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kuanika maovu ya ufisadi na vyombo hivyo lazima vilindwe na Watanzania wote wazalendo.

Akijibu hoja ya Mengi iliyotolewa jana kuwa yupo tayari kutupwa jela ikithibitishwa kuwa amedanganya na kumwomba Masha pia aseme kama atakuwa tayari kujiuzulu iwapo ukweli wa maneno ya Mengi yatathibitishwa, Masha aliliambia Nipashe Jumapili kuwa hawezi kujiuzulu kwa sababu nia yake ya kuwaagiza polisi kufanya uchunguzi ni kumlinda Mengi.

Alisema kutokana na taarifa ambayo Mengi aliipeleka kituo cha polisi cha Oysterbay, polisi wameamua kuifanyia uchunguzi ili kuhakikisha maisha yake yanakuwa salama.

``Nia ya serikali ya kuchunguza tuhuma zilizotolewa na Mengi ni kuhakikisha kuwa tunamlinda,`` alisema Masha na kuongeza kuwa hana tatizo na maneno yaliyotolewa na Zitto ili mradi awe na ushahidi.

Amesema, hata kama hawamuamini, basi waupeleke huo ushahidi kwa Rais au Waziri Mkuu kuuonyesha na kama ikibainika kama ni kweli yeye ndiye anayemhujumu Mengi, basi atajiuzulu.

Akasema kuwa yeye hakusema kuwa atamshughulikia Mengi kama alivyonukuliwa kwenye baadhi ya magazeti ila alisema kuwa sheria itachukua mkondo wake kama ikibainika kuwa tuhuma zilizotolewa ni za kweli.

Akiongea na TBC1 juzi, waziri Masha, alisema kuwa kama Mengi ana ushahidi wa tuhuma alizotoa, serikali haitapata shida ya kuhangaika na ushahidi na imemtaka apeleke ushahidi huo.

Kuibuka kwa sakata hilo kunatokana na Mengi kumtuhumu waziri mmoja kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

Alimtuhumu waziri huyo kuwa amekuwa akimtumia ujumbe wa vitisho kutokana na vyombo vyake vya habari kuwa mstari wa mbele katika kupigia kelele ufisadi.

Akifungua kongamano la kuwajengea uwezo vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa vijana wa chama hicho, John Mnyika, aliwataka vijana kuendeleza vita ya ufisadi na kutokatishwa tamaa na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Aliwakumbusha vijana kuwa ni wajibu wao kupigania haki zao kwa manufaa ya taifa na kwamba wanapaswa kukosoana pindi mwenzao anapofanya vibaya.

``Kwa maoni yangu naona kama kauli ya Masha ya kumtaka Mengi awasilishe ushahidi ndani ya siku saba ni ya kukurupuka kwa kuwa mbona nilipotuhumiwa na Mtikila kwamba nimeshiriki kumuua Chacha Wangwe hakusema lolote hadi leo?

Tunashangazwa sana na kauli ya Masha, tulidhani labda angechunguza kwanza kabla hajazungumza na katika hili nawaomba vijana muwe makini na vijana kama hawa na muwakosoe waziwazi,`` alisema.

Alionya kuwa iwapo vijana hawatakosoana jamii itapoteza imani juu ya utendaji wao na kuondoa matumaini ya taifa kuhusu umuhimu wa vijana.

Hata hivyo,alisema vita dhidi ya ufisadi bado ni kubwa kwa kuwa ni asilimia 10 tu imetekelezwa.

``Msibweteke na ushindi huu, ufisadi unaozungumziwa ni wa utawala wa Mkapa, katika awamu ya nne kuna ufisadi kama wa Richmond na Buzwagi kwa hiyo tunapaswa kupambana zaidi,`` alisema.

SOURCE: Nipashe

Hapa kuna utamu kweli kweli. This time Masha hana jinsi hata kama akikauka kama Kambale lazima aachie UTAJO/UTAMU wa uwaziri arudi kule kunako mfaa IMMA.
 
Hivi Masha kweli ni msomi mahili wa sheria ? Mbona hata hivyo kama kiongozi anaonekana kuwa mtu wa majigambo na fitina kibao ? Sasa naanza kuunganisha mistari hapa na tukio la Kubenea.Matamshi yake mbele yangu juu ya Kubenea na leo kwenye sakata hili la Mengi na jinsi alivyo kuja na siku saba nadhani kijana kalewa madaraka kabla hayajamkaa vyema .
 
Nakumbuka nilisema hapa kuhusu huyu masha kujumlisha JK kujumlisha Ridhiwani kujumlsha degree zake za hapa US. Then wengine mksemaa ooohh hatumpendi Masha... EPA jumlisha IMMA sawa sawa na nini?

Mzee FM Field Marshall Upo hapo kaka? Tuliongea sana utendaji wa huyu bwana wakati tunauliza kuhusu yeye kulitishia gazeti mmoja kwamba atalipeleka mahakamani sababu gazeti ilo lilidai kwamba kupewa kwake kazi ni free lunch sababu ya Ridhiwani.

Mimi binafsi nilisema kiongozi huyu kijana ambae hajui kitu kuhusu Public service siwezi kumlaumu mpaka nione atakavyo fanya kazi. Now the blue litimus paper has turned red. Sidhani kama bwana FMES unaweza kumtetea huyu bwana tena. I think hii imeonyesha poor judgement kwake, imeonyesha kiwango kikubwa cha ujinga na mwisho ni aibu kwa vijana wote sababu anachofanya Masha kilitakiwa kifanywe na kingunge.

Now I smell rat kuhusu EPA & IMMA. Mwanzoni mwa mwaka nilisema labda IMMA haiusiki na EPA. I need to recall that statement.
Kwa kuangalia mjadala uliopita unaweza kucheki hapa https://www.jamiiforums.com/habari-...es-link-jakaya-kikwetes-son-5.html#post153010
hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka.
 
Labda tupate picha, je ukiacha maendeleo yake binafsi, amewasaidiaje ndugu zake wengine kupata maendeleo kupitia mafanikio yake kibiashara kabla hata hajausaidia umma wa Tanzania?

- Mkuu kama hili ni valid basi Tanzania hatuna uongozi kabisa, maana hivi kweli unasema viongozi wote tulionao toka Mwalimu wamewahi kuwasaidia ndugu zao kwanza kabla ya taifa na wananchi wake?
 
Marekani unaweza kukosa kazi unayotaka hata kama una elimu ipi! Kinachoangaliwa zaidi si elimu tu bali ni ulifanyia nini elimu yako baada ya kuhitimu. Umeneja wa amusement park haukuhakikishii kazi katika Benki ya Dunia.

- Lakini ukamuhakikishia uwaziri Tanzania, sasa tofauti iko wapi?
 
Hivi Masha naye anaweza kuwa anaropoka mambo bila kutumia akili?

Bado mtoto huyo. Kabemendwa na mama wa kichagga huyo. Akili aipate wapi. Tunamsubiri mtaani. Huenda mkulu asimtake tena. Hafikirii kabisa huyu, si alienda kujipendekeza kwa Mramba na Yona kule keko labda akitemwa wanaweza kumpa kibarua! Taabu tupu.
 
FMES amesema Masha aliacha kazi WB ndiyo akarudi nyumbani. Kwa kuelewa kwangu ni kwamba huyu bwana aliisha ajiriwa na WB aka-resign kazi hiyo ili arejee nyumbani. Tukumbuke kuwa ajira ( FMeS amesema kuwa " Lau tayari alikuwa na ajira") inaanza pale unaposaini mkataba na mwajiri wako na si pale unapoletewa barua ya kukubaliwa maombi yako!

Halafu chini yake FMeS anasema tena kuwa alikuwa anasubiri kupata Green card yake ili aweze kuanza kazi WB. Alipoipata hiyo Green card akaghairi na kuamua kurudi nyumbani! Hii si tu inapingana na maneno yake ya awali kuwa aliacha kazi bali inaongeza utata kwa kuonyesha kuwa kilichomzuia kuanza kazi WB kilikuwa ni kukosekana kwa Green Card. Wanaojua mambo ya WB wameshaonyesha kuwa hii haiwezekani maana hauhitaji Green Card kufanya kazi WB. Kwa hiyo kama alikubaliwa kazi WB angeweza kuanza mara moja bila kusubiri chochote. Kinachowezekana ni kuwa Masha alikosa kazi WB ( sio dhambi hili) lakini hakutaka kuwaambia wenzake ukweli huo kwa sababu zake binafsi (which is totally understable). Akatumia kisingizio cha Green Card nao wakamwamini.

Alichotusaidia Kisura ni kuondoa lile pazia la ukaribu na kusema kuwa haya yote si ya kweli na ameyasikia kutoka kwa mhusika mwenyewe. Sasa ni juu yako kumuamini Kisura au FMeS kwenye ishu hii. Mimi namwamini Kisura kwa sababu nilizoziainisha hapo juu. Simjui Kisura kama vile nisivyomjua FMeS kwa hiyo hata kwake yeye siwezi ku-vouch kuwa kweli aliwahi kumsikia Masha akizungumzia suala hili. Kwangu mimi, alichokisema ni more probable kuliko alichokisema FMeS.

Wengine wetu tumechoka kuambiwa kuwa inabidi tuwanyenyekee wote wanaotoka majuu kwa sababu wametufanyia fadhila kwa kurudi nyumbani. Wote wapimwe kwa utendaji wao hapo walipo na si kwa madigiri yao, kiingereza chao, ukoo waliotoka, nchi walizowahi kuishi au kazi walizowahi kufanya. Kutetea udhaifu wao kwa kutumia vigezo hivi ni kututukana sisi watanzania. Wakati wa kushukuru kulishwa makombo umepita!

- At best irrelevant na chuki pamoja na wivu, nothing new kwa wale tunaelewa vizuri.

Anyways naona hakuna hoja ya msingi tena kuhusu ishu ya Mengi na Waziri, kwa hiyo wakuu naomba ku-retire unless kuna hoja ya msingi kuhusu the ishu, otherwise naamini nimesema ya kutosha kuhusu Lau, tena as much as I know mengi sikusema kuheshimu privacy yake, lakini bado nina heshima naye kama kiongozi na ninategemea kuwa anayoyafanya yote katika hii ishu na mwananchi Mengi, yako ndani ya sheria, Mengi pia nina mheshimu sana lakini sikuabliani kabisa na njia aliyoitumia katika hili tatizo lake na serikali, mwisho ni matumaini yangu kwua sheria iatchukua mkondo wake.

Michango ilikuwa mizuri kama kawaida huwa sina tatizo kusimama upande mmoja peke yangu, badala ya kufuata upepo tu, kwa kushinikizwa na chuki pamoja na wivu usiokuwa na msingi hapana, ukeli ni lazima usemwe hata kama upande wa pili una wengi kuliko ukweli na at any cost.

thanxs wakuu sasa saaa ya kazi, yaani kibaruani, labda tukutane next debate othersiwe unless kuna points za muhimu tutajibu ikibidi..
 
- At best irrelevant na chuki pamoja na wivu, nothing new kwa wale tunaelewa vizuri.

Mkubwa FMES nadhani katika kipindi hiki tete cha kupigana na Ufasadi, Mr Masha ameonyesha poor Judgement, unprofessional na hali ya kutisha. Kwanza kwa nini awe ana run undergraund movement ya kuzima vyombo vya habari?

Mwanzo nilitetea sana swala la Masha na EPA nikasema hata kama IMMA imefanya kazi na wezi wa EPA then inaweza kuwa ilifanya hivyo bila kujua. Lakini sasa pua zangu zinanusa harufu ya panya aliyekufa.......

Mzee FMES huoni kama kuna jinamizi nyuma ya carten?
 
Mkubwa FMES nadhani katika kipindi hiki tete cha kupigana na Ufasadi, Mr Masha ameonyesha poor Judgement, unprofessional na hali ya kutisha. Kwanza kwa nini awe ana run undergraund movement ya kuzima vyombo vya habari?

Mwanzo nilitetea sana swala la Masha na EPA nikasema hata kama IMMA imefanya kazi na wezi wa EPA then inaweza kuwa ilifanya hivyo bila kujua. Lakini sasa pua zangu zinanusa harufu ya panya aliyekufa.......

Mzee FMES huoni kama kuna jinamizi nyuma ya carten?

- Huu ni mtizamo wako tu lakini sio lazima uwe ukweli, maana na mimi nina mtizamo wangu na sio lazima uwe ukweli.

Kuna viongozi wengi wanaosubiri kwenda kwenye sheria kuhusu EPA Lau sio mmojawao, na EPA kumbuka haikuanza leo ilianza toka enzi za Mwalimu ila kwa njia tofauti na hizi za juzi, lakini in the end hela za taifa zilichukuliwa bila idhini yetu wananchi, kwa maneno mengine umekwua ni wizi tu siku zote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom