Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Halafu nani anasema Mzee Ndesamburo Muongo??.Na bado kila kitu kitakuwa wazi,Hivi Bwana Spika amesikia haya Mahojiano?Mzee Ndesamburo usiwe muoga,sema kila kitu ili ukweli ufahamike!.Na tuwaachie Wadanganyika waamue nani mkweli!.Hii issue ndogo tu ya Ugomvi wa kitoto wa Malima vs Mengi tunadanganywa, vipi yale Makubwa ya Richmond na BAE?
 
SAKATA LA NDESAMBURO
CHADEMA yaamua kumgeukia Lowassa
.Yamtaka atoe tamko la kukubali au la
.Serikali yakaa kimya, yamsubiri Mengi

Na Tamali Vulu, Tanzania Daima
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemwandikia barua Waziri Mkuu, Edward Lowassa , kikimtaka atoe tamko kuhusu kuhusishwa kwenye tuhuma za rushwa kwa wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge zilizotolewa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Barua ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbroad Slaa ya Januari 15,2006, kwenda kwa Lowassa, inaeleza kushangazwa na ukimya wake pamoja na tuhuma hizo nzito zilizotolewa na Ndesamburo.

Taarifa ya uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu zinaeleza kwamba , barua hiyo imeshafika katika meza ya kiongozi huyo wa tatu kimamlaka serikalini, baada ya Rais na Makamu wa Rais.

Hata hivyo jitihada za gazeti hili kuwasiliana ama na Lowassa mwenyewe au mwandishi wake wa habari, Said Nguba ili kupata maoni yake kuhusu swala hili, zimekuwa zikigonga ukuta kwa takribani wiki moja sasa tangu Ndesamburo alipotoa tuhuma nzito wiki iliyopita, sambamba na Kutangaza kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Ofisa mmoja wa juu serikalini aliyezungumuza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa jina, alisema Waziri Mkuu amekaririwa akiyaeleza maneno hayo ya Ndesamburo kuwa yasiyo na ukweli wowote.

Alipotakiwa na Tanzania Daima aeleze hatua ambazo Lowassa amepanga kuzichukua dhidi ya suala hilo ambalo kauli yake inahusishwa, ofisa huyo alisema, vyombo vinavyohusika vitalishughulikia.

“Sisi tunajua ni kwa nini Ndesamburo kasema maneno hayo, Tunajua kila kitu kinachoendelea kuhusu jambo hili. Ni vyema tukanyamaza. Waziri Mkuu anajua anachofanya, hawezi akasema maneno ya namna hiyo. Ipo siku ukweli utabainika,” alisema ofisa huyo wa serikali.

Baada yake, ofisa huyo wa Serikali alieleza pia kushangazwa kwake na ukimya wa Mengi ambaye ndiye aliyetajwa na Ndesamburo kumwimbia maneno hayo kuendelea kukaa kimya pasipo kutamka hadharani, iwapo ni kweli alifikisha maneno hayo au la.

“Ninyi mnamtafuta Waziri Mkuu atoe tamko, mbona hatujasikia Mengi akisema hadharani ni kweli kuwa alimwambia Ndesamburo meneno haya? Si yuko na anapatikana mbona amekaa kimya?’’ alihoji ofisa huyo.

Slaa katika barua aliyomwandikia Lowasa anasema: “Pamoja na uzito wa tuhuma hizi na hasa ukizingatia uzito wa nafasi yako ya Uwaziri Mkuu mpaka sasa hujajitokeza wewe mwenyewe kukanusha au kukubali taarifa hii.

“Kwa vyovyote ukimya wako katika suala hili kadiri unayoendelea unaweza kuwafanya wananchi kupoteza imani kuhusu msimamo wako katika vita dhidi ya rushwa na jitihada za kuleta utawala bora nchini.

“Kama kweli wewe ulifahamu kuwa kuna mtu ametoa rushwa kwa wabunge na hukuchua hatua zinazostahili, kwa vyovyote ni kinyume cha sheria, maadili ya uongozi, na dhamira ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ya kupambana na rushwa bila kumfumbia macho mtu.

“Kwa upande mwingine, tuhuma kwamba mhimili wa serikali unaingilia mhimili wa Bunge zinakuelekea wewe (Waziri Mkuu) moja kwa moja kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Suala hili ni kinyume na utawala bora na mgawanyiko wa madaraka uliomo katika sheria na katika ya nchi ambayo umeapa kuilinda,” ilieleza sehemu ya barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge, Samwel Sitta.

Tayari Spika amemwandikia barua Ndesamburo akimtaka kumwandikia kwa maandishi tuhuma za rushwa alizozitoa dhidi ya kamati hiyo.

Wiki iliyopita, Ndesamburo alitangaza kujiuzulu ujumbe katika kamati hiyo ya madai kuwa alielezwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP, Reginald Mengi, kuwa aliambiwa na kiongozi mwandamizi wa serikalini kwamba, wajumbe wa kamati hiyo wamepewa rushwa kutoka kwa mfanyabiashara, Yusuf Manji, ili asitendewe haki kwenye kezi yake na Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima.

Ndesamburo alieleza kuwa anahofia usalama wa maisha yake na hataki kuhusika na maamuzi ambayo yanagubikwa na tuhuma za rushwa, huku akitaka kuitwa na Mengi na Mengi na kiongozi huyo ili kuthibitisha madai hayo.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Malima alimtuhumu Mengi kuwa kujipa muda mwingi kujitangaza kwenye matukio yanayomhusu huku akitoa muda mfupo katika matukio yanayomhusu Rais na Waziri Mkuu.

Kutokana na tuhuma hizo, Mengi alilalamika kwa Spika kuwa Malima hakumtendea haki kumtuhumu sehemu ambako hawezi kujitetea.

Baada ya malalamiko hayo , Spika alilipeleka mashauri hayo kujadiliwa kwenye kamati hiyo , hatua iliyozusha malalamiko kutoka kwa baadhi ya wabunge kuwa haikuwa haki.

Tayari Manji ameshatoa tamko kukanusha kuhusika kwa namna yoyote kuwapa rushwa wabunge na ametaka Ndesamburo aeleze kile ambacho alidai kinafichwa katika suala hilo zima.
 
•
...Wapinzani kuandamana Dar

Habari Zinazoshabihiana
• Mwanry akamia kumfuatilia Mbowe 10.01.2007 [Soma]
• Mbatia alia wabunge kulipwa mamilioni 17.10.2005 [Soma]
• Mbowe: Makamba hawezi kuua Upinzani 04.01.2007 [Soma]

*Kuzungumzia rada na fedha za mifuko ya hifadhi
*Waahidi kuanika ya Ndesamburo kujitoa kamati
Na Mwandishi Wetu
VYAMA vya siasa vya CUF, CHADEMA, TLP, UDP na NCCR-Mageuzi kwa kushirikiana na kambi ya upinzani bungeni, vimendaa maandamano na mkutano wa hadhara kesho.

Taarifa iliyotolewa jana na Bw. John Mnyika, ambaye ni
mjumbe wa Kamati ya maandalizi, ilisema maandamano hayo yataanzia Ubungo (mkabala na TRA/Ubungo Maji) kuanzia saa 5 asubuhi kupitia barabara ya Morogoro mpaka uwanja wa Jangwani na kufuatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara.

Lengo la maandamano hayo kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni kuunganisha nguvu ya umma kulaani walichodai ni ufisadi uliokithiri katika Serikali inayoongozwa kwa utawala mbovu na CCM, unaojitokeza katika nyanja mbalimbali ambao ni chimbuko la kuendelea kwa umaskini miongoni mwa Watanzania.

Ilisema maandamano hayo pia yatatoa ujumbe wa mshikamano kuunga mkono jitihada za wabunge wa upinzani za kukabiliana na vitendo vya rushwa
vinavyoendelea kufumbiwa macho na Serikali na tuhuma zingine za kuingiliwa kwa shughuli za Bunge.

Katika maandamano hayo, masuala yenye mazingira ya
rushwa kubwa yatawekwa wazi na athari zake kwa wananchi zitawekwa bayana ili Watanzania waweze
kuelewa athari za vitendo hivyo vya ufisadi kwa
mustakabali wa Taifa, ilisema taarifa.

Baadhi ya masuala yatakayozungumziwa ni kashfa ya
ununuzi wa rada, tuhuma ya rushwa kwa wabunge na
mhimili wa Serikali kuingilia Bunge kama ilivyoibuliwa
na Mbunge wa Moshi Vijijini, Bw. Philemon Ndesamburo na kashfa ya mikataba katika sekta ya nishati ikiwamo Richmond na IPTL.

Mambo mengine yatakayozungumziwa ni pamoja na
mazingira ya rushwa katika mikataba ya madini, ujenzi
wa jengo la gharama kubwa la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na matumizi ya fedha za mifuko ya hifadhi za jamii (NSSF/PSPF), nk.

Maandamano na mkutano huo wa hadhara vitaongozwa na
viongozi wakuu wa vyama na wabunge wa kambi ya
Upinzani.

"Tunawaomba Watanzania wote bila kujali itikadi, kufika
kwa wingi katika maandamano na mkutano huo ili kujua siri zilizomo katika masuala hayo na athari zake kwa maisha ya wananchi ya kila siku.

Katika mkutano huo maazimio maalumu yatafikiwa kuhusu mwelekeo wa kukabiliana na ufisadi nchini.


nafikiri kuna one of the member here alishauri kuwa wapinzani ndio muda wao sasa kuionyesha serikali makosa yake,one step ahead,je wataweza?????
 
mzee Ndesamburo,ulidhani unazima moto,kumbe ulikuwa ndio unaumwagilia petrol,je una semaje?kama kamati ilihongwa ina maana bunge limehongwa,na wewe ukaamua kwa mihasira yako kujitoa katika kamati,ambapo ungewaku ndani ya kamati unge stand better chance ya kutetea,kwa hoja ya ko ya kamati amabo ni bunge kuhongwa kwanini basi hata katika hilo bunge lenyewe usijiuzuru?kuonyesha kuwa bunge lenyewe wala rushwa?niliuliza siku moja je wewe mwenyewe katika kugombea ubenge huku honga?au katika hiyo kamati na wewe hukuvuta?Ushahidi wa tape upo acha zionyeshwe,ndipo utakapoona kuwa ni wazi kuwa ulikuwa unatetea kwa kutumia uchagga wako,wachagga ache kutugawa,wewe ndesamburo wakati Mengi anatoa kanda yake ya uongo wa kutumia dakika chake si ulikuwepo?Na Adam Malima alipoonyesha kanda ambayo ni the same na ya Ndesamburo si uliona?Ipi ilikuwa ya Uongo?Jibu ni kuwa ya Mengi ilifanyiwa EDITTING nyingi kupunguza muda,Mengi tukubali tusikubali anatumia vyombo vyake VIBAYAAAAAAA!!!
 
mzee Ndesamburo,ulidhani unazima moto,kumbe ulikuwa ndio unaumwagilia petrol,je una semaje?kama kamati ilihongwa ina maana bunge limehongwa,na wewe ukaamua kwa mihasira yako kujitoa katika kamati,ambapo ungewaku ndani ya kamati unge stand better chance ya kutetea,kwa hoja ya ko ya kamati amabo ni bunge kuhongwa kwanini basi hata katika hilo bunge lenyewe usijiuzuru?kuonyesha kuwa bunge lenyewe wala rushwa?niliuliza siku moja je wewe mwenyewe katika kugombea ubenge huku honga?au katika hiyo kamati na wewe hukuvuta?Ushahidi wa tape upo acha zionyeshwe,ndipo utakapoona kuwa ni wazi kuwa ulikuwa unatetea kwa kutumia uchagga wako,wachagga ache kutugawa,wewe ndesamburo wakati Mengi anatoa kanda yake ya uongo wa kutumia dakika chake si ulikuwepo?Na Adam Malima alipoonyesha kanda ambayo ni the same na ya Ndesamburo si uliona?Ipi ilikuwa ya Uongo?Jibu ni kuwa ya Mengi ilifanyiwa EDITTING nyingi kupunguza muda,Mengi tukubali tusikubali anatumia vyombo vyake VIBAYAAAAAAA!!!

Hapa mzee mzima wa London (kule kwa bwana Blair ambaye yuko radhi waTanzania tufe kwa njaa, kukosa dawa mahospitalini, maji salama ya kunywa, watoto wetu wakose elimu na huduma nyingine muhimu ati ali mradi tu waingereza wake waishi maisha ya raha etc) naona hapa kuna jambo hulioni. Kuna mwana forum some where ame hint kwamba most of us Tanzanian are thinking and reasoning out side our minds - that is exactly where yoiur category is.

The whole essence of this argument is that 'bribery' existed from outside that maadili comittee so that justice could be denied! HAPO tu basi! Na wala sio kuanza ku derail kwamba Mzee Ndesa naye is sailing in the same boat.. Na sidhani kama alituhumu bunge zima, siyo, ila alituhumu baadhi ya wabunge wa Kamati iliyoikuwa inachunguza kesi ya Malima na Mengi ikiwa yeye hajihusishi na rushwa. Upo Hapo.

To resign and distance himself from that maadili comitee Mr. Ndesa has been an hero of a week (my honest opinion)! You have to be a Daresalimite per sa to kow characters like Manji, Suchack Patel, Azm Dewji, Kassim Dewji, Zakharia, Ismail Hotel (Abdallah), Bora, Fida Hussein and Moh'd Dewji (Mohamed Enterprises) howa they are 'STICK' holder of the dancing puppets!! NDESA KAKTAA KUWA PUPPET!!

KIDOGO KIDOGO MZEE WA Big Ben
 
Mimi nilisha sema kwamba watu wa London hawa wana matatizo.Ukimuona mtu anaacha kujiita Mzee wa Kibiti ila anajiita wa London na bado anatak kuongelea issue za Tanzania inanipa wasiwasi sana .Yaani huku London watu wa kila aina na uwezo wa kufikiria mambo naona una kikomo.

Mimi nilikiwa Moshi wakati nimekutana na Mangula Phillip kwenye hotel fulani ambayo ni ya mwana CCM . Huyu Mzee alikuja kuhakikisha kwamba Mbowe na Mzee Ndesa hawaendi popote . Wewe ulikuwa London na bado wewe ni Mzee wa London hata hujui hali iloivyokuwa . Je kweli Ndesa anawe kuhonga nawe ukajua na mabwana zako CCM wakajua wakaaha kuingia Mahakamani ?Unajua ilichukau muda kwa matokeo ya Moshi mjini kutangazwa ? I share a hotel na Mangula nasema niliona kuanzia RPC na wakubwa wengine wanaumia kichwa juu ya hili .

Mzee Ndesa amefanya kazi ndiyo maana alipita . CCM walitumia tume sana kuhonga hata mawakala wakaambiwa hakuna kitu .Polisi alitumika kutisha watu lakini uliza bado watu walisea tuna hesabu zote hapa wewe tangaza tu .Ilikuwa ni kasheshe . Wewe unakula beacon za wazungu hata akili yako imekutuma kujiita Mzee wa London sasa una boyongoka tu hata hujui usemalo.

Malima swali lake juu ya Mengi ama tuuma zake juu ya Mengi na vyombo vyake vina msaada gani wa maisha ya kila siku na watu wa Mkuranga ?Umesha sema ni vyombo vya habari vya mengi na si CCM wala Serikali ni mtu huru kufanya lolote na vyombo vyake .Sasa Malima alitumwa na watu wa Mkuranga kuuliza swali hilo ?

Umesha fika huko Mkuranga ama uko London tu ?Bara bara , shule , maji , Umeme, Zahanati, viko taabani .Yaani kweli hakuna haja ua kuongelea hivyo ?

Unasema Mengi anatumia vyombo vyake vibaya ni kweli maana miaa yote anaitetea CCM na hata leo magazeti yake nk ni pro CCM nalo unasemaje hili ?

Anatugawa ? Wewe umesha gawanyika uko uhamishoni hata leo unajiita Mzee wa London sisi hatuoni habari ya Uchaga hapa . Kama ni Uchaga EL kampigia simu na kumpa nyeti za wabuge wale wachache na si Bunge lote naye ni EL ni Mchaga ?

Mzee Ndesa hajasema Bunge limehongwa japokuwa ni kweli kwamba CCM wabunge wengi wamepita kwa rushwa hata Rais wa Nchi JK alitembeza rushwa na siasa chafu za kashfa kufikia hapo ndiyo maana hana uchungu anakula na marafiki zake wengine walisha kula mgao wao .Wewe ni Mzee wa London huwezi kujua haya .

Pole sana na kukusaidia tu ni kwamba Mzee Ndesa kasema Kamati ya Bunge na baadhi ya wabunge wamekula pesa kwa mujibu wa EL kinara wa CCM . Unasemaje ?Mbona hajakanusha wala Mengi kuhojiwa ili tusikie anasemaje kuhusiana na sakata zima ?Ama kweli watu wa London akili zenu hazina akili ndiyo maana mnavaa makofia ya kijani Hezbollah na kijana kama Hamas .
 
Binafsi nimependa hoja ya Bwana "Supika" kuwa shauri la Mengi v/s Malima linaweza kutumika kufafanua HAKI ZA WANANCHI dhidi ya BUNGE na kinyume chake. Tangu huko nyuma sikupenda baadhi ya madai kuwa suala lililokuwa linajadiliwa halina maslahi ya taifa zaidi ya kuwa ni mgogoro wa Mengi na Manji.

Pitia habari hii...

Shauri la Mengi, Malima limeibua mambo mazito’
Shadrack Sagati
HabariLeo; Friday,January 19, 2007

Sitta asema baadhi ya sheria zinaweza kurekebishwa

SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta amesema shauri la Reginald Mengi na Adamu Malima limeibua mambo mazito na yenye manufaa kwa taifa hivyo gharama za Sh 100 milioni zilizotumika siyo kitu.

“Kuna mambo mengi yameibuka na mtashangaa lakini yote yameweka msingi imara wa utawala bora…hivyo Sh milioni 100 si kitu kikubwa ukilinganisha na kazi iliyofanywa na kamati,” alisema Sitta wakati akizungumza na gazeti hili jana.

Alisema kuwa shauri hilo limeisaidia kamati hiyo kutoa ushauri kwa Spika kwa ajili ya kuweka misingi imara ya utawala bora na kuna uwezekano wa baadhi ya sheria za nchi zinaweza kubadilishwa.

Sitta alisema kuna maswali mengi ya taratibu na sheria ambayo yamekuwa na utata, yamepatiwa ufumbuzi kwenye kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo. Alisema katika ripoti iliyowasilishwa kwake kamati imetoa ushauri mzuri kwa spika. “Kwa mfano kumekuwa na swali la msingi kuhusu kikomo cha kinga ya mbunge ni wapi…je mbunge anaruhusiwa kumkashifu mtu yeyote anapokuwa bungeni?..Kwa sababu kinga inamruhusu mbunge kusema chochote bungeni,” alisema Sitta.

Alisema maswali ya namna hiyo yamejibiwa na ni ya manufaa kwa wananchi, hivyo ni dhana potofu kudhani kuwa shauri la Mengi na Malima lilikuwa binafsi na halikuwa na manufaa kwa jamii.

Spika alisema hata yeye wakati analipeleka shauri kwenye kamati aliona utata wake lakini baadaye aliona haki ya mtu haiwezi kuchezewa kwa sababu tu ya kuogopa gharama zitakazojitokeza.

Alisema kuwa Mengi analalamikiwa kukashifiwa ndani ya Bunge kwa hiyo ana haki kikatiba kulalamika wakati Malima naye anadai kuwa na kinga ya Bunge hivyo alikuwa huru kuzungumza. “Kutokana na utata huu ndio maana nikaipa kamati kushughulikia,” alisema.

“Hizi gharama zinazolalamikiwa kutumika wakati wa shauri hili sio kitu, hakuna uwiano kati ya haki ya mtu na gharama zilizotumika,” alisema Spika akitetea kutumika kwa kiasi hicho cha fedha. Spika alisema kuwa migongano ya mtu mmoja mmoja ndiyo chanzo cha kupatikana maamuzi yanayoweka misingi.

Alisema malalamiko ya Mengi dhidi ya Malima yameweka misingi imara kwa ajili ya kizazi kijacho. “Angalia Mtikila (Mchungaji Christopher) amekuwa anafungua kesi yeye binafsi, lakini maamuzi yake yanatolewa na majaji kwa manufaa ya taifa zima,” alisema.

Jana gazeti hili limeripoti habari za wabunge wa kamati ya maadili, haki na madaraka ya Bunge kutumia Sh milioni 100 wakati wa kusikiliza shauri hilo kutokana na vikao zaidi ya 60 walivyofanya.

Yamekuwapo malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa suala hilo halina manufaa kwa taifa hivyo kutumia Sh milioni 100 ni kutowatendea haki Watanzania kutokana na kutumika kwa fedha hizo za walipa kodi.

Katika mazungumzo yake ya jana, Spika alisema haki za raia sio suala binafsi bali ni utaratibu wa sheri ulioko ndani ya katiba ya nchi. Alisema suala hilo halikupaswa kushughulikia juujuu kama wengine wanavyodai. Aliainisha ibara ya 100 kuwa ndiyo inayotoa haki kwa raia yeyote kwenda katika vyombo vya kutoa haki mara anapoona kuonewa au kukashifiwa kama alivyofanya Mengi.

“Huyu Mengi aliona sehemu ya kupata haki ni bungeni, ndiyo akalalamika kwa Spika,” alisema Spika na akaipongeza kamati hiyo kutokana na kuzama ndani kuhusiana na shauri hilo kwani wametoa mifano kadhaa kutoka nje ya nchi.

Wakati huohuo Spika amekataa kutoa hadharani ripoti ya kamati hiyo akisema ni ya kwake na atakachofanya baada ya kuisoma na kuichambua na kutoa uamuzi kuhusiana na shauri hilo mbele ya Wabunge.Alisema hawezi kuitangaza hadharani kama baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wananchi wanavyotaka afanye.

Alisema ripoti hiyo aliipokea juzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Suleiman N’hunga ikiwa na machapisho yapatayo tisa ambayo yamenukuliwa kwenye hansard tangu kamati hiyo ilivyoanza kazi yake Oktoba mwaka jana.

Baadhi ya wananchi pamoja na vyama vya siasa vimekuwa vinataka ripoti ya kamati hiyo ianikwe hadharani kutokana na migongamano ya itikadi waliyo nayo wajumbe pamoja na madai ya rushwa yaliyotolewa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo. Sitta alisema kanuni za Bunge zinaelekeza Spika anapoamua kupeleka shauri kwenye kamati linakuwa lake na sio la nchi nzima.

Alisema kanuni hizo zinaelekeza kamati iripoti kwake baada ya kukamilisha kazi na yeye ndiye atajua cha kufanya.
 
Bado hawajasema kama Mzee Ndesa ni mzushi ama vipi . Tuhuma za rushwa kwa wabunge wa kamati zilizo tolewa na EL zinabaki zimesimama . Wewe Mzee wa London na Mpuuzi mwenzio Mtetezi mko wapi ?
 
Moyo wangu utafarijika kumsikia Mh. EL akizungumza!Alifumba kabisa masikio suala la Richmond,mpaka mvua zikanyesha,na kama kawaida wadanganyika wakakaa kimya,sasa wanataka kubadilisha baadhi ya vipengele vya kanuni za Bunge ili tatizo lionekane kama ni muundo mbaya wa utendaji wa kamati za Bunge.Hapa suala ni RUSHWA na si vinginevyo,Mh.EL toka chumbani useme kidogo,ili TUKUSIKIE!
 
Mwawado maneno mazito haya . Huyu EL bado anangoja kusikia ligisics za kuleta mvua toka kulee kuliko jaa rushwa ambako yeye ni marafiki zake wakubwa , serikali ikawekwa pembeni kwa ufisadi.Ama kweli maji hayapandi mlima.Ndiyo maana EL anawajuwa wala rushwa wenziwe akaenda kuomba mvua huko .
 
Nashukuru Lunyungu umesaidia kupunguza hasira zangu kwa kumueleza ukweli huyo kiraka wa London.Mimi kwanza nashindwa kuelewa kwa nini watu kama hawa "Mzee wa London" wanapatikana??Wanataka kumfurahisha nani wanapoongea pumba kama hizo akae chumbani na kimada wake ndo amsimulie.
Huyu Mengi kawasaidia sana kafanya mambo mengi kwa manufaa ya CCM.Moja ambalo nalikumbuka vizuri alifuta kipindi cha MALUMBANO ili ambacho kilikuwa kikiibua Issue nyingi za CCM kama ya Mama Mkapa kununua NBC builidingkwa bei poa.
 
Reginald Abraham Mengi, industrialist and media tycoon, twice nominated the second most respected Chief Executive Officer (CEO) in East Africa -in 2001 and 2002- is owner and Executive Chairman of Tanzania's IPP Media Group and one of Africa's leading and most influential businessmen.

A chartered accountant by training, Reginal Mengi created the IPP business conglomerate in the mid 1980s, after serving as Chairman and Managing Partner of Coopers & Lybrand in Tananzia. The IPP Group, which started as a small scale, hand operated ball point assembly plant in Dar Es Salaam has expanded and diversified to become one of the largest industrial groups in Eastern Africa. Among other activities, it encompasses a Financial Consulting firm -IPP Consulting- a bottling company in joint venture with Coca-Cola -Bonite Bottlers Ltd.- Tanzania's leading manufacturer of soaps and toothpaste -Bodycare Ltd.- as well as eleven newspapers, three radio stations and a television company operating in Tanzania, Kenya and Uganda. These include ITV-Independent television Ltd., Radio ONE Ltd and The Guardian Limited, which publishes some of Tanzania's leading weekly and Sunday newspapers: The Guardian, The Sunday Observer, The Daily Mail and the Financial Times in English and Nipashe, Nipashe Jumapili, Alasiri, Kasheshe and Taifa Letu in Kiswahili.

His long experience and success in doing business in Africa has taken him to participate in a large number of national and international business fora as well as taking an active interest in private sector development. To this effect, he has been a long-time advocate of promoting good governance in Africa as well as enhancing technical and managerial skills in the private sector, as key mechanisms for improving the business environment and attracting foreign direct investment to the African continent. However, as a leading media tycoon, he has also called on the African press not to follow the international media's inclination to portray only the negative aspects and constraints of doing business in Africa, since these only reinforce certain stereotypes, overshadow the business opportunities that exist in the continent and has a detrimental effect on potential foreign investors.

As a leading member of the business community Reginald Mengi has served as Chairman of Tanzania's national Board of Business Accountants and Auditors, of Tanzania's Chapter of the International Chamber of Commerce (ICC), and of the Tanzanian Chapter of the Commonwealth Press Union (PCU). He has also participated in several fora organised under the New Partnership for Africa's Development (NEPAD), met with various African and Latin American leaders and is a member of the Board of Management of the Commonwealth Business Council (CBC).

In addition to his interests in business and industry, Reginald Mengi has been involved in a number of charities and other social activities, especially in the areas of health, environmental management and poverty alleviation. He has been a leading advocate of involving the private sector in the prevention and treatment of HIV/AIDS, and was appointed member of Tanzania's Commission for AIDS (TACAIDS). During his term as a commissioner of TACAIDS, he sparked a nationwide debate over the use and distribution of condoms, giving him the nickname of "Mr. Condom" and putting him in confrontation with Christian and Muslim leaders, after criticising them for their position against the use of condoms as a central instrument in the fight against the propagation of HIV/AIDS. In relation to his interests in environmental issues, he is Chairman of the National Environment Management Council (NEMC), the Poverty Alleviation and Environmental Committee (PAEC), patron of the LEAD Global Environmental Network in Tanzania and treasurer of Leadership for Environment and Development (LEAD) international. This non-governmental, non-profit organisation established in 1991 by the Rockerfeller Foundation, is committed to sustainable development and provides training for selected mid-career professionals from a variety of sectors in society. He has also been an important sponsor and benefactor of the Kilimanjaro Forestation Campaign and of several projects for youth employment and disabled people.

In recognition to his work, leadership and contributions in a wide range of business and social activities Reginald Mengi has been awarded the Order of the United Republic of Tanzania, the Order of the Arusha Declaration of the First Class for his exemplary contribution to Tanzania's Development, The East African Environment Leadership Award, the Environmentalist of the Century Award 2000 in the Kilimanjaro region and has been nominated twice the second most respected CEO in East Africa.

What else do you know about this man?

Lets Share!
 
"Controversial" philanthropist with interests in gemstone mining; a Simanjiro Maasai elder (Laibon); a major shareholder in the Africa Media Group (AMG) which owns DTV, Channel Ten among others; a founding member of NICO...
 
What about "dark side" of Mengi?, Mercedes Benz?.......

Lets not discuss people please!!!!

FD
 
Ole wao wadanganye, nitawaumbua - Ndesamburo



na Irene Mark


MBUNGE wa Moshi Mjini (CHADEMA), Philemon Ndesamburo, ameionya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kutokudanganya bunge kuhusu kesi ya Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi na Mbunge wa Mkuranga (CCM), Adam Malima.


Akizungumza katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, jana, Ndesamburo alisema, ikiwa kamati hiyo itathubutu kutoa taarifa za uongo bungeni, atawamaliza kwa kusema ukweli, kwa kuwa alishiriki katika vikao vyote vya kamati hiyo kuhusu mgogoro huo.


Hivi karibuni, mbunge huyo alitangaza kujiuzulu ujumbe wa kamati hiyo kutokana na madai kuwa, baadhi ya wajumbe wa kamati walikuwa wamehongwa na Yusuf Manji ili wamkandamize Mengi.


Alisema, anafahamu kinachopaswa kuwa katika ripoti hiyo iliyowasilishwa hivi karibuni kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta.


“Juzi (Jumatano), waliwasilisha uamuzi wa mgogoro huo kwa Spika, sasa kwa kuwa najua kila kitu tulichojadili, wakijaribu kulipotosha Bunge na jamii, nitawaumbua… waache tu.


“Nilijitoa kwenye kamati hiyo kabla ya kikao cha conclusion (majumuisho), najua hadi uamuzi uliotakiwa kupelekwa kwa Spika,” alisema Ndesamburo huku akitoka nje ya ofisi hizo.


Katika hatua nyingine, Mengi amekataa kusema chochote kuhusu sakata hilo, hadi atakapotakiwa kuzungumzia suala hilo na vyombo vinavyohusika.


Wakati hayo yakiendelea, mjumbe mwingine wa kamati hiyo na Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka, naye amewasilisha ripoti yake kwa Spika Sitta, inayopingana na iliyopelekwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nh’unga, Mbunge wa Dole (CCM).


Kesi hiyo inaonekana kuchukua sura mpya kila kukicha, hasa baada ya mjumbe huyo kutoa ripoti ya kupinga maelezo ya mwenyekiti wake.






juu
 
"...........Wakati hayo yakiendelea, mjumbe mwingine wa kamati hiyo na Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka, naye amewasilisha ripoti yake kwa Spika Sitta, inayopingana na iliyopelekwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nh'unga, Mbunge wa Dole (CCM).........."

ala-haula!!, ripoti ya pili!!!!???
 
Fikiraduni

Why not talk about Mengi?

Is he a share holder of JamboForums.com too??


Jasusi, Samahani, nilikosea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom