Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
Nimesoma kwa makini maelezo ya watu mbalimbali akiwamo Mswahili. Watanzania tumekua na kawaida ya kuchukulia juu kila kitu hata mambo mazito ya kijamii. Hapa suala la msingi RUSHWA. Upo uwezekano wa kutokuwapo ushahidi wa kimahakama, lakini katika mlolongo mzima wa habari husika, utaona wazi RUSHWA ipo kweli. Kwanza kesi yenyewe haina uzito wa kuchukua vikao zaidi ya 60. Kila Mbunge katika wabunge 15 wanalipwa Sh 125,000 kwa siku za kikao. Siku ambazo hakuna kikao wanalipwa Sh 55,000. Kwa hiyo unaongeza hapo na usafiri. Utakuta karibu Sh milioni 100 zimetumika.
Mbali ya kikao kurefushwa, baadhi ya wajumbe walikataa hata kwenda Ulaya katika safari za Kibunge waking'ang'ania kuhudhuria kikao hicho, KUNANINI? Tangazo la MANJI linazungumzia kuhusu tape kughushiwa. Manji si mjumbe na wala hahusiki na kesi hiyo kwa vyovyote, amejuaje ya ndani ya kikao? Jambo la msingi ni kwamba MANJI ni mtu asiyetaka kuguswa na WAKUBWA wanamuogopa sana. Jambo la mwisho MSWAHILI amezungumzia kuhusu tape kughushiwa kutoka dakika kumi na kuwa mbili. Kwa taarifa dakika taarrifa ya habari nzima inaweza kuchukua dakika kumi, kwa hiyo hakuna mtu anayeweza kupewa dakika kumi. Ni uongo mtupu. Huhitaji mtaalamu, kaa katika TV yako na uangalia dakika kumi zitakuwapo habari ngapi. Lakini KUBWA KULIKO YOTE NI KWANINI WAZIRI MKUU AHUSIKE? KWANINI AHALALISHE RUSHWA? KWANINI AONE RUSHWA KUWA KIGEZO CHA UTOAJI HAKI?ATATUSAIDIAJE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA? TUWE WAKWELI NA WAZALENDO, NCHI INAANGAMIA