Zamani,nilikuwa nadhani ubaguzi ni kitu kibaya sana.Baadye nikaelimishwa kuwa kuna ubaguzi wenye manufaa.Na huo ndio naomba utumike hapa.Let's be realistic,forum hii ni babkubwa zaidi ya zote.Pengine haijulikani sana lakini la uhimu sio kujulikana kwa sababu,kwanza,kizuri chajiuza chenyewe,na pili,ijulikane sana ili iweje.Uzuri wa forum hii ni mkusanyiko wa vichwa vyenye kujua uchambuzi na vyenye uchungu wa dhati wa nchi yao.Kwa matinki hiyo,ni dhahiri kuwa tukiwaacha bila kuwadhibiti hao wanaotufanya tukutanike hapa (wala rushwa,matapeli,wanasiasa uchwara,majambazi,wababaishaji pamoja na wapambe wao) basi tutakuwa tunajaribu kushindana na kanuni za asili kwamba maji na mafuta kamwe hayachanganyiki.Nikishauri kuwabagua simaanishi kuwa watu wasiojulikana mttizamo wao wasiruhusiwe kuposti mada.Hapana,wanaopaswa kudhibitiwa kwa nguvu zote ni hao wanaotumwa kuharibu forum hii.Nasema wanatumwa kwa vile tunawajua wanaokula nchi yetu ni wavivu wa kutembelea sehemu kama hizi,wanaacha kazi hiyo kwa vibaraka na wapambe wao.
Kwa hiyo Bwana Administrator,mimi naomba kutoa hoja:ubaguzi wenye manufaa unahitajika kwenye forum hii,na kwa namna flani hilo limewezekana.Uhuru ni mzuri lakini uhuru bila sheria ni vurugu.Na sheria ni neno lenye tafsiri tofauti.Kwangu,sheria ni muhimu katika kudhibiti vurugu.Kwa mpambe wa mla rushwa anayetaka kuharibu forum hii,sheria zitazomdhibiti zitaonekana kwake kama unyanyasaji au uonevu.But who cares?Acha walalamike lakini waungwana tunakutana hapa kujaldili hatma ya nchi yetu.Trust me,jamboforums ni for the time being THE best among TZ forums,na naamini kuwa ina nafasi nzuri ya kupanuka hadi kwenye forms nyingine kama majarida au hata redio (sifa za forums zitazagaa,wafadhili watajitokeza,hasa wale wenye uchungu na nchi yao na wale wanaopigania haki duniani,na mwishowe tunaweza kujikuta na Jambo as a magazine au Jambo Radio...Let's keep it up!!!