Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 151
- 182
Nimemsikia na kumuona mfanyabiashara wa Tanzania, Rostam Aziz akitangaza kuinunua Kampuni ya Media ya Nation (NMG) ya Kenya. Amenunua hisa za familia ya Aghakhan zinazozidi asilimia 50. Kutokana na taratibu za biashara, Rostam saa ndiye mmiliki wa vyombo vyote vya habari vya NMG ambavyo viko Kenya (Nation, Taifa Leo), Uganda (Monitor) na Tanzania (gazeti la Mwananchi, Mwanaspoti).
Ikumbukwe kwamba Rostam ananunua NMG wakati Kenya inaelekea kwenye uchaguzi - utafanyika 2027, ambao huzongwa na mambo mengi kupitia vyombo vya habari na kikubwa ni kwamba NMG na Rais Ruto hawakuwa na uhusiano mzuri, hivyo kuna dalili kwamba ununuzi wa Rostam, huenda unabeba kivuli cha Rais Ruto.
Pia, Rostam alinunua magazeti ya RAI, Mtanzania yaliyokuwa yakimilikiwa na waandishi nguli, Jenerali Ulimwengu, Salva Rweyemamu, Dk Gideon Shoo, Johnson Mbwambo na wengine ambapo alitumia magazeti hayo kuchafua wagombea wengine wa urais wa Tanzania 2004-2005. Haya magazeti yalimchafua sana Dk. Salim Ahmed Salim na kuharibu taswira yake, na jamaa zake wanadai yaliangusha na kukatiza ndoto zake.
Yaani sasa namuona mgombea urais wa nguvu ya upinzani Kenya, akianza kuchafuliwa na magazeti ya NMG.
Yangu macho- nakaa paleeee nasubiri kipyenga kupulizwa na kufuanua haya nayoyaona sasa.