Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

mengi is not that clean is manji...let mengi come out na atuambie zile pesa za SKUVI na ule mradi mzima unaendeleaje...
 
The issue right now si SKUVI wala nini bali hongo kwa wabunge ndiyo core issue . Mengi ni mchafu, mzimaji, na mtoa rushwa na anapashwa kulaaniwa sana . Kumbeni alivyo tumia vyombo vyake mwaka 1995 kuonyesha mauaji ya Rwanda na Burundi kama watu wangali uchagua upinzani. Lakini yote haya yako kweney rekodi sasa tuna deal na issue ya EL , Mengi na rushwa kwa Wabunge ndiyo swala kwa sasa .Mengine haya CCM ama serikali haiwezi kumgusa kama vile Mahita ama Mahalu hawezi kuguswa maana alifanya kwa msaada na amri ama baraka za CCM na Serikali yake .
 
Moto aliouwasha Ndesamburo wasambaa



na Mwandishi Wetu


MOTO aliouwasha aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maadili, Madaraka na Haki za Bunge, Philemon Ndesamburo, umedakwa na wanasiasa, na sasa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amejitumbukiza kwenye sakata hilo.


Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, Mbatia amemtaka Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuiweka bayana ripoti iliyoandaliwa na kamati hiyo, wakati ilipokuwa ikijadili kesi iliyofunguliwa na mfanyabiashara Reginald Mengi dhidi ya Mbunge wa Mkuranga (CCM), Adam Malima.


Mbatia anakuwa mtu wa pili kuvutwa na sakata hilo baada ya wiki iliyopita, mfanyabiashara mwenye mgongano na Mengi, Yusuf Manji, naye kuhoji kauli ya Ndesamburo, kwamba kamati hiyo ilihongwa ili kumkandamiza Mengi.


Katika taarifa yake, Mbatia ametoa sababu kadhaa kuhalalisha ombi lake la kumtaka Sitta kuiweka wazi ripoti hiyo. Kubwa ya sababu hizo, inaonekana kusimama kwenye haki ya umma wa Watanzania kuujua ukweli kuhusu jambo hilo.


Mbatia anasema katika taarifa yake kuwa, Bunge linawajibika kutoa ripoti hiyo kwa kuwa ni mtoto wa katiba, ambayo inatoa haki kwa umma wa Watanzania kupata habari.


Mbatia anadai kuwa, suala la Mengi na Malima litaachwa liendelee kama linavyoendelea hivi sasa kwa kuwa lina mgongano wa kimaslahi binafsi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


“…kwani Mh. Spika, Mh. Malima, ndugu Mengi na wajumbe waliobaki katika Kamati ya Bunge ya Maadili, Madaraka na Haki za Bunge ni wanachama wa CCM. Pia lina mgongano wa kiitikadi za kisiasa kati ya CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),” anabainisha Mbatia.


Mbatia anasema kwamba, kwa kuwa si busara kwa kesi ya nyani kumpelekea ngedere, ni vema Sitta, kwa mamlaka aliyopewa na Katiba na Kanuni za Bunge, aiweke wazi ripoti yote ya kamati kupitia vyombo vya habari.


“Mheshimiwa Ndesamburo amesema kamati imekutana zaidi ya mara sitini, lakini haijafanikiwa kutatua tatizo la ndugu Mengi na Mh. Malima kwa kutumia fedha nyingi za walipakodi,” anadai Mbatia katika taarifa hiyo ya kurasa mbili.


Ndesamburo, ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Mjini kupitia CHADEMA, aliibua sakata hili wiki iliyopita baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari kwa kutangaza kujiuzulu kwake kutoka katika kamati hiyo kwa madai kuwa ilikuwa imehongwa na Manji ili imkandamize Mengi katika shauri lake dhidi ya Malima

inamaana manji ameishikilia serikali ya jk kiasi hicho?mbona hawa magabachori wametukalia hivi,yaani vitu vya ndani ya system wao ndio wanatajwa.kweli serikali yetu ndio maaana inadharauliwa sana.
 
Mengi-Malima report ready



THE Parliamentary Privileges, Ethics and Power Committee has finalised a report on the case involving the Mkuranga legislator, Mr Adam Malima (CCM) and the IPP Group Executive Chairman, Mr Reginald Mengi.

Committee Chairman Suleiman Nhung'a told the 'Daily News' yesterday that the report would be presented soon to the Speaker of the National Assembly, Mr Samwel Sitta.

“The report is ready. It is just waiting to be presented to the Speaker, which will be very soon,” said Mr Nhung'a. He declined to mention a specific date.

http://www.tzuk.com/index.php?option=com_content&task=view&id=2741&Itemid=39
 
report ipi kama Mzee Ndesa anasema hawakuelewana na hawakumaliza kazi . Ni Report ya kutomaliza kazi ama report ipi ?
 
Lunyungu kama wajumbe wengine wote wakisema tumemaliza kazi, na mzee Ndesa akisema "hapana hatukumaliza" utamuamini nani?
 
Kwanza mimi najiuliza wamemaliza kivipi ? Ulimsikia Mzee Ndesa akisema walikubaliana watu waitwe na sasa baadaye ikawa hakuna kuitwa na Kikao kikavunjika hiyo kazi inakuwa imemalizika vipi ?

Acheni ubishi wenu wana CCM nyie .Mkapa aliulizwa kama kuna Account Uswisss akasema hapana sasa haya yanatoka wapi leo ?

Yaani hakuna anaye ongelea tuhuma za Ndesa wanakimbia na reports tu kazi kubwa
 
Hawa wasitufanye sisi wajinga hapa

They have got to COME OUT CLEAN FIRST BEFORE THEY RELEASE THEIR ##*/@@%^## REPORT!!!!!!
 
Tunawaomba wahusika Ripoti iwekwe wazi,na isiwe mambo ya ndani ya Bunge.Hakuna lolote lililoharibika hapa,kila kitu kitakuwa wazi.Nafikiri kuwa wamejaribu kumaliza/kuandika ripoti haraka haraka ili kupoteza maana ya malalamiko ya Mbunge Ndesamburo.Mimi naamini kuwa always UKWELI unakuwa wazi,kwa maana hiyo tusiwe na Hofu UKWELI utachomoza tu!.
 
Kwa mujibu wa Daima walikaa siku sitini bila kutatua suala hilo!!!!Nini cha mno kilichowasababisha wakae siku zote hizo bila kumaliza??
 
Watanzania tumeliwa jumla jumla, yaani tuhuma nzito kama hizi mpaka mmoja wa wabunge anajitoa kwenye kamati; lakini hakuna hata presha yoyote kutoka kwenye chama chochote au taasisi yoyote hata media inayowabana hawa wabunge wakanushe au kukubali hizo tuhuma?
 
Mwawado,

Ripoti hiyo haifai hata si kusomwa tu bali hata kutizamwa kwa macho, kinyume cha hapo maana yake ni kwamba:

1.Kamati Yote haina Nidhamu/Adabu! (Very funny, kamati ya Nidhamu/Adabu haina Nidhamu/Adabu!!!)
2.WAMEKUBALI KUWA NI CORRUPT

Wajisafishe kwanza!!
 
Home News More in this Category!
Speaker demands specific charges from Ndesamburo
JIANG ALIPO
Daily News; Tuesday,January 16, 2007 @00:08

THE Speaker of the National Assembly, Mr Samuel Sitta, said in Dar es Salaam yesterday that he will not entertain unclear claims and has asked the Moshi Urban Member of Parliament, Mr Philemon Ndesamburo (Chadema), to put in writing specific charges against each MP he says was bribed.

Mr Ndesamburo claimed that some members of the Parliamentary Privileges, Ethics and Power Committee, who are handling the case between Mkuranga MP, Mr Adam Malima (CCM) and IPP Group Executive Chairman, Mr Reginald Mengi, were bribed.

Mr Sitta told the 'Daily News' he could not work on vague charges from Mr Ndesamburo. "I have advised Honourable Ndesamburo to write what he told me. He told me money exchanged hands. He said he talked to Mr Mengi over the phone. He talks about members of parliament. This is vague statement; members of parliament include the Speaker. That is why I have advised him to write specific charges against those members of parliament."

Mr Ndesamburo could not say yesterday when he would present a written statement to the Speaker. He said he must talk to the Speaker before making a press statement. "Call me tomorrow because I have to talk to the Speaker before I react to your question."

The Speaker is scheduled to get the committee's report today, but Mr Sitta said he will not make public the committee's findings. He will report to parliament session when it meets later this month.

Even at that stage, the Speaker said, "the entire report cannot be made public because it is Speaker's report. I will just present a summary and my decision to parliament," he said.

Mr Ndesamburo resigned from the Committee last Wednesday, citing dissatisfaction with the way the case was handled by the committee and raised corruption charges.


HAYA MAMBO YAMEANZA TENA
 
HAYA MAMBO YAMEANZA TENA

Even at that stage, the Speaker said, "the entire report cannot be made public because it is Speaker's report. I will just present a summary and my decision to parliament," he said.


Mhhh hakuna kitu hapa Dua.

Umeona hiyo para hapo speaker anavyodai....atatoa SUMMARY..!!
 
Sasa leo watu wanadhani Mzee Ndesa muongo bad wakati hata report haitoki kwamba ni ya Spika ? Kazi kubwa sana
 
Inakuwaje katika nchi ya kidemokrasia au ile inayojaribu kujenga jamii ya kidemokrasia kwamba kuna mtu au taasisi fulani inayodai haki isiyokuwa nazo? Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka kuhusu kesi ya Mengi dhidi ya Mhe Malima inawasilishwa baadaye leo. Mhe. Spika Bw. Samuel Sitta hata hivyo amesema hiyo "Ni ripoti ya Spika" na haitawekwa hadharani. Kwa mara nyingine tena Bw. Sitta anatumia nafasi yake ya Uspika kujitwalia madaraka na uwezo asiokuwa nao!! Tumelikataa kwa Rais kuwa Mungu Mtu, tumekataa kwa Wabunge kuwa Miungu watu, na kwa hakika tunakataa kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kujiona yeye ni Mungu Mtu!! Mheshimwa Spika, hapo umepotoka! naungana na Watanzania wengine kutaka ripoti hiyo iwekwe hadharani mara tu baada ya kuwasilishwa Bungeni!

Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili, na Madaraka imepewa majukumu matatu:

1. Kuchunguza masuala yote yahusuyo haki, kinga, na madaraka ya Bunge yanayopelekwa kwake na spika.
2. Kushughulikia masuala ya maadili yanayohusu Wabunge
3. Kufikiria jambo jingine lolote litakalopelekwa kwake na Spika.

Hakuna mahala hata pamoja panaposema kuwa Ripoti za Kamati za Bunge ni "Za Spika". Hadi hivi sasa kuna ripoti kadhaa kutoka Kamati nyingine za Bunge ambazo ziko hadharani na hazikudaiwa kuwa ni za siri. Miongoni mwa ripoti hizo ni hizi:

http://www.parliament.go.tz/bunge/Docs/Report/Committee/0506/Ujenzi.pdf
http://www.parliament.go.tz/bunge/Docs/Report/Committee/0506/Kilimo.pdf

Lazima tuelewe kuwa ripoti hii hahihusu madai ya Mbunge wa Moshi Mjini Bw. Ndesamburo bali kwa mujibu wa maagizo waliyopewa ilikuwa inachunguza madai ya Mbunge wa Mkuranga Mhe. Adam Kighoma Ali Malima kuwa mmiliki wa vyombo mbalimbali vya habari Bw. Reginald Mengi anatumia vyombo vyake kujitangaza zaidi na kutotoa nafasi ya kutosha kwa viongozi wa serikali hususan matukio yanayomhusu Rais. Ni hapo Bwana Mengi alipoamua kujibu madai hayo ya Bw. Malima kwenye vyombo vya habari na pia kuamua kuleta malalamiko yake Bungeni.

Hapo mwanzo, baadhi ya Wabunge walipinga kabisa kitendo cha Spika kukubali kupokea malalamiko ya Bw. Mengi na wengine walidai kuwa amevunja Katiba! Wengi walidai kuwa wanachosema Bungeni kina kinga! Bw. Sitta aliwajibu wabunge hao na kuwaambia kuwa "hawako juu ya sheria" na pia kuwa wabunge hawawezi kutoa kashfa bungeni, au kumtukana mtu bungeni wakijidhania kuwa wana kinga kwa vile tu wao ni wabunge!

Hata hivyo hatujui kama ripoti hii imekamilika vipi wakati mmoja wa wajumbe wake amejiengua? Je, inakuwaje ripoti hii ikamilike wakati tuhuma nzito dhidi ya wajumbe wa kamati hiyo zimetolewa na hazijajibiwa? Mmoja wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amedai kuwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano amemwambia Bw. Mengi kuwa tume hiyo kuwa imepokea rushwa toka mpinzani wa kibiashara wa Bw. Mengi aitwaye bw. Yusuph Manji ili tume imkute Bw. Mengi na hatia ya kutumia vyombo vyake vya habari vibaya?

Ni wazi kuwa ripoti hii haiwezi kuwa kamili na ili kutafuta haki, mambo kadhaa lazima yafanyike.

a. Madai ya Mbunge wa Moshi vijijini ni mazito na kama yana ukweli basi ni lazima uchunguzi huru ufanyike. Bunge haliwezi kujichunguza lenyewe!! Hivyo, Rais Kikwete ateue tume huru itakayoongozwa na jaji wa mahakama kuu ili ifuatilie madai ya Bw. Ndesamburo na kuwaita wale wote wanaotajwa katika madai hayo! Je Bw. Mengi aliambiwa na Waziri Mkuu kuwa Manji ameihonga tume ya Maadili? Je, Waziri Mkuu alimwambia Bw. Mengi juu ya hongo hiyo ya Bw. Manji, na yeye alipata wapi habari hizo? Njia pekee ya kufahamu ukweli wa jambo hilo ni kuwaita Bw. Ndesamburo, Bw. Mengi, na Bw. Edward Lowassa ili kutafuta ukweli. Tume iwe na uwezo wa kuitisha mashahidi (subpoena power)

b. Kama Bw. Sitta hataki ripoti hiyo iwekwe hadharani, basi ripoti hiyo isiletwe Bungeni kabisa na aikatae kwani mchakato wa upatikanaji wake umevurugika kutokana na tuhuma nzito.

c. Kamati ya Maadili ivunjwe na Kamati mpya iundwe ili kuchunguza suala la Mengi na Malima. Ama sivyo, Kamati Maalum ya Bunge iundwe kufanya hivyo. Kwa vyovyote vile Kamati iliyopo sasa kutokana na unyeti wa majukumu yake haiwezi kumtendea haki Mbunge mmoja wa upinzani ambaye wanamuaona ana matata! Kamati maalum itakayoundwa iwe na uwiano sawa wa wajumbe. Maazimio ya kamati hiyo lazima yawe ya wingi, na ikitokea kura kufungana basi suala hilo linapelekwa kwenye Bunge zima!

d. Serikali ihakikishe kuwa Mbunge wa Moshi Mjini anapatiwa ulinzi na hakuna mtu yeyote anayetumia madaraka yake kumuonea au kumuadhibu kwa namna yoyote ile. Endapo Bw. Ndesamburo atapatwa na madhara yoyote, wananchi watapoteza imani na viongozi wao.

Tuhuma za rushwa dhidi ya chombo cha Bunge ni tuhuma nzito na lazima zipewe uzito unaostahili. Kujaribu kuzidharau tuhuma hizo kisa tu kuwa zimetolewa na Mbunge wa upinzani ambaye huko nyuma aliwahi kutoa kauli zisizothibitika ni kutokomaa kisiasa. Kila hoja na madai lazima yasimame peke yake na tusimhukumu Bw. Ndesamburo kwa makosa yake ya nyuma.

Watanzania wanataka kujua. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Bw. Edward Lowassa alimwambia Bw. Mengi kuwa Kamati ya Bunge ya Maadili imepewa Hongo na Bw. Manji? Je, Bw. Mengi anakumbuka kuambiwa maneno hayo na Waziri Mkuu? Waziri Mkuu alipata wapi taarifa hizo za rushwa na hatua gani alichukua!? Kama Bw. Mengi na Bw. Lowassa watakanusha chini ya kiapo kuwa hakukuwa na mazungumzo ya namna hiyo, Bw. Ndesamburo yuko tayari kuomba radhi Bunge la Tanzania na wajumbe wenzake na wananchi wenzake ambao wameshtushwa na kuumizwa na tuhuma hizo nzito dhidi ya chombo chetu cha kutunga sheria? Kama tutapa majibu sijui, lakini kuuliza tutaendelea kuuliza!!
 
Sure we should see this report, so far tumeshailipia about Tshs. 100M!

Wajumbe wa kamati wako 16, wamekaa vikao zaidi ya 60, na kila mmoja anapata posho ya vikao Tshs. 95,000 kwa siku (ikiwa haijaongezwa to 120K kama ilivyokuwa inapendekezwa).

Na kwa sura iliyopo ni kuwa it is far from over ... as ni jambo limezua jambo, it is likely to cost us a lot more. Suala lilianza bila kichwa wala miguu.

____________________________________________________________
Daily News Editor's Comment

Yes, publish the report
Editor
Daily News; Tuesday,January 16, 2007 @00:01
http://dailynews-tsn.com/page.php?id=5307

WE concur with NCCR-Mageuzi Chairman James Mbatia that the report of the Parliamentary Privileges, Ethics and Powers Committee, on allegations facing IPP Chairman Reginald Mengi of misusing his television station, should be published without further delay.

The committee, chaired by the Dole MP, Mr Juma Suleiman N'hunga (CCM), is reported to have met more than 60 times to investigate the allegations by the MP for Mkuranga, Mr Adam Malima, that the ITV news bulletin was allocating longer airtime to proprietor Mengi than that given to national leaders.

The committee's findings from extensive interviews and examination of videotapes were to be tabled during the last parliamentary session in Dodoma, but it is understood that the final report is yet to be submitted to the Speaker.

Whether it should take so many sessions to determine the matter is debatable, but the findings should be made public now to avoid further distortion of the case by one of the committee members, Mr Philemon Ndesamburo (Chadema-Moshi Urban)

By resigning from the committee last week on the extraneous claim that some of his colleagues were bribed to deny Mengi justice, the opposition MP is deliberately working to divert attention from the real issue, which is whether Mengi allocated himself too much time on his TV. Some analysts see the desperate move, which Ndesamburo attributes directly to Mengi, as lending credence to speculation that the committee findings are unfavourable to the IPP media owner.

If that holds true, Mengi would have an interest in derailing the investigation or censoring the report and since Ndesamburo has insinuated that MPs are driven by bribery, we wonder who sponsored his move.

The public expects the other members of the ethics committee and the Speaker to launch a separate investigation on Ndesamburo's bribery claims, which must be proven or retracted for the sake of integrity of parliament.

Having said that, Mengi and Ndesamburo should be reminded that the IPP chairman's conflict with Yusuf Manji is not a national issue and must not be smuggled into every forum, least of all the National Assembly.
 
Jamani....Tz tutaamka lini? Kuna kitu bado hatujafahamu kuhusu tofauti kati ya Mengi na Manji....is it Yanga? or Jengo la Samora?Quality Plaza? Pesa za NSSF? sijui walikwaruzana kwenye dili gani. Au uzalendo unamponza Mengi? Redio mbao zinasema, "Manji was financed kampeni za Adam Malima."On the other hand ni kweli any issue kuhusuMengi ITV itasemwa weEEEE.......even 15 minutes. Vitu vya muhimu wanavikatakata hata haawaonyeshi main points. Angalau sasa baada ya kusemwa wanaanza kujirekebisha. Sishangai pia wabunge kuhongwa....imezoeleka. If I was given a chance hii kesi ningeitupilia mbali sioni inatufaidisha nini!Kama hoja ya Malima ingewekewa umuhimu....mfano he argued if there was any law inayowataka media owners kuweka utaifa mbele zaidi ya maslahi binafsi. Kuonyesha viongozi wa kitaifa etc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom