Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Huyu kweli ni Mzeewalondon. wacha tuangalie kasi yake . Hii awamu ya 4 ina wadudu si mchezo. Jamaa kagawa madaraka kama njugu sasa hata tukiibiwa na kudhulumiwa wataibuka watetezi .Kama Mzee kachukua Rushwa anaweza kuja na kusema haya ? Jamani Mzee Ndesa achukue Rushwa akitaka nini hasa ?
 
mwanaKJJ

Naona unauliza masawali mazuri sana lakini kitu unachosahau ni kwamba tupo Tanzania. Siyo kila ushahidi unakubalika kwenye mahakama zetu (siyo sawa na huku nje) jaribu kupitia Criminal Code ya Tanzania (CAP 16) na Sheria ya kuendesha Mashtaka ya Jinai (1984) na Witnesses Evidence.

Kama hizi evidence unazosema zilikuwa zinachukuliwa serious au kukubalika kirahisi kwenye mahakama zetu basi ungekuta hamna msongamano wa kesi. kwani hao PCB wana tape kiasi gani au nakala za maandishi lakini hamna kilichofanyika.
 
jamani msiwe na mashaka mtamsikia mzee mwenyewe akielezea.

Nimemuuliza: Kama hana ushahidi kwanini kusema aliyosema?
Je, anaamni Waziri Mkuu anataka kumdhuru?
Je, amejaribu kuzungumza na Waziri Mkuu kusikia maelezo yake
Je, Bwana Mengi yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya Kamati hiyo kuwa WM alimuambia maneno hayo

na maswali mengine Kemkem
 
Haya mzee wa london karibu nawe. Sijafahamu unachotaka kusema hapo juu-unajaribu kuhalalisha rushwa au namna gani? Yaani kama Ndesamburo alitoa rushwa (kama kweli una ushahidi na hili) ndio kusema basi rushwa imeshakuwa haki na kwamba ilikuwa ni sawa hao wabunge kuhongwa na Manji?

Jamani, nyie wageni mchukuage muda kidogo wa kutafakari kabla hamjarukia hoja, eboooo!

Sio wageni wala kitu gani ni jamaa mmoja anaingia na majina tofauti tofauti. Ni dalili za uoga na kukosa hoja kudhani ili upinge mtazamo wa watu wengine lazima ujibadilishe jina.
 
Sio wageni wala kitu gani ni jamaa mmoja anaingia na majina tofauti tofauti. Ni dalili za uoga na kukosa hoja kudhani ili upinge mtazamo wa watu wengine lazima ujibadilishe jina.

Nami naafikiana nawe asilimia 101.Pengine ni vema kama Administrator akaangalia namna ya kudhibiti utoto wa namna hii.Sidhani kama mwanabodi serious wa jamboforums anahitaji kuingina na jina zaidi ya moja.Uhuru ni kitu kizuri lakini uhuru bila mpaka unavutia vurugu.
 
Kama wewe ni shabiki wa Lowasa uko hapa ama wewe ni pro Govt na uko hapa usibadilishe majina kuwa nganga muda wote na tetea hadi mwisho kubadili majina ni ulimbukeni sana . Sema what you believe in .
 
Wewe si Africansista bali ni Rushwasista mpuuzi wewe . Unaleta hadithi za Mkapa kuomba ushahidi wa rushwa kwenye mikutano ya hadhara ?Walio kutuma kuja hapa na hoja mbuzi rudi waambie hapa tuko macho . Kwanza wewe ni mgeni na kamba mguuni na matongotongo .

This type of intimidation is totally uncalled for. You have no more or less right in this discussion forum than anyone else; unless you own it!
 

Shutuma za Ndesamburo zatikisa Bunge, viongozi

Shadrack Sagati
HabariLeo; Friday,January 12, 2007

Adaiwa kukiuka kanuni zake


Foka asema lazima ukweli ubainike

TUHUMA za rushwa dhidi ya baadhi ya wabunge zilizotolewa na Mbunge wa Chadema wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo zimeelezwa kuwa ni nzito na zimewashitua wabunge na viongozi wa chombo hicho.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa Bunge unatafakari hatua za kuchukua dhidi ya tuhuma hizo za kuhongwa na mmoja wa wafanyabiashara ili wabunge wapindishe haki katika shauri la Reginald Mengi na Adam Malima, Mbunge wa Mkuranga. Viongozi wa Bunge ambao walizungumza na gazeti hili jana, walisema tuhuma hizo zimewashitua na ni lazima ukweli uweze kubainika na utangazwe mbele ya wananchi.

Naibu Spika wa Bunge, Anne Makinda aliliambia HabariLeo kuwa Ndesamburo ametoa shutuma nzito dhidi ya wabunge wenzake na hatua yake ya kuzitangaza kwenye vyombo vya habari ni kuvunja kanuni za Bunge. Anne alisema Ndesamburo alishajadiliana na Spika Samwel Sitta na kueleweshwa hatua za kuchukua, hivyo hakustahili kujiuzulu wala kutangaza mambo hayo kwenye vyombo vya habari.

“Spika baada ya kujadiliana naye alimshauri vizuri tu kwamba asijiuzulu na badala yake kingeundwa chombo kingine cha kuwahoji wajumbe wa kamati hiyo pamoja na watu wengine ambao Ndesamburo alitaka wahojiwe,” alisema Anne.

Naibu spika alisema Ndesamburo alikuwa anataka Mengi na Waziri Mkuu, Edward Lowassa wahojiwe, jambo ambalo Spika alimshauri avute subira iundwe kamati nyingine ya kuchunguza tuhuma hizo.

“Wewe uliona wapi watuhumiwa waanze tena kuwahoji watuhumiwa wenzao
, isingewezekana. Ndiyo maana Spika akashauri kiundwe chombo kingine cha kuchunguza tuhuma hizo,” alisema.

Alisema katika suala hilo Spika alishauri wajumbe wa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge wangeandika ripoti kuonyesha kama wameshindwa kuendelea na shauri hilo kuhusiana na tuhuma hizo. Naibu Spika alisema kuwa licha ya ushauri huo mzuri, Ndesamburo aling’ang’ania Mengi na Waziri Mkuu waitwe. “Baadaye akaleta barua yake ya kujiuzulu,” alisema.

Alisema Ndesamburo hakupaswa kuzungumzia suala hilo kwenye kamati tu bali pia alitakiwa aende kuzitoa tuhuma hizo kwenye Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) ambayo ndiyo yenye uwezo wa kuchunguza tuhuma hizo.

Naye Katibu wa Bunge, Damian Foka alisema Ndesamburo alipaswa kupeleka malalamiko yake kimya kimya kwa Spika yaweze kufanyiwa uchunguzi badala ya kwenda kutangaza kwenye vyombo vya habari.

Tunajifunza nini kweye sakata hili??
 
Hakika tuhuma ni nzito.Kubwa kabisa hapa Bwana Ndesamburo,kwanza wewe mwenyewe katika kugombea Ubunge hukutoa Rushwa?
Pili madai yako na kauli yako ni kielelezo tosha,kwamba hata wewe mwenyewe inaonyesha huyo Mengi kakupa kitu kidogo!!!Je unabisha juu ya hilo?


Inaonyesha badala ya kubaki na focus kwenye main point juu ya PM kusema wabunge wake wamepokea rushwa wewe...unamtafuta Ndesamburo uchawi. Kama alitoa rushwa kupata ubunge au kama alipewa hela na Mengi, suala hapa ni MOJA: Edward Lowassa akiwa kama Mbunge, Waziri Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Bungeni amesema kuwa Wabunge wamehongwa...FULL STOP.
 
Hapa iko kazi CCM wameanza cover up . Mzee Ndesa he knew what would follow baada ya kukataa longolongo ya CCM.PCB they are not late . Wanaweza kumhojo Mengi , Ndesa na Lowasa kuna ubaya gani ? Hapa ndiyo patamu maana Ndesa kasema anataka wahojiwe sasa hata haki ya yeye kujiuzuri nayo ni makosa ? CCM jamani . Kumbe ndiyo maana HabariLeo imeanzishwa ni baada ya kuona magazeti ya Mengi siku moja yatafungiwa inavyo onekana . Lakini hakuna dhambi inaweza kufichwa sana . Uozo wa vikao na Kamati za Bunge la CCM ni mengi na nyingi. Hongera Mzee Ndesa kusema wazi na sasa PCB tafuteni ukweli .Msilete kisingizio .
 
Mswahili,
Acha ukabila wako. The real issue here is Lowassa as waziri mkuu. Yeye alishajua kuwa wabunge wamehongwa na anayo madaraka ya kuchukua hatua kwa nini kakaa kimya? That is the issue here na si Wachagga. DrWho, Lowassa ni kiongozi wa serikali. Anajua kuwa wabunge wake wameshahongwa. The question here is what has he done to make sure justice is served?





As PM angefanya nini juu ya wabunge..??..answer is nothing..hana madaraka yoyote juu ya wabunge. As Mbunge au Raia wa Tz angeripoti kwenye kamati ya bunge (kama Mengi alivyofanya)...tatizo ni kuwa kamati yenyewe NDIYO INAYOTUHUMIWA KWA UOVU HUO...!! Kasheshe...au ndio kusema Spika angemuambia avute subira aunde KAMATI nyingine..(what a JOKE..!!)

SWALI LA MSINGI: Kwa NINI wabunge wa kamati husika ambao ni WATUHUMIWA; WAMEKAA KIMYA, je tuamini kuwa ni kweli wamepokea rushwa kama EL alivyomwambia Mengi au Lah...Au wanaweza kumuuliza EL atoe ushahidi wa wao kuchukua Rushwa. Watuhumiwa (wabunge wa ccm) wakikaa kimya basi EL hana kesi ya kujibu..
 
Lord hapa watu wamesha ona soo maana mulungula umesha toka .Sasa wafanye nini ? Makinda ana bwabwaja
 
inashangaza jinsi habari hii iiliyowekwa mnachukulia kuwa ndio hali halisi ilivyo na ukweli...ushahidi wa kuwa EL anajua na akaweka hadharani kuwa wambunge wamepewa hongo na akamweleza Mengi uko wapi?? na kwa nini amweleze Mengi, na ili iweje?? hata kama PM anaissue zake basi sio kila jambo azushiwe tuu...

nahisi utakuwa umetokea TZUK

karibu sista
 
Kwanza mie nnaendelea kulaani kwa sana tabia chafu ya tibwili bwili au mie ntamwita kwa lugha ya kwetu pwani bojole, maana huu si ulimwengu wa kutishana na kutukanana, sie tunaikemea serikali iache vitisho kumbe pia na hata humu wamo mabarazuli wanaendeleza vitisho, ama kweli mkolozi mkoloni tu hata awe mweusi. na mshenzi mshenzi tu hata awe msomi. huu ni wakati wa kuheshjimu mawazo ya wengine japo huyakubali na hoja hujibiwa kwa hoja.

ama kuhusu hili suala limeenda pazuri, maana huuu ulimwengu wa uwazi tubataka tujue ukweli uko wapi? jee madai ya huyo ndesamburo yana ukweli au ndo kujijenga kisiasa? maana wana siasa na nyie mna mengi, mie nataka ukweli uwe hadharani waitwe wahusika na wahojiwe kwanza aje huyo mkuu wa hili atoe ushahidi wake tujue .

jengine kama nilivyosema kuna watu humu wamekuwa biased sana maana wao lolote lile linalohusiana na upande fulani hulipa tick kubwa na kutoa hukumu sio sahihi jamani. kwanza lkazima tusikilize pande zote mbili kisha ndo tuseme si tukurupuke ati kwa kuwa kasema na kajiuzulu ni kweli acheni umamluki juooo

😉
 
Kwanza mie nnaendelea kulaani kwa sana tabia chafu ya tibwili bwili au mie ntamwita kwa lugha ya kwetu pwani bojole, maana huu si ulimwengu wa kutishana na kutukanana, sie tunaikemea serikali iache vitisho kumbe pia na hata humu wamo mabarazuli wanaendeleza vitisho, ama kweli mkolozi mkoloni tu hata awe mweusi. na mshenzi mshenzi tu hata awe msomi. huu ni wakati wa kuheshjimu mawazo ya wengine japo huyakubali na hoja hujibiwa kwa hoja.

ama kuhusu hili suala limeenda pazuri, maana huuu ulimwengu wa uwazi tubataka tujue ukweli uko wapi? jee madai ya huyo ndesamburo yana ukweli au ndo kujijenga kisiasa? maana wana siasa na nyie mna mengi, mie nataka ukweli uwe hadharani waitwe wahusika na wahojiwe kwanza aje huyo mkuu wa hili atoe ushahidi wake tujue .

jengine kama nilivyosema kuna watu humu wamekuwa biased sana maana wao lolote lile linalohusiana na upande fulani hulipa tick kubwa na kutoa hukumu sio sahihi jamani. kwanza lkazima tusikilize pande zote mbili kisha ndo tuseme si tukurupuke ati kwa kuwa kasema na kajiuzulu ni kweli acheni umamluki juooo

😉
 
Mzee Ndesamburo si mtu mbabaishaji - ni mtu makini saana na ndo maana kafanikiwa katika biashara zake pamoja na kwamba yuko upande wa upinzani! Rekodi zake za kodi ni clean na nafikiri huko PCB wachilia mbali na mahakama hana rekodi mbaya.
Hivi jamani kuna mtu anayewzeza kutupa wasifu wa bwana Yusufu Manji? Quality Group Ltd ilitoka wapi?
 
Wambandwa,
Umeuliza swali zuri. Na mimi nina shauku ya kupata data za huyu Manji.
 
Manji ni mwana mtandao ambaye pesa zake kesha ziweka kwa Lowasa na sasa anatesa tu anangoja Ubunge na uwaziri ama haitoshi sifa hii ?
 
Wala rushwa hawawezi wakaonyeshwa hadharani kama hakuna ushahidi wa kutosha,je wewe jina lako likionyeshwa hadharani bila ya ushahidi ili mradi tu wajue wewe ni mla rushwa hiyo halali?Issue hiyo Ndesamburo ni MUONGO,yeye anatumiwa tu na Mengi,lazima ieleweke wazi,Mengi alitoa Million mia tatu(3m)za kukodo Helkopta aliyofanyia kampeni Chairman wa CHADEMA,therefore this is paybeck time for CHADEMA na WACHAGGA.Kwa hiyo Ndesamburo hana jipya.Yeye mwenyewe ni MLA RUSHWA vile vile!!!!
 
Hivi kama wanasiasa wamekuwa wanabehave namna hii je kuna haja ya mtu wa kawaida pale TRA kushitaki kuhusu rushwa

Ndesamburo anaweza akawa anapoint lakini jinsi alivyolitoa hiii issuendio nina tatizo nalo kwani huyu bwana aliakuwa na access na siri nyingi za serikali na hiii inanifanya ni question SANITY yake . At least angewasiliana na ma lawyer wake kwanza kabla ya kukurupuka ...in the end anaonekana kama ame liPOLITICISE issue ya muhimu na haieleweki sasa tumweke katika fungu gani ...so far sitaki kuwa judgmental lakini nadhani yuko close zaidi na MREMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom