Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Hivi inakuwaje watu wanaiona PCB kuwa kimbilio pale wanapotaka ushahidi, nje ya hapo wanaituhumu kuwa ni sehemu ya kuendeleza rushwa? ukweli wenyewe hatuna system ambayo inaweza kumshawishi mpenda haki yeyote yule kuwa muadilifu kwa system. Nafikiri wapenda haki wote kwa system yetu, kubwa wanaloweza kufanya ni kujiuzulu ili wasiendelee kupakwa matope kama wengine, lakini wengi wanaamua kuendelea, hivyo kwa hili tumpongeze tu Ndesamburo.
Kubwa naloliona hapa, ni kashfa kwa viongozi kutumia nafasi zao kulizima suala zima. Kwa spika kumwambia Ndesamburo afuate taratibu za Bunge, huku akijua wazi kuwa hakuna Mbongo yeyote atakayejua kwani taratibu za kamati si kila mtu anazijua, kuwa hakuna kitu kitakachotolewa nje!!!
 
DRwho,
Anzisha topic nyingine inayohusiana na huyo Bill Gates, hapa sio mahali pake, hata kama umesema "off topic" haitoshi kuhalalisha kuweka mchele kwenye mtori.
 
Hivi ni lini nchi hii wala rushwa watawekwa hadharani hata kama hatuna ushahidi. Kuwataja tu inatosha.
 
Kwenye huu mgogoro Lowasa na Manji wanahusika na Manji ni mwana mtandao wakati Mengi ni mzawa. PCB haiwezi kuwa na nguvu maana mkuu wa Rushwa ni Lowasa sasa watafanya nini na hawana meno na sheria zinawalinda akina Lowasa ?Kazi bado hii ni skandali kubwa lakini watanzania watasoma na kukaa kimya .Mwanasheria gani anaweza kuanza vurugu ? Haogopi kufutiwa leseni ?
 
Tulikwishasema dhambi ina tabia ya kuumbua. Sasa hii serikali lazima itafika mahala itaumbuka na machafu. Huu ni mwanzo. Ila hiyo ndio hivyo tena kama kawaida kuna watu wameshaanza kuyeyusha issue kwa kusema ni ukabila, tena kwenye forum hii hii, tuna kazi kwelikweli!
 
inashangaza jinsi habari hii iiliyowekwa mnachukulia kuwa ndio hali halisi ilivyo na ukweli...ushahidi wa kuwa EL anajua na akaweka hadharani kuwa wambunge wamepewa hongo na akamweleza Mengi uko wapi?? na kwa nini amweleze Mengi, na ili iweje?? hata kama PM anaissue zake basi sio kila jambo azushiwe tuu...
 
inashangaza jinsi habari hii iiliyowekwa mnachukulia kuwa ndio hali halisi ilivyo na ukweli...ushahidi wa kuwa EL anajua na akaweka hadharani kuwa wambunge wamepewa hongo na akamweleza Mengi uko wapi?? na kwa nini amweleze Mengi, na ili iweje?? hata kama PM anaissue zake basi sio kila jambo azushiwe tuu...

Kwanza,karibu kwenye forum maana hii ndio posting yako ya kwanza.Pili hongera kwa kasi ulokuja nayo ya kutaka kukanusha ishu ilhali huna hoja za kutosha.Je umesoma gazeti la Uhuru la leo?In case you didnt here is the story

Ndesamburo azushia wabunge rushwa

Ni kuhusu shauri la Mengi na Malima

Ajiuzulu ujumbe kamati ya bunge

Akaidi ushauri wa spika

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Moshi Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo, ameibuka na madai kwamba wajumbe wenzake wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, wamehongwa na mfanyabishara Yusuf Manji, ili wasitende haki.
Ndesamburo alisema kuwa hongo hiyo imetolewa ili kamati impendelee Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, aliyelalamikiwa na mfanyabiashara Reginald Mengi, kwamba alimkashifu katika hoja yake bungeni.
Ndesamburo aliwambia waandishi wa habari jana katika ofisi za Bunge kuwa, alitaarifiwa habari hizo na Mengi, aliyedai aliambiwa na Waziri Mkuu Edward Lowassa, katika mazungumzo yao binafsi.
Ndesamburo aliongeza: "Mwaka jana, Waziri Mkuu alimuita Mengi na kumwambia, usipoliondoa shauri utashindwa, Manji amewahonga wabunge wengi."
Kutokana na sababu hizo, Ndesamburo jana alitangaza kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, akidai anajiengua kutokana na kashfa ya rushwa iliyoighubika.
Mengi analalamika kukashifiwa na Malima kwamba katika kikao cha Bunge lililopita, alidai matangazo ya tevisheni ya ITV humpa mmiliki wake (Mengi) muda mrefu kuliko viongozi wa kitatifa.
Kwa mujibu wa Ndesamburo, licha ya Mengi kuarifiwa kupitia mazungumzo binafsi, aliona 'halivumiliki' na kuamua kumtaarifu yeye (Ndesamburo), jambo ambalo alilifikisha kamati husika, ambayo yeye pia ni mjumbe.
Aliendelea kudai baada ya kupewa taarifa hiyo kutoka kwa Mengi, alilifikisha kwenye kamati ambako hakuridhika na hatua inayochukuliwa.
Ndesamburo aliendelea kumkariri Mengi kwamba, kwa mara ya pili baada ya Waziri Mkuu Lowassa kupata taarifa kwamba suala hilo limefikishwa kwenye kamati, alimuita Mengi kwa mara nyingine ili amkane yeye, jambo ambalo Mengi alilikataa.
Hata hivyo, licha ya kumtambua Lowassa kama rafiki yake, hakueleza ni sababu zipi zilizomfanya asimfuate kumuona binafsi kuhoji ni kwa nini amechukua hatua hiyo.
Suala la Mbunge Malima na Mengi, sasa linajadiliwa kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kwenye kamati husika.
Alisema, viongozi wa bunge wakiongozwa na Spika Samuel Sitta, wamemsihi kwa muda mrefu hadi jana asubuhi asiendelee kulikuza suala hilo na aachane na azma yake ya kujiuzulu, lakini hakukubaliana nao.
Katika hatua ya kutatanisha, Ndesamburo aliamua kuita mkutano wa waandishi wa habari, kuliweka hadharani suala hilo, kwani alidai anahofu "maisha yake yako hatarini,"
Alipotakiwa kufafanua, alidai "Waziri Mkuu ni mtu mkubwa" na aliongeza hata binafsi asipokuwa na nia hiyo wapo wafuasi wake wanaoweza kumdhuru, japo alikiri hana ushahidi wowote wa madai hayo yanayomtia hofu.
Katika barua yake ya Kujiuzulu ya tarehe ya jana (Gazeti hili lina nakala yake), kwa sehemu inasomeka:
"Kwa masikitiko makubwa, naomba kukutaarifu sitoweza kuendelea kuwa mjumbe wa kamati kuanzia leo (jana) kutokana na kutoridhishwa na mtiririko wa kesi ya mheshimiwa Malima na Mengi."
Barua hiyo iliorodhesha sababu hizo kuwa ni: "kuwepo kwa madai kwamba wabunge wamepewa rushwa na Manji na kamati kutolifuatilia suala hili kujua ukweli wa mambo kabla ya kesi ya msingi kuamuliwa."
Sababu ya pili ni: "Kuwepo kwa mazingira ya mhimili wa utawala kuingilia mhimili wa Bunge ambayo ni kinyume na utawala bora na mgawanyo wa madaraka.
"Dhamira yangu inanisukuma kuamini kwamba mambo haya ni kikwazo cha ukweli na haki hivyo sitawatendea haki Watanzania walionichagua kuwawakilisha bungeni kama nitaendelea kushiriki katika kamati husika."


Ushauri wa bure ni kwamba kabla hujakurupuka kum-criticize mtu jitahidi kupata data za kutosha ili criticism yako iwe na maana.Wht about paying visits to our "normal" sources of daily news from TZ kabla ya hapa? (Sources hizo ni pamoja na ippmedia.com,uhuru.ifno.dailynews-tsn.com,majira.co.tz,mwananchi.co.tz,freemedia.co.tz...etc





tatizo ni kuwa hakuna mwenye hamu na magazeti ya bongo kwani mengi yanakuja kunyonya mambo humu
 
Mheshimiwa Philemon Ndesamburo amekuwa nyota njema ya alfajiri wacha in'gare mpaka kuche!! Hongera sana mheshimiwa kwa KUKUBALI KUISIKILIZA NAFSI YAKO AMBAYO INGEKUSUTA KAMA UNGEKUBALIANA NA UNAFIKI wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Sasa mambo yako hadharani: PCB mtafanya nini kwa hili? Rais kawapa mamlaka ya kutoingiliwa na mtu au chombo chochote (tayari hii imeisha kuwa sheria ndogo nadhani) itakuwa vizuri mkianzia na shahidi wa kwanza aliyetoa tuhuma hizi kwamba Manji kawahonga wabubge wengi - Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowasa.
PCB mtakuwa hamtendei haki walipa kodi kama madai haya hamtayafatilia kwa kina. Hili ni shauri ambalo mnapaswa kuliangalia kwa upana zaidi, Mheshimiwa Ndesamburo ni mbunge wa upinzani (anafanya biashara zake binafsi hivyo kwa kusema uongo rungu la dola analijua) hivyo alichosema ana uhakika nacho: Manji kahonga wabunge wengi!

kuna mtu anaweza kutufungua kuhusu kesi ya MENGI na MALIMA bila a kuwa biased?

Mwaka jana Mheshimiwa Malima alimtuhumu Mengi kwamba vyombo vyake vya habari hususani television vinapeperusha kwa muda mrefu zaidi mambo yake (Mengi) kuliko ya Rais hivyo Mengi akapeleka hili swala kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akidai amekashifiwa.

Sijui kama hii kamati ina mamlaka kama ya Mahakama kuweza kuhukumu au vinginevyo.
 
Wewe si Africansista bali ni Rushwasista mpuuzi wewe . Unaleta hadithi za Mkapa kuomba ushahidi wa rushwa kwenye mikutano ya hadhara ?Walio kutuma kuja hapa na hoja mbuzi rudi waambie hapa tuko macho . Kwanza wewe ni mgeni na kamba mguuni na matongotongo .
 
DrWHO,
The point I was trying to make was that the PM has said, either in public or in private, that MP's have been bribed by Manji. It is not up to me to come with the evidence, but the Prime Minister and as a leader of the government what steps has he taken to deal with this illegal act? That was my question, and still is.
 
Mzee Jasusi you have thrown a very tough question which I am sure Mswahili , Africasista and the likes will never get back to this forum with any answers. The ball is in CCM's court. Will you come out and explain in details about these allegations Mr. PM ?
 
tibwilitibwili

inasikitisha kuona kuwa huna busara na kutukana ovyo wenzio, huyo africansister katoa maoni yake sasa kama ww hujarizika jibu kistaarab, na ati kuwa ndo katuma mara moja kuwa ndo mshamba, ww ndo mshamba zaidi na mie ntukane basi. maana maneno yako manyaufu yanaonyesha ulivyokuwa huna busara. au na ww wa kule kaskazini msipingwe MKIPINGWA HUWA NOMA, AU ww ndo bora kuliko wote.
inashangaza kutokuwa mstaarab. ustaarab ni bure. jirekebishe tabia yako na umuombe radhi hazarani paka weeee
 
haya ndiyo mambo ya kina Trump, Rosie, na Barbara Walters.. nani alisema nini na wapi ni vigumu kweli kulipatia ushahidi isipokuwa kama kuna barua, video au rekodi ya mazungumzo hayo! Vinginevyo ni kujitafutia mashtaka yasiyo ya lazima.

Kama kweli Ndesamburo amehisi kuna ubaya huo angejitahidi kurekodi mazungumzo hayo na wakati anajiuzulu angesema anao ushahidi!! Haya ya kusema "Wamenitishia kuniua" walikutishaeje anaulizwa anasema "sina ushahidi" ni madai ya kitoto!

Kama hakuridhika na jinsi shughuli inavyoendesha ana kila haki ya kujiuzulu. Lakini kama anajiuzulu kwa sababu "amesikia" au "ameona" hili ama lile lakini hana ushahidi nalo basi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, hachezi!
 
Kwa hiyo MwakJJ unataka kusemaje ? Maana sijakuelewa unachotaka kutueleza kwamab Ndesambura ni muongo ama hakuna ukweli ?Tusaidie .
 
tibwilitibwili

inasikitisha kuona kuwa huna busara na kutukana ovyo wenzio, huyo africansister katoa maoni yake sasa kama ww hujarizika jibu kistaarab, na ati kuwa ndo katuma mara moja kuwa ndo mshamba, ww ndo mshamba zaidi na mie ntukane basi. maana maneno yako manyaufu yanaonyesha ulivyokuwa huna busara. au na ww wa kule kaskazini msipingwe MKIPINGWA HUWA NOMA, AU ww ndo bora kuliko wote.
inashangaza kutokuwa mstaarab. ustaarab ni bure. jirekebishe tabia yako na umuombe radhi hazarani paka weeee kasoro mkia
 
Ndesamburo might have a point here, lakini kwa namna alivyoiweka ni ngumu sana kuiprove ... na rahisi sana yeye kugeuziwa kibao.
 
Hakika tuhuma ni nzito.Kubwa kabisa hapa Bwana Ndesamburo,kwanza wewe mwenyewe katika kugombea Ubunge hukutoa Rushwa?
Pili madai yako na kauli yako ni kielelezo tosha,kwamba hata wewe mwenyewe inaonyesha huyo Mengi kakupa kitu kidogo!!!Je unabisha juu ya hilo?
 
Wacha tuone kamati nyingine ya Bunge imwite maana ndiyo wabunge wa CCM wanapenda sana kuliko kujadili mambo ya maendeleo kwa Tanzania .Naamini Mzee Ndesa anaujua ujasusi wa CCM na kaamua kusema he knows well how to get out of that mess.
 
Mzee ndesa ni shujaa, amejitoa muhanga, ninahakika anajua nini anachosema hawezi na hajawa na historia ya kukurupuka ni mtu wa hoja hata wapinzani wake wa moshi mjini wanamjua kwa hilo.

Tukipata watu 100 wasioogopa kufa kama mzee Ndesa ufedhuli utakwisha
 
Hakika tuhuma ni nzito.Kubwa kabisa hapa Bwana Ndesamburo,kwanza wewe mwenyewe katika kugombea Ubunge hukutoa Rushwa?
Pili madai yako na kauli yako ni kielelezo tosha,kwamba hata wewe mwenyewe inaonyesha huyo Mengi kakupa kitu kidogo!!!Je unabisha juu ya hilo?


Haya mzee wa london karibu nawe. Sijafahamu unachotaka kusema hapo juu-unajaribu kuhalalisha rushwa au namna gani? Yaani kama Ndesamburo alitoa rushwa (kama kweli una ushahidi na hili) ndio kusema basi rushwa imeshakuwa haki na kwamba ilikuwa ni sawa hao wabunge kuhongwa na Manji?

Jamani, nyie wageni mchukuage muda kidogo wa kutafakari kabla hamjarukia hoja, eboooo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom