Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Waislamu wote ambao walijitahidi kupata elimu wakanyimwa, au kujiendeleza wakakatazwa, au wakanyimwa kupandishwa vyeo kwa sababu ya dini yao tu wanyoshe mikono !!
 
Mwanakijiji
wasiliana na professor Hamza Njozi-Head of literature Department-University of Dar-es-salaam,
wasiliana na Mzee Abood Jumbe Mwinyi au soma kitabu chake cha miaka 30 ya dhoruba au the partnership-kwani alifanya kazi bega kwa bega na Nyerere.
wasiliana na Mzee skykes hawa familia yao ilimlea na kumsaidia sana Nyerere,
wasiliana na chief Fundikira,
pia pitia kitabu cha Mohammed -Said kilichochapishwa na Minerva-press-London(1998)
jitahidi uwapate hao wazee maana bado wapo hai.
Professor njozi anayo orodha na unaweza kupata contact zake kwenye website ya UDSM.

Administrator
nimemchimba nani? au unaamua tu kutoa onyo?anyway wewe ndio umeshika mpini
 
Mwanakijiji
Nimekupa vyanzo vya watu walioonewa kwa ajili ya dini yao.mbona kimya? au zoezi gumu?
wasiliana na Professor Tigiti Sengoh huyu Nyerere aliacha waraka asipate kazi kwa ajili ya uislam wake.
 
Mzee Mengi anadaiwa na International Finance Corporation IFM-ya Washington hadi november mwaka jana deni lilikuwa limefikia dola milion 10.
Mzee Madeni hadi kwenye kope, ndani na nje ya nchi.
Na familia ya professor Mazengo iko mbioni kumfungulia kesi, alipokelewa na Familia hiyo na kuishi naye UK, akatumia credit kadi za MAREHEMU Professor Mazengo na hakulipa. fadhila yote aliyopewa na bado kawazika?
 
Mswahili unajua habari hizi unaweza kumwandikia Mengi moja kwa moja kwa urahisi badala ya kutuletea hapa habari za umimi na uwewe na Mengi ? Hapa issue ni moja nayo ni NSSF mengine sidhani kama yana msaada kwa wachangiaji . Huna mambo mengi ya kusema ila kuwashambuliwa watu usio wapenda kila siku ?
 
mswahili said:
Mwanakijiji
Nimekupa vyanzo vya watu walioonewa kwa ajili ya dini yao.mbona kimya? au zoezi gumu?
wasiliana na Professor Tigiti Sengoh huyu Nyerere aliacha waraka asipate kazi kwa ajili ya uislam wake.

Mswahili, nitashukuru ukinipatia contacts za watu hawa:

Padre Camillus Lwambano
Mzee Skyes
Mzee Jumbe
Kardinali Pengo
 
wanabodi,

Hapa napata utata hivi kweli Mh Jumbe anaweza kusema au aliyoaandika kwenye hicho kitabu ukatilia maanani? Huyu mtu alituhumiwa kuwa hautaki muungano, and is the same person amenyanyuliwa na kuamua kuishi bara kwa watu ambao alikuwa hawataki, hivi kweli huyu ni mtu wa kuaminika?

Jasusi,
Unaneno la kuongezea hapa? kwi kwi kwi
 
Mr. Hussein Abdallah a.k.a Mlalahoi.
Pole sana kwa kubadili jina ili kuwadanganya wanaforum, utawaongopea wajinga tu. Toka lini Mlalahoi akawa Hussein?

Unasema masuala ya Mengi hapa sio mahala pake jee nipeleke wapi? au kwenye gazeti lako la Msemakweli?

Ukitizama kichwa cha mjadala huu ni Mengi + IPP NA MABILIONI YALIYOPTEA au huoni?
pili Mjadala huu uliletwa na Nungwi kwa kichwa cha habari Reginald Mengi na mabilioni yaliopotea ambapo wewe Hussein a.k.a Mlalahoi ukaja na jazba zako za kidini na kusema hiyo ni jihad ukamshambulia sana Kulikoni, kipindi hicho mie ni msomaji tu. nikaona nikufahamishe nini maana ya Jihad na mujahidina ni nani? toka hapo ukaanza kunishambulia kwa matusi yasio na mfano(ukasema mimi ni mwanao wa kambo).

kwa vile nakujua sikujibu kitu, nilijua kabisa nani anakutuma(Mengi) na niliweka wazi hilo mapema.
Unaposema hapa tusiweke mambo binafsi sio wewe uliotudanyanga kuwa mwezi huu kuwa JK atarudi marekani kwa kimwana wake? na ukasema umeongea na dada mmoja,jee hiyo ulikuwa unajadili NSSF? kwanini usimtumie ujumbe moja kwa moja JK? au kwanini usimtumie professor Kapuya moja kwa moja? kuliko kuleta humu hoja zenu binafsi?

Hata huo ujumbe wako wa konono wapelekee CCM unaleta humu wa nini? kwa maelezo yako unataka kusiwe na majina ya watu, tutajadili vipi hoja bila kuwataja wahusika? na wewe ukitaja hakuna dhambi, nikitaja skendo za watu unakuja juu, najua hadi mpango wako wa kutaka kuvuruga mjadala huu mapema sana nami nikamwambia kuwa kuna watu wamechukua kitu kidogo kuja kumkingia kifua Mzee Mengi.

ukitazama maandiko yangu ya Jana nimezungumzia kuhusu DENI LA MILION 10 DOLA ZA WASHNGTON NA HATA KICHWA CHA HABARI KINAZUNGUMZIA MAMILIONI YALIPOTEA KWA JINA LA MENGI, sasa wapi nimetoka nje ya mstari? kwanini usifuatilie huko Washington na ukasema Mswahili muongo? ila unadakia kuwa hapa hazungumzwi mtu binafsi.

unadai nawachukia watu kwani wewe unavyomshambulia JK unamchukia au unamuelekeza jinsi ya kutenda?

Mie simchukii Mengi ila nitakemea vitendo vyake viofu ili ajirekebishe, mtu kawazima watoto wa Professor Mazengo badala ya wewe kuwafuatilia hawa vijana walidhulumiwa au ungefanya utafiti kuwa habari hii sio ya kweli unakupuka tu kutetea hata Mzungu wa watu alivyozimwa wewe ukaja juu kuwa hakuna madhara kwa mzungu kudhuliwa na akina Mengi akishirikiana na kaka yake Benjamin tukakwambia suala lile liko House of Commons na nchi inapakaziwa wewe ulitiza tumbo lako tu,
Acha hizo. mie habari hizi kanipa Hagu mtoto wa PROFESSOR Mazengo fuatilia uone kama majungu au laa.

Mwanakijiji.
Uko serious na kazi yako ya habari au nawe unakuja na mambo ya udini? kweli umeweza kumuhoji Mnyika na hujui wapi utapata contact za Mzee wetu PENGO? umeweza kumpigia cm mhariri wa mwananchi huku hakujui wala nini na ukamshawishi na kupata interview naye, mbona hukuniuliza contact za kina Dr.Slaa? Umeweza kumuhoji Waziri wa habari, leo wewe wakuniuliza mie contact za Mzee JUMBE? wewe mwandishi wa KLH NEWS inayokaribia kusikika nchi 50 duniani hujui utampa vipi padre Lwambano? wewe mwandishi wa KLH NEWS hujui Sykes utampata vipi? kifupi ukiwauliza waandishi wowote wa magazeti watakupa contact zao.
mtumie email Balile atakusaidia.
umeweza kuwajua akina Ponda na Khalifa Hamisi leo hujui wapi utapata contact za hawa watu maarufu? umeweza kupata contact za Richmond na familia yote umetutajia, leo hujui contact za Kardinar Pengo? umeweza kutuletea maelekezo ya msiba wa vijana wetu Marekani hadi maziko(ulifanya kazi nzuri sana nakupongeza)nadhani unanitania.

nimekwambia kwa waislam walioonewa wasiliana na Professor Njozi jee umeshafanya?

pia magazeti yote, radio zote,TV zote za dunia zilitangaza habari za pope kuwa kashfu watu wa dini nyingine
with exceptional of KLH NEWS ambapo kauli mbiu yake 'yote yanasema hapa haugopwi mtu hapa'.

Nimekuwa msikiliza mzuri wa Radio yako karibu kila siku na nakupongeza kwa juhudi yako nahisi unajitolea hulipwi na mtu, ila kama utakuwa busy kujua ofisi za richmond lakini hufuatilii Washington kujua kama Mzee MENGI alipoteza vipi pesa za UN kwa ajili ya ukimwi huku akiwa chairman wa masuala ya ukimwi TZ kwani hizo pesa hazikuwa zake ni za taifa.
naomba uwe kama mwanabodi mmoja humu FD kauli mbiu yake " Mtazama pande mbili za shiling"
 
mswahili, nilipoomba contacts za watu hao ni kwa sababu nilifikiri ungeweza kunisaidia. Ni kweli nina uwezo wa kutafuta contacts hizo kwa njia nyingine na nilikuwa sikutanii. Kuhusu mambo mengine usiwe na wasiwasi.. tofauti ya KLH News na vyombo vingine vya habari vya kibongo maslahi yetu ni Tanzania na Tanzania peke yake. So, usiwe na shaka rafiki yangu KLH News iko busy kuwaletea habari from the news makers of today!!!
 
inaelekea kumekuwa na kimya kingi kuhusu kesi ya hawa watu wawili au ndio kesi ya DITO inawakeep bize huko mahakamani?

Je na ile kesi iliofunguliwa na WARIOBA iliishia wapi?

kuna update zozote?
 
Labda kuteuliwa kwa majaji wapya kutafanya kesi ziende kwa kasi mpya!

Wazee wa data, DPP mpya atakuwa nani? Prof Abdallah Safari??
 
KESI ZIPO NYINGI SANA

Usishangae kesi zipo nyingi sana na matatizo ni muda wa kusikiliza kesi zenyewe. Halafu mizegwe mingi - ushahidi n.k.

Lakini ya braza Dito yeye alie tu atakaa si chini ya miaka minne labda rafikiye aingilie kati.
 
Ndesamburo azushia wabunge rushwa

Ni kuhusu shauri la Mengi na Malima

Ajiuzulu ujumbe kamati ya bunge

Akaidi ushauri wa spika

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Moshi Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo, ameibuka na madai kwamba wajumbe wenzake wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, wamehongwa na mfanyabishara Yusuf Manji, ili wasitende haki.

Ndesamburo alisema kuwa hongo hiyo imetolewa ili kamati impendelee Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, aliyelalamikiwa na mfanyabiashara Reginald Mengi, kwamba alimkashifu katika hoja yake bungeni.Ndesamburo aliwambia waandishi wa habari jana katika ofisi za Bunge kuwa, alitaarifiwa habari hizo na Mengi, aliyedai aliambiwa na Waziri Mkuu Edward Lowassa, katika mazungumzo yao binafsi.Ndesamburo aliongeza: "Mwaka jana, Waziri Mkuu alimuita Mengi na kumwambia, usipoliondoa shauri utashindwa, Manji amewahonga wabunge wengi."

Kutokana na sababu hizo, Ndesamburo jana alitangaza kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, akidai anajiengua kutokana na kashfa ya rushwa iliyoighubika.

Mengi analalamika kukashifiwa na Malima kwamba katika kikao cha Bunge lililopita, alidai matangazo ya tevisheni ya ITV humpa mmiliki wake (Mengi) muda mrefu kuliko viongozi wa kitatifa.


Kwa mujibu wa Ndesamburo, licha ya Mengi kuarifiwa kupitia mazungumzo binafsi, aliona 'halivumiliki' na kuamua kumtaarifu yeye (Ndesamburo), jambo ambalo alilifikisha kamati husika, ambayo yeye pia ni mjumbe.
Aliendelea kudai baada ya kupewa taarifa hiyo kutoka kwa Mengi, alilifikisha kwenye kamati ambako hakuridhika na hatua inayochukuliwa.
Ndesamburo aliendelea kumkariri Mengi kwamba, kwa mara ya pili baada ya Waziri Mkuu Lowassa kupata taarifa kwamba suala hilo limefikishwa kwenye kamati, alimuita Mengi kwa mara nyingine ili amkane yeye, jambo ambalo Mengi alilikataa.

Hata hivyo, licha ya kumtambua Lowassa kama rafiki yake, hakueleza ni sababu zipi zilizomfanya asimfuate kumuona binafsi kuhoji ni kwa nini amechukua hatua hiyo.

Suala la Mbunge Malima na Mengi, sasa linajadiliwa kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kwenye kamati husika.Alisema, viongozi wa bunge wakiongozwa na Spika Samuel Sitta, wamemsihi kwa muda mrefu hadi jana asubuhi asiendelee kulikuza suala hilo na aachane na azma yake ya kujiuzulu, lakini hakukubaliana nao.Katika hatua ya kutatanisha, Ndesamburo aliamua kuita mkutano wa waandishi wa habari, kuliweka hadharani suala hilo, kwani alidai anahofu "maisha yake yako hatarini,"

Alipotakiwa kufafanua, alidai "Waziri Mkuu ni mtu mkubwa" na aliongeza hata binafsi asipokuwa na nia hiyo wapo wafuasi wake wanaoweza kumdhuru, japo alikiri hana ushahidi wowote wa madai hayo yanayomtia hofu. Katika barua yake ya Kujiuzulu ya tarehe ya jana (Gazeti hili lina nakala yake), kwa sehemu inasomeka:

"Kwa masikitiko makubwa, naomba kukutaarifu sitoweza kuendelea kuwa mjumbe wa kamati kuanzia leo (jana) kutokana na kutoridhishwa na mtiririko wa kesi ya mheshimiwa Malima na Mengi." Barua hiyo iliorodhesha sababu hizo kuwa ni: "kuwepo kwa madai kwamba wabunge wamepewa rushwa na Manji na kamati kutolifuatilia suala hili kujua ukweli wa mambo kabla ya kesi ya msingi kuamuliwa." Sababu ya pili ni: "Kuwepo kwa mazingira ya mhimili wa utawala kuingilia mhimili wa Bunge ambayo ni kinyume na utawala bora na mgawanyo wa madaraka. "Dhamira yangu inanisukuma kuamini kwamba mambo haya ni kikwazo cha ukweli na haki hivyo sitawatendea haki Watanzania walionichagua kuwawakilisha bungeni kama nitaendelea kushiriki katika kamati husika."

Source:JANUARI- 11,2007
 
Hongera Philemon Ndesamburo kwa kuweka ukweli nje, na mwenye macho haambiwi tazama. Sasa haya ndio mambo ambayo wabunge wetu wanatakiwa kuiga mfano na tunataka yasiishie kwenye vyombo vya habari ni lazima Mtoa rushwa na wapokeaji wachukuliwe hatua. Ushahidi mkubwa kabisa huu hatuwezi kunyamaza.

Vile vile ni lazima JK aunde kamati nje ya vyombo vitakavyoshughulikia rushwa kuchunguza mwenendo wa Waziri Mkuu EL katika maswala yote yanayomuhusu kiutendaji.
 
Wachagga(Mengi na Ndesamburo.

wameona hakuna muelekeo wa kushinda sasa wanatafuta sababu. kuwepo Ndesamburo kwenye kamati ni makosa sababu yuko BIAS hawezi kumuacha mchaga mwenzie anaumbuka.
Mengi Maji shingoni kuna tape aliifanyia usanii kwa kuikata na kuwa na dakika 2 na nusu huku original ilikuwa na dakika kumi. na bunge wanayo yenye dakika kumi.
Ndesamburo kama rushwa PCB wapo kwanini usiripoti?
 
This is a serious issue na nashangaa kwa nini malawyer bongo wameilalia hili kwani hapa pesa ni nje nje

Ndesamburo ametoa madai mazito ambayo yanaweza kuiangusha serikali kwa sababu madai ya rushwa inamaana kesi inamuunganisha

MENGI,WAZIRI MKUU na MALIMA

sina details kamili lakini najua hapa kuna uwezekano mkubwa wa kufungua kesi ya madai

on a fli side


kuna mtu anaweza kutufungua kuhusu kesi ya MENGI na MALIMA bila a kuwa biased?

naomba mrefrain kupaste article za magazeti kwani wao nao wanakuja kunyonya habar humu
 
Mswahili,
Acha ukabila wako. The real issue here is Lowassa as waziri mkuu. Yeye alishajua kuwa wabunge wamehongwa na anayo madaraka ya kuchukua hatua kwa nini kakaa kimya? That is the issue here na si Wachagga. DrWho, Lowassa ni kiongozi wa serikali. Anajua kuwa wabunge wake wameshahongwa. The question here is what has he done to make sure justice is served?
 
Alijuaje?

evidence alipewa?

je kama kulikuwa an hongo taasisi ya kuzuia rushwa wanayo taarifa?

sasa justice itakuw served on article za magazeti?

nikuulize unajua kesi za rushwa ngapi zimelaa mpaka leo

issue ni nzito na inahusiana na rushwa lakini nadhani ni bora vyobo vya serikali kama polisi vikafanya uchunguzi then kama kuna kesi ya kujibu hapo sasa faili lipelekwe wa wafungua mashtaa then watuhumiwa waitwe ajiteteee kisha hukumu itolewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom