Mchina jela miezi mitano kwa kuua tembo 511, Mtanzania jela miaka 60 kwa kukutwa na meno ya tembo na kiboko

Siku za karibuni katika mtandao wa Whatsapp na Twitter imekuwa ikisambaa picha iliyounganishwa ikionesha hukumu za matukio mawili yanayohusisha watuhumiwa waliokamatwa na nyara za serikali (Meno ya tembo).
Ya kwanza ni taarifa ya Disemba 16 2019 inayomhusu Bi Haika Mgao na inasomeka:

"Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu, Haika Mgao (26) kutumikia kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno ya tembo na ya kiboko yenye thamani ya Shilingi milioni 69.5, mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

View attachment 2449815

Ya pili ni ya tarehe 15 Disemba 2019 inamhusu Rais wa China China, Liang Hu na inasomeka:
"Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu raia wa China, Liang Hu kulipa fidia TZS 50 milioni kwa kosa la kuua tembo 511 wenye thamani ya TZS 7 bilioni. Pia alitakiwa kulipa faini TZS 300,000 au kifungo cha miezi mitano jela. Mtuhumiwa aliandika barua kwa DPP kukiri makosa yake."

View attachment 2449819

Matukio yote mawili ni ya mwaka 2019 na hukumu zake zilipishana siku tano tu, tena ikianza ile ya raia wa kigeni kisha ikafuata ya binti wa miaka 26 tu.

"Wakati tunapiga kelele kusema alikuwa ra**s wa wanyonge tukumbuke alimfunga miaka 60 binti wa miaka 26 kisha akamuachia huru kinara na malkia wa mauaji wa tembo aliyeua tembo zaidi ya 510"
Hujamuona Nanyaro Ephata alipoileta hapa?
 
Hivi meli ya kinana iliyokamatwa na meno yake ya tembo kutoka kwenye uwindaji haramu ilipewa adhabu gani?
Ebu tukumbushane kidogo.
 
Kuna Raia wa CHINA amehukumiwa kulipa Faini Sh Mil.50 baada ya kuua Tembo 511 wenye thamani ya Tsh Bil.7 tena kwa MAKUBALIANO na DPP

Pia kuna mtanzania kakutwa na MENO ya Tembo yenye thamani ya Tsh.Mil.69 kafungwa Miaka 60 Jela. Kuna KESI ya CAG Iliyomkuta RAis Magufuli na Hatia ya KUKIUKA KATIBA ya NCHI kwa Kumfuza kazi CAG kinyume na KATIBA

Jambo la Ajabu Mwanasheria Mkuu wa Serikali anataka Kukata RUFAA dhidi ya Hukumu ya Rais MAGUFULI ya Kukiuka KATIBA wakati hata TIJA yake Kitaifa haipo .Binafsi ningempongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Endapo angekata RUFAA kesi ya RAIA wa CHINA Aliyehukumiwa kulipa FAINI ya Tsh Mil.50 kwa Kuua TEMBO 511 na kukutwa na Meno yenye Thamani ya BIL.7 Kesi ambayo ina TIJA kwa TAIFA.

hilda_newton_chadema_1671258830290419.jpg
 
Mbele ya macho ya Sheria "status " inaamua uwekwe kundi lipi??
Sasa huoni huyo mchina alivyopewa adhabu ndogo kwa kosa kubwa na hao watanzania waliopewa adhabu kubwa kwa kosa dogo.
Unafikiri sababu ni nini labda?
Au yule mfanyabiashara wa Mwanza aliyeua watu 2 kisha akaachiwa huru unafikiri sababu ni nini?
 
Hao tembo Ni raia wa wapi bongo tembo huwezi ua kiasi hicho maana hawako hifadhi moja wote hao

Kwa hio tembo mzima million 13 tu
Nimeona hii habari mtandaoni imenishangaza kama sio kosa la kiuandishi.Raia wa China amekutwa na kosa la kuua jumla ya tembo 511 wenye dhamani ya bilioni 7 amehukumiwa jela miezi mitano au kulipa faini ya laki tatu.

Kwa upande mwingine Mtanzania aliyekutwa na meno yenye dhamani ya milioni sitini na tisa kalambwa miaka 60

Wadau wa sheria tusaidieni hapa!


View attachment 2449142
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom