Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,810
- 11,978
MENO YA TEMBO YAMPELEKA GEREZANI MIAKA 30.
Na Steven Augustino, Tunduru
Hakimu Mkazi mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Honorus Kando amemhukumu mkazi wa Kijiji Cha Nalasi Bw. ISSA Salumu Makale (35) kutumikia kifungo Cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande 13 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 35.25 vyenye Thamani ya shilinngi za Kitanzania 104,041,350,000 Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Hukumu hiyo imetolewa April 18 mwaka huu baada ya Mahakama kujiridhisha bila kutia shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na mashahidi 7 wa upande wa Jamhuri.
Akisoma shauri hilo la uhujumu uchumi namba 30/2022 Mbele ya Hakimu Kando Mwendesha Mashtaka Mkaguzi msaidizi wa Polisi Bw. Ernest Machiya alisema kuwa mtuhumiwa huyo alinashwa na mtego ulio andaliwa na maafisa wanyama pori waliojifanya wanunuzi wa meno hayo Mey 27/2022.
Alisema kwa kufanya hivyo mtuhumiwa huyo alitenda kosa kinyume Cha kifungu namba 86(1) na (2)(c)(1) Cha sheria ya uhifadhi wa wanyama pori namba 5 ya mwaka 2009 ikisomwa pamoja na paragraph ya 14 ya Jedwali la kwanza na kifungu namba 57 (1) na 60 (2) Cha sheria ya uhujumu uchumi na makosa yaliyo angaliwa sura ya 200.