Je, Israel iko tayari kwa taifa huru la Palestina?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141

Je, Israel iko tayari kwa taifa huru la Palestina?​


fgvcgf
Vita vya kutisha vinaendelea kati ya Israel na Hamas kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Maelfu ya watu kutoka pande zote mbili wamepoteza maisha. Mwisho wa vita hivi haujuulikani.

Vizuizi vya kufikia makubaliano ya kumaliza vita vimekuwepo kwa miongo kadhaa. Mipaka ya Israel na Palestina, hadhi ya mji wa Jerusalem, kurudi kwa wakimbizi wa Palestina na matumizi ya ghasia kama silaha ya kisiasa - haya yote yamekuwa kikwazo cha amani.

Makazi ya Walowezi ni Kikwazo​

FDVC


Wakati Mkataba wa Oslo ulipotiwa saini mwaka wa 1993, kulikuwa na walowezi wapatao 110,000 wa Israel katika Ukingo wa Magharibi na wapatao 140,000 huko Jerusalem Mashariki.

Suala la makazi lilipaswa kutatuliwa baadaye, na mikataba iliyotiwa saini na Israel na Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) ilipiga marufuku kuundwa kwa vitongozi vipya. Miaka 30 baadaye, zaidi ya Waisraeli 700,000 wanaishi katika ardhi za Palestina, kwa mujibu wa B'Tselem, shirika la haki za binadamu katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Kati ya walowezi hao, takriban laki tano wanaishi Ukingo wa Magharibi na karibu laki mbili wanaishi Jerusalem Mashariki.

Dov Waxman ni mkurugenzi katika Kituo cha masomo ya Israel katika Chuo Kikuu cha California anasema.
"Kupanuliwa kwa makazi ya walowezi ni kikwazo cha amani," aliiambia BBC. "Sio tu kwa sababu ya idadi ya makaazi, lakini kwa sababu Wapalestina wanaona hii kama ishara kwamba Israel haitaki kabisa kuruhusu taifa huru la Palestina."

Vita kati ya Israel na majirani zake nchi za Kiarabu vilimalizika baada ya mapigano ya 1949. Baada ya hapo, kile kinachojulikana kama Green Line. Mstari wa Kijani uliogawanya Jerusalem katika sehemu mbili uliwekwa. Pia pakawekwa mipaka ya Ukingo wa Magharibi na Gaza.

Wakati wa Vita vya Siku Sita 1967, Israel iliteka Jerusalem Mashariki, Gaza na Ukingo wa Magharibi. Serikali za Israel ziliendelea kujenga makazi ya Wayahudi, na kupuuza Mstari wa Kijani. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, makazi haya yote ni kinyume cha sheria.

2005 Israel iliharibu makazi ya walowezi huko Gaza na kujiondoa. "Ujenzi wa makazi ulianza miezi miwili tu baada ya vita vya 1967. Umeendelea chini ya serikali zote za Israeli, bila kujali itikadi zao za kisiasa," anasema Eyal Haruveni, mtafiti anayehusika na masuala ya makazi kutoka B'Tselem.

Makubaliano ya Oslo II yaligawa Ukingo wa Magharibi katika maeneo matatu: A, maeneo ya miji ya Palestina. Yalipaswa kuwa chini ya udhibiti wa raia na polisi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina (PNA). Kanda B - chini ya udhibiti wa Palestina na jeshi la Israel na Kanda C - chini ya udhibiti wa jeshi na raia wa Israel. Eneo C ni takribani asilimia 60 ya ukingo wote.

Wapalestina na mashirika kama B'Tselem wanalaani Israel hairuhusu Wapalestina kujenga katika eneo C, huku ikiruhusu makazi ya Wayahudi kujengwa na kuongezwa.

Asilimia 20 ya Ukingo wa Magharibi na sehemu kubwa ya Bonde la Jordan, ambako kuna vyanzo vya maji, yamechukuliwa na Israel kama maeneo ya kufanya mafunzo ya kijeshi. Wapalestina hawaruhusiwi kwenda huko. Khaled Abu Tomeh, mtafiti wa masuala ya Wapalestina katika Kituo cha Sera za Umma mjini Jerusalem, anasema, makazi haya ni kikwazo cha kuundwa kwa taifa huru la Palestina.

Mgawanyiko wa kisiasa​

rtfgbv


Baada ya kuanzishwa kwa Hamas mwaka 1987, harakati ya kitaifa ya Palestina iligawanyika. Hamas ilipata udhibiti wa Gaza kufuatia ushindi wa ubunge wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina. Hii ilizidisha mgawanyiko kati ya Wapalestina.

Hamas ilitawala Gaza, huku PA iliyokuwa inaongozwa na Fatah ikiendelea kudhibiti Ukingo wa Magharibi. Tangu wakati huo hakuna uchaguzi wa marudio uliofanyika na Rais wa Mahmood Abbas anasalia katika wadhifa wake.

Mtafiti kutoka taasisi ya Chatham House, Elham Fakhro anasema Israel ilikataa kufanya mazungumzo na Hamas na Hamas ilikataa kufanya mazungumzo na Israel. Hakuna mazungumzo kati yao.

Marekani na Umoja wa Ulaya wanachukulia Hamas kama shirika lenye msimamo mkali. Na mazungumzo yalitatizika zaidi kutokana na mabadiliko ya siasa za Israel na serikali kuwa ya mrengo mkali wa kulia.

Serikali ya sasa ya Israel ndiyo serikali ya mrengo mkali wa kulia katika historia yake ya miaka 75. Mawaziri wa Waziri Mkuu Binyamin Netanyahu wanaamini Israel inapaswa kukalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi.
Kwa mujibu wa wachambuzi, msimamo wa serikali za Marekani na Kiarabu katika miaka ya hivi karibuni pia umeathiri mchakato wa amani.

Fakhro anasema tangu Rais Donald Trump, Marekani imejikita kuzungumza na nchi nyingine za Kiarabu ili kukuza uhusiano kati yao na Israel kupitia Mkataba wa Abraham badala ya mazungumzo na Wapalestina.
Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na Morocco, Falme za Kiarabu na Bahrain yalibadilisha mwelekeo wa nchi za Kiarabu. Nchi hizi kwa miaka mingi zilikataa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel hadi makubaliano ya amani na Wapalestina yafikiwe. Katika miezi ya hivi karibuni, Saudi Arabia na Israel pia zimekuwa na mazungumzo.

Kuongezeka Vurugu​

tgfbv

Maelezo ya picha: Watoto wakimbizi wa Palestina

Mwaka jana ulikuwa mbaya zaidi kwa Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi. Kumekuwa na ongezeko la visa vya mauaji. Mashambulizi yameongezeka tangu Oktoba 7 mwaka huu. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Wapalestina 158 wakiwemo watoto 45 wameuawa.

Vilevile ghasia za wanamgambo wa Kipalestina ni kikwazo kikubwa cha amani. Israel ilikumbwa na mauaji makubwa zaidi tangu kuanzishwa kwake Oktoba 7 - wanamgambo wenye itikadi kali wa Hamas walipovuka na kuingia Israel, na kuua zaidi ya watu 1,400 na kuwateka nyara wengine 245.

Kwa sasa zaidi ya watu 10,000 wameuawa katika hatua ya kulipiza kisasi ya Israel huko Gaza. chanzo. Je, Israel iko tayari kwa taifa huru la Palestina? - BBC News Swahili
 
Back
Top Bottom