TANZIA Mchekeshaji maarufu MC Pilipili afariki dunia

TANZIA Mchekeshaji maarufu MC Pilipili afariki dunia

Taarifa zilizotufiukia hivi punde katika chumba chetu cha habari, zinaeleza kuwa mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Emmanuel Mathias almaarufu MC Pilipili, amefariki dunia ghafla mchana leo, Novemba 16, 2025.

Taarifa zinaeleza kuwa, MC Pilipili alisafiri kuelekea jijini Dodoma ambapo jioni ya leo alitarajiwa kwenda kufanya kazi yake ya ushereheshaji jijini humo, lakini akafikwa na mauti.

Global TV imezungumza na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi ambaye amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.


View attachment 3502851

Source: Global TV Online
Hiyo picha ya pili akiwa amevaa hayo manguo ya laana ya kijani umeiongezea ya nini? Kwani amekufa akiwa katika harakati za chama? Au ni chambo unataka watu wachafukwe? Iondoe bana!
 
Kiukweli toka aachwe na yule mkewe, MC hakua sawa, nishawahi kuwa nae karibu ktk event fulani hivi, the way alivyokua ana act, ni km mwenye depression, yaan sijui nisemeje.

Apumzike salama!
Yah, kuna namna naweza kukuelewa na kuwaelewa wale wanaoteswa na wanawake/ndoa mana hata mm kuna namna nilishawahi kupitia humo japokuwa haikuwa ndoa.

Tujifunze kupenda kwa kiasi, kupenda sana na kuweka matarajio makubwa kunaumiza mno hasa unapopenda sehemu isiyo sahihi.
 
Back
Top Bottom