Mbivu na mbichi za Wagombea Uspika wa CCM kujulikana leo Januari 19, 2022

Dalili ya mvua ni mawingu, 2025 ndio watalogana haswa, hii tabia ya majina ya mfukoni hawajakoma wamuulize JK kilichomkuta kwa Membe
 
Sie tunasubiri mzee wetu wavijisenti mzee wa dili atoe msimamo tunamuunga mkono😂😂😂
 
Je CCM wakipitisha mtu wao ,katibu wa bunge akienda kumtia kapuni sijui patakaaje
 
Ili kumpata mkuu yeyote wa mhimili wa utawala, ama nafasi nyingine za juu za uongozi hapa nchini hutegemea sana ushauri ambao Rais aliyepo madarakani anaupata na kisha kuuridhia kutoka kwa marais wastaafu pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama. Licha ya watu wengi kufikiriwa kuwa wana uwezo, lakini kiuhalisia wapo watu wachache wenyekuaminika ambao huonekana kuwa wanafaa kushika nafasi hizo.

Unaweza kuangalia chaguo la Kassim Majaliwa ama Philip Mpango ndipo utatambua ukweli huu. Watu wanaweza kuwa na maoni tofauti juu ya wale ambao wanawaona kuwa wanafaa katika hii orodha ya wana CCM 71 waliotia nia katika nafasi ya Spika wa Bunge.

Yatapita majina ya watu ambayo watu hawakuyatarajia, na miongoni mwao atatokea Spika aliyependekezwa. "Party caucus" ya CCM utafanya "endorsement" tu, kwa kuwa itaelekezwa kwenda tu kukamilisha ratiba ya kumpata mtarajiwa.

Majina kama Thomas Kashilila watu wasiyachukulie poa. Moshi mweupe ukitoka ndipo watu watakapo tambua kuna watu na viatu. Katibu wa sasa wa Bunge ni Bi. Nenelwa Mwihambi, kweli kuna uwezekano wa Spika kuwa naye ni "madam" ambaye alikuwa kipenzi cha Mzee aliyepita!?

Sikati kuzungumzia uteuzi wa yule balozi aliyekuwa msaidizi wa DAS Mtwara na hatimaye kuwa balozi kamili nchini Austria.
 
Ninasubiri kwa hamu maoni yako kwa jina litakalopendekezwa na ccm kuwa spika. Maana nakumbuka Pascal Mayalla ulikuwa miongoni mwa wahanga wa uongozi wa spika aliyepita.
Maoni yangu niliisha yaanza
P
 
Ninasubiri kwa hamu maoni yako kwa jina litakalopendekezwa na ccm kuwa spika. Maana nakumbuka Pascal Mayalla ulikuwa miongoni mwa wahanga wa uongozi wa spika aliyepita.
Spika ajaye ni huyu
P
 
Hii ndio taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Chama hicho Shaka Hamdu.

Taarifa zinaeleza kwamba kuahirishwa kwa kikao hicho kunatokana na kusambaratika kwa wajumbe wa kikao hicho kulikoibua Makundi yanayonyukana , huku kila kundi likitaka mgombea wake awe Spika .

Mwanzo wa sekeseke hilo ni fununu za kuwataka Wajumbe lazima wamchague Dr Kashilila ambaye ni Mgombea wa Mfukoni wa Wakubwa .

Usikae mbali na JF ili uendelee kupata kila kinachojiri kwenye mnyukano huo , YUKO NZI WANGU NDANI YA VIKAO VYAO .
ccm ni mnana wa babeli, Mungu yupo kazini
 
CCM kwa aibu wanaweza kumpitisha Tulia among wale watatu kwa vile tu ni Naibu Speaker. Litabaki kuwa jukumu ka wabunge wa CCM kumfyekelea mbali kwenye uchaguzi wao wa ndani

Bila shaka watafanya hivyo. Chenge au Zungu wanaweza kuwa machaguo bora zaidi ya Tulia au Masele ambao bado wana safari ndefu kisiasa, as such, watakuwa na tendecy ya kujipendekeza kwa Rais kama mmoja akiwa Speaker

Chenge hana la kupoteza sana na anaweza asikubali kuburuzwa
 
Chenge ondoa huwezi jaza wakristo watupu au wasukuma wawili kwenye nafasi tatu chenge msukuma masele msukuma

Na huwezi weka wote wakristo watupu wote watatu muislamu lazima awemo
Nchi haina dini wala Kabila. Tunaangalia mwenye uwezo.
 
Tul
Wote hao wakristo mkristo mwenye uzoefu mkubwa kwa wagombea ni Tulia

Kumbuka Wanaotakiwa kupendekezwa in watatu tu

Kwa waislamu muislamu aliyegombea mwenye uzoefu mkubwa bungeni ni Zungu

Kwa wasukuma mwenye uzoefu mkubwa na bunge kiuongozi ni Masele Aliyekuwa naibu spika bunge LA Afrika


Tulia ana uzoefu upi mkubwa kumzidi Singh na Masele ameweka labda kuwakilisha wanawake
 
Back
Top Bottom