Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Samia yaridhia Daniel Chongolo kujiuzulu Ukatibu Mkuu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kimeridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Daniel Chongolo

Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda imeeleza walioteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti kwa mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza pamoja na Wilaya za Mpanda na Kusini Unguja.

---
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Pia soma:
- Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Screenshot 2023-11-29 at 20.29.54.png
Screenshot 2023-11-29 at 20.30.06.png
 
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sbu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
Ccm mbele kwa mbele!
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. a nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
Kwa hiyo siku hizi hakuna Siri Kwa nini?
 
Back
Top Bottom