Mbivu na mbichi za Wagombea Uspika wa CCM kujulikana leo Januari 19, 2022

Mwakilishi wa Wakatoliki ni yupi hapo? Na Wasabato? Kumbuka hao siyo Wakristu kwa tafsiri ya walokole
Wote hao wakristo mkristo mwenye uzoefu mkubwa kwa wagombea ni Tulia

Kumbuka Wanaotakiwa kupendekezwa in watatu tu

Kwa waislamu muislamu aliyegombea mwenye uzoefu mkubwa bungeni ni Zungu

Kwa wasukuma mwenye uzoefu mkubwa na bunge kiuongozi ni Masele Aliyekuwa naibu spika bunge LA Afrika
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakutana kesho Alhamisi ya tarehe 20 Januari 2022 katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika mitandao ya kijamii ya CCM Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan ndiye atakayeongoza kikao hicho.

Moja kati ya mambo yanayosubuliwa baada ya kikao hicho ni majina ya wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania yatakayoteuliwa na kupelekwa kwa wabunge wa CCM kwa ajili ya kupigiwa kura ili kupitisha jina moja litakalokwenda bungeni kwa ajili ya kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Spika wa Bunge la Tanzania mapema mwezi wa Februari 2022.

Ikumbukwe kwamba Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa Ndg. Solomon Itunda alitoa taarifa siku ya Jumamosi 15 Januari 2022 wakati wa kufungwa kwa mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na Chama kugombea nafasi ya Spika kuwa wanachama 71 walichukua fomu na waliorejesha ni 70 huku mmoja akishindwa kurejesha mpaka muda uliowekwa kuisha.

272098728_470136524481072_2370247161103047363_n.jpg
 
Kila la heri wagombea wote. Spika atakayechaguliwa akumbuke kuwa yeye ni mmoja tu aliyekabidhiwa dhamana nyuma yake kuna Watanzania zaidi ya 55,000,000
 
Wakuu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma mabadiliko ya tarehe ya vikao vya kitaifa vya mwezi Januari, 2022 kama ifuatavyo:-

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambacho Kitaongozwa na Chief Hangaya Kitafanyika tarehe 20 Januari, 2022 badala ya tarehe 18 Januari, 2022 katika ofisi za Makao Makuu (White House), Dodoma.

Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Vikao Hivi Ndivyo Vitakavyofanya Mchujo Wa Kumpata Spika Mpya Wa Bunge la JmT.

Maandalizi ya vikao vyote hivyo yamekamilika.

Karibuni Dodoma Wajuba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa taarifa, kwa vyovyote vile fanyeni muwezalo mtuletee jina la mtu mwenye sifa ya kuwa spika mkuu wa mhimili asiye jipendekeza na kujishusha kwa mkuu mwenzake wa mhimili.
 
Kila la heri wagombea wote. Spika atakayechaguliwa akumbuke kuwa yeye ni mmoja tu aliyekabidhiwa dhamana nyuma yake kuna Watanzania zaidi ya 55,000,000
Chama Cha Mapinduzi naamini watatoa wagombea makini na kisha tutapata mgombea moja makini atakayekiwakilisha Chama. Kazi Iendelee.
 
Naatabiri watatu kuteuliwa ugombea uspika kupitia CCM ni Tulia Ackson,Masele na Azzan Zungu

Sababu ya kwanza Zungu kuwakilisha waislamu...
Tatu bora yangu ni
1. Tulia Ackson.
2. Andrew Chenge.
3. Stephen Masele.
Iwapo Tulia akipata uspika naibu wake ni Masele
 
Tatu bora yangu ni
1. Tulia Ackson.
2. Andrew Chenge.
3. Stephen Masele.
Iwapo Tulia akipata uspika naibu wake ni Masele
Chenge ondoa huwezi jaza wakristo watupu au wasukuma wawili kwenye nafasi tatu chenge msukuma masele msukuma

Na huwezi weka wote wakristo watupu wote watatu muislamu lazima awemo
 
Naatabiri watatu kuteuliwa ugombea uspika kupitia CCM ni Tulia Ackson,Masele na Azzan Zungu

Sababu wa kwanza Zungu kuwakilisha waislamu

Tulia kuwakilisha wakristo

Masele kuwakilisha Sukuma gang lililokabidhi kiti kwa Mama Samia wasukuma wengi wamechukua fomu mwakilishi wao atakuwa Masele

Hawa hawana makandokando yeyote akipata sawa

Hao jamii haina mikashfa ya kuwatuhumu wakipitishwa hakutakuwa na miguno wala maneno maneno ya kuponda CCM ndani na nje
 
Back
Top Bottom