CCM yateua Wagombea katika ngazi ya Mkoa na Wilaya. Baba wa Sabaya (aliyekuwa DC Hai), ateuliwa kugombea Arusha

bloggerboy

JF-Expert Member
Nov 13, 2017
568
1,211
Chama cha Mapinduzi kimefanya Kikao cha Kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kilijadili hali ya Kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama

Aidha, kimefanya uteuzi wa Mwisho wa Wagombea wa nafasi za Uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali

Katika uteuzi huo, Loy Thomas Sabaya, ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ametuliwa kuwa mmoja wa Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha

IMG_8353.jpeg


IMG_8351.jpeg


IKUMBUKWE
Mwaka 2015, Loy Thomas Sabaya aliteuliwa na CCM kugombea Ubunge kupitia chama hicho katika Jimbo la Arumeru Magharibi. Jimbo hilo lilienda kwa Gibson Blasius Meiseyeki wa CHADEMA

Pia, ameshawahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti.

Pia soma; Sabaya Senior (Loy Sabaya) apata Ushindi wa Kishindo Uenyekiti CCM Arusha
 
Baba hana ubaya. Mfedhuili ni mwanaye Sabaya
Huyu mzee si ndiye alikuwa na kashfa ya kuchoma moto nyumba wanavijiji akalindwa lindwa na PM wa wakati huo, Sumaye hadi kesi yake ikawa inakosa hakimu?

Ama nimemfananisha tu? Naye alikuwa DC kama sikosei? Kama siye huyu mniambie tu.

Ova
Ngoja tusubiri kama ni mvua au jua.
 
Back
Top Bottom