Mbeya: Mwimbaji wa Wimbo wa "Mnatuona Nyani" afikishwa Mahakamani, tuhuma za Uchochezi zayeyuka yawa kesi ya kusambaza Uongo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kwa mujibu wa Wakili Jebra Kambole ambaye yuko upande wa utetezi, amesema Watuhumiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini humo kwaajili ya kusomewa Mashtaka yanayowakabili.

Sifa Bujune, Mkazi wa Isyesye anashikiliwa tangu Septemba 13, 2023 pamoja na Mtayarishaji wa muziki aitwaye Ezekiah wakituhumiwa kuandaa wimbo wa “Tanzania Inaelekea Wapi?” unaodaiwa kuwa na maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali.

================

1.jpg

2.jpg

3.jpg


Wakili Jebra Kambole amesema waliosomewa mashtaka watu watatu karika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini wote shtaka lao ni moja ambalo ni "Kusambaza Taarifa za Uwongo kwa njia ya Mtandao".

Mtuhumiwa wa kwanza na wapili wote ni waimbaji ambao ni Sifa Boniventure Bujune na Salome Mwampeta, wa tatu ni mtayarishaji (prodyuza) Hezekiel Millyashi George.

Amesema "Baada ya kusomewa mashtaka watuhumiwa wote wamekana mashtaka, upelelezi haujakamilika na hivyo wameruhusiwa kupata dhamana kesi yao itarejeshwa Mahakamani Oktoba 3, 2023, tupo tunashughulikia suala la dhamana."

Watuhumiwa walishikiliwa tangu Septemba 13, 2023 wakituhumiwa kuandaa wimbo wa “Tanzania Inaelekea Wapi?” unaodaiwa kuwa na maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali.


Pia soma : Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Back
Top Bottom