Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa "Mnatuona Nyani tu" amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.

manyani.jpg

================== ==================
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha huduma ya kiroho bila kibali.

Akizungumza na JamiiForums, Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha ukamilishwaji, pia Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa."

Ameongeza "Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini, tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023)."

=================​
Pia soma: 'Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi' Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi
 
Mchungaji Pastor Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa Mnatuona Manyaji amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali...
Wamempiga mchungaji na kondoo wataenda wapi sasa?
 
Mchungaji Pastor Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa Mnatuona Manyaji amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali...
Akisema ana kibali cha Mungu, serikali itasemaje? Serikali itaingilia kibali cha Mungu? Hapo si kuingilia mambo ya imani na kuvunja haki za binadamu?

Serikali kutaka kutoa vibali vya kuendesha kanisa si kuvunja haki ya kikatiba ya watu kuwa na uhuru wa kuabudu?
 
Sheria inayoruhusu kuanzisha nyumba za ibada inasemaje ikibainika nyumba ya ibada haina usajili?
Kwa nini nyumba ya ibada iwe na usajili serikalini katika nchi inayotoa uhuru wa kuabudu kikatiba kwa kila mtu?

Serikali hata kodi haikusanyi kutoka nyumba za ibada, sasa zinasajiliwa kwa nini?

Nikisema hii habari ya kusajili nyumba za ibada serikalini ni namna ya serikali kudhibiti ibada na kuingilia uhuru wa kikatiba wa kuabudu nitakuwa nakosea?
 
Sahihi
 
Back
Top Bottom