BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,800
Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili ni Mustapha Kuhenga(28) ambaye ni mtaalamu wa Tehama na mkazi wa Mwenge.
Washtakiwa hao wanadaiwa kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.
Jacob na mwenzake wamefikishwa Mahakamani hapo jana jioni Jumanne, April 23, 2024 na kusomewa mashtaka hayo na wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi.
Mbilingi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya, kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 10709/2024.
Akiwasomea mashtaka yao, Wakili Mbilingi alidai katika shtaka la kwanza ambalo ni shambulio la mtandao linamkabili mshtakiwa Jacob, pekee yake.
Jacob anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 11, 2024 katika sehemu isiyofahamika katika jiji la Dar es Salaam.
Inadaiwa siku hiyo, Jacob anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa nia ya kumtisha, Adam Mihayo.
Shtaka la pili ni shambulio la mtandao linalomkabili Kuhenga pekee yake, tukio analodaiwa kulitenda kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 sehemu isiyofahamika, jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa siku hiyo, Kuhenga anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.
Shtaka la tatu ni kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa Kijamii wa WhatsApp Messenger.
Wakili Mbilingi alidai, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kulitenda kosa hilo, Desemba Mosi 2023 na Machi 2024, sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walichapisha picha za video za ngono kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii WhatsApp za Adam Mihayo.
Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao, wamekana kutenda na kisha kuomba dhamana.
Hakimu Mbuya alitaja masharti ya dhamana ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa wawe na barua mbili na moja wapo kati ya hizo iwe inatoka kwenye taasisi inayotambulika kisheria.
Pia, wadhamini hao wanatakiwa kusaini dhaman ya Sh 3milioni. Washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana na wapo nje kwa dhamana. Hakimu Mbuya aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa.
Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu
MWANANCHI