Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1689234596061.png

Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza (Kombi ya HGL) usiku wa kuamkia Julai 11, 2023 walilazimika kulala darasani ikidaiwa kuwa ni baada ya mwalimu wa bwenini kuondoka na funguo za bwenini kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kupitia vyanzo vyake vya taarifa anasema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo.

Homera ameeleza kukerwa na tukio hilo kwenye shule ya Loleza anayosema ni ya mfano ikikusanya watoto kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini hivyo hata kama watoto walifanya kosa ilifaa kupewa adhabu walizojiwekea shuleni hapo na si kuwalaza darasani ikizingatiwa na musimu huu wa baridi.

Mwalimu anayedaiwa kuondoka na funguo za bweni ambaye ni msimamizi wa watoto hao bwenini Sabina Haule anasema chanzo ni ukorofi wa watoto hao lakini hakuwaamuru kwenda kulala darasani kwakuwa baada ya kufunga bweni alirudi baadaye majira ya saa nne usiku na kuwaelekeza kwenda kulala mabweni mengine ambayo hayana wanafunzi lakini watoto hao walikaidi na kwenda kulala darasani kimyakimya hivyo kuomba msamaha kwa mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Shule ya Loleza Mwal. Mkuu Betiseba Nsemwa alipoulizwa juu ya suala hilo amesema alikuwa akiendelea kushughulikia suala hilo kwa kuwakutanisha mwalimu wa nidhamu na msimamizi huyo wa bweni.

Baadaye mkuu wa mkoa Juma Zubery Homera akapata nafasi ya kutembelea hadi darasa ambalo wanafunzi wanadaiwa kulala usiku mzima kisha kuzungumza na wanafunzi hao akiwaasa kuzingatia nidhamu wawapo masomoni na kumuagiza afisa elimu mkoa Mwalimu Ernest Hinjo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwalimu husika.

JAMBO TV
 
View attachment 2686443
Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza (Kombi ya HGL) usiku wa kuamkia Julai 11, 2023 walilazimika kulala darasani ikidaiwa kuwa ni baada ya mwalimu wa bwenini kuondoka na funguo za bwenini kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kupitia vyanzo vyake vya taarifa anasema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo.

Homera ameeleza kukerwa na tukio hilo kwenye shule ya Loleza anayosema ni ya mfano ikikusanya watoto kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini hivyo hata kama watoto walifanya kosa ilifaa kupewa adhabu walizojiwekea shuleni hapo na si kuwalaza darasani ikizingatiwa na musimu huu wa baridi.

Mwalimu anayedaiwa kuondoka na funguo za bweni ambaye ni msimamizi wa watoto hao bwenini Sabina Haule anasema chanzo ni ukorofi wa watoto hao lakini hakuwaamuru kwenda kulala darasani kwakuwa baada ya kufunga bweni alirudi baadaye majira ya saa nne usiku na kuwaelekeza kwenda kulala mabweni mengine ambayo hayana wanafunzi lakini watoto hao walikaidi na kwenda kulala darasani kimyakimya hivyo kuomba msamaha kwa mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Shule ya Loleza Mwal.mkuu Betiseba Nsemwa alipoulizwa juu ya suala hilo amesema alikuwa akiendelea kushughulikia suala hilo kwa kuwakutanisha mwalimu wa nidhamu na msimamizi huyo wa bweni.

Baadaye mkuu wa mkoa Juma Zubery Homera akapata nafasi ya kutembelea hadi darasa ambalo wanafunzi wanadaiwa kulala usiku mzima kisha kuzungumza na wanafunzi hao akiwaasa kuzingatia nidhamu wawapo masomoni na kumuagiza afisa elimu mkoa Mwalimu Ernest Hinjo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwalimu husika.

JAMBO TV
Wapo depo au????

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kuna siku nilimsikia binti yangu wa Standard Two akisema mwalimu wake hana akili. Aisee, nilimwambia atubu na akamwombe msamaha mwalimu wake. Kama mwalimu hana akili, maana yake na mwanafunzi hana akili. Akaleta mambo ya "Why, why, dad?" Nikasema, "Mkubwa akikosea, unamwambia kwa heshima. Huwezi pwayuka kuwa mwalimu hana akili. Jifunze kupuuzia wajinga na kujifunza kuacha kufanya ujinga kimya-kimya, and not shouting 'mwalimu hana akili.' Tabia mbaya za kijeuri nyingine zinaendelezwa na wazazi."
 
Mwalimu ajulikanaye kwa jina la Sabina Haule amewapa adhabu wanafunzi wake wa shule ya msingi kwa kuwafungia darasani usiku kucha wakipigwa na baridi huku yeye akienda kulala nyumbani na mume wake. Adhabu hii imedumu kwa muda sasa hadi pale wazazi walipoenda kulalamika kwa mkuu wa mkoa, ndugu Homela.

Baaada ya wazazi kumpa taarifa RC alifanya ziara ya kushtuka shuleni hapo usiku wa manane ambapo aliwakuta wanafunzi hao wakipigwa baridi huku wakiwa hawana blanketi za kujifunika wala nguo za kuwakinga na baridi. Ndipo mkuu wa mkoa alipochukua jukumu la kuvunja mlango na kuwakoa wanafunzi waliokuwa wakitetemeka kwa baridi kali ya usiku.

Kufuatia tukio hili, RC amewaomba wanafunzi kuwa na nidhamu kwa walimu huku akiahidi kumshughulikia mwalimu aliyehusika na tukio hili hasa ukizingatia wanafunzi waliolazwa darasani bado ni watoto wadogo. Aidha, aliwashauri walimu kutoa adhabu kwa wanafunzi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni. Ikumbukwe wiki iliyopita mwalimu mmoja alitiwa mbaroni mkoani humo kwa kuwachomeka mimba wanafunzi wawili huku akimchomoa mimba mmoja wao.

Chanzo: RFA; habari na matukio 13/07/2023

MAONI YANGU
Hili liwe fundisho kwa wanafunzi wenye tabia mbaya na wasiowaheshimu walimu. Wanafunzi wa kizazi hiki wana vichwa vigumu sana. Hawasikii. Hii inatokana na malezi mabovu kutoka kwa wazazi na jamii inayowazunguka. Wazazi tuongeze juhudi za kuwalea watoto wetu kuwa na nidhamu ya kuwaheshimu walimu na watu wengine katika jamii.

Nawasilisha.
 
RC hana kazi za kufanya, ni sawa na yule DC wa tunduru aliyekwenda kufumania.

USA na wenzie wa Europe wangekuwa na viongozi kama hawa sidhani kama wangefika huko Mars au kutengeneza drones na haya masmart phone.

RC na DC mjifunze kudeal na mambo makubwa makubwa yanayoleta tija kwenye ustawi wa jamii kwa kutumia akili zenu kubuni mambo tofauti tofauti.
 
Loleza girls ina manyanyaso sana
Hayaanza bure
Kuja muda mwalimu anamkalisha mtoto nje kwenye mvua aiseee ni unyama.

Naongea nikiwa na uhakika wa kutosha,, I've been there for yrs.
Hakuna Mwalimu anaenyanyasa mwanafunzi ambae sio mtukutu ingawa kuna shule nilisoma kuna Mwalimu alikua anaitwa Ngozie Ila sio Mwalimu by profession maana alikua ana fani ya fine arts (mchoraji) alikua hana fani ya ualimu hata cheti Cha ualimu alikua hana akapewa ukuu wa shule yule alichokua anakifanya alikua anajua mwenyewe, kwa hio walimu wachunguzwe ni walimu by profession au kuna kingine hapo wamevamia fani za watu
 
Ndio maana nilikataa kazi ya ualimu tangu nasoma maana ni kazi ya kitumwa.

Just imagine huyo mwalimu saiv anavyohaha kwa kitendo alichodhani ni sahihi kukifanya.

Ualimu ni wito, mlioitwa nendeni mkaihudumie jamii kwa utumishi uliotukuka.

Mimi ningeua watoto wa watu.
 
Hakuna Mwalimu anaenyanyasa mwanafunzi ambae sio mtukutu ingawa kuna shule nilisoma kuna Mwalimu alikua anaitwa Ngozie Ila sio Mwalimu by profession maana alikua ana fani ya fine arts alikua hana fani ya ualimu hata cheti Cha ualimu alikua hana akapewa ukuu wa shule yule alichokua anakifanya alikua anajua mwenyewe, kwa hio walimu wachunguzwe ni walimu by profession au kuna kingine hapo wamevamia fani za watu
Ni kweli wanafunzi ni watukutu ila adhabu ziangalie utu wa wanafunzi,
Adhabu nyingi zinazotolewa zinakiuka hadi za binadamu.
 
Ndo maana nilikataa kazi ya ualimu tangu nasoma maana ni kazi ya kitumwa.
Just imagine huyo mwalimu saiv anavyohaha kwa kitendo alichodhani ni sahihi kukifanya.
Ualimu ni wito ,mlioitwa nendeni mkaihudumie jamii kwa utumishi uliotukuka.
Mimi ningeua watoto wa watu.
Wamuache tu
Ni vile yeye tu kibao kimemuangukia
Ila kuna walimu wenzie wengi tu wanaotoa adhabu kali sana kuliko hata yeye.
 
Back
Top Bottom