Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Kufaulu kwao kunashangaza wengi na wala hawanunui mitihan bali wanafanyiwa michujo mkali sana, yani ile ininterview ya kuingia tu watoto wanaweza kuwa elf 3 ambao ni vipanga wote ila wanahitajika 100 tu, yaani mtoto kuingia tu hapo inabidi awe kipanga na bado kuna michujo mikali ya maksi za juu sana, inaendelea wakianza shule, hadi mtoto aweze kufuzu kufanya mtihani wa kidato cha nne kapambana sana.
mfumo wao wa usomaji ni tofauti, mfumo wao unamlazimu wanafunzi kujua namba ya kujibu mitihani muda mwingi tangu akiamka hadi kwenda kulala, mazingira yao ni mazuri ila ni kwajili ya kujua mtindo wa kujibu maswali sio kula upepo ama kuotea jua ama michezo, testi kibao za kuzoesha wanafunzi kuweza kujibu mtihani, nadhani hata ukifeli likizo unaweza ukabaki shule ili upigwe brashi kujifunza mtiririko mzuri wa kujibu maswali ya necta, usipofikisha wasatani wa shule umekwenda, bonasi na zawadi nono pindi matokeo yakitangazwa zinawapa walimu presha kubwa kuhakikisha wanakomaa na wanafunzi wao mpaka kieleweke .
Mpaka kufikia form 4 kwenye mwezi wa sita ule kila mwanafunzi anakuwa kama kasuku, yaani kuanzia definition, factors,advantages, feautures, n.k. wanaweza kuzijibu kama mashine ya kutoa kopi, past papers wanakuwa wameshasolve zimekuwa kama kiitikio cha muziki hakuna swali jipya mbele yao, wanachosubiri hapo huwa ni kulishangaza taifa kwa msururu wa division 1 za single digit.
Tatizo linaanza hao wanafunzi wakienda shule nyingine advance ama chuoni ukikutana nao wanarelax kwasababu hawakutani tena na heka heka za kubanwa ama mazingira ya kulazimishwa kusoma kama mwanzo.
Wanakuwa na uhuru kwa mara ya kwanza baada ya msoto mkali ndio mana wanaanza kufel, hawajazoea uhuru tofaut na wanafunzi wengine waliotoka shule za kawaida wakiwa na uhuru na bado wakatoboa, kwao uhuru ni kitu cha kawaida tofaut na wale wa saint francis ambao walikuwa wanatumia muda mwingi kusoma