Mbeya: Wamiliki wa Shule watakiwa kuhakikisha 'School Buses' zikakaguliwa na Polisi kabla ya kubeba Wanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Mrakibu wa Polisi SP Hussein Gawile amewataka wamiliki wa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kuhakikisha magari yao (School Buses) yanakaguliwa na wakaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi kabla ya kuanza kufanya kazi ya kubeba wanafunzi.

Rai hiyo imetolewa Januari 05, 2024 katika muendelezo wa zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kubeba na kusafirisha wanafunzi hapa mkoani Mbeya.

027d1fa5-2cdf-40a0-a7fd-8a21d50cd9ea.jpeg

b6a52b22-80bb-4a43-92e1-43099d567c90.jpeg
Mrakibu wa Polisi Gawile amesema kuwa, "tangu kuanza kwa zoezi la ukaguzi wa mabasi ya wanafunzi Desemba 11, 2023 hadi Januari 05, 2024 jumla ya mabasi 36 yamekaguliwa kati ya hayo mabasi 23 yamebainika kuwa na mapungufu mbalimbali ambapo wamiliki wametakiwa kuyarekebisha na kisha kuyarudisha kwa ajili ya ukaguzi mwingine (Re Inspection)" alisema SP Gawile.

Aliongeza kuwa, zoezi hilo limekwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa madereva hususani umuhimu wa kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani pamoja na udereva wa kujihami ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Nao waangalizi wa wanafunzi katika magari hayo wamekumbushwa umuhimu wa usalama wa watoto pindi wanapowachukua na kuwarudisha nyumbani, kuhakikisha wanawavusha barabara kwa umakini ili kuepuka madhara.

Mapema Januari 08, 2024 Shule za Awali, Msingi na Sekondari zinatarajiwa kufunguliwa hivyo Jeshi la Polisi nchini kwa kutambua usalama wa abiria na vyombo vya moto vinavyotumika kusafirisha wanafunzi limeanza kukagua vyombo hivyo ili kuhakikisha usalama wake kabla ya kuingia barabarani.
fe58a5fe-fe82-400e-8acd-0c36ced49671.jpeg
 
Back
Top Bottom