Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kufanya ziara katika Halimashauri ya Wilaya ya Tanganyika ikiwa ni katika kuangalia hali ya Wanafunzi kuripoti shule ambapo amekuta hali hairidhishi, hivyo ikamlazimu kuagiza Watendaji wa Mitaa na Vitongoji kwa kushirikiana na Maafisa Elimu kuhakikisha Wanafunzi wote wanaopaswa kuwa darasani wanafika ili kuendelea na masomo.
Aidha, ameagiza Halmashauri zote mkoani humo kumpatia kila siku taarifa ya hali ya Wanafunzi kuripoti shule huku akisisitiza Wazazi na Walezi kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi wawapo shule.
Naye, Halima Naison ambaye ni Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mpandandogo na Fredrick Kalele ambaye ni Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Ifukutwa wamesema mbali na idadi kutoridhisha lakini watajitahidi kushirikisha viongozi wa dini ili kuwapata wanafunzi hao huku Katibu Tawala wa Halmashauri ya Tanganyika, Lincolin Tamba akisisitiza Maafisa Elimu na Maafisa Tarafa kufuatilia Wanafunzi ambao hawajaripoti shule.