A
Anonymous
Guest
Mwalimu huyu wa Shule ya Msingi Mungu Maji aangalizwe, ananyanyasa Wanafunzi
Shule ya Msingi Mungu Maji iliyopo Tarafa ya Mungu Maji, Kata Unyamikumbi, Wilaya ya Singida Mjini, kuna changamoto, Wanafunzi wa Darasa la Kwanza lina Watoto 180 wanaosoma darasa moja.
Wanafunzi wanabanana, hawapo katika mazingira rafiki ya kusoma kwa kuwa pia kuna Walimu wawili tu wanaofundisha darasa hilo.
Nashauri Serikali iangalie juu ya hilo, changamoto nyingine ni kuhusu Mwalimu mmoja kati ya hao wawili anaitwa Kiwale amekuwa akiwanyanyasa Wanafunzi kiasi kwamba baadhi ya Watoto wamekuwa wakigoma kwenda shule kutokana na kumhofia Mwalimu huyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mungumaji, Charles Kirimba, sisi wazazi tumekulisha mara kadha akuhusu tabia za mtumishi mwenzako ambaye yupo chini yako, ukaahidi kushughulikia lakini bado mambo yamekuwa ni yaleyale.
Hatujui nini hasa ambacho kinamfanya Mwalimu huyo kuwa na jeuri licha ya sisi wazazi kumlalamika mara kadhaa.
Imefikia hatua baadhi ya Wanafunzi wanakimbia au wanatoroka pindi wanapojua kuwa ni zamu ya Mwalimu kiwale kuingia darasani.
===== ===
MAJIBU YA MKURUGENZI WA MANISPAA
JamiiForums.com ilipomtafuta Mkurugenzi wa Manispaa, Jeshi Godfrey Lupembe kwa ajili ya ufafanuzi wa madai hayo amesema “Siwezi kulizungumzi hilo suala, Andika barua leta malalamiko yako, pia sina kibali cha kuzungumza, muulize Mkuu wa Mkoa au Katibu Tawala ili watoe ruhusa.
“Kazi za Serikali huwezi kutoa majibu bila kuwa na maandishi.”
MAJIBU YA AFISA ELIMU
Akijibu hoja hizo, Afisa Elimu Msingi, Omari Maje amesema “Kwanza Wanafunzi waliopo ni 130 na sio 180 kama alivyosema, tuhuma sio za kweli, mtoa mada anatumia mtandao vibaya, Serikali ipo kazini, aje ofisini kwangu aone mamlaka husika, kama suala lake ni la kweli tulifanyie kazi mara moja.”