Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mkuu usirudi haraka kiasi hicho kwenye katiba mpya,

Tuna kazi ya kufanya baada ya hili tukio, kabla hatujarudi kwenye mizimu inayotutafuna kama vile tanesco, inflation na hiyo katiba mpya.

dah! mkuu nalog off kwanza, ww ndo umekuja kwa spidi hadi nkataka kuanguka maana wakunishika mkono ni regia na ameshatutoka,
 
Hakika tumemaliza.

Salamu za shukrani kutoka kwa familia.

Nawashukuru nyote mlionipa ushirikiano nilipokuwa na post kwa uchache sana.Asanteni kwa kunisahihisha pale nilipokosea.

Tutaendelea kuwa pamoja.

Regia alisema,JF ni shule na pia ni numbani,ni kweli haijawahi kupita siku bila kungulia JF.

ASANTENI SANA.

Ahsante sana mama kwa kazi nzuri sana uliyofanya pamoja na kuwa katika mazingira magumu.Um

etuwezesha wale tuliokuwa mbali na eneo la tukio tushiriki moja kwa moja katika shufhuli ya kumhifadhi mpendwa wetu katika makazi yake ya kudumu.

Tunawatakia kila la kheri wote mlioshiriki kutuhabarisha hapa jf, mnaporudi maeneo yenu mbalimbali katika kuendelea na majukumu ya kulijenga taifa huku mkitafakari namna bora zaidi ya kumuenzi Regia.

Mungu awabariki sana.
 
Hakika tumemaliza.

Salamu za shukrani kutoka kwa familia.

Nawashukuru nyote mlionipa ushirikiano nilipokuwa na post kwa uchache sana.Asanteni kwa kunisahihisha pale nilipokosea.

Tutaendelea kuwa pamoja.

Regia alisema,JF ni shule na pia ni numbani,ni kweli haijawahi kupita siku bila kungulia JF.

ASANTENI SANA.

ahsante na wewe coz ni kama nilikuwepo msibani.Umejitahidi sana kwa nafasi uliyokuwa nayo.Pongezi kwa baba kwa kukuchagua wewe!
Dada etu Regia kwaheri ya kuonana!nitakumiss sana
 
Mkuu Barubaru asante lakini kuna bandiko lako limenikwaza sana unajua nakuheshimu sana katika hali kama hii unategemea neno la faraja toka kwa msomi wa kariba yako.Dharau na kejeli tuwaachie wenyewe wewe si miongoni mwa wanajamvi wapuuuzi.

Kwa wale wote mliohudhuria maziko.

Ni vizuri sana kushika wasia wangu.

Kwa wale wanaotumia vyombo vya moto ni vizuri sana kufuata sheria za barabarani ikiwa pamoja na kufunga mikanda wakti chombo kinakwenda na wale wa vyombo vya matairi mawili au matatu ni vizuri kuvaa kofia ngumu.

Vile vile kumbukeni mwendo kasi ni khatari kubwa.
Msisahau kuwa Pombe ni khatari kubwa kwenu jiepusheni na pombe mnapoendesha vyombo vya moto.

Lakini pia tunajuwa wengi mumechoka sana hususan katika harakati mzima za maziko. Kuweni makini na dereva kusinzia akiwa njiani.

Kumbukeni tunawapenda sana wote na tunawatakia safari njema na Mola awatangulie.
 
Hakika tumemaliza.

Salamu za shukrani kutoka kwa familia.

Nawashukuru nyote mlionipa ushirikiano nilipokuwa na post kwa uchache sana.Asanteni kwa kunisahihisha pale nilipokosea.

Tutaendelea kuwa pamoja.

Regia alisema,JF ni shule na pia ni numbani,ni kweli haijawahi kupita siku bila kungulia JF.

ASANTENI SANA.
\

Mama yetu,
Sina cha kusema kukushukuru.Hakika umenifanya nione kama nilikuwa msibani.Umefanya kazi kubwa mama.Kwani ni wangapi wako huko na hawajajituma kama wewe? Mama unastahili pongezi na heshima ya pekee.Kwangu mimi baada ya kazi kubwa uliyofanya hapa JF tangu msiba utokee unafaa kuwa mama wa wana JF wote.Nasema tena asante mama na kila la kheri!

RIP Regia.
 
Mama yetu umeonyesha uchungu wa moyoni na kudhihirsha kuwa women have two brains-can handle multi duties than men. Unasononeka but still unatujuza kile kinachoendelea hapo sehemu ya tukio. Inadhihirisha Dr.hakufanya makosa kwa kukuchagua kuwa mwenzi ili muweke bongo zenu pamoja kwa ajili ya Tanzania ya kesho. Dada Regia amekuwa ana unabii.

Musa alikufa kabla hajaingia nchi ya ahadi mbali na kuongoza Taifa la Mungu. Papa Yohana wa XXII aliyeongoza Mtaguso wa Pili ulioleta mabadiliko katika Kanisa Katholiki naye alikufa akiwa anaelekea kuhitimisha mkutano. Mchago wa Regia ndani ya CDM na Taifa kwa ujumla ni mbegu ilipondwa kwenye udongo mzuri. Tutaipalili na kuimwagilia ili matunda tuvune sisi, watoto , wajukuu na vijukuu.

Mungu Ibariki CDM.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie Regia. Apumzike kwa amani.Amina
Hapo umenena Mkulu, sawa kabisa bidii iongezeke binti Regia katoa mwanga, kazi ni kwa waliobaki sasa!!!!!!!!!! ALUTA CONTINUA, MAPAMBANO BADO YANAENDELEA!!!!!!!!!!!!

Umati wa waombolezaji unapita kwenye heshima za mwisho.
Jamani Wakristo wenzangu, lazima tufike mahali tukubali tukatae, wenzetu Waislamu wametuzidi kidogo katika ustaarabu wa taratibu za heshima za mwisho kwa kuaga bila kuangalia mwili!.

Just imagine Ile Jumatatu ameagwa kwa kuangaliwa pale nyumbani Tabata. Baadae ameagwa kwa kuangaliwa pale kanisani kwenye misa!. Jana tumemuaga kwa kumwangalia pale Karimjee!. Leo pia ameagwa tena kwa kuangaliwa hapa Ifakara!.

My own opinion, its more than enough, baada ya kuagwa na familia kwa kumwangalia, the rest wangepita tuu mbele ya jeneza kwa heshima na mwisho huku wakiangalia ile picha ya smiling innocent baby face yake ndio ikabaki kama kumbukumbu yetu ya mwisho ya Regia!.

Sasa imetosha na kupitiliza, tumpumzishe shujaa wetu apumzike kwa amani!.

Pumzika Regia!.

Mbona Nyerere alikaa siku 3 kama sikose pale uwanjani? kwa kuwa ni utaratibu uko hivyo, wacha uendeleeeeeeee, maana huwezi sema kwa kuwa aliagwa dar basi, ifarakara nao wanahaki
 
Jamani, kuna kitu au vitu mimi kiasi nashindwa kuvielewa hasa juu ya mambo yanayosemwa na watu mbalimbali juu ya Marehemu wetu Regia.

Nikisikiliza hayo maneno na sifa zinazotolewa juu yake na nikiangalia umri alofariki nao, kiasi fulani nashawishika kusema MANENO KAMA PENGO LAKE HALIZIBIKI AU HATATOKEA MTU KAMA HUYU, naona kama zinasemwa kwa UNAFIKI TU, given the young age of her, ni lipi/yapi hasa aloyafanya kiasi cha kupata hii attention yote.

Ni wangapi wema zaidi ya Regia wamefariki na hawakupata attention yoyote??? Nafikiri kuna haja ya jamii yetu kujiangalia kwa undani je tunayoyafanya kweli yana maananisha hicho kilichopo moyoni mwetu au ni ile tu watu waseme na yeye alisema???

kama huna cha kuandika acha! huu si ustaarabu!
 
Dada Josephine,
Tunakushukuru sana kwa kutupa yote yaliyokuwa yanajiri (pamoja na JF members wengine wote mliokuwa mkifanya hivi),
hakika hakuna atayebisha kuwa JF inaongoza kwa kutoa habari, tupo mbali lakini ni kama tumehudhuria live.
Ngumu kuamini lakini safari ya mpendwa wetu Regia kwa hapa duniani imehitimishwa, na Mungu ampe mwanga wa milele na furaha ya milele amuangazie.
Tunawaombea safari njema mrudipo majumbani, na Mungu atutie nguvu sote.
Pumzika kwa amani Regia

Hakika tumemaliza.

Salamu za shukrani kutoka kwa familia.

Nawashukuru nyote mlionipa ushirikiano nilipokuwa na post kwa uchache sana.Asanteni kwa kunisahihisha pale nilipokosea.

Tutaendelea kuwa pamoja.

Regia alisema,JF ni shule na pia ni numbani,ni kweli haijawahi kupita siku bila kungulia JF.

ASANTENI SANA.
 
Mkuu Barubaru asante lakini kuna bandiko lako limenikwaza sana unajua nakuheshimu sana katika hali kama hii unategemea neno la faraja toka kwa msomi wa kariba yako.Dharau na kejeli tuwaachie wenyewe wewe si miongoni mwa wanajamvi wapuuuzi.

ndugu umezoea kudharau na kukejeli ? kwa mawazo yangu sijaona dharau bali ni katika kukumbushana kibinadamu. Ajali zinaepukika.

Pumzika kwa amani Rejia. Pumzika Dotto. Ulotumwa kuyafanya pengine ulishayakamilisha. Kazi kwetu tuliobaki
 
WanaJF
nimesikia concern zenuzenu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nimekwenda mwenyewe kwa wenye mitambo na nimekuta wakihangaika na network. Tunatambua umuhimu wa kuwajuza kinachojiri. Tutaendelea kuboresha mitambo. Nashukuru baada ya picha zimeanza ku postiwa. Tunawashukuru wana JF na wapenzi wote wa Regia kwa ushiriki wa kina kumsindikiza mpendwa wetu.
Asante Dr, tunasubiri kwa hamu, maana nilishasema angekuwepo Regia tungeshapata picha za matukio yote. R.I.P Regia.
 
Mkuu Barubaru asante lakini kuna bandiko lako limenikwaza sana unajua nakuheshimu sana katika hali kama hii unategemea neno la faraja toka kwa msomi wa kariba yako.Dharau na kejeli tuwaachie wenyewe wewe si miongoni mwa wanajamvi wapuuuzi.

Ngongo.

Wakti nipo Tanganyika hususan Dar na mwanza, bukoba . Kulikuwa na kitu kinachoitwa utani wa makabila. Na utani huu unashamiri sana pale watu wanapokuwa msibani au kwenye matanga. Utashangaa mnaweza mkawa mnalia na wengine wanakuja na ngoma na kuanza kucheza. (Sina hakika kama siku hizi kuna watani)

mara ya mwisho niliona pale Upanga mtaa wa mazengo kwa jirani yangu Ditopile. watani walikuja juu sana wakti wa mazishi yake mpaka wakapewa pesa. Nakumbuka pesa za utani wa wasukuma alichukua Endrew Chenge na ilikuwa ni shilingi 200 za tanzania.

Hayo yote ni matani. Lakin yakiwa na nia ya kuboresha. haiwezekani watu wate muwe serious lazima pawe na mas'khara kidogo kupunguza tension.

Samahani kama nilikuwa nimekukwaza. Lakin kwangu ilikuwa ni joke tu.

Tusimame pamoja kumuombea Regia apokewe kwa amani huko Kwa Muumba.

Pole sana.

Jamani asanteni sana kwa updates, maana nasi tumeshiriki japo kwa kupitia computer zetu. Ninawaombea wote msafiri salama, na kuwa waangalifu jiani. Mungu awalinde mfike salama.

Mbarikiwe wote.
 
dah! mkuu nalog off kwanza, ww ndo umekuja kwa spidi hadi nkataka kuanguka maana wakunishika mkono ni regia na ameshatutoka,

Pole sana kiongozi wangu, unajua wakati mwingine tunajikuta tunataja vitu hivyo bila kutarajia.
 
Hakika tumemaliza.

Salamu za shukrani kutoka kwa familia.

Nawashukuru nyote mlionipa ushirikiano nilipokuwa na post kwa uchache sana.Asanteni kwa kunisahihisha pale nilipokosea.

Tutaendelea kuwa pamoja.

Regia alisema,JF ni shule na pia ni numbani,ni kweli haijawahi kupita siku bila kungulia JF.

ASANTENI SANA.
Asante sana Mama yetu kwa taarifa,kwan tumejikuta tumeshinda kwenye computer na nyie na kushiriki mazishi YA MPENDWA WETU kwa pamoja kupitia taarifa zako,
Mungu atakulipa kwa wema wako,
Nakiri leo Nimekukubali rasmi kuwa mwanamke wa kwanza kwan sijawahi kushuhudia mwanamke wa kwanza yoyote nchi hii aliyewahi kufanya haya hata alipofariki kiongozi mkubwa nchini,UBARIKIWE SANA.

FA Nadhani unazungumzia usichokifahamu.

ndugu umezoea kudharau na kukejeli ? kwa mawazo yangu sijaona dharau bali ni katika kukumbushana kibinadamu. Ajali zinaepukika.

Pumzika kwa amani Rejia. Pumzika Dotto. Ulotumwa kuyafanya pengine ulishayakamilisha. Kazi kwetu tuliobaki
 
Josephine tangu nimeanza kusoma hizi updates nilikuwa naona kawaida tu, kumbe ni kweli! nimeshindwa kuzuia machozi, eeh Mungu mwanga wa milele umuangazie Regia apumzike kwa amani.

Asante Josephine, duh siamini

Network inasumbua,lakini hatimae tumemuingiza kwenye nyumba yake ya milele.
 
Back
Top Bottom