Maxence Melo ateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Balozi Adadi Mohammed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na Bi. Fatma Mohammed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (MB.), kwa Mamlaka aliyopewa na Ibara ya 8(2) ya Sheria ya Ulinzi wa Tarifa Binafsi Na. 11 ya 2022, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kipindi cha miaka 3;

1. Bw. Ramadhan Athumani Mungi, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi;

2. Bw. Edward Samweli Lyimo, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Benki ya Biashara ya Taifa (NBC);

3. Bw. Hamid Haji Machano, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar;

4. Bi. Frida Peter Mwera; Mwandishi wa Sheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na

5. Bw. Maxence Melo Mubyazi, Mkurugenzi Mtendaji, Jamii Forums;

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 18 Disemba, 2023 hadi tarehe 18, Disemba 2026.
IMG-20231218-WA0010.jpg
 
Hongera nyingi kwa waliochaguliwa ama kuteuliwa.

Pongezi za haswa kwa melo, anatupa sana matumaini ya mafanikio, japo kuna kupanda na kushuka kwingi lakini wakati fulana utafikia mafanikio na jamii itakuona na kukuhitaji kuitumikia, hongera nyingi kwake.
 
Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Balozi Adadi Mohammed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na Bi. Fatma Mohammed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (MB.), kwa Mamlaka aliyopewa na Ibara ya 8(2) ya Sheria ya Ulinzi wa Tarifa Binafsi Na. 11 ya 2022, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kipindi cha miaka 3;

1. Bw. Ramadhan Athumani Mungi, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi;

2. Bw. Edward Samweli Lyimo, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Benki ya Biashara ya Taifa (NBC);

3. Bw. Hamid Haji Machano, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar;

4. Bi. Frida Peter Mwera; Mwandishi wa Sheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali; na

5. Bw. Maxence Melo Mubyazi, Mkurugenzi Mtendaji, Jamii Forums;

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 18 Disemba, 2023 hadi tarehe 18, Disemba 2026.
View attachment 2846438
Mkuu Analogia Malenga habari za masiku chekwa?
 
Back
Top Bottom