Maxence Melo: Kanuni za Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi zimeweka utaratibu wa kumalizana nje ya Mahakama kwa kila upande kupata stahiki sahihi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akiwa kwenye kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM ameeleza kuwa Kanuni ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi - "Kanuni Za Taratibu Za Kushughulikia Malalamiko ya Ukiukwaji Wa Misingi ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi" zimeeleza namna ambavyo watu wanaweza kumalizana pasipo kufika mahakamani lakini kila moja atapata haki stahiki.

Amesema "Wakati tunapeleka mapendekezo kwa Serikali au Mamlaka na Nchi, tulibaini Watu wengi watakuja na kesi za ajabu, hivyo tukashauri. Mwanzo wakati Sheria inatungwa hakukuwa na dirisha la kumaliana nje ya Mahakama, kwamba muongee na mmalizane"

Akitolea mfano suala hilo amesema "Mfano Kampuni A taarifa zako zimetoka ndivyo sivyo au namba yako au watu wameweza kupata miamala yako, mnaweza kumalizana nje ya mahakama ila msimalizane kizembe. Katika kuhakikisha wewe unapata haki yako mamlaka kupitia Tume [Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi] au kupitia Bodi [Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi] itakikisha kama kuna fidia basi unapata fidia stahiki"


My Take
Huyu mwamba ametupambania sana na anaendelea sana kutupambania watu wa Mtandaoni. Pokea maua yako Kaka Maxence Melo
 
Back
Top Bottom