Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 imeanza kutumika rasmi Mei 2023 ambapo pamoja na kuwepo kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutakuwepo na Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo itakuwa ni chombo cha usimamizi wa Tume.

Hata hivyo, ili kudumisha uadilifu wa Tume na kwa madhumuni ya kuepusha mgongano wa maslahi, mtu hatakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume iwapo kutokana na aina ya madaraka aliyonayo anaweza kuwa na ushawishi kwa Tume.

MAJUKUMU YA BODI
Kifungu cha 9 (1) na (2) cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kinaeleza Majukumu ya Bodi hiyo ambayo ni pamoja na:

9. (1). Bodi itasimamia utendaji wa Tume ili kuhakikisha kuwa utendaji huo unazingatia sheria na taratibu zinazosimamia Tume.

(2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1), Bodi itakuwa na wajibu wa;
a. Kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda sera za uendeshaji na usimamizi wa Tume;

b. Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa menejimenti ya Tume;

c. Kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali, ikijumuisha kuidhinishwa kwa mpango kazi wa mwaka, bajeti ya mwaka na bajeti ya nyongeza;

d. Kuidhinisha mipango ya uwekezaji ya Tume;

e. Kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume;

f. Kuidhinisha kanuni za maadili kwa watumishi wa Tume;

g. Kuidhinisha na kusimamia taratibu za usimamizi wa fedha na kanuni za utumishi wa Tume;

h. Kuidhinisha uondoshaji wa mali za Tume; na

i) Kutekeleza wajibu mwingine wowote kwa kadri Tume itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutimiza malengo yake kwa mujibu wa Sheria hii

IMG_8574.jpeg

IMG_8573.jpeg
 
View attachment 2849511
View attachment 2849512
Hii sio kama NEC tu?
 
Back
Top Bottom