OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums ameteuliwa kuwa mmjoa wa wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa muda wa miaka mitatu. Suala hili limezuia mijadala hata kwa wanachama wa JamiiForums wakidhani uhuru wao utakuwa umeminywa.
Unayopaswa kujua
Bodi inayoundwa ni kwa ajili ya kuisimamia Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi, bodi ina majukumu haya,
9.-(1) Bodi itasimamia utendaji wa Tume ilikuhakikisha kuwa utendaji huo unazingatia sheria nataratibu zinazosimamia Tume.
(2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1),Bodi itakuwa na wajibu wa-
10. Bodi inaweza, kwa madhumuni ya kutekelezamajukumu yake kwa ufanisi, kuunda na kuteua kutokamiongoni mwa wajumbe wake, kamati zozote kadriitakavyoona inafaa.
Kutokana na majukumu hayo msingi ya Bodi, JamiiForums haitaathirika kwa teuzi hii bali itakuwa katika nafasi ya kuhakikisha yanayosemwa na wananchi yanafika kwenye tume ya ulinzi wa taarifa binafsi.
Aidha, Maxence Melo hajateuliwa kutokana na UCHAWA bali kutokana na mchango wake katika Ulinzi wa Taarifa binafsi. Mimi naona anaenda kuwa kama mwalimu kwa wengine ambao wapo lakini uelewa wao ni finyu kwenye masuala ya taarifa binafsi.
Aidha kwa sababu sio chawa, sidhani kama atashindwa kujiuzulu ikiwa atakutana na mambo ambayo hakubaliani nayo. Ikumbukwe mjumbe wa bodi anaruhusiwa kujiuzulu kwa kifungu cha 1(1)(3), kama ambavyo amekuwa akitetea suala la haki na faragha za watu, uteuzi huu hauko katika nafasi ya kumtoa katika kitu amesimamia miaka yote.
KWA WANA JF
Baada ya kujua kuwa Mkurugenzi ni Mjumbe wa Bodi, WanaJF wanakuwa na nafasi ya moja kwa moja ya kuishauri bodi kwa kuwa wakiweka mawazo yao hapa yana nafasi ya kuonekana na watu kuchukua hatua.
Maana yake ni kuwa, kama Maxence anaenda kushauri jambo anajua kutoka kwa wananchama anaweza kuthibitsha kwamba wananchi wanapitia hiki au kile. Hii maana yake wanachama wana nafasi kubwa ya kushiriki mchakato huu kwa uzuri.

(a) kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda seraza uendeshaji na usimamizi wa Tume;
(b) kusimamia shughuli na utendaji kazi wamenejimenti ya Tume;
(c) kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali,ikijumuisha kuidhinishwa kwa mpango kazi wamwaka, bajeti ya mwaka na bajeti ya nyongeza;
(d) kuidhinisha mipango ya uwekezaji ya Tume;
(e) kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume;
(f) kuidhinisha kanuni za maadili kwa watumishiwa Tume;
(g) kuidhinisha na kusimamia taratibu zausimamizi wa fedha na kanuni za utumishi waTume;
(h) kuidhinisha uondoshaji wa mali za Tume; na
(i) kutekeleza wajibu mwingine wowote kwa kadriTume itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutimizamalengo yake kwa mujibu wa Sheria hii.