Mama Samia Suluhu Hasan.

Mungu akulinde na akuzidishie hekima zaidi. Akuzidishie afya imara, ustahimilivu na nguvu zaidi. Mungu akujalie yooooooote mazuri na mengineyo kwa kadiri ya mahitaji yako kwake.

AMINA.
 
Rais Samia ameboresha sana sekta ya elimu, tunaimani atatubadilishia mfumo wetu wa elimu ili kuendana na mahitaji ya ulimwengu wa sasa. Pia nampongeza kwa nia yake ya kutaka kurudisha mchakato wa katiba mpya, Mh. Dkt Samia Suluhu ni kiongozi mwenye mitazamo chanya sana bila kujali itakadi za kichama, kikanda, au kidini. #mamayukokazini
 
Ongera Rais Samia kwa kuonyesha njia.Niwewe uliyeamua kuonyesha Nia yako ya kujenga Tanzania imara Tanzania iliyojaa Amani utengamano na utulivu .ongera kwa uthubutu tukiwa na wewe jemedari naiona Tanzania Tulivu Tanzania yenye neema kubwa
 
Hiki ndicho ninacho mpendea Mama Rais Samia Suluhu Hassan hiki Hapa chini anapenda Haki sio kudhıulumu watu au kuwaonea watu. Mungu amlinde Mama Rais Samia Hassan Suluhu mpenda Haki. Kazi iendelee.........hongera sana......


 
"Enendeni mkatende yaliyo ya haki, huwezi kutenda yaliyo ya haki kama huna upendo wa dhati"
Maneno haya yanapatika katika biblia takatifu. (most exalted book)
 
Wakuu salamaa?

Raisi wa nchi ni mtu mkubwa sana na ana uwezo wa kufanya jambo lolote lile bila hata kushindwa.

Mfano mimi ningepata nafasi ya kuwa raisi wa nchi ningefanya yafuatayo

1.Ningejenga shule za kata 5 kila wilaya Tanzania . Ningepandisha mshahara wa walimu ningeajri walimu wengi na ningetengeneza mazingira ya walimu yawe mazuri. Ningempa kila mwamlimu piki piki haijalishi anafanya kazi wapi na mafuta wangewekewa na serikali.

2. Ningejenga vituo vya afya kila wilaya sio chini ya vitatu na hospital 2 za rufaa kwa kila mkoa.
Hospital ningeweka vifaa vya kisasa na mazingira mazuri sana mdaktari ningewapa kipaumbele na kila daktari ningempa Bajaji kwa ajili ya usafiri services na mafuta ni serikali na kila baada ya Miaka mitatu nawapa mpya zile za zamani zimapigwa mnada.

3. Kilimo
Tanzani ina eneo kubwa sana so ningetafuta mikoa yenye ardhi yenye rutuba kama mbeya, morogoro, kilimanjaro, songea.

Nachukua wataalamu wa kilimo na wanafunzi fresh from school wanalima mazo kule alafu serikali ndo inanunua inawatafuta soko.

4. Viwanda
Ningeruhusu wawekezaji waje wawekeze Tanzania wajenge viwanada vikubwa asilimia 80 wafanyakazi wawe watanzania.

Mwekezaji anawekeza kwa miaka mitano bila kulipa kodi kabisa na ardhi unampa bure baada ya miaka mitano ndo wananza kulipa kodi.

5. Napandisha kima cha Mshahara kima cha chini kinakua ni laki 3 .
Nashusha bei ya vyakula vinakua chini saaana.

6. sehemu zote muhimu ziwe na bara Bara za lami .

7. Wafanya bishara kodi naifanya inakua sio ya kuumiza.

Ni mengi ila ningeaza na haya
 
Sijui kwa nini anashindwa kufanya hivi na wakati inawezekana
Mkuu, huko juu kuna mfumo uliowekwa na bepari kwaajili ta kumgandamiza masikini.
Pia kuna kitu hua inakua kisingizio kikubwa kwajina la budget haitoshi
 
Hapo kwenye 4. viwanda ungeferi kweli kweli. Huo utarstibu walishawahi kujaribu serikali. Mwekezaji anaeekeza miaka 4, anasepa, anakuja mwingine mi-4 anasepa, wakati serikaki haina mapato ya kuendesha nchi.

Mwalimu ungemnunulia honda na wabunge wako ukawaacha wasakate haya ma-V8 sijui kama bajeti hiyo ungeimudu
 
Ukija kusikiliza vizuri utasikia kuna neno linasemwa kwamba Rais ni taasisi. Hii maana yake kwa lugha nyepesi ni kwamba Rais akifata mfumo umemlimit kufanya maamuzi peke yake hadi wawepo watu flani flani ambao bila tashwishwi watakua wana faidika na mfumo husika (taasisi)
 
Back
Top Bottom