Manchester united kwa mara nyingine tena watakuwa uwanjani bila ya walinzi wao Erick Bailly na Phil Jones wakati watakapo ikaribisha Brighton

Majeruhi hao wamekosa michezo miwili ya hivi karibuni dhidi ya Newcastle na ule wa Ligi ya Mabingwa waliopoteza na Basel.
Hata hivyo United haitakuwa na shida sana kwenye eneo hilo la ulinzi kwa sababu ya urejeo wa Marcos Rojo ambaye alicheza kwa dakika zote katikati ya wiki, na anatarajiwa kuanza tena wikendi hii na Jose Mourinho amepania kupunguza gepu la pointi dhidi ya majirani zake Manchester City

TAARIFA MUHIMU KUHUSU TIMU
Rojo yupo kamili kwa ajili ya mchezo wa wikendi hii, Zlatan bado hayuko vizuri kwa ajili ya kuanza katika mchezo huo
Ashley Young, Juan Mata na Antonio Valencia ambao hawakusafiri kwa ajili ya Fc Basel wanatarajiwa kurejea dhidi wa Brighton Old Trafford. Kapteni Michael Carrick ataendelea kukosekana wiki hii kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu

Brighton hawana hofu kuhusu majeruhi katika safari yao ya kuelekea Old Trafford. Kiungo wa Israel Beram Kayak anatarajiwa kusafiri na kikosi baada ya afya yake kuimalika, ni Steve Sidwell ndiye hatokuwepo kutokana na matatizo binafsi

TAKWIMU MUHIMU
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu hizi kukutana tangu mwaka 1983, katika mchezo uliomalizika na sare ya 1 kwa 1 katika uwanja wa Old Trafford.
Brighton wameshinda mara moja katika michezo 16 waliokutana na Man Utd, sare mara 5 na kupoteza mara 10

MWAMUZI WA MCHEZO HUU
Neil Swarbrick ndiye refarii wa mechi hii akisaidiwa na Richard West pamoja na Marc Perr
 
.
 

Attachments

  • 23795744_10155309727572746_7246881746800862506_n.jpg
    23795744_10155309727572746_7246881746800862506_n.jpg
    91.9 KB · Views: 28
Back
Top Bottom