Mkuu unaishi mkoa gani nikuelekeze sehemu utakapojibiwa haya maswali yako yaliyo mepesi?Kwa kuandika mni ngumu sana kuelezea vitu.Kama nilivyosema tatizo lako ni aidha umesoma sehemu tu ya biblia na inawezekana umekuwa ukiisoma kutafuta vitu vya kukosoa na hivyo ukajifunga ufahamu wako.
Wewe pia hujui kama roho inaweza chukua sura ya kitu chochote?Yesu alivyokuwa anabatizwa na Yohana Roho wa Bwana alishuka juu yake kama mfano wa hua(njiwa) hii haimanishi Mungu ni njiwa.
Kuna sahemu kwenye biblia inasema
upepo ukavuma mara ya kwanza ,lakini Bwana hakuwemo
upepo ukavuma mara ya pili lakini Bwana hakuwemo
Upepo ulipovuma mara ya tatu Bwana alikuwa katika upepo ule,hii haimanishi Mungu ni upepo.
Mkuu hujui hata roho ya wachawi inaweza kuja kama panya au paka au mbwa?Bado elimu yako ni ndogo haya maswali watu watachoka kukujib u ,ushauri wangu nenda sehmu jifunze si lazima uamini wanachoamini kaa hapo jifunze neno la Mungu lakini hivi unavyotaka ujue huku moyo wako haujafunguka una mambo kibao utapotea.
Roho ya mwanadamu inakaa ndani ya mwili,Roho wa Mungu anaweza kaa ndani ya kitu ambacho Mungu ataamua ikae kwa wakati ule.Mussa aliambiwa aende kwa farao,Musa akamwuliza Mungu farao akiniuliza wewe ni nani nimwambieje.
Mungu akamwambia "Mini ni niko ambaye niko" in English " I am that I am".Nifuate kwa umakini hapa Mungu alivyosema "I am that I am" alimanisha anaweza akawa katika form yeyote atakayotaka yeye kwa wakati ule.Soma maandiko ndugu,kama website yangu ikiwa tayari kwa ajiri ya kuwaamusha mlio lala utajulishwa.