Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Habari wana Jamii..
Kwa masikitiko makubwa nimeamua kuandika uzii huu huku nikiwa na woga na hofu ya juu kwasababu ya Mada nitakayozungumzia haikufaa kuchambuliwa maana haichambuliki na ni makosa makubwa.
Kuna bwana mmoja ndani ya chumba chetu hiki cha wanaIntelligesia aliweka uzi ukisema "MAKOSA 10 ALIYOTENDA MUNGU"
Na akayaelezea ifuatavyo:-

"(1.KUMUUMBA SHETANI
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY)
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwani kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwani anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu again fuze wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATING THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:>Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani? )"
MWISHO WA KUNUKUU.

Naomba niseme kitu japokuwa tunauhuru wa kusema chochote hebu tuwe tunajitahadhari maana wakati mwingine ulimi uliponza kichwa MUNGU si mwanadamu na MUNGU hafikiliki kilahisi jinsi hiyo. Hata kipindi cha Nuhu MUNGU baada ya kumwambia Nuhu atengeneze safina watu wengine wlikua wakimcheka Nuhu kwa kile alichokuwa akifanya na hata kipindi cha mvua kilipokaribia aliwaita waingie ila walikataa na ku mkashfu vilevile lakini mwisho wake wote tunafahamu ilikuaje.
TUKUMBUKE KUWA HAIJALISHI UTOFAUTI WETU BINADAMU WA IMANI ZETU KATIKA DINI MBALI MBALI, LAKINI MWISHO WA SIKU KILA MTU ANAKILI MUNGU YUPO NA NI MKUU NA MUWEZA WA VYOTE NA ALIUMBA VYOTE, JARIBU KUWAZA NI VIPI ALIUMBA MBINGU PASIPO NGUZO ZA KUSHIKIA, NI VIPI ALITENGANISHA ANGA NA ARDHI NA NI VIPI ALIUMBA JUA NA KULIWEKA MBALI NA MWANADAMU ILI LISIMDHULU? KITU CHA MWISHO JARIBU KUFIKILI HIYO PUMZI UNAYOVUTA SASA INATOKA WAPI? UNAPOLALA JE UNAJUA UTAAMKA? AMA UNAEZA KULALA UKAPILIZIA HUKO HUKO MOJA KWA MOJA,JE UNAFAHAMU IDADI HARISI YA MUDA WAKO WA UHAI DUNIANI? JE WEWE NI NANI HATA KUJUA ZAID YA MUNGU? JE WEWE UNA ELIMU GANI KUBWA ZAID YA MUNGU?.
Sasa hebu ngoja nitoe mfano mdogo wa watu waliowahi kutoa kufuru kwa Mungu kwa kujiona wao wanajua zaid na ni wajuzi zaid ya MUNGU halafu tutajifunza kupitia hapo

HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA.

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la muziki the beatles. Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.

Kwa wale wanaotaka kujua mengi, wafungue GOOGLE na kisha kusearch haya "People who mocked GOD and died" Utasoma mengi tu.

NIMALIZE KWA KUSEMA KWAMBA ULIMI ULIMPONZA KICHWA, SIUNGI MKONO HOJA AMA THREAD ZA NAMNA ILE ZA KUMCHAMBUA MUNGU HEBU TUWE NA KIKOMO. AMA KABLA HUJAANZA KUMKOSOA MUNGU TUFAHAMISHE HASWA JUU YA ELIMU YAKO NA TAALUMA YAKO IKIWA WEWE NI PROFESA AMA MTAALAMU WA ELIMU YA JUU ZAID KUMZID MUNGU HUENDA UKAWA NA NAFASI YA KUMKOSOA IKIWA HUNA TAFADHARI USIJARIBU.

MUNGU hana damu na nyama hata ashindane na mwanadamu wala MUNGU hafi soma katika biblia kitabu cha Mwanzo 6:3, lakini pia Angalia usije siku moja ukafanya dhambi iliyokuu maana haitasameheka kamwe soma katika kitabu cha Marko 3:28-30 na Luka 12:10
naona unaleta siasa mbinguni aya subir unachokitaka utakipata....
 
Nakuelewa kabisa kila point unayoandika ney kaaya,
Swali langu umelikimbia.: labda ni hivi nitolee mfano kwako, je unaweza ukatengeneza kitu ambacho unajua kabisa kitakudhuru (100% unajua sio kizuri na kitaleta mabalaa makubwa kwako)..
sidhani kama kile shetani alichokifanya kumsaliti Mungu ndio lilikuwa lengo la Mungu kumuumbia kabisa lile lilitokea baadae ni matokeo ya yale mazuri aliyokuwa anayategemea kutoka kwake lkn yakageuka na kuwa mabaya mimi nafikiri nia ya Mungu ilikuwa njema kabisa kuumba lkn yy ndio alimgeuka Mungu mm nikuambie tu hakuna kitu Mungu kakiumba kwa bahati mbaya hata kimoja.
 
Ukiona umeacha kufanya shughuli za kimaendeleo na akili yako inahoji vitu kama hivi......basi jitahidi haraka sana kuonana nawashauri nasaha pengine akili inaanza kuruka ama unaanza kuchanganyikiwa taratibu.......maana msongo wa mawazo hupelekea mtu kuona hakuna thamani ya kuishi hapa duniani na hivyo basi ataanza kutafakari mambo ya ajabu ajabu kichwani pake.......kama unavyofanya hapa.........

Fanya haraka kutafuta msaada maana unapoelekea utasema wewe ndiye MUNGU ..........shetani unayemuongelea ndio yupo ndani yako.....si wewe hapo unayezungumza.......go find help haraka nenda kwa washaurj nasaha
 
Kuona post ya kitoto kama hii ya kwako kwenye huu uzi nimecheka sana.....Yaani kuuliza ama kuhoji ni dalili za kuchanganyikiwa???...kweli bado tuna safari ndefu kuelekea maturity.....mimi lazima niulize na kuhoji kila kinachonihusu!!!
 
Sasa si ndio nakusaidia maana naona post yako imejaa kiburi cha kibinadamu ambacho si cha kawaida......hii haina tofauti na kumuhoji baba yako anatafutaje pesa na maisha yake anayafanye nje ya familia.......unaweza muuliza ila ni kutoka nje ya maadili......sasa ndio wewe........unaambiwa kuwa unateleza bado unakomaa na kutetea hoja yako ambayo haina mashiko kabisa.......kukusaidia hii ni dalili mbaya sana......

Na kama utadharau ninachokwambia hapa......usubirie sasa MUNGU akuonyeshe uwepo wake katika maisha yako.......si kutishi ila nakuelekeza.....so pay attention to details..........
 
Nenda dampo ukaweke hizi taka...hapa jf sii maala pake!!!
 
Nenda dampo ukaweke hizi taka...hapa jf sii maala pake!!!
Inabidi na wewe nikakutupe sasa maana ni miongoni mwa taka nilizoziona hapa..........

Una akili mbovu sana.......ila soon utapata unachokitafuta............
 
sidhani kama kile shetani alichokifanya kumsaliti Mungu ndio lilikuwa lengo la Mungu kumuumbia kabisa lile lilitokea baadae ni matokeo ya yale mazuri aliyokuwa anayategemea kutoka kwake lkn yakageuka na kuwa mabaya mimi nafikiri nia ya Mungu ilikuwa njema kabisa kuumba lkn yy ndio alimgeuka Mungu mm nikuambie tu hakuna kitu Mungu kakiumba kwa bahati mbaya hata kimoja.
ney kaaya una maelezo mazuri sana kijana wangu kutoka pande za ntalikwa..

Nadhani binafsi unanijua sio mpiga Mungu ,
Swali: jee Muumba hakujua kama shetani atakuja kumsaliti ilihal anamuumba kwa uzuri? Au alikua anabahatisha?
Anyway me nadhan tukubaliane kuwa hivi vitabu vya dini bado vina utata ndan yake,(ndio mana wengine wanaviita riwaya za wazungu)
 
Nimeona Thread inayojaribu kuonyesha makosa kumi ya Mungu ndo maaana nikachukua hatua Yakinifu kuandika haya..Kwanza Kabisa na Ifaamike Mungu anajua yote na Kazi Yake kamwe haina makosa,ebu Tuanze
(whats a Mistake)? a wrong way of doing something,misguided action,inaccuracy!!!!!!!!
=>Kusema Mungu ana makosa ni sawa na kusema hajakamilika(perfection) Kwaio hana tofauti na sisi Jambo ambalo ni kosa,Lucifer Alitenda Hivi Hivi

1.KUMUUMBA SHETANI
Mungu hakumuumba shetani alimuumba Lucifer ambae alingiwa na wivu due to the status quo of Jesus akataka awe Miongoni mwa utatu mtakatifu eventually ule wivu ukasababisha atende dhambi unayoifanya ya kumkosoa Mungu(Imperfection)

2.KUISHI MAFICHONI
Mungu Hajifichi,dhambi zetu ndo zinathfarakanisha na yeye maana hawezi kukaa na sisi hakika tutakufa awali kulingana na Biblia mbona alikua akihukutana na Adam wakaongea sema tatizo ni pale alipotenda dhambi,Israel walitaka kumuona ILA kabla hajafika walighairi wakasema hawataki tena

3.MAFURIKO
Aim ya mafuriko ni kupunguza maasi na Age generally,sio kuondoa dhambi kabisa maana watu wangeendelea na nyendo zao Mungu alisahaulika kabsa lakini kutokana na UPENDO wake akaamua kuchukua hatua hio baada ya warning ya miaka karibia 500 kweli hata kama wee ni kiazi miaka yote hii
elewi concept tu???

4.SAFARI YA WANA WA ISRAEL
Lord promised abraham kuwa atampa nchi specifically ya CANAAN sio popote tu that was the Point kutimiza ahadi sio Ilimradi nchi tu na nyakati zile struggle Ili kusurvive Ilkua ni suala la kawaida ndo maana hata Israel walipokua wanazingua walichezea mkong'oto tuuu!

5.AHADI YA ABRAHAM
Ivii unajua dunia ina miaka mingapi???mimi mwenyewe sina uhakika lakini uzao wa abraham compared to na Generation ya awali uliongezeka japo hukufikia nyota za angani maana israel walikua wagumu mioyoni kwa sababu Mungu sio dictator hakulazimisha

6.ALLERGY 7.MUTATIONS NA 8.NATURAL CALAMITIES
Hivi vyote ni side effects za dhambi duniani,mwanzoni maisha yalikua Bomba vitabu vingine mpka vinasema adam alipoona Kondoo anakuja na kutoka damu walipokua wanatengenezema mavazi alilia sana,hakuamini kilichotokea maana alikua hajawahi ona alafu Mungu alilaani ardhi na dunia Generally ndo maana haya yote yanatokea,vingine sisi ndio chanzo kutokana na vitu kma ukuaji wa sayansi ya technolojia

10.JEHANAMU
Lengo la Moto sio kukomesha watu na sio kwamba God enjoys this kuprove hapendi ndo maana akamtuma mwanae hata kama tulishakataa mara nyingi,moto una lengo la KUTOKOMEZA DHAMBI Ili dunia ibaki salama tukutane na Mungu kma Ilivyokua awali.Na ingeweza kuwa njia nyingine sio lazima moto lakini akachagua njia hii na kuchomwa sio lazima ni Option making it more Fairer sijui binadamu upewe nini uweze kuona Haya.

Pamoja na majibu yako mazuri mkuu, ningependa kuuliza maswali machache ya nyongeza.
3. MAFURIKO.
Unataka kusema kwamba hakujua kama baada ya mafuriko bado uasi utaendelea? Akiwa mwenye nguvu na uwezo, mwenye mamlaka juu ya wakati ningetegemea tayari ajue kwamba baada ya nuhu na safina mbeleni itakuwepo sodoma na gomora. swali la msingi linabaki, kwamba usipotatua kiini cha tatizo utaendelea kushughulikia matokeo na mwishowe inaingia number 8, NATURAL CALAMITIES. is it that He cannot find the root cause of uasi au ameshindwa/hataki kushughulika nayo so anaamua kushughulika na matokeo yake.

4. SAFARI YA WANAISRAEL
Sasa kama aliwaahidi waisraeli Canaan, mbona aliruhusu watu wengine wakae pale? Angeweza kupafanya pawe pori lenye wanyama wakali kiasi ambacho binadamu wangepapotezea, au angeweka volcano ya muda, au angepafanya jangwa....na hayo ni mawazo yangu tu, nina uhakika Mungu ana namna kibao za kuhakikisha anawatunzia waisraeli siti. mwenyewe nilikuaga nabeba begi la mshkaji namtunzia seat kwenye lecture hall, was it really neccessary kuua watu wengi vile na kuwafukuza kwenye nchi yao? au waisraeli ni bora kuliko mataifa mengine? in that case Mungu ana ubaguzi?

6&7. ALLERGIES & MUTATIONS.
Nilibahatika kuchukua kozi ya immunology chuo, hivyo kidogo ninaelewa kwamba mzio na mutations ni vitu ambavyo kimsingi havizuiliki. baadhi ya mutations zina faida zake evolutionarily, lakini faida za allergies bado sijazielewa labda wanazijua wenye masters ya immunology. lakini unaposema kwamba vinasababishwa na dhambi, watoto wachanga wana dhambi gani? yaani dhambi afanye mwingine, halafu adhabu apewe mwingine mkuu? tena hata kabla hajapata uwezo wa kuanza kufanya dhambi zake mwenyewe?? hiyo mahakama ya Mungu mbona kali sana mkuu. kwa mtindo huo tutapona kweli?

Kimsingi binadamu tunahangaika sana kumuelewa Mungu, na kuelewa mapenzi yake ndio maana watu wa kila nyakati na mahali wanamtafsiri kivyao na mapenzi yake wanayaeleza kivyao. kujifanya authority wa mapenzi ya mungu mimi naona ni arrogance bordering on being delusional. Tukubaliane tu kwamba Mungu yupo, halafu tuishi kibinadamu tu kwa kujaliana halafu basi. Haya mambo ya kutafsiri mapenzi ya Mungu lazima majib yako yawe na mashimo
 
ney kaaya una maelezo mazuri sana kijana wangu kutoka pande za ntalikwa..

Nadhani binafsi unanijua sio mpiga Mungu ,
Swali: jee Muumba hakujua kama shetani atakuja kumsaliti ilihal anamuumba kwa uzuri? Au alikua anabahatisha?
Anyway me nadhan tukubaliane kuwa hivi vitabu vya dini bado vina utata ndan yake,(ndio mana wengine wanaviita riwaya za wazungu)
vina utata kama hujajikita kutaka kuvijua ila na ndio maana hata wanafunzi wa Yesu mahali pengine walikuwa wanamuuliza alikuwa anamaanisha nini coz ilikuwa kimafumbo biblia imeandikwa kimafumbo sana na ili huielewe ni lazima umuombe Mungu akufunulie kupitia roho wake maana anasema yeye ni mwalimu so atatufundisha wewe kubali tu Mungu akufundishe uone itakavyokuwa nzuri na utaipenda biblia na ukitaka kuijua Bibli tamani roho wa Mungu akufundishe yy utaifurahia na watu wengi huisoma biblia kama gazeti lkn hakuna kitabu kinamafumbo kama kile hakuna mtu awezaye kuyafumbua mafumbo ya Mungu ila Mungu mwenyewe sasa tumuombe yeye ili atufundishe yale tusiyoyaelewa na tusio yajua au yanayotutaztiza MUNGU AKUBARIKI sana na naomba Mungu ikute nia yako ilikuwa ni kujifunza tu na sivinginevyo.
 
Hay bhana, Asante mkuu.
 
Pamoja na majibu yako mazuri mkuu, ningependa kuuliza maswali machache ya nyongeza.
3. MAFURIKO.
Unataka kusema kwamba hakujua kama baada ya mafuriko bado uasi utaendelea? Akiwa mwenye nguvu na uwezo, mwenye mamlaka juu ya wakati ningetegemea tayari ajue kwamba baada ya nuhu na safina mbeleni itakuwepo sodoma na gomora. swali la msingi linabaki, kwamba usipotatua kiini cha tatizo utaendelea kushughulikia matokeo na mwishowe inaingia number 8, NATURAL CALAMITIES. is it that He cannot find the root cause of uasi au ameshindwa/hataki kushughulika nayo so anaamua kushughulika na matokeo yake.

4. SAFARI YA WANAISRAEL
Sasa kama aliwaahidi waisraeli Canaan, mbona aliruhusu watu wengine wakae pale? Angeweza kupafanya pawe pori lenye wanyama wakali kiasi ambacho binadamu wangepapotezea, au angeweka volcano ya muda, au angepafanya jangwa....na hayo ni mawazo yangu tu, nina uhakika Mungu ana namna kibao za kuhakikisha anawatunzia waisraeli siti. mwenyewe nilikuaga nabeba begi la mshkaji namtunzia seat kwenye lecture hall, was it really neccessary kuua watu wengi vile na kuwafukuza kwenye nchi yao? au waisraeli ni bora kuliko mataifa mengine? in that case Mungu ana ubaguzi?

6&7. ALLERGIES & MUTATIONS.
Nilibahatika kuchukua kozi ya immunology chuo, hivyo kidogo ninaelewa kwamba mzio na mutations ni vitu ambavyo kimsingi havizuiliki. baadhi ya mutations zina faida zake evolutionarily, lakini faida za allergies bado sijazielewa labda wanazijua wenye masters ya immunology. lakini unaposema kwamba vinasababishwa na dhambi, watoto wachanga wana dhambi gani? yaani dhambi afanye mwingine, halafu adhabu apewe mwingine mkuu? tena hata kabla hajapata uwezo wa kuanza kufanya dhambi zake mwenyewe?? hiyo mahakama ya Mungu mbona kali sana mkuu. kwa mtindo huo tutapona kweli?

Kimsingi binadamu tunahangaika sana kumuelewa Mungu, na kuelewa mapenzi yake ndio maana watu wa kila nyakati na mahali wanamtafsiri kivyao na mapenzi yake wanayaeleza kivyao. kujifanya authority wa mapenzi ya mungu mimi naona ni arrogance bordering on being delusional. Tukubaliane tu kwamba Mungu yupo, halafu tuishi kibinadamu tu kwa kujaliana halafu basi. Haya mambo ya kutafsiri mapenzi ya Mungu lazima majib yako yawe na mashimo
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kutambua matumizi ya ubongo wako na kuutumia kisawasawaa....Yaani umeongea mambo yanayo symbolise mental maturity, sina haja ya kurudia ulichoandika lakini hii ni miongoni mwa posti chache na bora zaidi kwenye hii thread.Yes! kuna watu wamejitia umeneja kwa Mungu...wanatumia jina lake ili kumanupulate watu wengine, kwamba wao ndio wanaojua Mungu anataka tutende lipi na tuache lipi ili hali kwa kiasi kikubwa wanajali maslai yao tu. Hapa Duniani tunatakiwa kuishi kwa amani na upendo tu vinginevyo ni mbwembwe na kunyonyana.Siwezi kusema yote ila kwa haya madini uliyotema hapa TZ inahitaji watu kama wewe mkuu....BRAVO BRAVO MAN.
 
M najiulizag tu kwanz mbinguni ni wapi? Au lile Anga la bluu lipo kwel km tunavyoliona ? Na je nyuma yake ndo uko mbngun au ? Vp kuhusu wale jamaa waliokuwag wanajenga mnara wafike mbinguni ni kwamba mbinguni ni juu tu km tunavyoamin wengi au ? Anyway I blv in God but sidhan kama Mungu yupo km tunavyomtengeneza vichwan mwetu. Au pengn hakuna maelezo ya kutosha kumuelezea hata angeamua kujieleza tusingeelewa. Mayb we are all right or wrong in our religious beliefs
 
Kosa kubwa sana la huyo mleta maswali ni uwezo wake wa kuelewa Uwezo wa Mungu. Kipimo anachotumia kujua hili ni kosa au sio kola la Mungu anacho mwenyewe kichwani
Kutusirikisha mauzauza yake ni mapungufu ya kimantiki
 
Mi Nina Mawili. Kuna Watu Kama Kiranga Humu Jf. Mbona Hawadhuriki? Kingine Mbona Ni Wazungu Tu?
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kutambua matumizi ya ubongo wako na kuutumia kisawasawaa....Yaani umeongea mambo yanayo symbolise mental maturity, sina haja ya kurudia ulichoandika lakini hii ni miongoni mwa posti chache na bora zaidi kwenye hii thread.Yes! kuna watu wamejitia umeneja kwa Mungu...wanatumia jina lake ili kumanupulate watu wengine, kwamba wao ndio wanaojua Mungu anataka tutende lipi na tuache lipi ili hali kwa kiasi kikubwa wanajali maslai yao tu. Hapa Duniani tunatakiwa kuishi kwa amani na upendo tu vinginevyo ni mbwembwe na kunyonyana.Siwezi kusema yote ila kwa haya madini uliyotema hapa TZ inahitaji watu kama wewe mkuu....BRAVO BRAVO MAN.

Thanks mkuu, hua ninafikiria pale waheshimiwa sana wachungaji wanapokomalia fungu la 10 huku mishipa imewasimama as if wamezifanyia kazi. Kwamba unamtolea Mungu wakati namuona kabisa Kakobe anainunulia prado mi hua sielewi kwa kweli. Na usipotoa unaonekana muasi, hakuna hata mmoja kati ya wanaokuhukumu anaekumbuka kwamba hilo kanisa analosali nalo lilianzishwa kwa uasi in the sense that mchungaji/askofu aliwahi kua wa kanisa fulani wakashindwana (mara nyingi sababu ya maslahi) na yeye akaanzisha kanisa lake. Mifano iko mingi tu ya watu kujipumbaza na kupumbaza wenzao kwa kisingizio cha Mungu, ifike mahala kijiko kiitwe kijiko tu kama kilivyo. Asilimia kubwa watu wanaenda kwenye nyumba za ibada just to find a place to belong, na wanatoa sadaka ili wajisikie kwamba wamefanya kitu chema walau katika mlima wa vitu vibaya wanavyovifanya.
 
Back
Top Bottom