Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Ukiona mambo ya kiimani yanakuwa na ugumu kuyafumbua, ujue hapo ndio ukomo wa akili z a binadamu.na ndio uwezo wa mungu wa vyote unapoanzia
 
Habari wana Jamii..
Kwa masikitiko makubwa nimeamua kuandika uzii huu huku nikiwa na woga na hofu ya juu kwasababu ya Mada nitakayozungumzia haikufaa kuchambuliwa maana haichambuliki na ni makosa makubwa.
Kuna bwana mmoja ndani ya chumba chetu hiki cha wanaIntelligesia aliweka uzi ukisema "MAKOSA 10 ALIYOTENDA MUNGU"
Na akayaelezea ifuatavyo:-

"(1.KUMUUMBA SHETANI
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY)
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwani kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwani anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu again fuze wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATING THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:>Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani? )"
MWISHO WA KUNUKUU.

Naomba niseme kitu japokuwa tunauhuru wa kusema chochote hebu tuwe tunajitahadhari maana wakati mwingine ulimi uliponza kichwa MUNGU si mwanadamu na MUNGU hafikiliki kilahisi jinsi hiyo. Hata kipindi cha Nuhu MUNGU baada ya kumwambia Nuhu atengeneze safina watu wengine wlikua wakimcheka Nuhu kwa kile alichokuwa akifanya na hata kipindi cha mvua kilipokaribia aliwaita waingie ila walikataa na ku mkashfu vilevile lakini mwisho wake wote tunafahamu ilikuaje.
TUKUMBUKE KUWA HAIJALISHI UTOFAUTI WETU BINADAMU WA IMANI ZETU KATIKA DINI MBALI MBALI, LAKINI MWISHO WA SIKU KILA MTU ANAKILI MUNGU YUPO NA NI MKUU NA MUWEZA WA VYOTE NA ALIUMBA VYOTE, JARIBU KUWAZA NI VIPI ALIUMBA MBINGU PASIPO NGUZO ZA KUSHIKIA, NI VIPI ALITENGANISHA ANGA NA ARDHI NA NI VIPI ALIUMBA JUA NA KULIWEKA MBALI NA MWANADAMU ILI LISIMDHULU? KITU CHA MWISHO JARIBU KUFIKILI HIYO PUMZI UNAYOVUTA SASA INATOKA WAPI? UNAPOLALA JE UNAJUA UTAAMKA? AMA UNAEZA KULALA UKAPILIZIA HUKO HUKO MOJA KWA MOJA,JE UNAFAHAMU IDADI HARISI YA MUDA WAKO WA UHAI DUNIANI? JE WEWE NI NANI HATA KUJUA ZAID YA MUNGU? JE WEWE UNA ELIMU GANI KUBWA ZAID YA MUNGU?.
Sasa hebu ngoja nitoe mfano mdogo wa watu waliowahi kutoa kufuru kwa Mungu kwa kujiona wao wanajua zaid na ni wajuzi zaid ya MUNGU halafu tutajifunza kupitia hapo


HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA.

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la muziki the beatles. Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.

Kwa wale wanaotaka kujua mengi, wafungue GOOGLE na kisha kusearch haya "People who mocked GOD and died" Utasoma mengi tu.

NIMALIZE KWA KUSEMA KWAMBA ULIMI ULIMPONZA KICHWA, SIUNGI MKONO HOJA AMA THREAD ZA NAMNA ILE ZA KUMCHAMBUA MUNGU HEBU TUWE NA KIKOMO. AMA KABLA HUJAANZA KUMKOSOA MUNGU TUFAHAMISHE HASWA JUU YA ELIMU YAKO NA TAALUMA YAKO IKIWA WEWE NI PROFESA AMA MTAALAMU WA ELIMU YA JUU ZAID KUMZID MUNGU HUENDA UKAWA NA NAFASI YA KUMKOSOA IKIWA HUNA TAFADHARI USIJARIBU.

MUNGU hana damu na nyama hata ashindane na mwanadamu wala MUNGU hafi soma katika biblia kitabu cha Mwanzo 6:3, lakini pia Angalia usije siku moja ukafanya dhambi iliyokuu maana haitasameheka kamwe soma katika kitabu cha Marko 3:28-30 na Luka 12:10
mimi si mpinga din,ila sijaelewa hoja yako
 
Nafikiri ungeweza kutoa majibu ya maswali ungekuwa umetusaidia sana watu wenye imani ndogo kuliko kuandika maneno mengi ambayo hayatusaidii kumjua mungu. Ukristo uislam znataka watu watafute elimu na waulize pale wasipopaju ila nashangaa siku hizi kila utakacho uliza utaambiwa ww amini tu. Huwezi kumjua mungu Wa kweli kama ww unaamini hata vitu visivyoaminika. Huu ni ujinga
umeongea point mkuu
 
Nimetaka kuandika kitu ila nkakumbuka MUNGU ananiona kifuatacho kitanigharimu
 
Mmmmh haya mi sisemi lolote najua mungu yupo alikuwepo na ataendelea kuwepo na kwake tutarejea hivo tu kila mtu ana siku yake ya kuondoka duniani so tusimjsdili mungu hapa weken mambo ya siasa na issue zingine za kijamii nimesoma post hiyo daa ni hatari mtoa post haogopi mungu ni mwema najua kamsamehe tyr
 
  • Thanks
Reactions: ram
Subhanallah, namuomba Mungu akujibu unachokitaka muda huu huu, uone ukubwa wako
 
Mleta mada umejazwa sana uoga. sijaona kibaya katika hoja hizi ukiondoa kwamba ni ngumu.
 
Mkuu ebu shughulisha kidogo akili yako umeongea Pointless kabisa hio mifano imekwisha sambaza sana wana propaganda wa dini aka wafia dini hamna lolote nyie kama Mungu angekuwepo angeingamiza America ambapo nusu ya taifa lile ni wasiomuamini na kumejaa starehe za kila namna. Mungu nu kwa maskini haswa afrika kwa nia ya kujifariji mnajitoa akili sana kuliko hata hao walio waletea hizo imani kwa nia ya kuwatawala
Labda nikusaidie kitu kidogo,wewe utakuwa ndo mvivu wa kuishughulisha akili yako hivi kwa kuwa mungu haonekani ndo itakuwa hayupo au nikwakuwa Huna chombo cha kumuonea?mfano kama ungekuwa huna simu alafu mmtu akwambie angani kuna maandishi ungeamini?bila shaka ungebisha lkini kwa kuwa unakifaa kinachokuwezesha kuyaona nakuyasoma huwezi kubisha,huo ni mfano mdogo wa simu,pia akili yako inakubali umewahi kuish tumboni kwa mama yako miezi tisa ukila ukinywa na hata kulala,kisha ukazaliwa unazaliwa tu unakuta tayar maziwa kifuani kwa mama yako yamesha andaliwa unaanza kunyonya tena ukila dhaifu kabisa hata akili huna,kwa maziwa ya mama tu viungo vyako vinaanza kuwa na nguvu mmpaka mwisho unajiona ushakuwa mmtu kamili na unajitambua pia akili yako inakubali kuna kufa kama unaamini mungu hayupo zuia usife kama huwezi kuzuia kufa baci yupo na utakuwa na naye,mfano wa 2.kama mungu hayupo niambie pumz unayovuta inatengenezwa kiwanda gani?ni haya tu kwa uchache mmkuu.
 
ndio sisi hatutambuliki kama wakirsto wa dini za uongo amabao wanafundisha falsafa badala ya biblia takatifu sisi ndio wakristo wa kweli ndio maana tupo tofaut na dini zote za uongo
Tatizo hata huku kwetu nako tunanyosheana vidole.kila mtu anasema kwangu ndio njia nyembamba iendayo Mbinguni matokeo yake mpaka sasa ukristo tu una njia nyembamba kama elfu 20.
pia kutona nilichojibu hakifuti post yangu wataelewa wengine wenye akili zinataka kuelewa wale ambao wanajua Mungu ni mwenye haki sikuzote
 
Mkuu naona umeandika Uzi mrefu ambao hauna maana kabisa
 
Naona wakristo kama kawaida yenu mmeanza kukosoana wenyewe kwa tafsiri zenu za biblia..kila mtu anajiona ni bora kuliko mwingine...hopeless.
Yaaani mkuu mi huwa nachanganyikiwa kwa nini tumegawanyika sana. sehem moja unaweza kukuta makanisa tofauti hata sita.
 
Labda nikusaidie kitu kidogo,wewe utakuwa ndo mvivu wa kuishughulisha akili yako hivi kwa kuwa mungu haonekani ndo itakuwa hayupo au nikwakuwa Huna chombo cha kumuonea?mfano kama ungekuwa huna simu alafu mmtu akwambie angani kuna maandishi ungeamini?bila shaka ungebisha lkini kwa kuwa unakifaa kinachokuwezesha kuyaona nakuyasoma huwezi kubisha,huo ni mfano mdogo wa simu,pia akili yako inakubali umewahi kuish tumboni kwa mama yako miezi tisa ukila ukinywa na hata kulala,kisha ukazaliwa unazaliwa tu unakuta tayar maziwa kifuani kwa mama yako yamesha andaliwa unaanza kunyonya tena ukila dhaifu kabisa hata akili huna,kwa maziwa ya mama tu viungo vyako vinaanza kuwa na nguvu mmpaka mwisho unajiona ushakuwa mmtu kamili na unajitambua pia akili yako inakubali kuna kufa kama unaamini mungu hayupo zuia usife kama huwezi kuzuia kufa baci yupo na utakuwa na naye,mfano wa 2.kama mungu hayupo niambie pumz unayovuta inatengenezwa kiwanda gani?ni haya tu kwa uchache mmkuu.
Mkuu Hivo vitu vyote unavyojaribu kutoa mifano Science imevielezea vyema sana kwa kweli sijifikiri hata nikupe uchambuzi kuwa Pumzi tunayovuta na inayofanya tusurvive ni oxygen science ya primary kabisa, Mungu wako hadhibitishikiki kiaina yoyote Sasa ukitolea mifano vitu kama simu naweza kukuchambulia A to Z sasa ww niambie Mungu anafafanaje anaishi wapi?
 
Ukiona mambo ya kiimani yanakuwa na ugumu kuyafumbua, ujue hapo ndio ukomo wa akili z a binadamu.na ndio uwezo wa mungu wa vyote unapoanzia
Mungu ametupa kila kitu na ametusistizia kuishika elimu na kuitafuta kwa nguvu zote kuliko dhahabu na fedha. ni wajibu wetu kupata majibu ya maswali magumu.
 
Hizi Habari za mungu na Malaika sijui shetani, ndo vimefanya bara hili watu kuwa maskini sana, wafia dini wengi ni masikini wa kutupa. Yani ufanye makosa kwa 50years halafu ukakae hell forever, embu tudanganyeni na kingine but sio hivi vitabu mmeandika.
 
Pole mkuu..Mimi niliamua tu kuwa mkristo huru.. Natafsiri bible navyoelewa na kufuata uelewa wangu, si wa padre, Mchungaji wala papa..na simshawishi mtu afuate imani yangu..matter of fact mwisho wa dahari ufikapo kila nafsi itahukumiwa kimpango wake...tusijelaumiana "ooh ulinipoteza" tuanze pigana huko Motoni (kama moto wenyewe upo)
Yaaani mkuu mi huwa nachanganyikiwa kwa nini tumegawanyika sana. sehem moja unaweza kukuta makanisa tofauti hata sita.
 
Pole mkuu..Mimi niliamua tu kuwa mkristo huru.. Natafsiri bible navyoelewa na kufuata uelewa wangu, si wa padre, Mchungaji wala papa..na simshawishi mtu afuate imani yangu..matter of fact mwisho wa dahari ufikapo kila nafsi itahukumiwa kimpango wake...tusijelaumiana "ooh ulinipoteza" tuanze pigana huko Motoni (kama moto wenyewe upo)
Mkuu...
Inaonekana wewe ni shabiki wa Kendrick...
Kuna wimbo wa Kendrick anaonekana kama yuko barabarani anatembea alafu kuna watu wanafariki anachofanya yeye ni kurap na kuziangalia zile pipo zilizofariki...
Unaweza kunitajia jina la huo wimbo mkuu..!
 
kwani mafundisho ya yesu na ukristo si ushaanza kupotea huko ulaya au wewe unaona kosa la hyo john lennon ni nini?
 
Jamani nawaomba ndugu zangu tusifikie huku binafsi naamini Mungu yupo na nnaomba hasira yake itulie kwa mijadala kama hii tuwe na mipaka wakuu
 
Back
Top Bottom