Makato ya Mshahara kwa Daktari mpya Serikalini, bado tuna safari ndefu sana

Waajiriwa mnalipwa mshahara na bado mnalialia
Wafikirieni jobless na watu wasio na sustainable income huwa wanapitia moyo wa aina gani kitaa ?
Na ndio muache zile kauli zenu za kebehi na dharau za " jiajiri "
Si mjiajiri ?
 
Kwa makadirio, mshahara wa daktari Serikalini basic ni 1,480,000

HESLB wanakata 222,000
74000 ya PSSSF
kodi ni 290,580
bima ya afya 44,400

Unabaki na 849,020

Toa kodi ya nyumba, bill ya maji, umeme, usafiri na chakula halafu niambie unabaki na sh ngapi?
Duuh
 
Daktari mpya ndio wa namna gani

Kodi kwa maendeleo ya wenye nchi.

Hapo inabidi wanunue magari ya ofisi na poa kujenga nyumba za viongozi

Kodi muhimu sana

Kwani mbunge mpya analipa kiasi gani?
 
Na sisi tunaolipwa laki tatu kwa mwezi tusemaje?

Tanzania issue siyo madaktari, Watanzania wote tunaishi kama mateka, tatizo ni Ccm.

Hapo kuna mtu kaishia la saba ana chukuwa take home million 14 kwa mwezi kwa kazi ya kugonga meza tu bungeni.
Kazi kweli kweli
IMG-20240119-WA0012.jpg
 
Kodi,umeme,maji,chakula havifiki laki nne
Kodi kwenye nyumba nzuri,Umeme wa kutosha usiokatika,Chakula Balanced Diet kwa familia standard,Usafiri wa kwenda kazini wenye hadhi ya Dktari ili afike kwa wakti,atoe huduma akiwa relaxed na afurahie kazi yake Inahitajika angalau Milioni 2 Kisha Ndo aweke akiba.

Akiishi kwa mkate tu kila siku kwa familia ya watu wanne.Asubuhi Mikate minne,Mchana Mikate minne,Jioni Mikate minne.Chai na sukari kwa siku chakula ni 35000 kwa familia yote ambayo kwa mwezi ni zaidi ya Milioni moja.Sasa Sijui wewe unaposema havfiki laki nne unataka watu waishi kama wafungwa mlo mmoja kwa siku 2? Daktari lazima ale Balanced Diet
 
Back
Top Bottom