Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,754
Tangu jana tarehe 20 Februari 2023 serikali imeweka utartibu mpya kwenye kituo cha mabasi cha Kimataifa cha Magufuli Bus Terminal pale Mbezi; ambao kimantiki ni utaratibu mujarabu unaoleta tija kwa jamii. Utaratibu wa kutumia kadi ya kieletronic ya N-Card kwa wananchi wanaoingia ndani.
Mantiki yake kama nionavyo mimi Msanii Mkuu wa Taifa ni:-
Serikali kupitia maelezo yake imesema matumizi ya kadi hizo ni kwa majaribio au uangalizi wa wiki kadhaa kuangalia utendaji wake na ufanisi wake. Sambamba na hilo imeweka utaratibu mpya wa kila anayeingia yaani wasindikizaji na abiria atalazimika kulipia kiingilio ambapo watalazimika kununua kadi au kutumia kadi za papo hapo ili waweze kuingia ndani ya kituo. Lengo zuri la serikali kukusanya mapato kama tulivyoiagiza kupitia sheria ya fedha iliyopitishwa na wawakilishi wetu Bungeni linaweza pia kuleta ukakasi kwenye utekelezaji wake. Hapa yanahitajika maelezo ya kina kutuelewesha wenye nchi mantiki ya utaratibu mpya wa abiria ambaye anakata tiketi yake kwa njia ya kieletronic na kulipia kodi ya serikali na pia ambaye kimantiki waendesha huduma za usafiri wanalipia kuingia pale kituoni kwa kuwachukua abiria ambao tayari kupitia tiketi zao wameshachangia pato la nchi.
Inawezekana lengo la serikali ni kutumia mapato yatokanayo na stendi kuu kuboresha huduma za jamii ikiwemo stendi husika. Lakini hii fractional collection iliyobuniwa inazidi kuleta ukakasi kwa wanaouangalia uchumi wetu kwa uwiano na vipato vya wananchi.
Katika hili ningependa kutoa ushauri wangu kwa serikali:-
Nawasilisha
Mantiki yake kama nionavyo mimi Msanii Mkuu wa Taifa ni:-
- Ufanisi wa kutunza muda wa wananchi wanaolazimika kupanga foleni kwa wakatisha tiketi pale kwenye mageti ya kuingilia
- Udhibiti wa upotevu wa mapato ya serikali unaotokana na kukosekana kwa usimamizi thabiti wa tiketi zinazotumika kuingilia ambapo inarahisisha wahuni kuchapisha zao na kutafuna pesa ya umma
- Kuondoka kwa wakandarasi wa kukusanya mapato ya kiingilio ambao walikuwa wanagawana na serikali kwa kila shilingi inahokusanywa ukiondoa zile zinazoingia mifukoni mwao moja kwa moja.
- Kuithaminisha N-Card ambayo kimsingi ni matokeo ya utafiti wa wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambao ilianzia kutumika Sabasaba, vivuko vya Kigamboni, kuingilia kwenye viwanja vya soka na sasa inaendelea kuunganishwa na huduma nyingi za umma hivyo kuleta urahisi wa upataji huduma kwenye maeneo ya umma.
Serikali kupitia maelezo yake imesema matumizi ya kadi hizo ni kwa majaribio au uangalizi wa wiki kadhaa kuangalia utendaji wake na ufanisi wake. Sambamba na hilo imeweka utaratibu mpya wa kila anayeingia yaani wasindikizaji na abiria atalazimika kulipia kiingilio ambapo watalazimika kununua kadi au kutumia kadi za papo hapo ili waweze kuingia ndani ya kituo. Lengo zuri la serikali kukusanya mapato kama tulivyoiagiza kupitia sheria ya fedha iliyopitishwa na wawakilishi wetu Bungeni linaweza pia kuleta ukakasi kwenye utekelezaji wake. Hapa yanahitajika maelezo ya kina kutuelewesha wenye nchi mantiki ya utaratibu mpya wa abiria ambaye anakata tiketi yake kwa njia ya kieletronic na kulipia kodi ya serikali na pia ambaye kimantiki waendesha huduma za usafiri wanalipia kuingia pale kituoni kwa kuwachukua abiria ambao tayari kupitia tiketi zao wameshachangia pato la nchi.
Inawezekana lengo la serikali ni kutumia mapato yatokanayo na stendi kuu kuboresha huduma za jamii ikiwemo stendi husika. Lakini hii fractional collection iliyobuniwa inazidi kuleta ukakasi kwa wanaouangalia uchumi wetu kwa uwiano na vipato vya wananchi.
Katika hili ningependa kutoa ushauri wangu kwa serikali:-
- Serikali itafakari upya hili suala la abiria wenye ticketi zao mkononi kulipia tena kuingilia kituo kikuu cha Magufuli. Hapo awali abiria walikuwa hawalipii lakini kuanzia tarehe 20 Februari wameanza kulipia na imezua manung'uniko makubwa. Tunaamini mkoa ndiyo wanaosimamia mapato ya pale hivyo wwtaalam watafakari namna ya kumpunguzia mzigo wa makato abiria ama wananchi wanaotumia kituo kikuu.
- Katika mapato yanayotokana na viingilio vya maeneo ya umma kama vile Kituo Kikuu cha Magufuli, Daraja la Nyerere na Kivuko cha Magogoni; serikali itenge asilimia 20% ya kila mapato ya siku iingie kwenye fungu la maboresho ya eneo husika. Nalisema hili kwa sababu mapato makubwa yanayokusanywa maeneo hayo hayalingani hadhi ya mapato yanayokusanywa. Leo ukipita daraja la Kigamboni utaona mkundombinu inayohitaji ukarabati wa mara kwa mara, ukienda fery ndiyo kabisaa hali si nzuri kwa sababu yale majengo ya kusubiria abiria ni hatarishi hayana escape safe plan endapo dharura itajitokeza. Pia msongamano unawezesha magonjwa ya maambukizo kwa njia ya hewa. Vivuko yaani pantoni hazifanyiwi ukarabati wa kikalenda ambapo hupelekea hasara kubwa kwa serikali kugharimia matengenezo makubwa ambapo ukararabati wa kawaida ungeweza kuepusha hasara kwa fedha za umma. Maeneo yote yanahitaji maboresho ambapo serikali ikiamua kutenga asilimia 20% ya mapato ya kila siku na kusimamia vyema itawezesha maeneo yetu kuwa na mwonekano wa kimataifa
- Serikali ione umuhimu wa N-Card kutumiwa kwenye maeneo mengi ya huduma za umma kama vile TANAPA, UDART yaani mabasi ya Mwendokasi na zitumike kwenye malipo ya huduma za kumwona daktari hospitali za umma kwa wananchi wasio na bima ya Afya.
- Serikali kupitia BOT kuanzisha dirisha la N-Card kwenye mabenki ili kuwezesha wananchi kurefill cards zao kwa urahisi. Benki nyingi zinaendesha huduma za uwakala mitaani hivyo wananchi hawatolazimika kupanga foleni ndefu kurefill cards zao kwenye mageti ya huduma husika.
- Serikali itoe elimu kwa umma bila kuchoka kuhusu umuhimu na manufaa ya matumizi ya electronic cards kwenye huduma za umma.
- Serikali iweke uangalizi
Nawasilisha