Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweke wazi kuhusiana na tozo mpya za kibenki na madhumuni yake kwa jamii

Zulu Man Tz

Member
Sep 23, 2020
73
99
Wananchi wapo katika hali ya kupigwa na butwaa kuhusiana na hayo makato mapya ya mihamala kibenki. Serikali yetu imekuwa ikifanya maamuzi ya tozo bila utoaji taarifa kwa wananchi husika ambao sisi ndio waathirika wakubwa wa tozo hizo kiuchumi, kila maamuzi yanapofanywa na serikali inayotambua nini maana ya demokrasia na umuhimu wake katika ushirikishwaji wa wananchi kwa Nyanja tofauti tofauti yanakuwa na kusudio maalumu. Swali ..Je serikali yetu ina ajenda gan kuhusiana na izo tozo mpya tuwekwe wazi..? . Siku zote maendeleo ya kweli hayana chama, tuongee kwa uhalisia mimi niko mwaka wa pili wa masomo ya uhasibu ya shahada yangu CBE uelewe kidogo ninao kwenye maswala ya fedha

Mfano. Ali anafanya kazi kwenye kampuni X na mshahara wake ni kiasi cha Tsh.650,000/= malipo ya mshahara yanafanyika kupitia benki Y. kutokana na sheria ya kipato cha kodi (Income Tax Act rev. 2017) Ali anatakiwa kulipa kodi ifahamikayo kama Pay As You Earn (P.A.Y.E) kwenye range ya mshahara aboveTsh.520,000 mpaka Tsh.760,000/= kodi itakayokatwa ni Tsh 20,000/= + 20% ya kiwango kilichoongezeka kutoka Tsh 520,000/=

Tsh.20,000 + (650,000-520,000)*20%= Tsh.46,000/= hii ni kwa P.A.Y.E pekee , aya NSSF inakata 10%, W.C.F inakata 0.6%, Kama alichukua mkopo wa elimu ya juu HESLB 15% inakata, NHIF ali alichukua bima category ya najali afya kwa mwaka analipa Tsh.192,000 hivyo kwa mwezi inakata 2.46%, labda pia alikata bima ya maisha au chombo chake cha moto kila mwezi itabidi acontribute, net pay ya Ali itakuwa Tsh. 486,000/ Ambayo bado iko kwenye benki Y, kutokana na kuhifadhiwa pesa zake Ali atahitajika alipe Monthly fees, akitaka kutoa pesa benki kwa A.T.M ( Kobe Ukuta) kuna benki charge za kuwithdraw plus na plus na GOVERNMENT LEVY plus na tozo izo mpya za kuamisha pesa kutoka benki kwenda kwenye simu au benki kuja mkononi, Bila shaka baadhi ya watu wataona ni non-sense izo tozo, transaction za above million 3 tozo ni tsh. 4000/= chini ya million 3 apo tozo hutofautiana kutokana na mgawanyo.

Huyo Ali akihamisha pesa benki kwenda kwenye simu , akitaka kutoa pesa kwenye simu kama pesa taslimu anakutana na tozo nyingne ya simu. Sasa hapo kuna mkanganyiko tozo zitakuwa zinajidouble ili jambo linaleta sitofahamu kwa wananchi. Labda fikiria tena Ali anataka kumtumia pesa mama yake ehe kahamisha pesa toka benki mpaka kwa simu alafu amtumie mama yake na mama yake Ali atahitaji kutoa pesa , kwenye mnyororo kama huo kutakuwa na tozo 3 tofauti tofauti.

Tujitahidi kusoma hiyo finance act iliyochapishwa july 1 2022, the national payment system act (CAP 437)

Maswali ya kujiuliza

  • Serikali inakata tozo mpya kimya kimya bila utoaji wa taarifa kwa wananchi, kisha watatoa ufafanuzi baadae , Je ukweli na uwazi unaoimbwa kila siku na viongozi hao una mantiki gani?
  • Je..! Benki nyingi zitakosa mapato ya kujiendesha ambayo wanategemea kutoka kwa wanachama wake?
  • Mwanzoni mwa mwaka huu kwenye mwezi wa 4 hivi tulielezwa na Raisi wa Jam.Ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akifanya mahojiano kupitia Azam TV kuwa Deni la taifa limepungua kutoka 40% mpaka 30% kwa kila Tsh.100/= ya mapato. Je mfumoko huu wa bei za bidhaa na mafuta ghafi sambamba na kuongezeka kwa kodi aina ya tozo serikali inatumia mfumo upi wa fiscal policy kujiendesha kiuchumi?
  • Je mfuko huo wa tozo tofauti tofauti lengo lake ni lipi?
 
Back
Top Bottom