Makapuku Forum

Makapuku Forum

TOP TEN
Week end huanza Ijumaa hivyo leo sitajadili siasa wala uchumi au mambo ya elimu ni burudani,udaku au starehe kama kawa
ce3e29b3091b4cf5be7bacc097daa6d9.jpg

Hapa Bongo hakuna asiyemjua Giggy Money(Muuza Supu) ana mzigo wa nguvu.....
.
.
Sasa leo tuwaangalie wale wasanii maarufu kumi wanaosifika kwa kujazia
Hakuna hakuna akina Masogange kwenye hii list maana wanaongelewa ambao ni maarufu zaidi
Karibuni
..........
Sawa sawa mkuu

Namsubiria Muuza supu
 
5/Peace Hyde
ca36d393a08d28af1d69ad0f61ef23d2.jpg
ce1f461aa7b45fefe04bff058ae67a59.jpg

Huyu ni binti wa Kighana
Ni mwongoza vipindi vya luninga na matamasha katika nchi za Ghana na Uingereza
Ni binti kichwa aliyepata Shahada ya kwanza bila kusapua !!! Ana Degree in Psychology(Hons) kutoka Middlesex University huko kwa Malkia
Ametajwa karibu kwenye kila jarida linalozungumzia wanawake wenyewe mvuto barani Afrika
........
Kweli anavutia

Cc SHIMBA YA BUYENZE
 
Muziki ni Maisha

Makapuku habari za kushinda, najua tumefurahia segment ya 'wadada waliojaariwa maumbo makubwamakubwa' kwa hisani ya Bitoz , sasa turudi kidgo kwenye mambo ya muziki na kama kawaida ni vionjo vya gitaa huufanya ,muziki uwe na utamu unaopendeza kwa wengi wetu.

Leo tupo hapa nyumbani, na zaidi pande za Bagamoyo. bagamoyo ni mji wa sana aa na unasifika kwa kuwa na chuo kikubwa kabisa na maarufu kwa kufundisha wasanii wa fani tofauti nchini na duniani kwa ujumla. Wapo wasanii wengi wamepita Bagamoyo, bahati mbaya sana wengi hawa hawana jina kubwa sana nchini na nyimbo zao nyingi hazipewi nafasi kwenye vituo vya radio au TV. Kuna sababu, unamjua Jhikoman, Ashimba, na Vitali? wanavuma nje ya mipaka ya Tanzania kuliko nyumbani. Sad.

Anajulikana sana hapa nchini kwa wimbo wake wa Sumu ya Teja, huyu ni Vitali Maembe. Vitali anajua kuimba, kutunga na kuandika mashairi.

Hupiga gitaa la nyuzi sita, na unapochanganya na sauti yake ya mchomoko basi hutachoka kumsikiza akiimba na kupiga gitaa lake.

Mara nyingi sana na nyimbo zake zote zinamfanya awe ni mwanaharakati zaidi, anapingana na rushwa na kutokana na aina ya muziki anaofanya keshaingia matatani na watawala mara nyingi ikiwemo kupigwa na kufutwa kwa ziara ya album yake yenye jina Chanjo ya Rushwa.

Ukipata nafasi isikize album hii, ipo bure mtandaoni kwani ilipata ufadhili wa Waswidi na ilikuwa wafanye ziara nchi nzima kugawa hii album lakini wenye mamlka hawakupenda, nadhani iliishia Dar na Bagamoyo tu.
Muziki una nguvu, na hivi ndivyo imekuwa wakati wote, hayupo wa kumpangia msanii nini cha kuimba na kama alivyowahi kusema Steve Biko ' naandika nnachopenda' ndivyo wasanii mahiri wataendelea kuisemea jamii ikiwa wabunge na wanasiasa watakaa kusema matumbo yao.

Msikize Vitali hapa akidonoa gitaa la nyuzi sita




Tujiandae na kusherekea Siku ya Mama

Hakika mkuu Jorowe leo kitu umeleta kitu cha jikoni haswaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom