OMBI....OMBI....OMBI!!
Kutokana na thread kuwa na post/comment/reply nyingi kuliko yoyote ile humu JF na kufuatiliwa na watu wengi na kuwa na spidi kubwa ya watu kupost hivyo.....
Napendekeza kila mwenye segment/mada/kipindi humu abuni au awe anaanza na title/heading/kichwa cha habari/utambulisho.....inapendeza zaidi kichwa cha habari likiwa kifupi
Hii itarahisisha wale wanaopenda vipindi fulani kuweza kufuatilia kwa urahisi hata kama wamechelewa maana watasearch hii option linapatikana kule juu pembeni Julia kwenye kila thread
Mfano iwe;
*Leo katika historia
*Unbelievable Facts
*Nukuu ya Leo
*Neno la asubuhi
*Magazeti ya Leo
*Burudani ya usiku
*Top Ten
*Je Wajua ?
*Did you know ?
*viwanjani Leo
*Vunja mbavu
n.k
Viandikwe kwenye utangulizi/post ya kwanza
.
.
.
Natanguliza shukrani
Nawatakia asubuhi njema
By
Nyangema
...........
Wazo zuri sana mdau, naamini kwenye kipande ambacho huwa napandisha wadau Makapuku wanaweza kupendekeza "title" yake.
Labda kwa uchache, kwangu kama ilivyo kwa wengi wetu, siishii tu kueleza utamu wa gitaa na mpigaji.
Gitaa katika muziki ni kinogesho wa kile kinachowasilishwa na mtunzi, mwandishi kwa hadhira yake.
Muziki ni maisha na bila muziki maisha yetu yangekuwa very boring, kila siku tungekuwa watu wa viwanda tu, vita tuu, kazi tuu na vitu vingine vinavyochosha. Muziki umerahisisha haya na kuyafanya yawe rahisi.
Muziki ni maisha, ni aina ya kipekee ambayo mtu anaweza kujieleza na akaeleka kwa urahisi. Wapo wasioweza kujieleza, wana aibu ila muziki unawapa kujiamini na kusikizwa.
Kwenye gitaa la muziki kuna kila kitu unachowaza, kuna sayansi, hesabu, mapenzi, siasa, kisasi, maendeleo, hisia, nia, mapinduzi, shukrani, imani/dini na chochote unachowaza. Nguvu ya muziki inajieleza katika haya niliyotaja
Niandike nini nisikuchoshe, nitakuwekea muziki na siku zote naamini tuliumbwa na anayependa muziki.
Weka pendekezo lako hapa. Tukutane baada ya muda mfupi nikikuletea mambo ya sauti tamu za gitaa.