Makapuku Forum

Makapuku Forum

Bwana asubuhi utaisikia sauti yangu, asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia

Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya mtu mwovu hatakaa kwako

Wajivunao hawatasimama mbele ya macho yako unawachukia wote watendao ubatili

Utawaharibu wasemao uongo Bwana humzira mwuaji na mwenye hila

Bali mimi kwa wingi wa fadhili zako nitaingia nyumbani kwako na kusujudu kwa hiko nikilielekea hekalu lako takatifu
ZABURI:5:7
Natawakia asubuhi ili njema sana mbarikiwe sana
 
89a4694b9d8680aea274a5fcbfe4425a.jpg
Mkuu mbona kuna alama ya wekundu?
 
4/Billy &Benny Loyd McCrary
a0bcae50d99cec9e86f21c19963e802d.jpg
261cd2559f27c06fcbddbb33bf21dcd0.jpg
8b4c30dde7a5ac2a230cc8a7e115fb5e.jpg

Walizaliwa Disemba 7 1946
Hawa ni mapacha wanaoshikilia rekodi ya kuwa mapacha vibonge zaidi kuwahi kutokea duniani
Walikuwa na uzito wa jumla wa Paundi 1468 (Kg 670+)
Mmoja alifariki wakati wakiendesha pikipiki ya pamoja(pikipiki pacha) mwaka 1979.....walipendelea kuendesha pikipiki
Mwingine akafariki mwaka 2001 kwa ugonjwa wa moto
Makaburi yao yamejengwa kwa kuyaunganisha sehemu moja

.............
Vibonge haswa

Kaka Bitoz samahani huo uzito ni wa mmoja au kwa wote?
 
Muziki: Wema na Ubaya, Cha Pili Kiache

Muda unakimbia sana Makapuku waheshimika, nani alijua kesho itakuwa ni Ijumaa! Ukisoma kiumakini utagundua kuwa sijauliza swali ila tu nimekuja kukusalimia wewe, yeah, wewe hapo unayenisoma muda huu. Pokea heshima nyingi sana usiku huu maana unastahili na stahili hii ni kwa sababu wewe unaunda timu inayoifanya KF iwe mahala pa kuvutia bila kutolewa mahari. Asante sana kwa kuwepo hapa.

Hivi kuna sababu yoyote ya kutofanya jambo zuri kwa mtu usiyefahamiana naye? Usiniambie kuwa dini zimetufundisha kuwa wema maana dini zetu hizi zina mazongo kibao, so weka pembeni jibu la dini yako jibu wewe kama wewe. Binafsi ninajiaminisha ukiwa mstaarabu (civility) huhitaji uijue dini ndo utende wema na uuchukie ubaya. Kuna bangi na bangili, hiyo ya kwanza inatibu sikio. Chukua hilo maana kubadilika ni tabia ya kila kiumbe hai. Hulazimishwi kubadilika, baki hivyo hivyo kama mother nature itakuruhusu.

Asanteni sana wadau mliotuamsha kwa magazeti, sala, BBC, kubwa 10, sogozi za mchana, michezo na zaidi asante kwa wageni waliotembelea hapa. Usijiulize mbona ninakaribisha sana kwani mimi ni nani hapa, mbona najidai kujua sana, well, la kwanza, mimi ni kama wewe tu, bando langu na kutaka kupata maarifa kwa kuwa hapa kunanifanya nije hapa na kuwaona wengine wakiwa hapa basi nawiwa kuwashukur maana maarifa yanaongezeka.

Muziki sasa, huwa nikimsikiliza nakumbuka mengi sana, mazuri na yenye utata ulionifanya nijiulize je hili nililolifanya (enzi hizo) ni sahihi. Hizi safari ziache tu na wengine tukiendaga ugenini lodging zina mapepo hatulali peke yetu, you know warra am saing'i. Ndivyo inavyokuwa na ndo unasema a blessing in disguise. Anaitwa Jose Chameleon, ana udokta wa heshima huyu kwa namna anavyotumia mali zake kusaidia wahitaji wanaomzunguka.
Burudika mdau


932d6af2055baf58aca3f3245a9f13ea.jpg
tuko pamoja mtaasisi
 
1/Ashley & Mary--Kate Olsen
416dc5e515340511ebd672d75b954e49.jpg
8b4670ad2ec1838964c1b4e3846faeac.jpg
7ef286a41d94e6b425b391fb4a88fbed.jpg

Walizaliwa Juni 13 mwaka 1986 nchini Marekani
Hawa umaarufu wao inatokana na pesa walizonazo.....hawajafikisha hata miaka 35 lakini wana mkwanja mrefu wa kuweza kuwahonga hadi Sizonje na Bashite waamue kuuza nchi nzima ya Bongo na kutuacha wananchi tukipiga miayo
Wanatajwa kuwa wanawake matajiri # 10 duniani
Pia pengine ndo mapacha wenye mpunga mrefu zaidi duniani
Utajiri wao ni zaidi ya USD milioni 300
.
.
.
.
.
.
.
.

Shukrani kwa mliosapoti mada
Niwatakie Usiku Mwema
Tukutane kesho
Mwisho
..........
Shukrani mkuu
 
Muziki wa Wadhamini

Kuna muziki na wanamuziki ukiambiwa wapo unaweza bisha lakini ukisikilizishwa nyimbo zao basi utagundua kuwa hujui mengi. Ndo inavyotokea kwangu na hii ni sababu tosha kabisa ya kuwa hapa na kama Fid Q anavyosema, usijue mengi bali jifunze mengi. Asante Shunie kwa wimbo wa Jidenna uitwao Bambi. Ni mzuri na japo jamaa ni kutoka US of A lakini anachanganya mipigo fulani hivi ya Kinaijeria na utapenda muziki wake. Chaguo la kwanza hilo, kumbuka yapo mawili


Great choice
 
Nawaza kuwa lile neno la ulinzi ndio linatimia au naota

BTW muwe na wakati mwema

Wale wakukazana waendelee
Wale wa kususa waendelee
Wale wa kujitoa in public waendelee
************Nitamalizia***********
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom