Makapuku Forum

Makapuku Forum

When you believe, there can be miracles.......

Asante sana Shululu kwa muziki was muda huu unaosindikiza thread ya mjomba kwa aunt yangu
Nimeona niwachombeze kidogo wakati wanatafuta usingizi

Unajua mimi wajomba zako nawapenda sana
 
Inaendeleaaaa.......


...........Asubuhi na mapema ndani ya Kijiji cha Mkuyuni kwenye nyumba ile ile ya mzee Mnyungunyungu ambayo shabaha na mipango ya Cj4 ilienda barabara na kutua sehemu husika kabisa na hesabu zake alizopiga awali ili kubaini kilichowakumba askari na kilichoikumba ile familia zaidi akitafuta ukweli wa huyo mr X.

Alijinyoosha pale ndani na kutoka nje asubuhi na mapema na kuelekea kule kwenye choo ambapo njia yake ilionesha kuwa na majani majani yaliyoashilia kuwa kile choo alichokuwa anaenda yeye hakikutumiwa muda mrefu kidogo.
Alitembea taratibu huku akipiga hesabu nyingi kichwani kutokana na maelezo aliyokuwa nayo juu ya tukio la mtu wa mwisho wa familia ile ambae inasemekana alikutwa amejinyonga ama amenyongwa pindi alipoenda chooni.
Kwa kutumia akili za kijeshi na mbinu hadimu alizokuwa nazo Cj4 alisimama ndani ya kile choo na kuangalia juu ambapo kulikuwa na matawi makubwa ya miti yaliyokatisha na kuvuka kile kipaa cha choo ambacho kilikuwa hakijaezekwa na alitumia dakika tano kutazama vizuri kule juu na kuanza kurudi nyuma huku akivuta taswira na kutengeneza picha kichwani mwake ambapo alianza kuona yule mtu alipoingia pale chooni na aliangalia kwa juu na kuona kamba iliyotengenezwa mtindo wa kitanzi kikubwa ikishushwa taratibu na kumvaa pindi aliposimama na kabla hajafurukuta kitanzi kikapandishwa na kumkaba shingoni.
Alizunguka kwa nyuma ya choo Cj4 harakaharaka huku ile taswira ikiwa bado kichwani mwake na kuangalia upande wa juu na kuona kuwa alilala mtu shupavu na makini aliyevaa nguo maalum na vifaa vya kininja akiwa anaivuta ile kamba kwa kuizungusha kwenye skurul aliyoifunga kwenye tawi ambayo ndio ilishikilia ile kamba maalum aliyomshushia na kumkaba yule bwana aliyekuwa chooni na kupanda juu taratibu huku akiwa anapapatika na kushindwa kutoa sauti kwa jinsi alivyokabwana na pindi alipofikishwa juu kabisa ya lile tawi alikuwa tayari ashakufa na alichofanya yule ninja aliyekuwa anamuona kwa taswira tu kuwa alichomoa skurul baada ya kuivinga kamba yenyewe kisha kumuacha yule mtu akiwa ananing'inia pasi na kumgusa mithili ya mtu aliyejinyonga mwenyewe.

Alizunguka tena Cj4 na kuendelea kuiona taswira kuwa yule Ninja alishuka na alipofika chini akaondoka kabisa eneo lile.
Ndipo akaanza kufata hatua alizohisi moja kwa moja alipita yule muuaji.
Wakati huo Cj4 alikuwa makini mno na akiwa anaendelea kutokomea kabla hajafika mbali alistuka baada ya kusikia mtu akipiga chafya na alipogeuka kumtazama alimuona kwenye kichaka kilichokuwa jirani na ule mti mkubwa na ilionesha wazi yule mtu alikuwa anamtazama kwa muda mrefu tu hasa kwa jinsi nae alivyostuka baada ya kutazamana uso kwa uso na Cj4

"Afadhali mzee nadhani wewe utanisaidia"
aliongea Cj4 na kupiga hatua kumfata yule mtu ambae alikuwa ameshika Mundu (panga la kienyeji) na kifuko kilichokuwa na maembe ambapo alijibainisha pale pembezoni mwa mti mara baada ya kujua kuwa kaonekana pindi alipokuwa anamshangaa yule kijana.
"Mh! mbona sikufahamu baba?"
aliuliza kwa hofu kidogo yule babu ambae alimtazama vizuri Cj4 na kupatwa woga nae wa ghafra hasa alivyomtazama sehemu za kifua na mikono huku uso wake ukionesha ni mtu wa tofauti sana kwa jinsi alivyokuwa bussy muda uliopita kabla hajamstua kwa kupiga chafya.
"Mi mgeni hapa mzee wangu nimeingia jana tu na nimesaidiwa na mjumbe kulala hapa lakini alinambia kuwa wenyewe waliikimbia hii nyumba na watu wengi wanaiogopa sasa ndipo nami nilipokuja chooni kujisaidia moyo umeniripuka na kujikuta nakuwa na woga sana ndio maana nilikuwa naondoka nikajisaidie kule porini."
"Hee! baba basi mi naenda shamba we kajisaidie tu huko hata wanakijiji wengine mbona wanajisaidiaga porini."
aliongea yule mzee na kuanza kuondoka huku moyoni mwake akiwa na hofu bado "
"Samahani lakini babu naomba nisikilize kama utakuwa na uwezo wa kunisaidia"
alisisitiza Cj4 na kumshika mkono yule babu aliyekuwa ameanza kuondoka eneo lile.
"Mwe!! haya nokutegeleza"
alijibu mtindo wa sitaki nataka yule babu na kusimama tena
"Ni hivi babu hebu njuu kwa huku kwanza nataka tuongee kitu muhimu na nitakupa pesa nyingi ili unifichie siri hii babu, ukweli mimi ni Polisi na nimetumwa hapa kupeleleza juu ya kilichotokea hapa juu ya mtu aliyenyongwa siku za nyuma, na nimekuja kuondoa uoga uliotawala eneo hili"
aliongea safari hii kwa sauti ya chini Cj4 na kumfanya yule mzee atulie na kusikiliza kwa umakini huku moyo wake ukifurahi ghafra kwa kujua kumbe yule ni mwanausalama.

Ndipo yule mzee alianza kumfata taratibu kwa kunogewa na story aliyokuwa anahadithiwa na Cj4 huku wakiingia kwa msituni kidogo kukwepa watu wasiwaone pia yule mzee alimuongoza Cj4 hadi maeneo yale yalipowahi kutokea mauaji ya Askali miezi kadhaa iliyopita baada ya kuulizwa kama anapafahamu.
"Mh! baba nakuahidi ambe hajatuona mtu tukiongea,! na eneo hili watu wengi wanaogopa kufika hadi sasa hivi, basi hatojua mtu yeyote habari zako baba Niamini."
aliongea yule babu pindi walipofika eneo lililoshona majani mengi na miti mikubwa.
"Ni kweli mzee, lakini tatizo hata Askali aliyekuja kupeleleza awali alifanya ujinga kwa kumuamini mzee kama wewe na mwishoe akamsaliti na kusababisha Mauaji kwa askali wengine."
Alinena kwa sauti tofauti iliyokuwa serious zaidi Cj4 na kumfanya yule mzee astuke hadi akaangusha kile kifuko chake cha maembe na na kabla hajageuka alistukia kashakamatwa kichwa kwa mikono shupavu ya Cj4 na kuanza kubinywa hadi sehemu za taya zikaanza kupishana na hakuwa na uwezo walau wa kutoa sauti ama kupiga kelele.
"Kawaambie huko uendako kuwa Umekumbana na mstari Mwekundu wa CJ4"
Mara Cj4 aliponena maneno hayo tu palepale alipindua kwa nguvu kichwa cha yule babu na kuivunja shingo yake kisha kumuachia na kudondoka kwenye manyasi ambapo alianza kupapatika pale chini kwa zaidi ya dakika kumi mpaka akatulia na kuaga dunia rasmi.

"Kama na wewe uliekwa na mr.X ufanye uchunguzi wa watu wataokuja kuchunguza hapa basi ajue kuwa mbinu zake zimezeeka"
aliongea Cj4 na kuchukua ile mundu ya yule babu na hapo aliuvinga mkono wake mmoja kwa kile kifuko kilichokuwa na maembe baada ya kumwagika pale chini kisha akatumia mkono ule wenye mfuko wa naironi kukamata sikio la yule babu na kuanza kukata ngozi yote upande wa sikio la kulia sambamba na sikio lenyewe kisha alimgeuza na kufanya vile vile upande wa sikio la lengine na kumuacha.
("sasa na waje tu wakupime pindi watapojua")
aliwaza moyoni Cj4 huku akiifuta futa damu ile mundu kwenye manyasi na kuzishika vizuri zile ngozi zenye vipande vya masikio na kuanza kupiga hatua kadhaa kuelekea kule alipotoka na alipokaribia kwenye ule mti wa awali alisimama na kuchimba kishimo cha futi moja na kuzizika zile ngozi kisha akafukia na kuweka weka nyasi juu yake ambapo ilikuwa vigumu sana mtu kubaini kama sehemu ile imechimbwa.
Alifanya hayo yote ili hata kama wataigundua ile maiti mapema na kuja wachunguzi kupima watachojua ni kuwa amevunjwa shingo tu, lakini hawatapata alama zozote za muhusika aliyemvunja hususani zile za mikono.
Baada ya kuhakikisha mambo safi huku akiwa makini asionekane na mtu yeyote alinyanyuka na kuelekea hadi pale kwenye kile choo kwa uangalifu na kuitumbukiza ile Mundu chooni
lakini alipotoka chooni tu na kufunua kile kigunia kilichofungwa kama mlango alikutana uso kwa uso na mtu akiwa kasimama pale pale mlango wa choo.




.....................
 
Ndo maana nikakuambia kuwa mtulivu cha kwanza hakihitaji mbwembwe, umeona muziki umeshindwa kufunguka hadi cha pili haina cha tako tatu ule wimbo wa jana
Cha kwanza hapo binamu umemaanisha nini tena ambacho hakina mbwembwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom