Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kuna msemo unasema

Money is what money does

Wachumi waamnini Hela ni tool of exchange baada ya maisha ya better trade..

Money can be changed for goods or service as far it has been accept by the surrounding society...

Nirudi kwenye picha sasa;

Kuna mahusiano baina ya mwanamme na mwanamke ambayo yanasababishwa na nguvu ya hela na ndio kulichopo kwenye picha hapo..

Mwanaume anatumia hela kumpata mwanamke..! Utaona hela zimetumika kama ngazi/ kiunganishi kwa mwanamke kumfata mwanaume...

Mwisho;

Wanaume Tutafuteni hela wakuu.

I stand to be corrected..
upo sahihi mkuu amna correction kwenye maelezo yako
 
Kuna eye-hole moja kwenye simu ila zipo nyingi pembeni

Ila kuna vitu watumiaji wa simu hatukijui..! And i want to put this clear kama na IT hapa ataongeza.

Ukipiga picha kwenye simu yako utajua kuwa wewe ndie mwenye accessibility tuu ila sio kweli..

Social netwerks zinanasa sana picha za kwenye simu zetu..! Ukipiga picha na kupost humu afu ukaifuta , hapo umeifuta kwako tuu..ila jf itakuwepo milele..

Nenda fb au insta kule..post picha! Baada ya muda ifute ile picha...ila owners wa fb na ista watakuwa na picha yako kwenye data base zao milele..


So hivyo vitu kama macho ni media ambazo ziko aware na picha/video unazopiga kwa simu yako..


I stand to be corrected
2dfe58930b6a108de8e15c80bae3543e.jpg

Pia Ujinga/ujanja huufanyao leo unaweza kukugharimu kesho

......
 
Jiamini utusaidie
Kila mtu amejaaliwa maarifa

Na madada wote akina Husna,Shumy,Mama Mchungaji &,Tumosa tusaidieni kidogo

......
Nitasema kidogo hizo ni codes kwa kiswahili ni vichokoo hutoa tafsiri kutokana na mtazamaji na mazingira aliyopo haziwezi kuleta tafsiri inayofanana kwa wote ni mtindo unaofaa kuibua mijadala kufundisha watu wazima kuleta mabadiliko ya kisiasa kiuchumi kiimani kijamii kimila nk unaweza tumia wakati wowote kuwasaidia watu kuleta majadiliano chanya ya kusaidia kubadili hali fulani, vinatakiwa viambatane na masuali Mf 1 umeona nini 2umeonaje. 3hali hii ipo ktk mazingira yenu 4 nini kifanyike 5 umejifunza nini? kutumia au kukiondoa nk. Ni mchakato fulani hivi kwa kuwa ni vingi ngoja nitapitia kimoja nitoe mrejesho wa nilichojifunza
 
Nitasema kidogo hizo ni codes kwa kiswahili ni vichokoo hutoa tafsiri kutokana na mtazamaji na mazingira aliyopo haziwezi kuleta tafsiri inayofanana kwa wote ni mtindo unaofaa kuibua mijadala kufundisha watu wazima kuleta mabadiliko ya kisiasa kiuchumi kiimani kijamii kimila nk unaweza tumia wakati wowote kuwasaidia watu kuleta majadiliano chanya ya kusaidia kubadili hali fulani, vinatakiwa viambatane na masuali Mf 1 umeona nini 2umeonaje. 3hali hii ipo ktk mazingira yenu 4 nini kifanyike 5 umejifunza nini? kutumia au kukiondoa nk. Ni mchakato fulani hivi kwa kuwa ni vingi ngoja nitapitia kimoja nitoe mrejesho wa nilichojifunza
Ni kweli sikutoa maelezo mazuri mwanzoni
Siku nyingine nikizipata nitazileta kiserious
.....
 
Kavaa uhusika wa aina mbili binadamu na robot ...fikiria kwanza apo
Still bado kuna computer ...
Ukianggalia usoni lijamaa kama limepigwaa butwaa uku uso umelimitiwa na mbao sio fc wababe wa yanga

kwanza kutoonesha kioo cha komputa ...kwanza sisi hatujui kinachoendelea na yeye kwa uso tu hajui hakifanyachooo
Sijakuelewa hapa
 
NGUMU KUMEZA ...

Kwa wale wapenzi wa gozi/mpira chukua dk 4 kupitiaa ...

GOLDEN BOY MAPUNG'O: MPIRA ULIOTUACHIA UKIWA UMETOBOKA HATUJAUZIBA BADO...

88aaf3e7251404ef3dc03eb082e3996a.jpg


Siku watu waliokaa chini na kujadili mambo mengi kuhusu mpira, huku kwetu tulikuwa Bado hatuja funguka macho, ndio kwanza almasi na dhahabu tulitumia kama kete za draft na bao..... Siku walipokaa tena na kuunda mpira wao, huku kwetu babu zetu walikuwa wanawashangaa wakoloni na familia zao wanapiga piga mpira kila jioni....... Siku walipokaa tena na tena kwaajili ya maboresho ya gozi lile, sisi Bado tuna shangaa na kuendelea kuwaona wakoloni wajinga kwa kupoteza muda wao kukimbia kimbia uwanjani.......

Walichotunyima ni sisi kuwa kama wao, ila walichoturuhusu tu ni sisi kuwaiga wao....... Ndio maana hakuna kilicho andaliwa huku kwetu kikaenda kufanyiwa kazi kule kwao tofauti na nguvu zetu tu, ndio maana kila kitu walikiandaa wao na sisi tukaruhusiwa kutumia Bila kubadilisha ata nukta......

Sheria 17 za gozi lile wanajua wao walipozitoa na ni kwanini wameweka....... Sisi Leo 2017 Bado hatujafika walipopita mwaka 1999... Ndio maana hatua zetu ni ndefu kama mawazo yao lakini ajabu ni kwamba hazigusi chini kama malengo yetu.

Ndio maana nyasi bandia zinafika kwetu sasa ila kwao zilishapita na wameshaziacha.... Ndio maana kucheza michezo usiku wao wameshazoea ila sisi ndio tunajitutumua, ndio maana sheria zao haziitaji vikao vingi, sisi Bado tuna ukakasi, ndio maana Transfer matching system (TMS) tunaanza kuitumia sasa ila kwao ni kitu kizee......

Rangi zetu nyeusi ndivyo zilivyo ambatana na weusi wa maamuzi yetu katika soka, weusi wa mapambano yetu katika soka, weusi wa kujituma katika soka, weusi wa kuridhika na mafanikio kidogo katika soka, weusi wa kupambana na weusi wa ujanja wa kuchuma.....
Ukiachia weusi wetu katika soka Bado Mungu alitujaalia busara, hekima, nguvu, vipaji na upambanaji wa kujitoa...... Ndio maana Zama zile wakitumika kuleta utajiri wa ulaya mababu zetu wale wa kale katika biashara isiyo huru na wao wakatuachia mipira ile waliyokuwa wanaicheza kila siku jioni.....

Wakati tukipishana na wanaojua mipango katika soka, mbinu na namna ya kupiga hatua katika soka, nashukuru Mungu hatukubaki nyuma katika kuwaiga kwa namna moja ama nyingine......

Wao walituletea bablish zenye picha za wachezaji ila sisi tukawanogeshwa na jarida/gazeti la Sun na ligi ya utawala wa wajanja wa bush.

Riziwani Reagan Ridhwani.... Huyu mwanadamu alihusika kunifanya nimiliki daftari lililojaa picha(stika) za wachezaji wa ulaya enzi hizo, ila pia alinifanya kumiliki majarida/gazeti la Sun lililokuwa na ligi pendwa ya picha zenye maneno..... Kupitia yeye nilimuona Golden boy Mapung'o katika ubora kuliko uhalisia wa George Opong Weah, kupitia yeye niliweza kuwafahamu wachezaji watatu tu duniani waliokuwa wakicheza mpira wa miguu huku wakiwa na kofia na hata mawani..... Edger Davies na mawani yake katika picha, ila pia Peter Manyika katika kofia yake na mikono yake katika kurasa za mbele za magazeti, vipi kuhusu Mtaalam wa chimbo na kuopoa kwa fedha mzee Lord lofa na lile kofia lake uwanjani..

Zama hizo ndizo Mimi na Andrea Zlatan Mushi tulikuwa tunahadisiwa kuhusu ubora wa Zama za Sandy Manara Computer huku tukimsoma Golden Boy Mapung'o na umaridadi wake......

Zama hizo ndio ndizo kulikuwa hakuna mashine za kupunguza ukubwa wa jezi na kuwa saizi ya kila mchezaji kutokana na umbo... Na Bado Zama mpaka sasa hatujaweza kuuziba mpira ule uliotuachia.

Imefika mahali sasa tunaweza kukaa kiti kimoja pale taifa na kuwaangalia Brazil na Robinho wake, kuwatizama Ivory coast na Drogba wake, senegal na kamara wao..... Dah Zama zinapita sana tangu Golden boy Mapung'o uondoke, huku mtaani kila jioni baada ya mechi tumekuwa tukisema umeondoka na mpira wako, umeondoka na timu yako umeondoka na mbinu na utaalamu wako.... Hapa mpira ulikuwa una slow pancha.

Zama hizi sasa hakuna tena zile hadithi za Peter Tino, hakuna tena zile soga za Pele wa mwanza ili kina Ramadhani Singano na Hassan Kessy waziige..... Leo maandishi yote na maneno yote yanakuhusu wewe Golden boy Mapung'o na timu yako katika Zama zako......

Tunamisi mpira uliochezwa viwanjani na kidogo ukachezwa mezani, tunamisi mipango iliyokuwa kwenye makaratasi na kidogo kichwani...... Tunakulaumu umeondoka na vitu vyooote ulivyotuandalia.

Ndio maana Leo tunahadisiana tu hadithi mpya za Ludovic wa mbao fc na African Lyon, lakini pia Mubarak Yusuph wa Kagera, Simba na Azam fc...... Tunakukumbuka sana mzee wa bush japo wewe na kizazi chako cha dhahabu mliwatesa kiasi waamuzi kuliko goli la mkono wa Chirwa, offside ya Ajibu na hata kadi tatu za Mohammed.

Golden boy Mapung'o..... Marcio Maximo aliondoka najua unajua, Jan Poulsen aliondoka najua unajua lakini pia Kim Poulsen naye aliondoka pia najua pia hilo unalifahamu...... Kabla hajaja Martin Noij najua unajua Kodi ya mishahara ya waalimu hawa haikuwa katika zile pretty cash za pale maeneo..... Ila pia Bado tumekosa kutambua tofauti ya Serikali na Mamlaka ya mapato katika mishahara unayoijua Golden boy Mapung'o.

Golden boy Mapung'o ule mchezo mtamu wa kombolela naona sehemu kubwa duniani wameshabutua kopo..... FIFA kabutua Infatino, lakini UEFA walizinga ila katibua Cefferin, usisahau swahiba Issah Hayatu alizinga Ahmad Ahmad kabutua...... Sasa kopo limepelekwa Dodoma sadakalawe ipo dar es salaam.

Watu Wengi wanajiuliza kama kuna timu ya kutufikisha ilipotufikisha Bush Stars yako...... Ndoto kila siku zimekuwa ni zile zile na cha ajabu panawahi kukucha na mpira bado hatujauziba.

Timu yetu ya sasa haina Golden boy Mapung'o wa sasa, inamkosa Kipepe, inamkosa baba ubaya lakini pia kiokote, madenge na Lord lofa....... Najiuliza tu nyie mlikujaje najiuliza pia nyie mliondokaje.....? Bush Stars.

Nashukuru kwa kukushuhudia mzee maana ipo siku ntakuja kusimulia juu yako...... Ila sondano, Uzi na patex utusaidie hata kwa mawazo ili tuuzibe na kuucheza.

Macho na ubongo ndio vinaweza kuelewa ila macho pekee hayatoambilia kitu.....
 
Nimeziweka ili tusaidianekuzitafsiri maana zina maana kubwa iliyojificha

Picha moja inaweza kuwa na maana/tafsiri hata tatu
Tujuze ulichoelewa
Zingine zishapata majibu huko nyuma
....
nimekupata mdau ujue nilisoma comment za kati hapo kwaiyo sikuelewa na picha nyingine sikuziona, lakini nimeshakusoma na nimezicheki nyingine za nyuma... sa tupo pa1
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom